MAOMBI YA KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI, WASAIDIZI WAKE PAMOJA NA TAIFA YAFANA JIJINI MWANZA.

January 13, 2016
Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (wa pili kushoto walioshikilia bendera), katika Maombi ya Kumuombea Rais Magufuli na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group (BMG)
Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza kwa kushirikiana na Umoja wa Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam jana January 13,2015 ulifanya Mamombu Maalumu ya Kumuombea Rais wa wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake.

Maombi hayo yalifanyika katika Uwanja wa Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali na Dini huku pia wananchi wakijumuika pamoja na waumini wa dini mbalimbali katika maombi hayo.

Mgeni Rasmi katika maombi hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae katika hotuba yake, aliwasihi Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa ili kuondokana na vikwazo mbalimbali ambapo alidokeza kuwa kupitia maombi kama yaliyofanyika jana, migogoro mbalimbali ikiwemo ya kisiasa kama iliyopo Zanzibar itamalizika.

Viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Askofu Charles Sekelwa, Makamu wake Zenobius Issaya pamoja na Kiongozi wa Kundi la Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam la Good News For all Ministry Askofu Dr.Charles Gadi pamoja na viongozi wengine wa dini kutoka mikoa mbalimbali nchini waliliombea Taifa na kuhimiza utuliza nchini.

Wasaidizi wa wa Rais Maguguli ambao ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu, Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Mhe.Othman Chande, Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wa Serikali wa awamu ya tano waliombewa ili kuliongoza vema taifa kwa kuendana na kasi ya Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, ia maombi hayo yalijumuisha toba kwa taifa, kumuomba Mungu kukomesha mauaji ya Vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na kuombea taifa mvua zisizo na madhara. 
Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Wa tatu kushoto) katika Maombi ya Kumuombea Rais Magufuli na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wa dini
Maombi ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Jijini Mwanza jana
Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Kulia ni Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Zenobius Isaya akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Zenobius Isaya akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mmoja wa Viongozi wa dini akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Askofu Charles Sekelwa  akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Kiongozi wa Kundi la Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam Askofu Dr.Charles Gadi akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Viongozi wa dini
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akizungumza katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akizungumza katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Kwaya ya EAGT Mabatini Jijini Mwanza ikitumbuiza katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Wanahabari katika kunasa habari kwenye Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Meneja wa HHC Alive Fm Radio ya Jijini Mwanza (Kulia) akiwa pamoja na GB Pazzo (Kushoto) katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.

RC MAHIZA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA BANDARI YA TANGA.

January 13, 2016


MKUU WA MKOA WA TANGA,MWANTUMU MAHIZA AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA BANDARI LEO MARA BAADA YA KUITEMBELEA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,ABDULA LUTAVI NA KULIA NI KAIMU MENEJA WA MAMLAKA YA BANDARI MKOANI TANGA,HENRY ARIKA
NA TANGA RAHA BLOG.
IMEELEZWA kuwa agizo la Rais John Magufuli kusitisha safari za nje kwa watendaji wa serikali nchini zimesababisha Bandari ya Tanga kufanyakazi chini ya kiwango na kulazimika kukodi vifaa kwa gharama kubwa nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa bandari ya Tanga Arika wakati mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alipofanya ziara ya siku mmoja kukagua shughuli zinazofanywa na bandari hiyo.
 
Alisema kuwa hatua hiyo ya kusitishwa kwa safari mpaka vibali
imechangia bandari hiyo kupata hasara na kulazimika kukodi Tug ya kupakuwa mizigo kutoka nangani kwenye meli hadi katika pwani ya bandari hiyo.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa japo agizo hilo linafaida kwa serikali lakini tunamuomba Mheshimiwa Rais angalie upya agizo hilo kwani kuna baadhi ya taasisi zinazojiendesha kibiashara zinaathirika na utendaji wake wa kila siku kushuka”alibainisha Kaimu Meneja huyo.

Aliiomba serikali kuangalia namna bora ya kutenganisha taasisi hizo katika utoaji wa vibali kwani kwa hili limesababisha kushindwa kupelekaTug meli ya kukokotea vyombo vya majini yao kwa ajili ya ukarabati nchini Kenya.
 
“Tagi tuliyonayo katika bandari ya Tanga ni mmoja pekee na manahoza waliisimamisha kufanyakazi toka mwezi Novemba mwaka jana hivyo tumelazimika kukodi Tug kutoka mjini Mombasa ili kurahisisha utoaji wa mizigo”alisema Arika.

Ambapo aliongeza kuwa hali hiyo situ inakwamisha utendaji kazi bali inachangia hasara kwa Mamlaka kwani hulazimika kutumia gharama kubwa kwaajili ya uwendeshaji kifaa cha kukodisha.
 
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa uwamuzi wa Rais ni kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana kwa haraka na kwa kutumia raslimali kwa uwangalifu.

Alisema kuwa sambamba na hilo ilikuweza kuongeza ufanisi katika
bandari ameahidi kuunda tume itakayokuwa ikishughulika na kutatua kero mbalimbali zinazoikabili bandari hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi .

MKUU WA MKOA WA TANGA,MWANTUMU MAHIZA KULIA AKIJIANDAA KUINGIA KWENYE BOTI KWA AJILI YA KUFANYA ZIARA YA KUZUNGUKA BANDARINI

KAIMU MENEJA WA MAMLAKA YA  BANDARI YA TANGA(TPA)HENRY ARIKA AKIZUNGUMZA WAKATI ZIARA YA MKUU WA MKOA MWANTUMU MAHIZA LEO WA KWANZA KUSHOTO NI MKUU HUYO WA MKOA NA ANAYEFUATIA NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,ABDULLA LUTAVI





SPIKA WA BUNGE ALIPOKWENDA KUMFARIJI MAMA MARIA NYERERE

SPIKA WA BUNGE ALIPOKWENDA KUMFARIJI MAMA MARIA NYERERE

January 13, 2016

ndu1
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiweka saini kitabu cha maombolezo  alipokwenda kutoa pole Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Leticia Nyerere leo tarehe 13 Januari Msasani jijini Dar es Salaam.
ndu2
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimfariji Bi. Rose Nyerere binti wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipokwenda kuwafariji kufuatia kuondokewa na Mpedwa wao Leticia Nyerere.
ndu3
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsalimia Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipokwenda nyumbani kwake kumpa pole kufuatia kifo cha mkwewe wake Leticia Nyerere.
ndu4
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (aliyekaa katikati) wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mkwewe wake Leticia Nyerere. Aliyekaa kulia ni Mmoja wa Wasemaji wafamilia Bw. John Shibuda.
ndu5
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na  Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mkwewe wake Leticia Nyerere. Aliyekaa kushoto ni Bi. Rose Nyerere.
ndu6
Spika wa Bunge akiwa na wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akiwemo Mama Maria alipokwenda kuwafariji kufuatia kifo cha mpedwa wao Leticia Nyerere.
ndu7
Spika wa Bunge akiwa  katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akiwemo Mama Maria alipokwenda kuwafariji kufuatia kifo cha mpedwa wao Leticia Nyerere.
ndu8
Spika wa Bunge akisalimia familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipokwenda kuwafariji kufuatia kifo cha mpedwa wao Leticia Nyerere.
(Picha na Ofisi ya Bunge)
DK. SHEIN AMWAPISHA MKUU WA WIALAYA YA WETE LEO

DK. SHEIN AMWAPISHA MKUU WA WIALAYA YA WETE LEO

January 13, 2016


we1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu]
we3
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu]
we4
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akisalimiana na kumpongeza Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo baada ua kuapushwa katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu]
WAZIRI MBARAWA AWATAKA TEMESA KUFUNGA MITAMBO YA ELEKTRONIKI ILI KUONGEZA MAPATO

WAZIRI MBARAWA AWATAKA TEMESA KUFUNGA MITAMBO YA ELEKTRONIKI ILI KUONGEZA MAPATO

January 13, 2016

UJE1
Kaimu mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme TEMESA Eng. Prisca Mkama akitoa taarifa ya utendaji wa kivuko cha Magogoni kwa Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano profesa Makame mbarawa kushoto na mkurugenzi wa ufundi dkt. William Nshama kulia akifuatilia.
UJE2
Mkuu wa kivuko cha magogoni Eng. Charles Irege akimwonesha Waziri waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano profesa Makame mbarawa namna ya kufuatilia mapato ya kivuko cha magogoni kwa njia ya elekroniki.
UJE3
Mkuu wa kivuko cha Magogoni Eng. Charles Irege akimwonesha Waziri  wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano profesa Makame mbarawa namna ya kukagua tiketi za kielekroniki kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye kivuko
UJE4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano profesa makame mbarawa mwenye suti  akizungumza na wasafiri wa kivuko cha magogoni eneo la kigamboni kabla ya kuanza safari kulia kwake ni Kaimu mtendaji mkuu wa TEMESA Eng. Prisca Mkama.
UJE5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano profesa Makame mbarawa mwenye suti akishuka kwenye kivuko cha mv. kigamboni mara baada ya kukagua shughuli za kivuko hicho.
UJE6
Abiria wanaotumia kivuko cha Mv. Kigamboni wakielekea kupanda kivuko hicho kutoka magogoni  kwenda Kigamboni.
………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Prof. Makame Mbarawa amewataka Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kufunga mfumo kamili wa elekroniki katika kivuko cha Magogoni ili kudhibiti mapato yanayopotea kiholela.
Amesema takriban asilimia 20 ya abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni na Mv Kigamboni wanavuka bila kulipa nauli hali inayoathiri mapato stahiki ya kivuko hicho.
“Nawapa miezi mitatu muwe mmefunga mfumo kamili wa kupokea nauli wa elektroniki ambao utadhibiti ukwepaji wa kulipa nauli ili kuongeza mapato na kufikia shilingi milioni 25 kwa siku,” amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amesema nia ya wizara yake ni kukusanya mapato stahiki kutoka katika vivuko  vyote ili kuwezesha kununua kivuko vipya na  kukarabati vivuko vingine kadri iwezekanavyo.
Aidha ameagia ufanyike uboreshaji wa bwalo la kupumzikia abiria upande wa magogoni ili liweze kuhudumia watu wengi na katika hali nzuri na kuagiza uboreshaji huo kuanza mara moja.
Amezungumzia umuhumi wa wafanyakazi wa vivuko vya Magogoni na kigamboni kuwa na lugha nzuri kwa abiria wao na kuwasaidia wale wenye mahitaji maaalum ili kuboresha huduma ya usafiri ya vivuko hivyo.
Ameitaka TEMESA kuweka mfumo wa tiketi za msimu zitakazowezesha wafanyakazi kulipa kwa awamu moja au mbili kwa mwaka na hivyo kunufaika na punguzo maalum na kuondoa usumbufu wa kulipa nauli kila siku.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Prisca Mkama amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mapato ya kivuko cha Magogoni yataimarika hivi karibuni kufuatia mikakati madhubuti wanayoifanya katika kuboresha huduma zao hususani eneo la Kigamboni.
Tariban abiria elfu 60 hutumia kivuko cha Mv. Magogoni na Mv. Kigamboni kuvuka kwa siku katika harakati za shughuli za kijamii na kibiashara.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AKUTANA NA MABALOZI WA MISRI NA DENMARK.

January 13, 2016

WAZIRI wa Maji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge leo amekutana na mabalozi wa Misri na Denmark kwa nyakati tofauti ofisini kwake, Makao Makuu ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Ubungo Maji.

Huu ni mwendelezo wa mazungumzo ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Lwenge na washirika wa maendeleo na wadau wa Sekta ya Maji ya kuweka mikakati ya kuinua na kuendeleza Sekta ya Maji nchini, mara baada ya juzi pia kukutana na Balozi wa Ubelgiji, Mhe, Paul Cartier.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akizungumza na Balozi wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf na Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Hamza Sadiki.
  Balozi wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf akimpa zawadi Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge.
  Balozi wa Denmark, Mhe. Einar H. Jensen akisaini Kitabu cha Wageni, kwenye ofisi ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, akiwa na msaidizi wake, Kansela wa Uchumi na Usimamizi wa Fedha za Umma , Mette Melson.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na Balozi wa Denmark, Mhe. Einar H. Jensen.

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, Balozi wa Denmark, Mhe. Einar H. Jensen na Mkurugenzi wa Maji Mijini, Inj. Dkt. Justus Rwetabula.