RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA UJUMBE WA WATAALAMU KUTOKA NCHI BRAZIL IKULU ZANZIBAR

June 26, 2024

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Kiongozi wa Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchini Brazil wa Mradi wa kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto Bi. Camila Guedes Ariza, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 26-6-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchini Brazil Wanaojishughulisha na Mradi wa kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto, ulioambatana na Mwakilishi wa Heshima wa Brazil Zanzibar Mhe. Abdulsamad Abdulrahim (kulia kwa Rais) na Kiongozi wa Ujumbe huo Bi.Camila Guedes Ariza, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 26-6-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wataalamu Maalumu kutoka Nchini Brazil Wanaojishughulisha na Mradi wa kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto (kulia kwa Rais) ukiongozwa na Bi.Camila Guedes Ariza na (kushoto kwa Rais) Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar ukiongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 26-6-2024.(Picha na Ikulu)

RAIS DKT. SAMIA ATOA MHADHARA WENYE MADA YA FARSAFA R4 AMBAYO ANAITUMIA KUONGOZA SERIKALI

June 26, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Wanadhimu Wakuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi- Tanzania kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Mhadhara wenye mada ya Falsafa R4 ambayo anaitumia katika kuongoza Serikali ya Awamu ya Sita . Mhadhara huo umefanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi- Tanzania kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Juni, 2024. Falsafa ya R4 ya Mhe. Rais Samia ni Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reforms (Mageuzi) pamoja na Rebuilding (Kujenga upya)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa kwa heshima na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Meja Jenerali Wilbert Augustin Ibuge mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 26, Juni 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wanadhimu Waandamizi Waelekezi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi  mara baada ya kuwasili  katika Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi (NDC), Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 26, Juni 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Mhadhara wenye Mada ya Falsafa ya R Nne (4Rs) ambayo anaitumia katika kuongoza Serikali ya Awamu ya Sita. Mhadhara huo umefanyika  katika Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi (NDC), Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 26, Juni 2024. Falsafa yake ya R4 ni: Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reforms (Mageuzi) and Rebuilding (Kujenga upya).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi (NDC), Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 26, Juni 2024.

RAIS MSTAAFU DKT . KIKWETE AONGOZA JOPO WAZEE WA JUMUIYA YA SADC NCHINI

June 26, 2024
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 26 Juni, 2024, yuko katika Ufalme wa Lesotho kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Jopo hili la Wazee wa SADC ambalo Makamu Mwenyekiti wake Mheshimiwa Paramasivum Pillay B. Vyapoory, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Mauritius, limekutana na Serikali na wadau mbalimbali ndani ya Ufalme wa Lesotho, kama mwendelezo wa juhudi ya kusaidia upatitanaji wa utulivu wa kisiasa katika Ufalme huo.

Jopo limekutana na Mhe. Ntsokoane Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Lesotho; Mhe. Nthomeng Justina Majara, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge; Mhe. Mamonaheng Mokitimi, Mwenyekiti wa Seneti; Viongozi wa Vyama vya Upinzani; Mhe. Constance Seoposengwe, Balozi wa Afrika Kusini nchini Lesotho; na wadau mbalimbali.

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanianna jopo la Wazee wa Jumuiya ya SADC wamekutana na Mhe. Ntsokoane Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Lesotho mjini Maseru leo June 26, 2024


Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanianna jopo la Wazee wa Jumuiya ya SADC wamekutana na Mhe. Constance Seoposengwe, Balozi wa Afrika Kusini nchini Lesotho na wadau mbalimbali mjini Maseru leo June 26, 2024



Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanianna jopo la Wazee wa Jumuiya ya SADC wamekutana na Mhe. Nthomeng Justina Majara, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge pamoja na Mhe. Mamonaheng Mokitimi, Mwenyekiti wa Seneti; Viongozi wa Vyama vya Upinzani;mjini Maseru leo June 26, 2024.

PICHA NA OFISI YA RAIS MSTAAFU