SUBASH PATEL WA M.M.I STEEL AMKABIDHI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MABATI YENYE THAMANI YA SH.MILIONI 200 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE

March 14, 2016

 Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wa kwanza kushoto), mabati yenye thamni ya sh.milioni 200 Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa M.M.I Steel, S.K. Modi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymund Mushi na kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, 
 Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (kulia), akizungumza katika makabidhiano hayo.
Wanahabari na wadau wa maendeleo wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akitoa shukurani kwa msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumuzia changamoto ya madarasa katika wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa shukurani baada ya kupokea msaada huo.
Mwanahabri Renatus Mutabuzi wa Kituo cha Televisheni cha ITV akiwa kazini kuchukua taarifa hiyo.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.

Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Viwanda vinavyoshughulika na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi nchini umemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mabati yenye thamani ya sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi msaada huo Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel alisema waliguswa mno na changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi ndio maana akawaomba wenzake wasaidie.

"Kampuni yangu imetoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 100 na Kampuni ya Ujenzi ya Estim imetoa sh.milioni 50 wakati Export Trading imetoa sh. milioni 50" alisema Patel.

Patel alitumia fursa hiyo kuyaomba makampuni mengine kujitoa kusaidia shughuli za maendeleo nchini hasa katika sekta ya elimu yenye changamoto za uhaba wa madarasa na madawati.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya madarasa jijini Dar es Salaam hasa katika Wilaya ya Temeke na Ilala ambapo katika shule moja kuna zaidi ya wanafunzi kuanzia 3000 hadi 5000.

Sadiki alisema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto hiyo katika jiji la Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema,  Ilala, Raymond Mushi na Mkurugenzi wake.

CCM NYAMAGANA KUMSAFIRISHA KWA NDEGE MSANII ALIETEMBEA KWA MIGUU KUTOKA JIJINI MWANZA HADI DAR.

March 14, 2016
Rafael Shilatu ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana (Kulia) akizungumza katika hafla ya kumpongeza msanii Rich4D.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Chama cha Mapinduzi CCM kimekubali kumsafirisha kwa ndege Mwanamuziki Chipukizi Richard Stanford maarufu kwa jina la Rich4D, alietembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es Salaam ili kumpongeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Raphael Shilatu, alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, katika hafla ya kumpongeza msanii huyo kwa matembezi yake baada ya kurejea Jijini Mwanza.

"Kwanza nimpongeze kwa matembezi yake ambayo ni ya kizalendo kabisa. Lakini niseme kwamba atakapopata fursa ya kwenda kuonana na Mhe.Rais, tutamsafirisha kwa ndege kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar na kumrudisha pia". Alisema Shilatu huku akimuomba Katibu Mkuu Mhandisi John Kijazi kumsaidia msanii huo ili aweze kuonana na Mhe.Rais Dkt.Magufuli.

Januari 16 mwaka huu Msanii Rich4D alianza matembezi yake kutoka Jijini Mwanza na kupita katika Mikoa Minane sawa na kilomita 1,200 hadi kufika Jijini Dar Februari 10, hii ikiwa ni siku 26 mfululizo za matembezi hayo ambayo mbali na kumpongeza Rais Dkt.Magufuli, pia yalilenga kuwasilisha kilio cha wasanii chipukizi wa Mikoani ambao wamekuwa wakikosa fursa mbalimbali ikilinganishwa na wasanii wakubwa walioko Jijini Dar.

"Kila Mkoa na Wilaya nilizopita nilipokelewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Maafisa Utamaduni na baada ya kufika Dar nilipokelewa na Viongozi wa Serikali akiwemo aliekuwa Katibu Mkuu Ombeni Sefue ambae aliniahidi kuonana na Mhe.Rais kabla mwezi wa mwili haujaisha kwani nilishindwa kuonana na rais baada ya kuambiwa yuko katika majukumu mengine ya Kitaifa". Alitanabaisha Rich4D na kumuomba Katibu Mkuu mpya Mhandisi John Kijazi kuhakikisha ahadi aliyoiacha Sefue inatimia.
Msanii Rich4D akionyesha Vibali alivyokuwa navyo kabla ya kuanza matembezi yake.
                    Bonyeza HAPA Kutazama Picha za Mapokezi.

GSM FOUNDATION YAIPIGA JEKI TIMU YA TAIFA YA RIADHA ILIYOKO KAMBINI WEST KILIMANJARO

March 14, 2016
Kocha wa timu ya taifa ya riadha Fracis John (kulia) akiwa na wanariadha wanaounda timu ya taifa ya riadha wakitizama msaada wa Track Suit ulitolewa na GSM Foundation kwa ajili ya wanariadha hao.
Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akitizama msaada wa track suit zilizotolewa na kampuni ya GSM Foundation.
Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akikabidhi msaada wa track Suit zilizotolewa na GSM Foundation .
Wanariadha wanaounda timu ya taifa wakichagua Track suit zilizotolewa na kampuni ya GSM Foundation .
Kila mmoja akichagua rangi anayopendelea.
Wanariadha wanaounda timu ya taifa ,wakiwa katika picha ya pamoja na rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka pamoja na kocha wao Francis John .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI MJINI ,JAFARY MICHAEL ATEMBELEA UWANJA MDOGO WA NDEGE WA MJINI MOSHI.

March 14, 2016
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael (katikati) akiwa na Diwani wa kata ya Korongoni Ally Mwamba (kushoto) walipotembelea uwanja wa ndege mdogo wa Moshi .
Meneja wa Uwanja mdogo wa ndege wa Moshi,Fredrick Kimaro akisoma taarifa ya uwanja huo kwa Mbunge wa jimbo  la Moshi mjini Jafary Michael alipotembelea uwanja huo.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini ,Jafry Michael akizungumza jambo alipotembelea uwanja huo kuona namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo.
Meneja wa Uwanja huo Fredrick Kimaro akisisitiza jambo wakati akitoa maelezo kwa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini alipotembelea uwanjani hapo.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael akiwa ameongozana na Mkuu wa usalama wa uwanja huo Macmilan Matili kuangalia maeneo mbalimbali ya uwanja huo.
Meneja wa uwanja mdogo wa ndege Moshi,Fredrick Kimaro akimuonesha Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael eneo la maegesho ya ndege katika uwanja huo.
Mbunge Jafary Michael na ujumbe wake wakiongozwa kupita katika eneo la kutua ndege uwanjani hapo.
Meneja wa uwanja wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro akimsikiliza kwa makini Mbunge Jafary Michael wakatia akishauri jambo baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huo.
Eneo la kukimbilia ndege katika uwanja mdogo wa ndege Moshi likionekana katika hali hii.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

UNDP YAZINDUA RIPOTI YA KAZI NA MAENDELEO YA BINADAMU, MAVUNDE AAGIZA KAZI YENYE STAHA

March 14, 2016
IMG_6050
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akiwasili kwenye uzinduzi wa ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) huku akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kulia) uliofanyika Machi 11, 2016 jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Antony Mavunde ametaka kuondolewa kwa changamoto maeneo ya kazi ili kazi isaidie maendeleo ya binadamu badala ya kujikimu.
Naibu Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015 inayoelezea kazi kwa maendeleo ya binadamu.
Alisema kwa sasa kuna figisu kubwa katika kazi nchini hasa kutokana na waajiri wengi kugeuza kazi kama sehemu ya kujikimu kwa wafanyakazi wao kwa kutowapa stahiki husika ikiwamo mikataba ya ajira.
Alisema kazi inapokuwa ni ya kujikimu kunakuwa na migogoro mingi na kuvurugika kwa uzalishaji na kutishia maendeleo ya taasisi husika na maendeleo ya mtu binafsi.
Alisema Tanzania imefurahishwa na yaliyomo katika ripoti hiyo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kutokana na kuzungumzia jinsi kazi zinavyoweza kusaidia upatikanaji wa maendeleo.
Alisema wakati Tanzania inaelekea kujipanga kwa uchumi wa kati, Ripoti inaonyesha ni jinsi gani kazi inaweza kuboresha maisha ya Mtanzanzania kwa kuondoa kazi na kuwapatia wananchi kazi zenye staha na zinazoweza kuwasaidia wao binafsi na hivyo kukuza uchumi na ustawi wa jamii.
Alisema amekuwa akizungumza katika maeneo mengi ya kazi na kukutana na changamoto nyingi zikiwemo za kukosekana kwa mikataba, mazingira mabaya ya kufanyakazi, ujira usiokidhi na kutaka waajiri kufuata sheria za kazi kwa kuwapatia mikataba ya kazi na pia kuhakikisha kazi zinakuwa na staha.
Awali akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dar es Salaam, alisema kwamba uzinduzi wa kitaifa ambao unafuatia uzinduzi wa kimataifa uliofanyika mwaka jana mjini Addis Ababa, Ethiopia ni faraja kubwa kwa wadau wa maendeleo nchini.
Alisema uzinduzi huo unaweka ripoti hiyo karibu zaidi na wananchi na kuahidi serikali kuifanyia kazi kutokana na umuhimu wake hasa wa kuhakikisha kazi inasaidia maendeleo ya watu.
Anthony Mavunde
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kulia) kabla ya kuelekea kwenye uzinduzi rasmi wa ripoti ya maendeleo ya watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) uliofanyika Machi 11, 2016 jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na ESRF.
Anasema ripoti hiyo inaonesha namna ambavyo kazi inaweza kuchangia maendeleo na ustawi wa jamii.
Alisema wakati Tanzania inaelekea kuwa taifa ambalo limejengeka katika msingi wa maendeleo ya watu kama ilivyokusudiwa tangu kupatikana kwa Uhuru wake 1961, Ripoti hiyo ni chanzo kizuri cha maarifa katika kufanikisha mabadiliko yanayotakiwa kufanikisha maendeleo ya watu.
Alisema kazi ni msingi wa maendeleo kwa hiyo ni vyema kuboresha mazingira ya kazi na wafanyakazi ili kuleta maendeleo kusudiwa kwa kuwa na kazi zenye staha.
Alipongeza UNDP na wadau wengine kwa kufanikisha uzinduzi huo ambao alisema umeenda sanjari na dhima ya serikali ya kutumia maarifa yote yaliyopo kusaidia maendeleo ya watu.
Ripoti hiyo ya UNDP imetazama kwa undani kuhusu kazi, mahusiano ya kazi na maendeleo ya binadamu.
George Mulamula
Mshehereshaji wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) akisherehesha uzinduzi huo uliofanyika Machi 11, 2016 jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na ESRF.
Aidha imeangalia masuala ya usalama wa kazi na mahitaji ya utaalamu; masuala ya kulipwa na kutolipwa kazini, uangalizi, kujitolea ubunifu na kazi endelevu.
Pia ripoti hiyo inatoa majumuisha yanayostahili kufanywa bali mapendekezo ya utengenezaji wa sera unaotanua uzalishaji kwa kutoa fursa na kulinda wafanyakazi, ubora wa kazi, ujira stahiki, kazi yenye staha na kazi endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Kimsingi Ripoti hiyo inapendekeza kuongeza faida za maendeleo ya binadamu, kupitia utendaji kazi, kwa kupendekeza mikakati ya kujenga fursa za ajira, ili kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi, na kuendeleza maeneo yaliyolengwa, ambayo yatabadilisha hali halisi ya sasa.
Aidha ainaangalia Sera zilizopendekezwa, kuhakikisha utendaji kazi bora, utendaji kazi endelevu, ambayo inachangia usawa, badala ya kujenga ukosefu wa usawa, na kazi ambayo inaheshimu haki za wafanyakazi, na kuhakikisha usalama wao.
Human Development Report 2015, Tanzania
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma taarifa kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna hatua njema kwenye maendeleo ya watu katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwamo lakini ipo haja ya kuangalia pengo kubwa lililopo katika fursa mbalilmbali zikiwamo za kazi.
Imeelezwa ndani ya ripoti hiyo kwamba toka mwaka 2000 nchi ziloizo kusini mwa Jangwa la Sahara zimekuwa na ukuaji wa maendeleo ya binadamu( Human Development Index -HDI) wa kazi wa kiwango cha asilimia 1.7 kati ya mwaka 2000 na 2010 : asilimia 0.9 kwa mwaka 2010 na 2014.
HDI ni kipimo kinachotathmini maendeleo ya muda mrefu ya afya na maisha marefu, elimu na maisha yenye staha.
Kwa Tanzania kumekuwepo na ongezeko la HDI la asilimia 1.18% kati ya mwaka 1985 na 2014, ikiongezeka kutoka 0.371 hadi 0.521, ikiwa ni ongezeko la asilimia 40.5 juu ya ongezeko la nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara la 0.518.
Human Development Report 2015, Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (hayupo pichani) kuhutubia wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.
Mratibu wa Umoja wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza katika uzinduzi huo alisema kwamba ongezeko hilo si haba.
Hata hivyo aliwaambia wadau waliokuwepo kushuhudia uzinduzi huo kwamba Taifa bado linakabiliwa na changamoto nyingi zikkiwemo umaskini uliokithiri, kutanuka kwa pengo la usawa na kushindwa kuhimili matukio ya mabadiliko ya tabianchi na uchumi.
Aidha alisema kwamba :”Ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015, inaonyesha kuwa, kuimarisha maendeleo ya binadamu, kupitia utendaji kazi, inahitaji sera na mikakati katika maeneo makuu matatu: kujenga fursa za ajira, kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi na kuendeleza maeneo yaliyolengwa. Hii inaongeza kasi ya kutengeneza ajira nchini Tanzania.”
Tanzania ikiwa na zaidi ya watu milioni 12 wakiishi katika umaskini na wengi wao uliokithiri changamoto kubwa kwa Tanzania, ni kutafsiri uwezo huu katika miundombinu inayoonekana, kwa kujenga mazingira mazuri, na kuongeza ujuzi wa watu wake kama ilivoainishwa katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu mwaka elfu mbili na kumi na tano.
Human Development Report 2015, Tanzania
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akisoma hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) kwa niaba ya Waziri Jenista Mhagama, uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.
Alisema changamoto zote hizo ni za kweli na zenye uhusiano na maendeleo ya binadamu na ni vyema ilivyowekwa katika Muono wa maendeleo ya Tanzania kufikia 2025 na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Katika hotuba yake ya shukurani Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo, alisema kwamba taasisi yake ipo tayari kusaidia Tanzania na nchi nyingine kuwezesha kutambua uhusiano kati ya kazi na maendeleo ya binadamu katika utekelezaji wa Maendeleo endelevu (SDGs).
Human Development Report 2015, Tanzania
Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) na meza kuu wakijiandaa kuzindua ripoti hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo.
UNDP HUMAN DEVELOPMENT REPORT 2015 LAUNCH
Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 11, 2016.
Anthony Mavunde
Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani).
IMG_6200
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo kwa pamoja wakiwa wameshikilia ripoti hiyo.
Human Development Report 2015
Muonekano wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015). Kwa picha zaidi bofya link hii

SHULE YA KIBUGUMO YAPOKEA MSAADA KUTOKA BANGO SANGHO WENYE THAMANI YA MIL. 20

March 14, 2016
Bango Sangho- kibugumo Primary School
Meza kuu kwenye uzinduzi wa kambi ya upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo ya upimaji kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige, Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee, Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kibugumo, Mzamilo Ally, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi nchini (Bango Sangho) umetoa msaada wa kompyuta, printa, tanki la maji la lita 5000, umeme, madarasa saba yaliyofanyiwa ukarabati, madaftari na kalamu katika Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni ulio na thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na huduma ya kupima afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano.
Akizungumzia msaada huo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee alisema wameamua kutoa msaada huo kwa shule ya Msingi Kibugumo na huduma ya kupima bure kwa kutambua umuhimu wa afya na elimu bora kwa maendeleo ya sasa na baadae kwa taifa.
Alisema wamekuwa wakitoa misaada katika shule hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo na mwaka huu waliamua kuwaletea tena na huduma ya upimaji afya bure kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano ili wazazi wapate fursa ya kutambua hali ya afya za watoto wao lakini pia kuwajengea utaratibu wa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kujua hali zao za kiafya,
“Sisi tunapenda kuona hali nzuri ya elimu na tumeshasaidia kwa muda shule hii tumeshatoa madawati 100 na tulijenga madarasa mawili na leo tumeleta msaada mwingine na pia awamu hii tena tumeleta huduma ya afya ili watoto wapimwe afya zao,” alisema Banerjee.
Bango Sangho
Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee akisoma risala ya Umoja huo mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.
Nae mgeni rasmi katika halfa hiyo ya kupokea msaada kutoka Bango Sangho, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Sophia Mjema aliwashukuru Bango Sangho kwa msaada huo ambao wameotoa katika shule hiyo na huduma ya kupima afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kuwaomba kama ikiwezekana wawapelekee huduma hiyo ya kupima afya kila baada ya miezi mitatu.
Alisema wilaya yake bado ina changamoto nyingi katika sekta ya elimu na kupitia msaada huo utaweza kusaidia kuboresha elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo na kuwaomba kuendelea kuwasaidia.
“Wilaya yetu bado ina changamoto nyingi na kwa msaada huuu naomba niwashukuru sana na ninaomba muendelee kuwa na moyo huo,” alisema Bi. Mjema.
Aidha Bi. Mjema aliwataka wananchi wa wilaya yake ya Temeke kuwa na utaratibu wa kupima afya zao angalau mara moja kwa mwaka ili waweze kutambua magonjwa waliyonayo kabla hayajaanza kuwasumbua na hata wengine kupelekea kupoteza maisha kutokana na kutokuwa na utaratibu wa kupima hadi wanapoanza kusumbuliwa.
Nae Mratibu wa kambi ya upimaji, Dkt. Ali Mzige alisema kupitia huduma hiyo ya upimaji wa afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano wanataraji kupima watoto sio chini ya 400 na huduma zitakazotolewa ni kupima uzito, wingi wa damu, ushauri kuhusu lishe, afya ya kinywa na watoto watakaobainuka kuwa na matatizo watapewa rufaa kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke.
Alisema kupitia huduma hiyo wataweza kutambua magonjwa waliyonayo watoto lakini pia kuwapa elimu wazazi jinsi ya kuwalea watoto katika mfumo bora wa kiafya.
“Tunafanya huduma hii kwa watoto sababu asilimia 32 ya watoto nchini walio na umri chini ya miaka mitano wamedumaa na pia tutaweza kuwapa vipeperushi wazazi ili wajue jinsi ya kulea watoto na wanapougua wajue nini cha kufanya,” alisema Dkt. Mzige.
Nae mwalimu wa afya katka shule ya Kibugumo, Tatu Mhina aliwashukuru Bango Sangho kwa misaada ambayo wamekuwa wakiwapatia tangu mwaka 2014 mpaka sasa na kuwaomba kuendelea na moyo huo wa kusaidia elimu katika shule hiyo na kuzidi kuwapelekea huduma za kiafya katika jamii inayozunguka shule hiyo ili wanafunzi waweze kuwa na afya njema.
Bango Sangho Kibugumo
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema kutoa nasaha katika ufunguzi wa kambi hiyo.
Bango Sangho - Kibugumo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akitoa neno la ufunguzi wa kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam.
Bango Sangho - Kibugumo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akimpima uzito mtoto Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani, kama ishara ya kuzindua kambi ya huduma za upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk. Ali Mzige, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (wa kwanza kulia) pamoja na Muuguzi wa Zahanati ya Kibugumo, Agnes Mokiwa (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.
Bango Sangho - Kibugumo Primary Schoo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akiwa amembeba mtoto Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani, baada zoezi la kumpima uzito wakati akizindua kambi ya huduma za upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam.
Bango Sangho - Kibungumo Primary School
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikagua kadi ya kliniki ya maendeleo ya mtoto Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua kambi ya upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige na Kulia ni Muuguzi wa Zahanati ya Kibugumo, Agnes Mokiwa.
Bango Sangho-Kibugumo
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakigaiwa madaftari yaliyotolewa kama zawadi na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho).
Bango Sangho-Kibugumo Primary School
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akielekea kuzindua moja ya madarasa yaliyokaribatiwa na kuwekewa umeme na Bango Sangho.
Sophia Mjema
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikata utepe kuzindua moja kati ya madarasa yaliyokarabatiwa na Bango Sangho huku Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile wakishuhudia tukio hilo.
Bango Sangho - Kibugumo Primary School
Muonekano wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kibugumo baada ya kupakwa rangi na kuwekwa umeme na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho).
Bango Sangho - Kibugumo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikagua moja ya darasa lililokarabatiwa na Bango Sangho.