Tigo yajiongeza zaidi uboreshaji wa mtandao

July 18, 2017

Ofisa Mkuu wa Ufundi na Mawasiliano wa Tigo,Jerome Albou,akizungumza na wahabari mbalimbali jijini Dar es Salaam juzi,Juu ya Uwekezaji katika ku vya habari kwenye warsha ya uwekezaji katika kuboresha upatikanaji wa mtandao wa Tigo kote nchini.

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA NISHATI YA BIOGAS ILI KURAHISISHA MAISHA

July 18, 2017
Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear akiendelea kutoa elimu katika semina hiyo inayofanyika leo jiji hapa
wakwanza kulia ni Mratibu wa Ubunifu  kutoka ECHO  Harold Msanya akiwa anafafanua jambo mbele ya wakufunzi hao
baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiendelea kufanya kazi ya majadiliano  katika makundi

Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ndugu Rowah Spear akiwa anawaelekeza baadhi ya wadau waliouthuria semina jinsi biogas inaweza kufanya kazi
wadau wakiendelea kufatilia mada ilikuwa inaendelea



Mkurugenzi wa ECHO   Erwin Kinsey akiwa anaonyesha wakulima na wadau walioshiriki semina hiyo mmea aina ya gugukaroti ambalo ,alisema kuwa gugu ilo kwa asilimia 90% huku asilimia 10% ni gugu ambalo linaweza kutumika kutengeneza biogas(na woinde shizza,Arusha)
wadau wakiendelea na majadiliano katika makundi yao ikiwa ni sehemu ya kujifunza njia mbalimbali  na matumizi ya biogas
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
ESRF YAANDAA MKUTANO KUJADILI BIASHARA NA UWEKAZAJI KATI YA TANZANIA NA CHINA

ESRF YAANDAA MKUTANO KUJADILI BIASHARA NA UWEKAZAJI KATI YA TANZANIA NA CHINA

July 18, 2017
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango ametaka kuwapo na uratibu wenye maslahi mapana katika biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China. Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China. Alisema mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na China ambayo ni ya kihistoria yasitumike vibaya bali yanahitaji kuratibiwa kiuangalifu kwa maslahi ya pande zote mbili. Aliwataka washiriki wa mkutano huo wa mwaka kujadili kwa makini namna ya kuratibu vizuri vitega uchumi na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption] Alielezea kufurahishwa kuwapo na mada mbalimbali zinaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China na kusema mada hizo zitumike vyema kuweka misingi mizuri yenye manufaa kwa pande zote mbili. Aidha aliipongeza ESRF kwa kuona haja ya kuwapo kwa mazungumzo ya aina hiyo na kusema kupitia tafiti mbalimbali taifa hili litaenda mbele katika kujenga uchumi wa viwanda. Mkutano huo unaohusisha washiriki mbalimbali wa ngazi za juu wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China umeitwa kama sehemu ya mchango wa ESRF katika ujenzi wa uchumi wa viwanda wa Tanzania. “Sisi serikalini tunaridhishwa na juhudi zinazofanywa na taasisi za kitafiti kama hii zenye lengo la kusaidia juhudi za serikali za kuhudumia watu wake na kuongeza ustawi” alisema Mpango. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption] Mkutano huo ambao unazungumzia mahusiano ya kibiashara na uwekezaji umeelezwa na Mh. Dk Mpango kuwa moja ya mikutano inayotoa fursa za kuangalia uwekezaji wenye tija unaozingatia maslahi mapana ya mataifa husika. Alisema Tanzania na China zina uhusiano mzuri wa kihistoria na hadi sasa na kwamba kinachostahili ni kuoanisha uhusiano huo na kuuweka katika hali bora zaidi za kunufaisha pande zote mbili. Baadhi ya miradi mikubwa ambayo Tanzania imesaidiwa na China ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na kiwanda cha Urafiki; kuanzishwa kwa shamba la mpunga la Mbarali; kiwanda cha sukari cha Mahonda na mgodi wa mawe wa Kiwira. [caption id="attachment_2454" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption] Kwa sasa China ni moja ya taifa lililo na uwekezaji mkubwa nchini Tanzania pia ikifanya shughuli nyingi za ujenzi zenye gharama kubwa kama daraja la Kigamboni na barabara. Naye Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mpango alisema kwamba alisema kwamba mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja kati ya ESRF na Chuo kikuu cha Kilimo cha China. Alisema mkutano huo umewaleta pamoja wanazuoni wa Kichina na Kitanzania kuangalia mahusiano yaliyopo na kutengeneza mustakabli bora wa namna ya kushirikiana. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida amesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kusaidia serikali kwa njia ya utafiti ambapo majibu yanatumiwa kutengeneza sera au majibu ya changamoto mbalimbali. Mkutano huo ulifungwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim. [caption id="attachment_2455" align="aligncenter" width="1404"] Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania anayeshughulikia wa Masuala ya Uchumi na Biashara, Lin Zhiyong akizungumza kwa niaba ya balozi wa China wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_2459" align="aligncenter" width="1404"] Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda akiwasilisha mada inayohusu namna watanzania wanavyoweza kunufaika na fursa za kibiashara na uwekezaji China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.