HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 21,2023

September 20, 2023

 
























































SACP MISIME AWATAKA ASKARI POLISI KUBADILIKA KIFIKRA NA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA WELEDI

September 20, 2023

 




Na, Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) David Misime amefunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa,Wakaguzi na Askari wa Polisi kutoka Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma.




SACP Misime amewaeleza Askari hao kuwa mafunzo hayo ni mfululizo wa mafunzo yanayotolewa kwa Askari katika Vyuo ndani ya nchi, nje ya nchi na kazini kwa lengo la kuwabadilisha kifikra (mindset change) ili kutoa huduma bora kwa jamii.







SACP Misime amefungua mafunzo hayo Septemba 20, 2023 katika ukumbi wa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Yakifanyika kwa engo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi kwa Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu.







"Mkibadilika kifikra na kuhudumia wananchi kwa Nidhamu,Haki,Weledi na Uadilifu mtakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya wananchi kifua mbele na kwa kutumia Falsafa ya Polisi,wananchi waka waamini na kuongeza imani kwa Jeshi la Polisi ili waoneshe ushirikiano katika kubaini na kuzuia uhalifu".Amesema Misime.








Pamoja na hayo, Misime amewapongeza Askari kwa kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kazi kubwa wanayofanya huku akiwataka kwenda kuyafanyia kazi yale waliojifunza ili wananchi waweze kuona mabadiliko ya kifikra na kiutendaji kulingana na mageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi.






Awali akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto kutoka Makao Makuu ya Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Faidha Suleiman amewasisitiza Askari wa Kike kuzingatia maadili, kutunza familia, kujijengea uwezo wa kujiamini, kuwa wasafi na kuachana na vyanzo vyote vya mawazo kama vile kujiingiza katika mikopo isiyo na msingi ambayo muda mwingi huwapelekea kuwa ni watu wenye mawazo.




Hata hivyo, ACP Faidha Suleiman ambaye ni mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Makao makuu ya Polisi amewataka askari kuhakikisha wanafuata na kutekeleza miradi ya Polisi Jamii katika majukumu yao ya kila siku kwani miradi hiyo inagusa kila kitengo cha Jeshi la Polisi.




Amesisitiza katika kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto katika familia zao na jamii kwa ujumla ikiwemo wao wenye kutokujifanyia ukatili.




Naye Mkuu wa Dawati la mtandao wa Polisi wananwake (TPF Net) Makao Makuu ya Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Eva Stesheni amewataka askari kujifunza namna ya kuandika ripoti ya kazi zao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi pamoja na kuwasidia katika utunzaji wa kumbukumbu za nyaraka kwa kuwa na mpango kazi ulio mzuri ilikufikia malengo sahihi , Kuwasilisha taarifa, mawazo na kuendeleza ujuzi hususani kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto.





















Picha na Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AFAGILIA UWEKEZAJI WA SHABOUT NZEGA

September 20, 2023

 Na Mwandishi wetu, Nzega


KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim ameipongeza kampuni ya ASHARIQ CONSTRUCTION COMPANY LIMITED kwa uwekezaji mkubwa wa mradi wa maduka 74 uliopo Mjini Nzega Mkoani Tabora.

Akizungumza leo jumatano September 20 Kaim wakati mwenge wa uhuru ukiweka jiwe la msingi kwenye mradi huo wa majengo ya maduka ya SHABOUT.

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka huu amesema uwekezaji wa mradi huo ni mkubwa na utaendelea kuukuza mji wa Nzega, utachochea maendeleo ya eneo hilo na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo.

"Rais wa Serikali ya awamu ya sita Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo tumieni fursa hii kuwekeza, tunatambua jitihada za mwekezaji huyu hivyo mbio za mwenge wa uhuru kwa heshima kubwa tunaridhia kuweka jiwe la msingi la jengo hili," amesema Kaim.

Mkurugenzi wa kampuni ya ASHARIQ CONSERVATION COMPANY LIMITED Rashed Shabout Said amesema mradi huo wa maduka 74 ulianza mwezi Februari 2023 na unatarajiwa kukamilika Machi 2024.

Rashed amesema hadi mradi huo utakapokamilika utagharimu kiasi cha shilingi 800,000,000 na hadi kufikia sasa umefikia asilimia 70 ya gharama za ujenzi kwa shilingi 560,000,000.

"Fedha hizo zimetokana na ujasiriamali katika kodi za biashara za maduka ya SHABOUT SHOPPING CENTRE na ukandarasi katika kampuni ya ujenzi," amesema.

Amesema faida ya ujenzi huo ni pamoja na kuunga mkono sera ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzitaka sekta binafsi kuwekeza ili kuongeza ajira ambapo wanatarajia kuajiri watumishi zaidi ya sita, watakaotoa huduma mbalimbali katika jengo hilo ingawa kwa sasa wakati ujenzi ukiendelea wameajiri vijana zaidi ya 15 ikiwa ni pamoja na wataalamu 3.

Amesema faida nyingine ya uwekezaji huo ni pamoja na kuufanya mji wa Nzega uvutie sambamba na kulipa tozo na kodi mbalimbali Serikalini.

"Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kuruhusu uwekezaji kupitia sekta binafsi na kutia chachu kwa wawekezaji kutafuta mitaji," amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Lemeya Tukai amepongeza uwekezaji huo uliofanywa na kampuni ya ASHARIQ CONSERVATION COMPANY LIMITED kuwa utachochea maendeleo ya mji wa Nzega.

"Tunaomba ukague mradi huu na ikikupendeza tunaomba utuwekee jiwe la msingi, mwenge wa uhuru hoyeeee tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa," amesema DC Tukai.




SERIKALI IMETENGA HEKTA 60,000 KWA AJILI YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MPUNGA,RUFIJI-DKT SAMIA

SERIKALI IMETENGA HEKTA 60,000 KWA AJILI YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MPUNGA,RUFIJI-DKT SAMIA

September 20, 2023


Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji

Serikali imetenga eneo la ukubwa wa hekta 60,000 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa zao la mpunga katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa kauli hiyo, Septemba 20, 2023, akiwasalimia wananchi wa Kata ya Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Alisema kwa mwaka huu wamekusudia kulima hekta 30,000 za mpunga kupitia skimu ya umwagiliaji ambayo serikali imetenga kwa ajili ya shughuli za kilimo na kwamba mwaka ujao wanatalima nyingine 30, 000.

“Tumeamua kugawa eneo la bonde la Rufiji kwa ajili ya shughuli za kuzalisha umeme na nusu yake skimu za umwagiliaji na mwaka huu tunaanza kulima hekta 30,000, zitakuwa mahsususi kwa ajili ya kulima mpunga ambao utalisha mataifa mbalimbali kutokea hapa Rufiji “anasema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Hata hivyo aliwahamasisha vijana kuchangamkia fursa hiyo ya kilimo cha umwagiliaji kupitia mradi ya Jenga Kesho iliyobora (BBT) kwa kuzalisha mpunga kwa wingi ambao utauzwa ndani na nje ya nchi kutokana na kuwepo kwa soko la uhakika.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, alimshukuru Rais wa Tanzania kwa kutoa bure pembejeo za kilimo ikiwamo mbolea ya ruzuku katika zao la korosho ambalo amedai kutokana na hatua hiyo ubora na uzalishaji umeongezeka.

Alisema kwa sasa wanapata bure ruzuku ya sulphur na ya unga ambayo hapo awali walikuwa wanapata changamoto ya kudumu gharama za pembejeo za kilimo.

RAIS DKT. SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA VIOO MKURANGA MKOANI PWANI

RAIS DKT. SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA VIOO MKURANGA MKOANI PWANI

September 20, 2023

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi mara baada ya kuzindua Kiwanda cha Vioo cha Sapphire Floating Glass kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani tarehe 20 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kuzindua Kiwanda cha Vioo cha Sapphire Floating Glass kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani tarehe 20 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji mara baada ya kuzindua Kiwanda cha Vioo cha Sapphire Floating Glass kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani tarehe 20 Septemba, 2023Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi wengine wakati akikata utepe kuzindua Kiwanda cha Vioo cha Sapphire Floating Glass kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani tarehe 20 Septemba, 2023.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kwenye Kioo cha kwanza kutengenezwa katika Kiwanda cha Vioo cha Sapphire Floating Glass kama kumbukumbu mara baada ya kuzindua Kiwanda hicho kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani tarehe 20 Septemba, 2023.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji wakati akikagua Kiwanda cha Vioo cha Sapphire Floating Glass kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani tarehe 20 Septemba, 2023.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Kiwanda cha Vioo cha Sapphire Floating Glass kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani tarehe 20 Septemba, 2023.
    Viongozi pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Vioo cha Sapphire Floating Glass kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani tarehe 20 Septemba, 2023.