VODACOM NA TFF ZATILIANA SAINI MKATABA WA KUIDHAMINI LIGI KUU TANZANIA BARA

VODACOM NA TFF ZATILIANA SAINI MKATABA WA KUIDHAMINI LIGI KUU TANZANIA BARA

August 12, 2015

Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa wakijiandaa kutiliana saini mikataba yao. Kulia anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo, Boniface Wambura.
Malinzi na Twissa wakibadilishana mikataba huku Wambura (katikati) akishuhudia.

Malinzi akisistiza jambo kwenye mkutano huo.
Twissa akijibu maswali ya wanahabari hawapo pichani.Mkutano ukiendelea.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom leo imetiliana saini na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF mkataba wa kuendelea kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kipindi kingine cha miaka mitatu. Kampuni hiyo imeendelea kuidhamini ligi hii baada ya kuidhamini kwa miaka minane mfululizo iliyopita.
Mkataba huo umetiwa saini kwenye mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Makao Makuu ya Vodacom yaliyopo Mlimani City Jijini Dar es Salaam. 
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)
Rais Kikwete Aongoza Kikao Cha Halmashauri Kuu MJINI Dodoma

Rais Kikwete Aongoza Kikao Cha Halmashauri Kuu MJINI Dodoma

August 12, 2015

 2
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakipiga makofi pamoja na wajumbe wengine muda mfupi baada ya kuingia katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma tayari kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM leo jioni.
(Picha na Freddy Maro)
1
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo.
3
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt.John Pombe Magufuli wakiteta muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo.

BENKI YA CRDB YAFANYA SEMINA KWA WATENDAJI WA HALMASHAURI ZA NYANDA ZA JUU KUSINI

August 12, 2015
Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa amgeni rasmi katika semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  akifungua rasmi semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini.

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Beki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kutoa hotuba yake wakati wa semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyoandaliwa na benki hiyo na kufanyika jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Beki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwaongoza wageni waalikwa kuimba wimbo maalumu wa Benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  CRDB Dk. Charles Kimei akifurahia jambo na Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) wakati wa semina ya Benki ya CRDB kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyofanyika jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Nyirembe Munasa.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika semina ya Benki ya CRDB kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyofanyika jijini Mbeya 
  Baadhi ya washiriki wa semina ya viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyofanyika jijini Mbeya wageni wakiimba wimbo maalumu wa Benki hiyo. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  CRDB Dk. Charles Kimei akifafanua jambo kwa Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika halfa ya Benki ya CRDB kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  
Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya washiriki wa semina iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyofanyika jijini Mbeya.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  CRDB Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  CRDB Dk. Charles Kimei akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa CRDB tawi la Mbalali, Chibby Chibby (katikati) na Meneja wa tawi la Mwanjelwa, Ephraim Lwilla.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkaribisha Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Nyirembe Munasa wakati wa semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyoandaliwa na benki hiyo na kufanyika jijini Mbeya. (Picha na Francis Dande)
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Nyirembe Munasa (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyoandaliwa na benki hiyo na kufanyika jijini Mbeya. Katikati ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mwanjelwa,  Ephraim Lwilla.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akibadilishana mawazo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Nyirembe Munasa (kulia) wakati wa semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyoandaliwa na benki hiyo na kufanyika jijini Mbeya. Katikati ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mwanjelwa,  Ephraim Lwilla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe katika semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyoandaliwa na benki hiyo.

TFF, VODACOM ZASAINI MKATABA MPYA

August 12, 2015

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limesaini mkataba mpya wa miaka mitatu (3) wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania bara (VPL) wenye thamani ya shilingi bilioni sita (tsh bilioni 6.6) na kampuni ya simu ya Vodacom, halfa hiyo imefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo eneo la Mlimani City jijini Dar es salaam.

Akiongea wakati wa kusaini mktaba huo mpya, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya simu ya Vodacom Kelvin Twissa, amesema kampuni yao inafurahia kuendelea kuwa sehemu ya udhamini ya ligi kuu nchini, mafanikio ya timu bora na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa inatokana na kuwa na ligi bora ambayo inadhaminiwa na Vodacom.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru kampuni ya Vodacom kwa kukubali kuendelea kuidhamini ligi kuu kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3) na kuongeza sehemuya udhamini wao kwa asilimia 40%.

Tunaishukuru kampuni ya Vodacom kwa kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya mpira wa miguu nchini, udhamini wanaotupatia unavisaidia vilabu kujiandaa na kujiendesha na mikikimikiki ya ligi na kuifanya ligi kuwa na ushindani wa hali ya juu, msimu huu ligi itakua na timu 16 tunatarajia kuendelea kushuhudia uhondo huo chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Mkataba huo mpya wa udhamini kwa kipindi cha miaka mitatu, umeboreshwa na kuwa na ongezeko la asilimia 40% kutoka katika mkataba wa awali uliomalizika.

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.

TFF YAMPONGEZA JAJI MAMBI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Adam Mambi kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini.

Katika Salam zake kwa Jaji Mambi, Malinzi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Kikwete kwa kumteua mwanafamilia huyo wa mpira wa miguu nchini kushika wadhifa huo.

TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na watanzania wote inamtakia kila la kheri Jaji Adam Mambi katika majukumu yake mapya ya Ujaji katika Mahakama Kuu nchini Tanzania.

TRA KUENDESHA SEMINA YA KODI
Mamlaka ya Kodi na Mapato nchini (TRA) inatarajiwa kuendesha semina ya kodi kwa viongozi wa vilabu viliyopo jijini Dar es salaam, siku ya ijumaa tarehe 14 Agosti katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu.

TRA itaendesha semina hiyo kwa vilabu vilivyopo ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili ambapo viongozi wakuu wa vilabu hivyo, Katibu Mkuu, Mwenyekiti, na Mhasibu wanapaswa kuhudhuria semina hiyo.

Kwa kuanzia TRA itaendesha semina hiyo jijini Dar es salaa, na baadae kuendelea na semina hizo kwa vilabu vilivyopo mikoani kwa lengo la viongozi wa vilabu kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa wachezaji, makocha wanaowaajiri katika vilabu vyao.

Semina hiyo itaanza saa 3 asubuhi mpaka saa 5 kamili asubuhi katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu jijini Dar es salaam, vionggozi wa vilabu vya ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili waliopo jijini Dar es salaam mnaombwa kuhudhuria semina hiyo.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

-
Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania 

WATU WA CHINA WAZINDUA KAMPENI YA KUWALINDA WANYAMA DHIDI YA UJANGILI

August 12, 2015

Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya kupambana na ujangili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo imeanzishwa na watu wa China kwa ajili ya kuunga jitihada za watanzania katika mapambano hayo ya kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili hasa tembo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kinondoni, Faudhia Eddy katika uzinduzi huo. Balozi huyo alitoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira, Mwalimu Flora Lukali kutoka Shule ya Mount Pleasant kwa ajili ya shule hiyo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing akionyesha umahiri wa kuchezea mpira katika uzinduzi huo kabla ya kutoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
Wanafunzi wakiwa na vipeperushi vya bendera ya nchi ya china wakati wa uzinduzi huo.
Wasanii wa kundi la makhirikhiri wakitoa burudani katika 
uzinduzi huo.
Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wimbo wa taifa ukiimbwa.
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
Wanafunzi ndani ya uzinduzi huo. 
Siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani yaadhimishwa kwa shamrashamra nchini

Siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani yaadhimishwa kwa shamrashamra nchini

August 12, 2015


vi1
Baadhi ya vijana kutoka shule mbalimbali wakiandamana kuingia katika viwanja vya mnazi mmoja wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa leo jijini Dar es Salaam na kuhusisha mashirika mbalimbali ya mataifa yanayofanya shughuli za vijana yakiwemo UNFPA, IYF, UNIC, ILO, RESTLESS DEVELOPMENT, YUNA, AMREF, MARIE STOPES, pamoja na PSI.
vi2
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kulia) akipokea maandamano ya vijana (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi na wapili kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
vi3
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem akizungumza na vijana wakati wa Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
vi4
Kijana ambaye ni mwanachama wa asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) Bw. Hesein Melele akiwasilisha maazimio yaliyofikiwa na vijana wakati wa kongamano lililofanyika Agosti 10 mwaka huu kujadili ujumbe wa siku ya kimataifa ya vijana duniani na kuandaa maazimio yaliyowasilishwa kwa mgeni rasmi leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
vi5
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na vijana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara hiyo Prof. Hermas Mwansoko
vi6
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiwahutubia vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
vi7
Baadhi ya vijana wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
vi8
Vijana kutoka vikundi mbalimbali wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
vi9
Vijana kutoka vikundi mbalimbali wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
vi10
Vijana kutoka vikundi mbalimbali wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
vi11
Vijana kutoka vikundi mbalimbali wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
vi12
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Vijana Bi. Amina Sanga (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani yaliyoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo