MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA SONGWE AWATOLEA UVIVU MADIWANI, MBUNGE

March 14, 2017
Elias Nawera.
Na Brandy Nelson

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe mkoani  hapa,Elias Nawera ambaye ameingia mgogoro na madiwani wake, ameibuka na kutoa msimamo wake kwamba atafanya kazi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni  za utumishi wa umma na si kwa matakwa  ya wanasiasa.

Hivi karibuni  Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Songwe, Phillipo Mulugo  walidai kutoridhishwa na hawana imani na utendaji kazi wa mkurugenzi huyo kwenye kikao chao kilichoitishwa kwa dharula kwa lengo la kumjadili na kumuazimia kumfuka kazi.

Akizungumza juzi , Nawera alisema kuwa amepelekwa kwenye halmashauri hiyo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi  na siyo kumtumikia mtu mmoja mmoja kwani kufanya hivyo ni kukiuka  misingi ya utawala bora.

"Unajua baraza la madiwani ni wawakilishi wa wananchi na ni siasa, na siasa mara nyingi  ilivyo ni nani kapata nini wakati gani vipi, kimsingi ndiyo siasa, wilaya yetu ni mpya  na kuna watu wanataka kufanya kazi kwa namna  walivyokuwa wamezoea kufanya mambo yao, kitu ambacho siwezi kukubaliana nacho hata siku moja,"alisema. 

Alisema tangu  alipofika katika halmashauri hiyo Septemba mwaka jana, alikuta mazoea ya watu kama wana ufalme  kana  kwamba  Serikali haipo, hivyo yupo Songwe kufanya kazi kimfumo wa kiserikali na  siyo kumtumikia mtu mmoja mmoja ambapo  jambo hilo  limekuwa likikwaza watu.

"Mfano  kwenye  kikao cha halmashauri nililazimishwa kumpa mtu kazi kwa jina,kufanya biashara na mtumishi wa halmashauri ,nikiuke sheria ya manunuzi  kwa kusema sheria nini,vitu ambavyo sikubaliani navyo kwani kufanya hivyo nikukiuka sheria,taratibu na misingi ya utawala bora ".alisema 

Mkurugenzi  huyo alisema amekuwa akienda  vijijini kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za wananchi lakini amekuwa akizuiwa kufanya hivyo na kuambiwa abaki ofisini.

"Nimewahi kukatazwa nisiende  vijijini,mimi ninajua rais amenileta huku nitumikie watu na  Ilani yenyewe  ya chama cha mapinduzi inasema lazima  twende chini  tufanye kazi  na watu, kwa hiyo ukiniambia kitu tofauti na hicho miongozo, sheria kanuni  na  taratibu mimi sitokusikiliza kwa sababu nitataka kutumikia  wananchi na kumsikiliza yule aliyenileta.'alisema  

Alisema  hata Mkuu wa Mkoa wa Songwe,   Chiku Galawa mara nyingi amekuwa akiwaagiza watendaji kutoka ofisini na kwenda vijijini kwa wananchi, kwani pia kuna watumishi ambao wapo huko na wanahitaji huduma lakini hawana uwezo wa kufika wilayani hivyo hutumia fursa hiyo kuwasikiliza mahitaji yao.

POLISI KILIMANJARO YANASA SILAHA,DAWA ZA KULEVYA NA VIROBA VILIVYOPIGWA MARUFUKU

March 14, 2017
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandaizi wa Jeshi la Polisi ,Wilbroad Mutafngwa akionyesha silaha zilizomakamatwa pamoja na Dawa za Kulevya aina ya Mirungi na Bhangi.
Misokoto ya Bhangi iliyokamatwa.
Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa.
Silaha aina ya Bastola zilizokamatwa na jeshi hilo.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Kamanda wa Polisi,(hayupo pichani.)

NITAHAKIKISHA SHULE ZOTE ZA MAFINGA MJINI ZINAKUWA KATIKA UBORA UNAOTAKIWA: COSATO CHUMI

March 14, 2017


 MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi madawti kwa viongozi wa kata ya sao hill kwa ajili ya matumizi ya shule
 MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipongezwa na viongozi wa kata ya sao hill kwa jitihada wanazozifanya kuleta maendeleo katika jimbo la mafinga mjini
 
 Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo,mifungo 10 ya saruji,madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo

Na Fredy Mgunda,Mafinga.

MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ameendelea kutatua changamoto mbalimbali za jimbo hilo kwa kufanya ziara kwenye baadhi ya shuleza msingi zilizopo katika mjini wa mafinga na kukagua baadhi ya miundombinu inayoendelea kukarabatiwa kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Katika ziara hiyo Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo,mifungo 10 ya saruji,madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo ambayo yalitolewa na wakala wa shamba la miti Sao Hill huku chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mafinga Mji kupitia mwenyekiti wake  Yohanes Cosmas wakichangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za mbunge za kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo.

Katika hatua nyingine mbunge huyo alitembelea jengo jipya la ukumbi wa kisasa lililojengwa na kikundi cha Agape group ambalo lipo kwenye kata ya Kinyanambo kwa lengo la kuinua kipato cha halmashauri hiyo.

Baada ya mbunge kuona jitihada hizo alichangia 300,000 huku chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ikichangia 100,000 kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo.  

Shule ya Msingi Ifungo iliyopo wilayani Mafinga inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ikiwamo Umeme,maji ya bomba, madawati na nyumba za walimu jambo ambalo limedaiwa kuwa kukosekana kwa umeme limesababisha wanafunzi kushindwakufaulu vizuri.

 Kilio hicho kimetolewa mwishoni mwa wiki na walimu mkuu wa shule hiyo Tedy Captein wakati akizungumza mbele ya mbunge wa jimbo hilo Cosato Chumi (CCM) wakati mbunge huyo akiwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya jimbo hilo.

Mwalimu Captein alisema baada ya rais John Magufuli kutoa elimu bure wanafunzi wameongezeka na hivyo wanahitaji maji safi ya bomba badala ya kuelendela kutumia  maji ya tanki ambayo sio rafiki sana kwa wanafunzi hao.

Hata hivyo kutokana na ongezeko la wanafunzi wananchi wameamua kutumia nguvu kazi yao kwa kujenga jengo la darasa moja pamoja na ofisi ya mwalimu kwa gharama y ash.Mil. sita hadi kufikia kwenye lenta lakini walishindwa kumalizia.

Akijibu kilio cha shule hiyo kuhusu umeme mbunge Chumi alianza kwa kusema “Tutazungumza na shirika la umeme tanesco ili waweze kutuletea umeme ambao utasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa shule hii.”alisema Chumi.

MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA AWALI YA UTEKELEZAJI WA UAMUZI WA KUHAMIA DODOMA

March 14, 2017


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma uhakikishe unaondoa vitendo vya ukiritimba kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambavyo vinaweza kusababisha ucheleweshaji au kukwamisha ujenzi wa miji mipya mikubwa mitano ya kisasa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 14-Mar-2017 wakati akifanya mazungumzo na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kupokea taarifa ya Kikosi Kazi kilichoundwa na serikali kwa ajili ya kuratibu shughuli mbalimbali za Serikali kuhamia Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma kujiimarisha na kujipanga ipasavyo katika kupokea wawekezaji wenye nia njema ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani humo hasa wakati huu ambao serikali inahamia Dodoma.

Ameonya kuwa wawekezaji matapeli kamwe wasipewe nafasi ya kuwekeza Dodoma na ametaka uongozi wa mkoa wa Dodoma kuwa makini makundi hayo ili wasije kuvuruga mipango ya serikali ya kujenga Makao makuu ya kisasa katika Manispaa ya Dodoma.

Makamu wa Rais pia ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma kulinda na kuendeleza maeneo yote yenye uoto wa asili ili yasije yakaharibiwa kutokana na uwekezaji utakaofanyika mkoani humo.

Amesema amefurahishwa na kasi ya uongozi wa mkoa wa Dodoma jinsi unavyojipanga katika kuhakikisha azma ya serikali ya kuhamia Dodoma inafanikiwa kwa haraka ikiwemo utengaji wa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na huduma za kijamii.

Kuhusu maeneo ya wafanyabiashara wadogo, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa mkoa wa Dodoma wahakikishe wanatenga haraka maeneo maaluma kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo ili nao waweza kunufaika na mpango wa Serikali kuhamia mkoani Dodoma.

“Ni muhimu maeneo yote yatakayotengwa kwa ajili wafanyabiashara wadogo yawe huduma zote za msingi ili kusaidia wafanyabiashara hao waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi “Amesisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa ni muhimu kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma kuwashirikisha viongozi wa wafanyabishara wadogo kuhusu maeneo yatakayotengwa ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabishara hao kupewa maeneo yasiyofaa wa ajili ya shughuli zao.

Awali kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kuzungumza na viongozi wa mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Dodoma Jordan Rugimbana alimweleza Makamu wa Rais mipango na mikakati ya mkoa huo kuhusu azma ya serikali ya kuhamia Dodoma ikiwemo uimarisha wa huduma za msingi ikiwemo afya, miundombinu, maji na elimu.

Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana amesema mpaka sasa kazi ya kuainisha maeneo mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji, makazi na mahali ambapo ofisi za serikali na za mabalozi zitajengwa umeshakamilika.

Amesema uongozi wa mkoa wa Dodoma utaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali, mashirika ya kimataifa na mabalozi ili kuhakikisha maeneo yaliyotengwa yanaendelezwa haraka.

Ameeleza kuwa ujenzi wa miji Mitano mikubwa mkoani Dodoma na ujio wa wawekezaji mbalimbali utaufanya mkoa huo kuwa na uhitaji nishati ya umeme ya uhakika hivyo amehimiza ujenzi wa bomba la gesi asili kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ukafanyika haraka.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dodoma 14-Mar-2017
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Wadau wa mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa kazi ambapo Taarifa ya Awali ya mkoa wa Dodoma na utekelezaji wa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma iliwasilishwa katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
ZXCCC

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI ATAHADHARISHA WANANCHI UPATIKANAJI WA MAFUTA ISIWE SABABU YA KUBWETEKA

March 14, 2017


Msimamizi wa Kampuni itakayofanya Utafiti waUtafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Bell Geospace  Inteprises Limited Bwana Stephane Kunar kushoto akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi Kulia nanma ndege Maalum itakavyofanya utafiti huo katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar. Kati kati ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira  mhg. Salama Aboud Talib, wa nyuma yake ni Katibu Mkuu wake Nd. Ali Khalil Mirza na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mhmoud.

  Balozi Seif akiangalia baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyochunguza maeneo yenye daliliza uwepo wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
 Balozi Seif  akijaribu kugusa vifaa vitakavyotumika katika kazi kufanya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia sehemu zenye dalili ya uwepo wa Mafuta na Gesi Visiwani Zanzibar.
 Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
 Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametahadharisha Wananchi kwamba itakapofikia hatua ya kupatikana kwa rasilmali ya Mafuta na Gesi Asilia Visiwani Zanzibar isijekuwa chanzo cha sababu ya Wananchi kubweteka na mradi huo kwa kuacha shughuli zao za Kiuchumi ambazo huwapatia riziki zao za kila siku.

Alisema Rasilmali hiyo endapo itapatikana kufuatia utafiti unaoanza kufanywa hivi sasa itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto nyingi zinazoikabili Serikali Kuu pamoja na Wananchi kwa ujumla.Balozi Seif Ali Iddi alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa Ndege itakayofanya Utafiti na hatimae uchimbaji wa Rasilmali ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume nje kidogo ya Kusini ya Mji wa Zanzibar.

Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yakiwemo yale ya Bara la Afrika yaliyoanza kuzalisha miradi hiyo kwa matumaini makubwa ya kuimarisha Uchumi wao lakini hivi sasa zimekuwa na changamoto zaidi za Kiuchumi hali ambayo Zanzibar na Wananchi wake wanapaswa kuwa makini na
kujifunza matukio hayo.

Hata hivyo Balozi Seif alisema safari ya Zanzibar kuelekea kwenye uchumi Mkuu imeanza mara baada ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitisha Mswaada wa kuanzisha sheria inayoiruhusu Zanzibar kutafuta na kuchimba mafuta yake yenyewe na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mainduzi kusaini Sheria hiyo.

Alisema busara za Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete za kusimamia utaratibu wa kupelekwa mswada Bungeni zimepelekea suala la mafuta na Gesi Asilia hivi sasa kutoka katika mambo ya Muungano.

Balozi Seif alifahamisha kwamba Zanzibar na Wananchi wake wamefarajika na mwanzo mzuri wa hatua za awali za utafiti na baadaye uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ndani ya mipaka yake ya Visiwa vya Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Kampuni ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Nchini Ras Al – Khaimah { RAK GAS } kwa juhudi zake zilizoonyesha nia safi ya kushirikiana na Zanzibar katika Mradi huo mpya wa Mafuta na Gesi.

Alisema Rak Gas imekuwa mshirikia mkubwa wa Zanzibar katika harakati za kuwaondoshea dhiki ya huduma za Maji safi na salama Wananchi wa Zanzibar ambapo tayari Kampuni hiyo imeshafadhili nuchimbwaji wa visima 100 Unguja na Pemba. “ Tumeshuhudia juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Rais Al –Khaimah Kupitia Kampuni ya Rak Gas katika kuunga mkono harakati za Kijamii Visiwani Zanzibar ”. Alisema Balozi Seif.
 
Balozi Seif aliwataka Wananchi wote kutokuwa na hofu kwa ndege itakayohusika na utafiti wa Mafuta na Gesi katikia maeneo yanayodhaniwa kuwa na Rasilmali hiyo kwa vile itaruka katika maeneo ya chini zaidi na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida.

Mapema Mhandisi Muandamizi wa Kampuni ya Rak Gas kutoka Nchini Ras Al – Khaimah Dr. Osama Abdd – AAL ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuanza kuweka Historia mpya katika muelekeo wake wa mradi wa Kiuchumi wa Mafuta na Gesi Asilia.

Dr. Osama alisema Wananchi wa Zanzibar na ndugu zao wa Ras Al – Khaimah tayari wamekuwa na uhusiano wa Kihistoria uliopelekea kujenga ushirikiano zaidi katika uanzishwaji wa utafiti wa Mafuta na GesiAsilia Zanzibar.

Alisisitiza kwamba utiaji Saini Mkataba wa Utafiti wa Rasilmali hiyo uliofanywa na Serikali zote mbili Nchini Ras Al – Khaimah karibu miaka miwiliiliyoita ni uthibitisho wa uhusiano huo wa pande hizo mbili. Naye Msimamizi wa Kampuni ya Bell Geosace Interrises Limited inayofanya Utafiti huo Bwana Stephane Kunar alisema ataalamu wa Taasisi hiyo wako makini katika suala ya uhifadhi wa mazingira wakati wanapoendesha tafiti zao.

Bwana Kunar alisema hatua hiyo inakuja kutokana na uzoefu mkubwa waliyonao wahandisi hao kwa karibu miaka 70 sasa tokea kuanzishwa kwake ambapo Barani Afrika kazi hiyo wanaiendeleza kwa zaidi ya miaka 15 sasa.Alisema utafiti wao ambaowanaufanya kwa zaidi ya Mita 100 chini ya ardhi pamoja na maeneo ya Bahari kwa Afrika umeshafanyikka Afrikka kwa Nchi ya Botswana Brazil Barani Amerika ya Kusini.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
14/3/2017.

PROF. MUHONGO AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA PWANI.

March 14, 2017


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Kulia kwa Waziri ni Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa na kushoto kwa Waziri ni Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete. Wengine katika picha ni viongozi kutoka Mkoa wa Pwani, TANESCO, REA na kampuni ya Steg International Services itakayotekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo.
Watendaji kutoka kampuni ya Steg International Services wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani. Kampuni hiyo itatekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo wa Awamu ya Tatu.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye fulana ya Bluu) na Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakifukia nguzo ya umeme kwa udongo ikiwa ni ishara ya kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani.
MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AFUNGA SEMINA YA WATENDAJI, WENYEVITI NA MAKATIBU WA WILAYA NA MIKOA MJINI DODOMA LEO

MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AFUNGA SEMINA YA WATENDAJI, WENYEVITI NA MAKATIBU WA WILAYA NA MIKOA MJINI DODOMA LEO

March 14, 2017
MW1
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa baada ya kufunga semina yao katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.
MW2 MW3 MW4
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa wakati wa kufunga semina yao katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.
MW5
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa wakati wa kufunga semina yao katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.
MW6 MW7
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli  wakati akifunga kufunga semina ya watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa  katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.
PICHA NA IKULU
CCM1 CCM2

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA ATEMBELEA UJENZI WA MFEREJI WA MAGAONI UNAOJENGWA KUKABILIANA NA ADHA YA MAFURIKO

March 14, 2017
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku aliyevaa shati jeupe wa kwanza kulia akiangalia namna uchimbaji wa mfereji wa kupitishia maji wakati wa mvua unavyochimbwa wakati alipofanya ziara ya kuutembelea leo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku aliyevaa shati jeupe wa kwanza kulia akiangalia namna uchimbaji wa mfereji wa kupitishia maji wakati wa mvua unavyochimbwa wakati alipofanya ziara ya kuutembelea leo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku wa kwanza kulia akisisitiza jambo kwa mafundi wanaoendelea na ujenzi wa mfereji wa magaoni kwa ajili ya kupitishia maji ya mvua ikiwa ni mpango madhubuti wa kukabiliana na adha ya mafuriko nyakati za mvua
 Kazi  zikiendelea kama inayoonekana kwenye eneo hilo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku wa tatu kutoka kushoto akisisitiza jambo kwa msimamizi wa mradi huo Ephahim Lucas wakati alipotembelea ujenzi wa mfereji huo ili kuona kasi yake ya utendaji kama inakidhi viwango.

 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akitazama namna mafundi wakiendelea na uchimbaji wa mfereji mkubwa kwa ajili ya kupitisha maji ya mvua ikiwa ni mpango mkakati wa kuondokana na adha ya mafuriko nyakati za mvua
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akitazama ujenzi wa mfereji huo kulia ni msimamizi wa mradi huo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akiingia kwenye mfereji huo kwa ajili ya kuukagua wakati alipofanya ziara ya kushtukiza mapema leo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akitoka kwenye mfereji huo mara baada ya kuukagua mapema leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akitoka kwenye mfereji huo mara baada ya kuukagua mapema leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kulia akiwa na msimamizi wa mradi huo akikagua baadhi ya maeneo ili kuona namna unavyojengwa
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbarukuakiwa na msimamizi wa mradi huo wakitembelea kwenye mfereji ambao utatumika kupitisha maji yatakayojaa kwenye makazi ya wananchi wakati wa mvua
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akiingia kwenye moja ya chemba zilizopo kwenye ujenzi wa mfereji huo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa mradi huo mara baada ya kuutembelea leo kuona namna ujenzi wake unavyoendelea.

MASAUNI AWATAKA MAAFISA MAGEREZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI NCHINI, AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VITUO VYA MAGEREZA TANZANIA BARA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

March 14, 2017
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa Maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.  (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa  magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.  
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga (kulia waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo, mara baada ya Naibu Waziri huyo, kuufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Suleiman Msuya

NAIBU Waziriwa Mambo ya Ndani, MhandisiHamadYusuphMasauniamesemaSerikalihaitasitakuchukuahatuakwawakuuwamagerezanchiniambaowatashindwakutimizadhanayauzalishajimaliambayoniagizo la Rais John Magufuli.

Aidha, Jeshi la Magereza Tanzania limetajachangamototanokuuambazozinakabilijeshihilohaliambayoinakwamishaufanisikatikamipangoyao.

Masuanialisemahayowakatiakizungumzakatikamkutanowawakuuwavituovyamagereza Tanzania Bara unaofanyikakatikaBwalo la MagerezaUkongajijini Dar es Salaam.

NaibuWazirialisemaiwapowakuuwamagerezawatatumiawafungwawaliopouzalishajiutaongezekahivyokuondokananatabiayakulalamikaufinyuwabajeti.

Alisemapamojanavigezombalimbalivyakupimawakuuwamagerezakigezokinginekitakuwanikuangaliakasiyauzalishajikwaeneohusika.

Masauni alisema jeshi la magereza lina rasilimali nyingi kama mashamba na viwanda hivyo wanapaswa kutumia fursa iliyopo kuongeza uzalishaji na kuchochea uchumi wa viwanda.

“Napenda kuwa muwazi hatutavumilia mkuu yeyote wa gereza ambaye atashindwa kuzalisha na kuendeleza fursa ambazo zinamzunguka kwani Tanzania ya viwanda itafanikiwa kupitia vyombo vilivyopo katika wizara yetu,” alisema.

Naibu waziri alisema anaamini kupitia jeshi hilo ajiraz itaongezeka, uchumi utakuwa na maendeleo ya nchi yatapatikana kwa haraka hivyo lengo la 2025 kukamilika.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali Magereza, Dk. Juma Malewa alisema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ufinyu wabajeti, madeni ya watumishi, makaziduni, ukosefu wa posho na vitendea kazi kama usafiri.

Alisema katika kutatua changamoto ta usafiri wanatarajia kupokea magari 450 siku za karibuni katiya 905 ambayo wameahidiwa na Serikali hali ambayo itaweza kutatua changamoto hiyo.

Dk. Malelwa alisema pia wameanza kutatua changamoto ya makazi ambapo Rais Magufuli ametoa sh. bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 320 katikakambiyaUkonga.

Kamishna Jenerali Malelwa alisema hadi sasa wamepokea sh. bilioni 5 ambazo zimeanza kutumika kujenga nyumba hizo 320 zinazojengwanaWakalawaMajengonchini(TBA).

Alisema wao wamejipanga kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inapatikana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hivyo utatuzi wa changamoto hizo utakuwa suluhu sahihi kwao.

“Tumedhamiria kuongeza uzalishaji na kufufua viwanda mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lakini tunaomba changamoto nilizo zitaja zitatuliwe kwa wakati,” alisema.

Akizungumzia dhana hiyo ya viwanda Mkurugenzi waViwanda, Naibu Kamishna wa Magereza Edith Mallya alisema utekelezaji wa agizo la Serikali umeanza katika baadhi ya viwanda kama MbigiriMorogoro na Karanga.