MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA JIJINI DAR LEO

November 26, 2014

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa la kuchochea mwamko wa nafasi ya mabingwa wa uchunguzi tiba katika kuboresha huduma za tiba. Kongamano hilo linalofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, limewakutanisha mabingwa wa tiba za afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.

baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ufunguzi wa Kongamano hilo leo Novemba 26, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi waratibu wa Kongamano hilo wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach leo Novemba 26, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi waratibu wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi. Picha na OMR.

RAS CHIMA AWAFUNDA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO,AWATAKA MADEREVA KUACHA KUPAKIA MISHIKAKI

November 26, 2014
KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA,SALUM CHIMA AKISALIMIANA NA VIONGOZI WA MBALIMBALI  MKOANI HAPA KUSHOTO NI KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA,JUMA NDAKI


KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA,SALUM CHIMA AKIWAHUTUBIA WANANCHI WA MKOA WA TANGA WAKATI WA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA AMBAPO KIMKOA ILIADHIMISHWA KWENYE VIWANJA VYA TANGAMANO LEO

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA,JUMA NDAKI AKIONGEA

MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI,MKOA WA TANGA,ABDI ISANGO AKIFUATILIA VIKUNDI VYA SANAA VILIVYOKUWA VIKITUMBUIZA KWENYE KILELE HICHO LEO









MISS TANZANIA 2012 BRIGITTE ATOA MAFUNZO YA UJASILIAMALI KWA WALEMAVU WA NGOZI

November 26, 2014
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiteta na wanafunzi waliofika kuangalia jinsi mafunzo ya Ujasiriamali yakiendeshwa na Taasisi ya mrwembo huyo (BAF) na Taasisi ya Junior Achievements Tanzania.
 Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiwa katika pozi na wanafunzi waliofika kuangalia jinsi mafunzo ya Ujasiriamali yakiendeshwa na Taasisi ya mrwembo huyo (BAF) na Taasisi ya Junior Achievements Tanzania.
 Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiwa katika picha ya pamoja na walemavu wa ngozi mara baada ya kumaliza mafunzo ya usajisiriamali kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini.
*************************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) imeendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 50 wenye ulemavu wa ngozi.
Brigitte aliendesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na taasisi ya Junior Achievement Tanzania yalifungwa jana kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa na kupambwa na maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali mbalimbali ambao ni zao la mradi huo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Brigitte alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga mambo mbalimbali katika maisha ya kila siku ikiwa pamoja na kuwawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku.
 
Alisema kuwa BAF kupitia Taasisi ya Junior Achievement Tanzania kwa pamoja wameweza kutoa elimu ya kujitambua na stadi za biashara ili walemavu wa ngozi waweze kuthubutu, kuanzisha na kuendeleza biashara na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazo wapa ajira, kipato na kuinua ustawi wa maisha yao na familia zao.
 
Alisema kuwa mpango huu umekuwa wa kipekee kwa kundi hili kwa kuweza kuwajengea mtazamo chanya wakuthubutu, kujiamini na kuweza kufanya mambo makubwa katika maisha.
 
“Mpango huu umeanza  hapa Dar es Salaam,  ila Brigitte Alfred Foundation ina azma ya kuuendeleza nje ya Dar es Salaam na kufikia walengwa waliopo mikoa tofauti nchini kwa sababu umeleta manufaa na mabadiliko makubwa sana kwa hawa vijana wenye ulemavu wa ngozi katika muda mdogo na umeonyesha kwamba walemavu wakiwezewshwa,” alisema Brigitte.
 
Mrembo huyo alitoa shukrani  kwa Juniour Achievement Tanzania na wadhamini wakuu, kampuni ya  Azam  kwa kutoa mafunzo hayo ambayo anaamini wahitimu watayatumia kwa faida zaidi.
 
“Nawaomba wadau wengine waniunge mkono katika mpango huu kwani awamu inayofuata ambayo ni kutekeleza mipango yao ya biashara katika ujasiriamali ili kuendeleza vijana wetu wa Tanzania hususa walemavu ili weweze kujikimu na kuboresha maisha yao kwa ujumla,” alisema.

*KINANA AKIUNGURUMA NANYUMBU

November 26, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara baada ya kupokea taarifa za chama na serikali juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupasua mawe wakati wa ujenzi wa mradi wa maji Sengenya
 Ujenzi wa mradi wa maji wa Sengenya ukiwa unaendelea ambapo ukikamilika utasaidia vijiji vitatu wilayani Nanyumbu mkoa wa Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanga mawewakati wa ujenzi wa bwawa la maji la Sengenya ambalo litasaidia vijiji vya Sengenya ,Mara na Nangarinje.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Daktari Mkuu wa Wilaya wilaya ya Nanyumbu Dkt. Ahmad Mhando ambapo Katibu Mkuu wa CCM alitembelea kituo hicho cha afya cha Mangaka.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na  Daktari Mkuu wa Wilaya wilaya ya Nanyumbu Dkt. Ahmad Mhando baada ya kukagua  kituo hicho cha afya cha Mangaka
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia wakina Mama wakifyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya UWT wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara
 Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Dunstan Daniel Mkapa akihutubia wakazi wa Mangaka mji ni na kuelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mangaka wilaya ya Nanyumbu na kuwataka wananchi hao kujiandikisha kwenye madaftari ya wapiga kura .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mangaka  wilaya ya Nanyumbu ambapo aliwaambia CCM ya sasa itakuwa kali kuliko wakati wowote na itaisimamia serikali na kuipongeza inapofanya vizuri na itakapofanya vibaya itasemwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika  Mangaka mjini wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera mara baada ya kufungua shina la wakereketwa Maneme wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
 Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia daraja la Umoja lililopo mpakani na Tanzania.
 Daraja la Umoja.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye kutanzama daraja hilo linalounganisha nchi mbili za Tanzania mfumo.
 Shehena ya mbao zilizokamatwa ma TRA Mtambaswala
 Katibu Mkuu wa CCM akiondoka kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania zilizopo Mtambaswala
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa CCM wa wilaya ya Nanyumbu wakikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa jengo la ofisi ya CCM kijiji cha Chungu kata ya Nanyumbu.
 Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akiwasalimu wananchi wa kata ya Nanyumbu,wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
 Wananchi wakimfurahia kumuona mkuu wao mpya wa mkoa
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendego akiwasalimu wananchi wa kata ya Nanyumbu mkoani Mtwara
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akimkabidhi kadi ya CCM Ndugu Yasin Seleman maarufu kwa jina la Msouth aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti kupitia Chadema.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara  Ndugu Mohamed Sinani akihutubia wakazi wa kata ya Nanyumbu kabla hajamkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kianana.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Nanyumbu ambapo aliwaambia wananchi kuwa serikali lazima irahishe taratibu za kufanya biashara mpakani
Kila mtu anamsikiliza Kinana kwenye mikutano yake....

JAJI WARIOBA AKOLEZA MOTO KATIBA MpYA

November 26, 2014
Wananchi wakiwa katika foleni ya kuingia katika ukumbi wa mdahalo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanaharakati wa mambo ya vijana Humphrey Polepole na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba akzungumza katika mdahalo huo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Picha zote: Francis Dande
Waliokuwa wajumbe Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameendelea kuikosoa vikali Katiba inayopendekezwa na kusema kwamba haitakuwa na manufaa kwa Watanzania.

Kadhalika, wamesema Muungano uliopo kwa sasa upo katika hatari ya kuvunjika na kwamba hali hiyo itasababishwa na Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (BMK).

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba (pichani), akizungumza katika mdahalo wa kujadili katiba inayopendekezwa uliofanyika ukumbi wa City jijini Dar es Salaam jana, alisema Katiba hiyo imeondoa matarajio ya wananchi waliotegemea kupata katiba ya kuwakomboa katika miaka mingine 50 ijayo.

Alisema Muungano umefika hapa ulipo, umetokana na kudra za Mwenyezi Mungu na hekima za viongozi waliopita kwa kuuendesha kwa hekima licha ya katiba hiyo kubeba changamoto lukuki.

“Mimi nimeshangaa kuona waheshimiwa hawa wananitukana na kunikashfu eti nimemsaliti Mwalimu Nyerere, wanadiriki kutumia nguvu na maneno ya kashfa kupitisha katiba. Katiba haiwezi kupitishwa kwa namna hiyo, katiba ni maridhiano ambayo pia yanashirikisha maoni ya wananchi,” alisema Warioba na kuongeza:“Hata kama Nyerere angelikuwapo leo angeipinga Katiba hii inayopendekezwa.”

Warioba alisema hata kama wataipitisha kwa nguvu, lakini wanatakiwa kufahamu kuwa italeta matatizo baadaye na ni vizuri wafahamu kuwa hata kama itapita itakuwa na matatizo.

Humphrey Polepole, aliitaka serikali kusambaza Katiba inayopendekezwa pamoja na rasimu ya Tume hiyo kwa wananchi ili waisome na kuielewa kabla ya kuipigia kura ya maoni.

Kuhusiana na suala la elimu ya wabunge, alisisitiza kuwa ni vema wabunge wawe na elimu ya kidato cha nne, tofauti na katiba inayopendekezwa inayowataka wawe wanajua tu kusoma na kuandika.

Alisema endapo Katiba itapitishwa kama ilivyo kwamba wabunge wajue kusoma na kuandika pekee, itamuwia vigumu rais kupata mawaziri wenye elimu ya kutosha ya kusimamia shughuli za maendeleo ya nchi.

“Unawezaje kusema wabunge wawe wanajua kusoma na kuandika tu, isipokuwa mawaziri, je, wakichaguliwa wabunge wote ambao uwezo wao ni wa kusoma na kuandika tu, hao mawaziri watatoka wapi na shughuli za maendeleo wataendeshaje?” alihoji Polepole.

Kadhalika, alisema kuwa anashangaa mawaziri kuipigia chapuo Katiba inayopendekezwa na kuipinga serikali tatu, wakati hata wao walitoa maoni wakiitaka muundo wa serikali hizo.

“Mimi nilishiriki katika kikao cha kukusanya maoni ya mawaziri, walipendekeza serikali tatu, na hata baadhi ya mawaziri wakuu nao walipendekeza serikali hizo, na wasitake tufikie huko wanakotaka, wakibisha tunaweza kuwataja,” alisema huku walioshiriki mdahalo huo wakitaka awataje.

Kwa upande wake, Profesa Mwesiga Baregu, alisema Katiba inayopendekezwa ni dalili ya kuvunjika kwa Muungano.

“Nilishangaa sana kuona wajumbe wa lililokuwa Bunge Maaluma la Katiba kufanya sherehe na marais kusherehekea malengo ambayo yameshindwa kufikiwa katika katiba inayopendekezwa, ambayo wananchi wakiisikia wanapata uchungu,” alisema Profesa Baregu.

Aliongeza: “Dalili inavyoonekana hivi sasa Katiba hiyo ndiyo itakuwa chanzo cha kuvunja Muungano huo na tutegemee, huko ndiyo tunakokwenda.”

Mohamed Mshamba, ambaye naye alikuwa mjumbe wa Tume ya Katiba, alisema Tume ilikusanya maoni ambayo yalilenga kulipatia taifa katiba bora, lakini lengo hilo limevurugwa baada ya kuondolewa vifungu vya msingi.

Mdahalo huo ulitawaliwa na ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ambao walikagua kila alieingia katika ukumbi huo kwa kutumia vifaa maalum vya ukaguzi.

Pia, ndani ya ukumbi kulikuwapo na utulivu, tofauti na ilivyokuwa katika mdahalo uliopita ambao baadhi ya watu waliumia kutokana na vurugu zilizosababishwa na kikundi cha watu walisadikika kutoka Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapindiuzi (UVCCM).

Kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza katika mdahalo wa jana, ukumbi huo ulijaa na kupelekea polisi kuwazuia baadhi ya watu kuingia ndani kutokana na kukosekana na nafasi.

Hali hiyo ilisababisha askari polisi kupata changamoto ya kuwaelewesha wananchi hao ambao hawakutaka kukubali kubaki nje.

 
CHANZO: NIPASHE