WAZIRI PROFESA MAKAME MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) KUKAGUA UTENDAJI

April 17, 2018

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akizungumza na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati alipofika kwenye Ofisi za shirika hilo, kukagua utendaji katika Idara mbalimbali za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Meneja Masoko wa Shirika la Posta, David George akimpatia maelezo Waziri Profesa Mbarawa kuhusu mikataba ya Kibiashara iliyoingiwa na shirika.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia baadhi ya mikataba iliyoingiwa na shirika hilo.
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akimweleza jambo Waziri Profesa Mbarawa (kulia), katika ziara hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta, Agnes Mtango. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Usafirishaji ya Shirika la Posta, alipoangalia mfumo wa usafirishaji kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo.
Afisa Msimamizi wa Magari ya Shirika (Transport Officer), Mhandisi Lameck Francis (kulia), akimweleza Waziri Profesa Mbarawa namna ya mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo, unavyofanyakazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akikagua mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta ya shirika ya kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo.
Meneja Fedha wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Rajab Mngong'e (kushoto), akimweleza jambo Waziri Profesa Makame Mbarawa, alipofika katika Idara ya Fedha katika ziara hiyo.
Meneja Msaidizi Idara ya Fedha, Aron Samwel (kushoto), akimuonesha Waziri Profesa Makame Mbarawa, mfumo wa utunzaji wa fedha za shirika unavyofanya kazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akisindikizwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Elia Madulesi, mara baada ya kumaliza ziara hiyo.




WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Profesa Makame Mbarawa (MB) leo tarehe 17 Aprili, 2018 amefanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.

Mhe. Profesa Mbarawa ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kwa lengo la kukagua utendaji na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Posta, katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta Luteni Kanali mstaafu Dr. Haruni Kondo.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alitaka kujionea matumizi ya mifumo ya kielektronik na namna ambavyo Shirika limejipanga kuitumia mifumo mbalimbali ili kusimamia utendaji kwa ukaribu. Mhe. Waziri Mbarawa alitembelea idara ya Fedha, Idara ya Barua na Logistiki, Idara ya Sheria, Idara ya Masoko na pia alikagua mifumo udhibiti wa gharama za mafuta na mwenendo wa magari ya Shirika yanayosafiri kati ya Dar es salaam na mikoani.

Katika ziara hiyo Mh. Waziri ameitaka menejimenti ya Shirika kusimamia utendaji kazi na kuzingatia weledi na matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Mhe. Waziri alitoa msisitizo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi na kukuza tija kwa kila Idara ndani ya Shirka la Posta. Waziri amemwaagiza Kaimu Postamasta Mkuu Hassan Mwang’ombe kufuatilia utendaji wa kila idara na kupata taarifa za mara kwa mara ili kuimarisha utendaji wa shirika.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta alimshukuru Waziri Mhe. Mbarawa kwa kutembelea Shirika la Posta na kuahidi kuwa maagizo yote na maelekezo aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu ili kuleta tija na Ufanisi zaidi.

MZALISHAJI WA MBEGU APATA TUZO YA UJASIRIAMALI YA CITI FOUNDATION

April 17, 2018


Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu (kulia) akikabidhi cheti kwa mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Lydia Majoro wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mjasiriamali mlemavu aliyefanya vyema Aneth Geraw ambaye aliondoka na kitita cha dola za Marekani 2000 wakati hafla ya kukabidhi tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa mshindi wa pili wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Anney Sekulasa (kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.

Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) na Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati) kwa pamoja wakikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yetu Microfinance, Attemius Millinga (kushoto) ambapo taasisi yake imekuwa na ubunifu mkubwa wa bidhaa zake sambamba na mifumo ya kutolea huduma na methodolojia wakati wa hafla fupi ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwanamke aliyefanya vyema kwenye ujasiriamali mdogo, Lucy Kiongosi akipozi baada ya kupokea cheti kilichoambatana na dola za Marekani 2000 wakati wa hafla ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika mwishoni wa wiki jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso.

Mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Lydia Majoro akifurahi na kupozi na cheti pamoja na tuzo yake.

Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati) akikabidhi cheti kwa Mjasiriamali mdogo aliyefanya vyema mwenye umri wa miaka 18-25 tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Mopaya Madi (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia).

Mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Beula Seed and Co & Sons, Zabron Mbwaga (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu (wa pili kushoto), Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia).

Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa Ofisa mikopo Rose Chacha (kushoto) wakati wa hafla fupi za tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.


Na Mwandishi Wetu

Zabron Mbwaga ambaye ni Mzalishaji mbegu, aliyepo Viwanja vya NaneNane, Njiro mkoani Arusha ametwaa tuzo ya mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali ya Citi Foundation. Tuzo hiyo inaambatana na fedha taslimu dola za Marekani 7,500.

Mbwaga ambaye aliwezeshwa upanuzi wa shughuli zake kwa mikopo kutoka BRAC Tanzania, alianza kazi zake akiwa na mtaji wa shilingi milioni 2 kabla ya kuongezewa nguvu na BRAC.

Tuzo hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki zilitolewa kwa wajasiriamali 16 na ofisa mikopo mmoja.
Mshindi wa pili ni Anney Sekulasa akiondoka na dola za Marekani 6000 huku mshindi wa tatu ni Lydia Majoro ambaye aliondoka na dola za Marekani 4000. Nafasi ya mjasiriamali mlemavu iltwaliwa na Aneth Geraw aliyepata dola za Marekani 2000.

Zaidi ya shilingi milioni 70 za kitanzania zimetolewa kwa washindi wa kwanza hadi wa 16 . Pia Taasisi za kifedha za wajasiriamali wadogo na wa kati (MFI) zenye ubunifu mkubwa wa bidhaa zake na huduma, mifumo ya kutolea huduma na methodolojia pia ilipata tuzo. Safari hii Yetu Microfinance ndio walioinyakua.

Tuzo hizo za Citi Bank Foundation zimeendeshwa na Mtandao wa Asasi zinazotoa huduma za kifedha kwa wajasiriamali wadogo (TAMFI) ‘TAMFI’ na washindi wametangazwa na majaji walioshiriki kufanyakazi hiyo.

Tuzo hizo zimelenga kuhamasisha wajasiriamali kutumia taasisi za kifedha za watu wa kati na chini na kufaidika nazo.

Takribani wajasiriamali 209 waliwasilisha miradi yao lakini 22 pekee ndio waliweza kupenya na 16 ndio walipata ushindi wa tuzo tofauti.

Safari hii washiriki walitoka maeneo mbalimbali nje ya Dar es Salaam tofauti na ilivyokuwa kwa mwaka 2016 ambapo washiriki wake walikuwa ni wa Dar es Salaam pekee.

Washindi wengine ni Comelord Swai $ 1000, Prisca Kayombo $ 1000, Rahim Kalyango $ 1000, Emmanuel Lazaro $ 1000, Jumanne Findisha $ 1000, Salma Said $ 1000, Editha Lukindo $ 1000, Amon Kalumuna $ 1000, Salum Chumu $ 1000 na Doroth Sambi $ 1000.

Tigo yamwaga zawadi za simu kwa washindi 84 wa katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus jijini Dar es Salaam leo

April 17, 2018
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya kukabidhi simu janja aina ya Tecno R6 kwa washindi 52 kutoka Dar es Salaam wa wiki hii katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza. 







Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Tatu Shomari Kandi (kati) mjasirialimali n amkaazi wa Tabata jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa  Mariam Yatela Omari (kati), mhudumu wa saluni katika eneo la Kisarawe, Dar es Salaam baada ya kuibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa  Boni Japhet Sanga (kati) mjasirialimali n amkaazi wa Tabata jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.  

DC MATIRO AONGOZA MKUTANO WA WADAU WA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI MKOA WA SHINYANGA

April 17, 2018

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro amefungua na kuongoza mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga uliolenga kujadili namna ya kufanikisha zoezi la chanjo hiyo kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 mkoani humo. kutano huo umefanyika leo Jumanne Aprili 17,2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.

Akifungua mkutano huo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa chanjo imeanzisha chanjo mpya ya kuwakinga na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14.

Matiro alisema saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza nchini Tanzania kwa kusababisha vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti ambazo zote zinasababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akina mama vitokanavyo na saratani hivyo kunahitajika juhudi na ushirikiano zaidi kupunguza vifo hivyo.

“Lengo la kuanzisha chanjo hii ni kukinga mabinti kutokana na madhara makubwa yanayoweza kuwapata ambayo husababisha vifo vingi kwa wanawake,na walengwa wa chanjo hii mwaka huu ni wasichana wote wanaotimiza miaka 14 ambapo katika mkoa wa Shinyanga wasichana wasiopungua 29,479 watachanjwa”,aliongeza.

Alisema chanjo hiyo itatolewa bila malipo katika vituo vya kutolea huduma vya serikali na binafsi ,baadhi ya shule na maeneo katika jamii ambazo zitatolewa kwa njia ya huduma za mkoba.

“Saratani hii inachangiwa na vitu vingi ikwemo kuanza kujamiiana katika umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,ndoa za mitaala,kuzaa watoto wengi na uvutaji wa sigara”,alieleza.

Alizitaja dalili za saratani ya mlango wa kizazi kuwa ni kutokwa damu ya hedhi bila mpangilio,kutokwa damu baada ya kujamiiana,maumivu ya mgongo,miguu na kiuno,kuchoka,kupungua uzito,kukosa hamu ya kula,kutokwa uchafu wa rangi ya kahawia au wenye damu kwenye uke na maumivu ya miguu au kuvimba.

Hata hivyo alisema dalili mbaya zaidi zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na kuishiwa damu,figo kushindwa kufanya kazi,kupatwa na fistula na uvimbe wa tezi.

Kwa upande Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume alisema kati ya wasichana 7304 wanaougua saratani ya mlango wa kizazi nchini kila mwaka,4216 sawa na asilimia 58 wanafariki dunia hivyo ni muhimu zaidi kupata kinga kuliko tiba.

Alisema uzinduzi rasmi wa chanjo hiyo mkoani Shinyanga utazinduliwa siku ya Jumatatu Aprili 23,2018 katika manispaa ya Shinyanga.

Naye Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela alisema tayari pesa kwa ajili ya chanjo hiyo zimeshatumwa kwenye halmashauri kinachotakiwa ni utekelezaji tu ili kuhakikisha mkoa unafanya vizuri katika zoezi hilo la utoaji chanjo kwa wasichana. ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MKUTANO HUO HAPA CHINI



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog




Matiro alisema serikali imeamua kuanza kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa sababu saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa kuua wanawake wengi ukilinganisha na saratani nyingine nchini.



Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.


Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.

Mkutano ukiendelea...


Wadau wakiwa ukumbini..Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba na Afisa Tawala wilaya ya Kahama, Said Yasin


Kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngassa Mboje akiwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bakari Kasinyo

Wadau wakiwa ukumbini



Mkutano unaendelea


Mtakwimu (Mpango wa taifa wa chanjo), David Kayabu akitoa mada kuhusu zoezi la chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi


Daktari wa Meno mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya ambaye ni Mkufukunzi wa mafunzo ya chanjo ya HPV akitoa mada ukumbini kuhusu chanjo hiyo

Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga, Mohammed Kahundi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo

Picha za pamoja wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
Picha za pamoja wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi

Picha za pamoja wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi


Picha za pamoja wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WANANCHI JIJINI TANGA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA

April 17, 2018


WANANCHI Jijini Tanga wametakiwa kuwasaidia watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali mkoani Tanga ili kuwaepusha na vishawishi vinavyoweza kuwakuta na kukwamisha ndoto zao za kupata elimu bora ambayo inaweza kuwakomboa kimaisha.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM) Mustapha Selebosi wakati akifungua bweni Jipya la wasichana katika Taasisi ya Goodwill&Humanity Foundation ambayo imejikita kuwasaidia jamii inayoishi kwenye mazingira magumu na hali duni mjini Tanga.

Alisema lazima jamii itambue kuwa ukiwanusuru watoto wa kike utakuwa umeisaidia familia nzima hivyo umuhimu wa kuwajali kwa kuwaangalia kwa jicho la huruma unahitajika kwa kiasi kikubwa kwao kwa ajili ya kuwawezesha kufikia malengo yao.

“Ndugu zangu lazima tuwaangalie watoto yatima kwa jicho pana kwa lengo la kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao walizokuwa nazo kwani ukimnusuru mtoto wa kike umeinusuru familia na ukiamuacha utakuwa umeiangamizi dunia “Alisema

Hata hivyo aliitaka jamii inayoishi karibu na kituo hicho kuacha kutoa maneno ya kejeli ikiwemo kuwabuguzi watoto hao badala yake washirikiane nao kuweza kutimiza malengo yao ya kuhakikisha wanaishi kwa upendo na amani.

Aliwataka pia wakazi wa Jiji hilo kuwasaidie watoto hao kuwalea kwenye ,misingi ya kiimanio tusiwabuguhudhi kwa maneno ya kejeli kuwa wanasaidiwa,wale ambao hawawatakii mem watoto hao wazibitiwe ambao wanaweza kuiwafanya watoto hao kama wake zao.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Goodwill and Humanity Foundation Shekhe Sayyed Muhdhari alisema taasisi hiyo ilianzishwa kwa lengo la kusaidia makundi ya wasiojiweza ndani ya jamii ikiwemo kuleta usawa baina ya watu wa kaya tofauti.

“Pamoja na hayo ni kusimamia watoto wasiokuwa na wazazi wakulea katika maadili mema pia tulianzisha taasisi hii baada ya kufanya utafiti pamoja na sense ulibaini idadi kubwa ya yatima,wazee,walemavu na wagonjwa waishio kwenye hali duni wakiwa hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu “Alisema.

Kwa upande wake Mlezi wa kulea kituo cha kulea watoto yatima cha Casa Della Gioia Sista Consolata Mgumba aliitaka jamii kuwapenda watoto hao kwa kuwasaidia mahitaji mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao.

“Ndugu zangu yoyote anayependa kuwajali watoto yatima anapata Baraka kutoka kwa mwenyezi mungu hivyo nawaasa jamii kubadilika na kuona namna ya kuwaunga mkono waweze kupata malezi bora na elimu “Alisema.