WADAU WA NGUVU WATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA UONGOZI WA BIASHARA CHUO KIKUU CHA ESAMI ARUSHA

November 27, 2017

Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) ,Florian Mutabazi akipokea Cheti chake kutoka kwa Waziri wa Elimu wa Malawi,Bright Msaka baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA) Chuo Kikuu cha  Eastern and Southern African Management Institute(ESAMI) kilichopo jijini Arusha katika  mahafali yaliyofanyika chuoni hapo,wahitimu wametoka nchi 32 barani Afrika.Picha na Filbert Rweyemamu
Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Florian Mutabazi akiwa mwenye furaha baada ya baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA)
Mdau wa blog za kijamii ,Yotham Ndembeka ambaye ni mtumishi katika Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha akipongezwa na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha  Eastern and Southern African Management Institute(ESAMI)kilichopo jijini Arusha,Profesa Bonard Mwape baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA).
Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Florian Mutabazi(kushoto) akifurahia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Utawala na Fedha,Jesca Eriyo.
RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA JAJI MKUU WA TANZANIA ALIPOFIKA KUJITAMBULISHA LEO IKULU

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA JAJI MKUU WA TANZANIA ALIPOFIKA KUJITAMBULISHA LEO IKULU

November 27, 2017
C7lMmgLVUAA2uLA
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Kijarida cha Mahakama Kuu Tanzania na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Profesa Ibrahim Hamis Juma alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo 27-11-2017
DSC_5158
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Profesa Ibrahim Hamis  Juma alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo 27-11-2017.
DSC_5184
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa amefuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Profesa Ibrahim Hamis Juma, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha leo. 27-11-2017.9 Picha na Ikulu

HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGA PESA KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU

November 27, 2017



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina katika picha akiongea na wataalam wanahabari na viongozi wa Wizara hiyo kutoka katika sekta ya Uvuvi, baada ya kuonyeshwa zana zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu, katika kanda ya Dar es Salaam.
Katika picha baadhi ya zana zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi  haramu katika kanda ya Dar es Salaam.
Kushoto Bw. Obadia Mbogo, Afisa katika sekta ya uvuvi aliyeshiriki katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu, akimuonyesha Waziri Mpina na ujumbe wake aina ya baadhi ya vilipuzi vilivyokamatwa katika zoezi hilo katika kanda ya Dar Es Salaam.
NA MWANDISHI MAALUM

Akiwa katika zoezi la kupongeza kikosi maalum kilichoanza oparesheni ya kupambana na uvuvi haramau katika bahari ya hindi leo, zoezi lililokwenda sambamba na kuonyeshwa vifaa vinavyotumika katika uvuvi haramu vilivyokamatwa katika zoezi hilo lilioanza mwezi Julai mwaka huu, Waziri wa  mifugo na Uvuvi Mhe. Luahaga Mpana amezitaka halmashauri ambazo shughuli  za uvuvi zinafanyika kutenga fedha ili kuweza kupambana na uvuvi haramu.

Mpina ambaye ameshangazwa na kitendo cha Halmashauri hizo kukusanya fedha za ushuru zitokanazo na shughuli na uvuvi na kujisahau kabisa kuingia katika zoezia la kupambana na uvuvi haramu kwa kutenga fedha hususan za kufanya doria.

Aidha, Mpina Amewataka viongozi wakuu wa Wizara yake, Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba na Kaimu Mkurugenzi wa maeneleo ya  Uvuvi Bw.  Magese Bulayi kutembea na barua rasmi katika ziara zao za kikazi kwenye halmashauri husika  zilizokuwa tayari kuwawajibisha watumishi wazembe katika zoezi zima la kupambana na uvuvi haramu.

“Mkurugenzi wa maendeleo ya uvuvi na katibu Mkuu,nawaagiza mtembee na barua zilizotayari kusimamisha au kufukuza kazi watumishi wazembe katika halmashauri, barua hizo zibaki wazi katika sehemu ya kujaza majina yao tuu, na ndani ya mwaka mmoja nataka tukomeshe kabisa uvuvi haramu. “ Alisisitiza Mpina.

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

November 27, 2017

NENO LA DK. MWAKYEMBE LIGI YA WANAWAKE, AFANYA ZIARA ARUSHA

Hafla ya uzinduzi wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake imezinduliwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kwenye Uwanja wa General Tyre jijini Arusha.

Timu zilizokata utepe zilikuwa ni Alliance Queens ya Mwanza iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Panama FC ya Iringa.

Katika uzinduzi huo Waziri Dk. Mwakyembe aliwataka wachezaji wa timu zote kujituma kwa juhudi zaidi kwa kuwa mpira wa miguu kwa sasa ni ajira kubwa sana kwa vijana.

“Vijana wangu natambua mnapenda mpiwa wa miguu, naomba mzingatie vitu vitatu muhimu - nidhamu, juhudi na kujitunza,” amesema Waziri Dk. Mwakyembe akiwa na Rais wa TFF Wallace Karia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred na viongozi wa FA Mkoa wa Arusha.

Mara baada ya kufanya uzinduzi huo, Waziri akiwa na viongozi hao leo ametembelea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutazama maendeleo ya marekebisho yanayofanyika kwenye Uwanja huo.

Mbali na uwanja  huo pia waziri alifanya ziara fupi kwenye viwanja wmbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanja cha FFU kwa Morombo, Arusha  ambapo aliwapongeza kwa ukarabati mzuri wa nyasi za kuchezea.

Katika ziara nyingine Waziri pamoja na Viongozi wa TFF walitembelea shule ya Trust St. Patric Sports Academy ambacho ni kutuo cha kukuza michezo na timu zinazoshiriki ligi hiyo, zimeweka kambi.

WAAMUZI 18 TANZANIA WATAPA BEJI FIFA 2017/18

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA), limetoa beji kwa Waamuzi 18 katika msimu wa mshindano mwaka 2018.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, Waamuzi walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni Mfaume Ali, Elly Sasii, Emmanuel Mwandembwa na mkongwe Israel Nkongo na kwa upande wa wanawake wamo Jonesia Rukyaa na Florentina Zablon.

Waamuzi Wasaidizi walipewa beji hizo (Wanaume) ni Soud Lillah, Mgaza Kunduli, Mohammed Mkono, Mbaraka Haule, Ferdinand Frank Chacha na Frank Komba na kwa wanawake Hellen Mduma, Dalila Jaffari, Jeneth Balama na Grace Wamala.

Waamuzi wa mpira wa miguu unaochezwa ufukweni waliopata beji ni  Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.

JAPAN YAONESHA NIA KUIJENGA DODOMA KWA MIUNDOMBINU YA KISASA

November 27, 2017
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato walipokutana kwa mazungumzo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan –JICA nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase, alioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Bw. Hiroshi Kato (katikati) walipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na  Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa pili kulia) wakijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu, nishati, kilimo na maji, walipokutana Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato akizungumza kuhusu kuwepo kwa ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Japan katika suala la Maendeleo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe walioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato wakifuatiia kwa makini majadiliano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa JICA Bw. Hiroshi Kato, Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Hiroshi Kato (hayupo pichani) katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Elijah Mwandumbya akizungumzia mabadiliko ya Sheria ya Kodi yaliyofanywa hivi karibuni ambayo yanalenga kutoa misamaha ya kodi yenye tija kwa umma wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na  Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Kamishina Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akielezea kuhusu masuala ya kodi katika maendeleo ya Taifa katika mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na  Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), wa nne kushoto na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali ya Japan, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

SHIRIKA la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) limesema liko tayari kushirikiana na Serikali kujenga miundombinu ya kisasa ya usafiri, Nishati ya umeme, maji na usafi wa mazingira katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Bw. Hiroshi Kato wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Jijini Dar es Salaam.

Bw. Kato alisema kuwa mradi mwingine wanaotaka kuutekeleza katika mji wa Dodoma ni udhibiti wa taka ngumu na kwamba wanachosubiri ni Serikali kuainisha maeneo ya vipaumbele vilivyoko katika mpango mji wa Dodoma.

Aidha Makamu huyo wa Rais wa JICA alisema kuwa Shirika lake litaendelea kusaidia eneo la kilimo hususan kilimo cha mpunga ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuwakomboa wakulima.

SHAMBA LINAUZWA LIPO MKURANGA MKOANI PWANI

November 27, 2017

Mmiliki wa shamba hilo, akiwa amekanyaga bicon za mipaka ya shamba hilo.

Mmiliki wa shamba hilo akionesha bicon zilizopo katika shamba hilo.

SHAMBA LINAUZWA LIPO WILAYANI MKURANGA MKOANI PWANI KIJIJI CHA KIBUYUNI LIPO JIRANI KABISA NA SHULE YA SEKONDARY YA PANZUO. NAULI YA KWENDA KATIKA SHAMBA HILO KWA DALADALA NI SHILINGI, 3,000.

UMBALI KUTOKA KARIAKOO KWENDA KATIKA SHAMBA HILO NI KILOMITA 60 NA BEI KWA KILA HEKARI NI SH.2,999,999 KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA HIZO HAPO ZA ZAIN NAMBA 0687347676

CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461

November 27, 2017

Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi ya Mbeya Desemba 8 na Chuo cha Kampasi ya Dar es Salaam Desemba 22. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya mahafali hayo, Dk. Mrisho Malipula na katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Mrisho Malipula, akitoa ufafanuzi juu ya mahafali hayo.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, akitoa ufafanuzi juu ya mkutano wa Baraza la Masajili ‘Convocation’ utakaofanyika Novemba 29, 2017 Kampasi Kuu Morogoro.


Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.
 Morogoro, Tanzania-Novemba 27

MAHAFALI ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe yanatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 30, 2017, jumla ya wahitimu 3,461 katika mwaka wa masomo 2016/2017 wanatarajiwa kutunukiwa shahada, stashahada na astashahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas samatta, kati ya wahitimu hao
ni
*Shahada ya Uzamivu (PhD) ni 4 (0.12%)
*Shahada za Umahiri (Masters) ni 1,005 (29.04%)
*Shahada za Kwanza (Bachelors) ni 2,063 (59.61%)
*Stashahada (Diploma) ni 191 (5.52%)
*Astashahada (Certificate) ni 198 (5.72%).
Kati ya wahitimu wote waliohitimu Kampasi Kuu ni 2,119 (61.23%).
Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe Mbeya ni 734 (21.21) na Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe Dae es Salaam ni 608 (17.57%).
Mahafali hayo yanatarajiwa kufanyika Kampasi Kuu Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi Mbeya Desemba 8 2017 na Chuo cha Kampasi Dar es Salaam Desemba 22 2017.
Mahafali hayo yatatanguliwa na mkutano wa 17 wa baraza la Masajili Çonvocation’ utakaofanyika Novemba 29 2017 katika ukumbi wa mihadhara wa Fanon, uliopo kampasi Kuu. Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe kuanzia mwaka 2002 na wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Maendeleo (IDM) wanakaribishwa kuhudhuria mkutano huo.
Mjadala mahususi na nafasi ya wahitimu na wanachuo katika kuchangia maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe utafanyika.
Aidha Baraza la Masajili linaendelea kuwahamasisha wahitimu wote wa Chuo Kikuu Mzumbe na wadau wengine kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa hosteli ya wanachuo wa kike kupitia ‘Çonvocation Fundraising Account’namba 01o150209448900 iliyopo Benki ya CRDB, Tawi la Mzumbe.

WANAWAKE TANGA WAVUTIWA NA AMANA BANKI

November 27, 2017
Wanawake wanaojishughulisha na shughuli za ujasiliamali Mkoani Tanga wamesema wamevutiwa na programu ya ukopeshaji  wa vitendea kazi badala ya fedha taslimu unaoendeshwa na benki ya Amana na kudai unaweza kusaidia kuendesha miradi endelevu.

Walitoa maelezo hayo  wakati wa kongamano la jukwaa la wanawake wa Mkoa wa Tanga lililofanyika jijini hapa kwa lengo la kujadili mikakati ya kujiendeleza kiuchumi.

Wakizungumza baada ya mkuu wa idara ya miradi ya bidhaa na usimamizi wa mambo ya sheria wa benki ya Amana,Muhsin Mohamed (Pichani Juu) kuelezea kuwa benki hiyo inatoa mikopo ya vitendea kazi na uwezeshaji wa kuendesha miradi badala yafedha,wanawake hao walisema programu hiyo itaweza
kuwaendeleza kiuchumi.

“Sisi wanawake tunajijua wenyewe,ukinikopesha fedha taslimu nitaingia tama ya kwenda kupeleka kwenye vikoba badala ya kufanyia mradi niliokopea,ndiyo maana wengi wetu tunaishi kwa madeni na kunyang’anywa samani za nyumbani”alisema  Sophia Juma mkazi wa Chuda Jijini hapa.

Walisema kama benki hiyo itaweka mikakati mahsusi kwa ajili ya
wajasiliamali wanawake,wanaamini kuwa itawasaidia kuendesha miradi ya maendeleo bila vikwazo.

Akizungumza katika jukwa hilo,Muhsin alisema benki hiyo inayofuata misingi isiyokubali utoaji wa riba na kwamba inakopesha wafanyabiashara wakubwa wa ngazi ya kati,wadogo na hata vikundi.

“Ukiomba mkopo kwetu tutahitaji mpango wa mradi unaotaka
kuendesha,ukishakidhi vigezo  kama wewe ni uanataka kufuga kuku tunakununulia vifaranga,vyakula na kuliweka banda lako katika mazingira rafiki ya kiufugaji”alisema Muhsin.

Mwenyekiti wa jukwaa hilo,Mariam Shamte aliitaka benki hiyo
itakapofungua tawi lake jijini Tanga kutenga dirisha maalumu la
kuwahudumia wajasiliamali wanawake ambalo litakuwa na jukumu pia la kuwapa elimu ya namna ya kuendesha miradi mbalimbali.

MDAU EXAUD MTEI WA HABARI24 BLOG APATA NONDO YA ELIMU YA JUU

November 27, 2017
Mkurugenzi Mkuu wa Habari 24 Bw. Exaud Mtei akiwa katika pozi, mapema jana katika maafari yaliyofanyika Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama jijini Dar es salaamii.


Chuo cha ustawi wa jamii siku ya juzi kimefanya maafali yake ya 41 toka kuanzishwa kwake, na wameweza kuhitimu wanafunzi zaidi ya 300 kwa siku hiyo na mmoja wapo akiwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Habari 24 Media bw. Exaud Mtei.

Wahitimu wakisikiliza kwa umakini hotuba mgeni rasmi.
Muhitimu wa Shahada ya Ustawi wa Jamii Bw. Exaud Mtei akisherehekea siku ya maafari pamoja na wadau  kutoka media rafiki na Habari 24, kama East Afrika tv na Full Habari Media.
Mkurugenzi Mkuu wa Habari 24 Media Exaud Mtei akipewa hongera na Mkurugenzi mtendaji wa Full Habari Ndugu. Selemani Magari mapema jana jijini Dar es salaam

WAKAAZI WA ARUSHA WATAMBULISHWA BIDHAA BORA ZA UMEME WA JUA (SOLA)

November 27, 2017
Mkazi wa Arusha Mzava Nsanjiwa akitazama jiko linalotumia nishati ya jua katika banda la Kampuni ya Sola ya Sunking katika maonyesho yaliyofanyika kwa ajili ya kuhamasisha wakaazi wa Arusha kutumia bidhaa za sola zilizo bora, katika viwanja vya stendi ya Kilombero jijini Arusha.
Mkazi wa Jiji la Arusha Yohana (watatu kulia) akitazama bidhaa mbalimbali za majumbani zinazotumia nishati ya jua katika mabanda ya kampuni ya solar ya Sunking ,katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya stendi ya Kilombero jijini Arusha.

Mkazi wa Jiji la Arusha Yohana (watatu kulia) akitazama bidhaa mbalimbali za majumbani zinazotumia nishati ya jua katika mabanda ya kampuni ya solar Sister ,katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya stendi ya Kilombero jijini Arusha.
Mkazi wa Arusha Bi.Dora Mkini akitazama jiko linalotumia nishati ya jua kutoka katika kampuni ya Sunking katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya stendi ya Kilombero jijini Arusha.
HATIMILIKI ZA ARDHI KUTOLEWA NDANI YA WIKI MOJA

HATIMILIKI ZA ARDHI KUTOLEWA NDANI YA WIKI MOJA

November 27, 2017
LK0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akionyesha hati mbele ya Waandishi wa Habari alipokuwa akikagua maendeleo ya Mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi(ILMIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo Bw. Shaban Pazi. Mradi huo utakapo kamilika unaondoa matumizi ya karatasi katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala yake zitakuwa zianhifadhiwa katika Kompyuta.
LK1
Afisa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Irene Sarwat akimuelezea jambo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) alipokuwa akikagua maendeleo ya Mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi(ILMIS) leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo utakapo kamilika unaondoa matumizi ya karatasi katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala yake zitakuwa zianhifadhiwa katika Kompyuta.
LK2
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) akisikiliza maelezo toka kwa mmoja wa wafanyakazi katika cha Mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi(ILMIS) alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo utakapo kamilika unaondoa matumizi ya karatasi katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala yake zitakuwa zianhifadhiwa katika Kompyuta.
LK3A
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu urejeshaji wa ramani unavyofanyika toka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi inayoratibu uhimarishaji Mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi(ILMIS)  alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo utakapo kamilika unaondoa matumizi ya karatasi katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala yake zitakuwa zianhifadhiwa katika Kompyuta.
LK4
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (katikati) akionyesha faili lenye taarifa za Ardhi ya Kiwanja Kimoja mbele ya Waandishi wa Habari alipokuwa akikagua maendeleo ya Mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi(ILMIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mipango Miji wa wizara hiyo Bi. Irene Sarwat. Mradi huo utakapo kamilika unaondoa matumizi ya karatasi katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala yake zitakuwa zianhifadhiwa katika Kompyuta.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
……………
Jonas Kamaleki- MAELEZO
Serikali itaanza kutoa hatimiliki za viwanja kati ya siku moja na siku saba kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ifikapo Juni 1, 2018.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi.
“Tunataka kupunguza urasimu na kuongeza ufanisi katika kutoa hati kutoka ilivyo sasa ambapo hati hutolewa kati ya mwezi mmoja hadi miezi mitatu”, alisema Lukuvi.
Ameongeza kuwa mfumo huo utaondoa udanganyifu katika kutoa hati kwa watu wawili au zaidi katika kiwanja kimoja na kuondoa migogoro ya viwanja ambayo imekuwa kero kwa wananchi.
Lukuvi amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuondoa utapeli uliokuwa ukifanyika kuhusu ardhi na ndio maana imeanzisha mfumo huo ambao ameuita muarobaini wa migogoro ya ardhi.
Aidha, Waziri Lukuvi alisema kuwa hati ya kisasa itakuwa na ukurasa mmoja badala ya zamani ambayo ilikuwa na kurasa zaidi ya ishirini.
Kwa mfumo huo, maafisa ardhi hawatatumia tena karatasi bali watakuwa na kompyuta ambamo taarifa zote zitahifadhiwa, aliongeza Lukuvi.
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZINAZOHUSU SEKTA YA FEDHA NA BIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZINAZOHUSU SEKTA YA FEDHA NA BIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM

November 27, 2017
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo afungua kikao cha kujadili changamoto za Muungano zinazohusu sekta ya fedha na biashara katika ukumbi wa ofisi ya Makamu wa Rais ,Luthuli jijini Dar es Salaam.
Pix 00
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akielezea masuala mbali mbali ambayo yamejadiliwa na Mawaziri wa Tanzania Bara pamoja Visiwani.
Pix 01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akiongoza kikao cha  Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed aboud Mohamed na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
Pix 02
Baadhi ya Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mbali mbali zinazohusu Muungano zinajadiliwa.
Pix 03
Baadhi ya Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mabli mbali zinazohusu Muungano zinajadiliwa.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

ACACIA BULYANHULU WAKABIDHI MAKTABA WENYE THAMANI YA MILIONI 23 WILAYA YA NYANG’HWALE

November 27, 2017
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict
Busunzu akipatiwa maelezo na mkurugenzi wa Read International ,Bi Magdalena George wakati walipokuwa wakitembelea maktaba ya jamii ambayo hipo wilayani
Nyang’hwale ,katika kati ni katibu tawala wa Wilaya hiyo Fabian Sospeter.
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict
Busunzu akikata utepe na katibu tawala wa Wilaya ya
Nyang’hwale Bw,Fabian Sospeter wakati wa zoezi la kukabidhi maktaba hiyo.
Sehemu ya vitabu ndani ya maktaba ya jamii wilayani Humo.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA MELI YA HOSPITALI YA CHINA, AAGANA NA KUSHUKURU WANAMAJI NA MADATARI WALIOKUJA NAYO

November 27, 2017
c1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la wanamaji wa Meli ya Hospitali ya China alipotembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017 kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
c2 c3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la wanamaji wa Meli ya Hospitali ya China alipotembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017 kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
c4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali na Kiongozi Mkuu wa Meli ya Hospitali ya China Kamanda Guan Bailin   alipoitembele aleo Jumapili Novemba 26, 2017  kuwashukuru na kuwaaga wanamaji na madaktari waliokuja nayo baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
c5 c6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali na Kiongozi Mkuu wa Meli ya Hospitali ya China Kamanda Guan Bailin   alipoitembele aleo Jumapili Novemba 26, 2017  kuwashukuru na kuwaaga wanamaji na madaktari waliokuja nayo baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
c7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali na Kiongozi Mkuu wa Meli ya Hospitali ya China Kamanda Guan Bailin   alipoitembele aleo Jumapili Novemba 26, 2017  kuwashukuru na kuwaaga wanamaji na madaktari waliokuja nayo baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
c8 c9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akioneshwa video inayoonesha shughuli za Meli ya Hospitali ya China alipoitembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017  kuwashukuru na kuwaaga wanamaji na madaktari waliokuja nayo baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.