MATUKIO KATIKA PICHA LEO BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

MATUKIO KATIKA PICHA LEO BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

August 28, 2014

PIX 1. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia) ambaye pia ni mmoja wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzie leo 28 Agosti, 2014 katika eneo la Bunge mjini Dodoma.
PIX 2. 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge Maalum la Katiba wakitoka ndani ya Bunge leo 28 Agosti, 2014 mjini Dodoma.
PIX 4. PIX 5. PIX 6.
MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA, MHE. SAMUEL SITTA AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUANDIKA HABARI BILA KUPOTOSHA UMMA.

MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA, MHE. SAMUEL SITTA AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUANDIKA HABARI BILA KUPOTOSHA UMMA.

August 28, 2014

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongea na waandishi wa Habari huku akiwaasa kuacha chuki katika masuala yanayohusu mchakato wa Katiba PIX 2 PIX 4 
Mjumbe wa Kamati Namba Tatu ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Francis Michael akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
PIX 7 
Mjumbe wa Kamati Namba Kumi na Moja, Mhe. Hamad Massauni akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
28/08/2014
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amevitaka vyombo vya habari nchini kuacha uchochezi na chuki wakati vinapohabarisha umma kuhusiana na mchakato wa Katiba Mpya.
Kauli hiyo nimetolewa leo na Mhe. Sitta wakati alipokutana na baadhi ya waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma huku akiviasa vyombo vya habari kuachana na kuandika habari zenye kuleta uchochezi na chuki ili kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya .
Mhe. Sitta amesema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa na dhana tofauti kuhusu kazi ifanywayo na Bunge Maalum la Katiba, hivyo ni vema kuepukana nao na kuhabarisha umma taarifa sahihi ili Katiba Mpya iweze kupatikana.
”Kusema tunafanya kazi ya Tume ni upotoshaji mkubwa, sisi tunafanya kazi tuliyotumwa tena kwa uadilifu mkubwa.upotoshwaji mwingine unafanywa na baadhi ya watu ambao hawalitakii mema Taifa letu na hawapendi kuona mchakato wa Bunge la Katiba unaendelea vizuri,” alisema Mhe. Sitta.
Mhe. Sitta ameongeza kwa kutolea ufafanuzi juu ya baadhi ya makundi yaliyowasilisha mapendekezo yao katika Bunge hilo, kwa kusema kuwa maoni yanayoletwa na makundi mbalimbali kwa lengo la kuboresha Rasimu Mpya ya Katiba yanapokelewa lakini sio maoni tu ya mtu binafsi au mwananchi, bali wanapokea maoni kupitia makundi maalum kama yalivyo kwa wafugaji, Wasanii na Wakulima ambao wameshawahi kuwasilisha maoni na mapendekezo yao katika iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba lakini hayakuonekana na mengine yalisahaulika katika Rasimu hiyo.
“Tuna haki na wajibu wa kuyapokea makundi haya ili kutoa Katiba iliyo rafiki kwa wananchi wote,” alisisitiza Mhe. Sitta.
Wakati huohuo, baadhi ya Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge hilo, wamesema wamemaliza kazi ya kuchambua Rasimu hiyo vizuri katika Kamati zao.
Akizungumzia kuhusu kazi hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Namba Tatu ya Bunge hilo, Dkt. Francis Michael amesema suala la ardhi lilionekana kuwa nyeti katika Kamati yake.
Dkt. Francis aliongeza kuwa suala la kupokea mapendekezo kutoka kwa makundi mbalimbali si kwamba kila kitu kitawekwa kwenye Katiba Mpya bali ni yale mambo ya msingi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati Namba Moja ya Bunge hilo, Mhe. Ummy Mwalimu Ally na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Namba Kumi na Moja, Mhe. Hamad Massauni walisema kuwa katika Kamati zao majadiliano yalikwenda vizuri.

MKURUGENZI WA ZAMANI WA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS), CHARLES EKELEGE ATUPWA JELA MWAKA MMOJA KWA KOSA LA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA

August 28, 2014

 Charles Ekelege akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo ambapo alihukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kulipa faini ya sh.milioni 68.
 Hapa Ekelege akiwa amekaa nje ya Mahakama hiyo na familia yake  kabla ya kuhukumiwa. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Ekelege akiteta jambo na familia yake akiwa Mahakamani hapo.
 Askari polisi akiwa na familia ya Ekelege (wa pili kulia), wakati akitoka kwenye mahakama hiyo.
Ekelege akiteta jambo na kijana aliyedaiwa kuwa ni mtoto wake.

MWENYEKITI UVCCM TANGA ATEMBELEA KAMBI LA VIJANA WILAYA YA HANDENI LEO AKUTANA NA KAMANDA WA VIJANA MKOA WA TANGA WAZIRI KIGODA

August 28, 2014
KAMANDA WA UMOJA WA VIJANA MKOA WA TANGA(UVCCM) DR.ABDALLAH KIGODA KATIKATI AKIWA NA VIONGOZI WA UVCCM MKOA WA TANGA,KULIA NI ABDI MAKANGE MWENYEKITI WA UVCCM TANGA NA KUSHOTO NI KATIBU WA UVCCM MWAJUMA RASHID

MWENYEKITI WA UVVCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE KULIA AKISISITIZA JAMBO NA KAMANDA WA VIJANA MKOA WA TANGA,DR.ABDALLAH KIGODA LEO KUSHOTO NI KATIBU WA UVCCM TANGA MWAJUMA RASHIDI


KAMANDA WA VIJANA MKOA WA TANGA AMBAYE PIA NI WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA DR.ABDALLAH KIGODA KULIA AKITETA JAMBO NA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE LEO ALIPOMTEMBELEA

KATIBU WA UVCCM MKOA WA TANGA,MWAJUMA RASHIDI KULIA NA MWENYEKITI WA UVCCM WILAYA YA HANDENI MKOANI TANGA LEO



HAPA NI MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE WA TANO KUTOKA KUSHOTO AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA VIJANA WALIOWEKA KAMBI WILAYANI HANDENI MKOANI TANGA LEO KULIA KWAKE NI KATIBU WA UVCCM MKOA WA TANGA,MWAJUMA RASHID

BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA ALIPOMTEMBELEA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

August 28, 2014


BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA MHE. MARK CHILDRESS WAPILI KUSHOTO AKIWA KATIKA KIKAO NA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT. TITUS KAMANI WA KWANZA KULIA 
BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA MHE. MARK CHILDRESS AKISISITIZA JAMBO KATIKA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT. TITUS KAMANI  HAYUPO PICHANI
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI, MHE. DKT. TITUS KAMANI AKIMKABIDHI  BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA MHE. MARK CHILDRESS BAADHI YA NYARAKA ZINAZOHUSU SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI


BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA MHE. MARK CHILDRESS AKIELEZA JAMBO KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT. TITUS KAMANI BAADA YA KUPOKEA NYARAKA ZA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI 



WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT. TITUS KAMANI AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MGENI WAKE BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA MHE. MARK CHILDRESS
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT. TITUS KAMANI NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA MHE. MARK CHILDRESS KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAKURUGENZI WA IDARA ZA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI OFISINI KWAKE

BURUNDI YAZURU TANZANIA KUJIFUNZA KUHUSU MADINI ,NISHATI.

August 28, 2014
Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha mada kuhusu Sekta ya Madini – Tanzania kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake  (Kulia kwake) waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Upande wa kushoto ni Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.
Na Veronica Simba
Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. C̫me Manirakiza na Ujumbe wake wako katika ziara ya siku tano (24 Р28 Agosti, 2014) hapa nchini kwa lengo la kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.
Katika ziara yake, Waziri Manirakiza ametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam na kukutana na Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Wakiwa Wizarani, Waziri na Ujumbe wake walipata fursa ya kusikiliza mada zinazohusu Sekta za Nishati na Madini zilizowasilishwa na Wataalamu wa Wizara.
Ujumbe huo pia umepata nafasi kutembelea Taasisi na Mashirika mbalimbali yaliyo chini ya Wizara na yale yenye uhusiano na Wizara ikiwemo Mpango wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania (Tanzania Extractive Industry Transparency Initiative – TEITI), Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasimali Madini (SMMRP) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

*MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI NGONGO MKOANI LINDI

August 28, 2014

 Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete akiangalia kinu cha kusindika unga wa mhogo kinachomilikiwa na Tawi la Mkumbara katika Kata ya Jamhuri tarehe 27.8.2014.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ngongo iliyoko Lindi Mjini tarehe 27.8.2014.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ngongo iliyoko Lindi Mjini tarehe 27.8.2014.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia watoto baada ya kulitembelea Tawi la Mtanda lililoko katika Kata ya Jamhuri huko Lindi Mjini mara baada ya kufanya kikao cha ndani katika Tawi hilo tarehe 27.8.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia watoto baada ya kulitembelea Tawi la Mtanda lililoko katika Kata ya Jamhuri huko Lindi Mjini mara baada ya kufanya kikao cha ndani katika Tawi hilo tarehe 27.8.2014.Picha na John  Lukuwi

BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM.

August 28, 2014

 Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana.
 Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya.
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
 Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Phyllis Kandie  (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo  Wilbert Kaahwa.
Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika  Mashariki (EALA) wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge hilo Dkt. Margaret Zziwa (wa nne kutoka kulia waliokaa) na Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda, mara baada ya ufunguzi wa bunge hilo.

SERIKALI YASISITIZA KUHUSU MATUMIZI YA VYETI HALISI WAKATI WA UOMBAJI KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA

August 28, 2014


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mambo ya kuzingatia kabla ya kuomba kazi nchini kwa  waombaji waliopotelea na vyeti, kuibiwa vyeti au kubadilisha majina,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi hiyo Bw.Humphrey Mniachi.

Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Humphrey Mniachi akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani)Jinsi wanavyoshirikiana na Vyombo vingine serikalini katika Mchakato wa Ajira,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi Hiyo Bi. Riziki Abraham.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka  Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo
RAIS KIKWETE AZINDUA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA

RAIS KIKWETE AZINDUA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA

August 28, 2014
n6 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipata maelezo na kuangalia vifaa vya upimaji  eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka n3