TANAPA YAZINDUA KAMPENI KILIMANJARO YENYE KAULIMBIU “ WEKA MLIMA SAFI, TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE”

April 24, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro iliyokuwa na kaulimbiu “ Weka Mlima Safi, Tunza Mazingira Yakutunze” katika lango la Marangu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kati) na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki.
Wakurugenzi kutoka TANAPA wakifuatilia uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko, Mkurugenzi Utumishi na Utawala Bi. Witness Shoo, Mkurugenzi wa Mipango Dk. Ezekiel Dembe, Mkurugenzi wa Fedha Nassoro Mndeme na nyuma yake Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahim Mussa.
Wanafunzi kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Mwanza nao walishiriki katika kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wadau walioshiriki kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA pamoja na wadau kutoka Kampuni mbalimbali za mawakala wa utalii kutoka Kilimanjaro na Arusha wanaoshiriki Kampeni maalum ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Idadi kubwa ya wadau wa sekta ya utalii walishirikiana vema na TANAPA kusafisha Mlima Kilimanjaro.
Wageni waalikwa wakivaa ‘gloves’ kabla ya kuanza zoezi la usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mazingira safi yataendelea kuufanya Mlima Kilimanjaro kutiririsha maji kwa wingi zaidi.

Na Dixon Busagaga waGlobu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

BENKI YA CRDB YATANGAZA AJIRA KWA KIDATO CHA SITA JITEGEMEE JKT SHULE YA SEKONDARIBENKI

April 24, 2016
 Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB,  Joseph Wite (katikati), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), hundi yenye thamani ya sh.milioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia kujenga mifumo ya maji shuleni hapo katika Mahafali ya 22 ya kidato cha sita yaliyofanyika Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
 Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa na mgeni rasmi wakielekea ukumbini.
Maandamano ya wanafunzi hao yakielekea ukumbini.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Bendi  ya JKT ikitumbuiza.
Wimbo maalumu wa shule ukiimbwa.
Wanafunzi wa kidato cha sita wakiwa kwenye mahafali hayo.
Burudani zikiwa zimepamba moto.
Mkuu wa Shule, Luteni Kanali, Robert Kessy akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere akizungumza kwenye mahafali hayo.
 Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB,  Joseph Wite (katikati), akizungumza katika mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), akimkabidhi hundi iliyotolewa na CRDB, Mkuu wa shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
Mkuu wa Shule akimkabishi cheki hiyo, Meja Rehema  Wanjara Msarifu wa Shule. Wengine kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo na Utawala, Kapteni Benitho na Mjumbe wa Bodi ya Shule, Sebastian Inosh.
Kwaito likiwa limepamba moto.
Hapa mwanafunzi Khalifa Chege aliyekuwa namba moja katika masomo akikabidhiwa zawadi.
Mwanafunzi Ibrahim Pazi aliyeshika nafasi ya pili katika masomo akikabidhiwa zawadi.



Dotto Mwaibale

BENKI ya CRDB imetangaza ajira kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT watakao pata divisheni one ya pointi tatu baada ya kufanya mtihani wa taifa.

Ofa hiyo ilitolewa na Meneja wa huduma mbadala wa Benki ya CRDB Joseph Wite kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk. Charles Kimei katika mahafali ya 22 yaliyofanyika shuleni hapo Dar es Salaam jana.

Katika hatua nyingine Wite amewataka wanafunzi hao kutumia fursa ya ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani uwezekano upo endapo watafanya bidii katika masomo yao.

Alisema ni wakati wa vijana kuchangamkia fursa za ajira katika jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza kufikia malengo na kuondokana na dhana ya kwamba hakuna ajira nchini.

"Pamoja na kwamba vijana wengi wanahofia kuajiriwa nje ya nchini kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo kuogopa kwamba hawawezi kukidhi vigezo lakini mimi napenda kuwatoa hofu hiyo kwamba hata kama kiingereza huwezi kiswahili utashindwa kufundisha,"alisema Wite.

Aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha kwamba wanajiepusha na matendo mabaya  ambayo yatapelekea kujiunga na madawa ya kulevya na kuhatarisha maisha yao.

Alisema mtu anapojiunga na madawa ya kulevya ana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo ukimwi.

"Janga la ukimwi halichagui mwenye nacho au asiye nacho ukicheza unahatarisha maisha hivyo ni vyena mjihadhari nalo ili muweze kufikia malengo,"alisema.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa benki hiyo inachangia  kwa kutambua asilimia moja ya faida wanayoipata kwa mwaka kwa sekta zinazopewa ikiwemo elimu na afya.

Pia alisema benki hiyo itaisaidia shule hiyo milioni 2.5 kwa ajili ya kuboresha mfumo wa maji safi.
 Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Robert Kessy alisema wanafunzi wanaohitimu katika mahafali hayo ya 22 ni 558.

Alisema wamewalea wanafunzi hao  katika maadili mazuri pamoja na kuwafundisha nyezo zote hivyo wanatarajia kwamba watafanya vizuri na kuwa mabalozi wazuri katika jamii.


Mmoja ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo Hamisa Athumani aliipongeza shule hiyo kwa kufundisha masomo ya ukakamavu kwani yamewajengea uwezo wa kujiamini na kuwa na nidhamu. 

CHAMA CHA UDP CHAPATA PIGO VIGOGO WAKE WAWILI WAKIMBILIA CCK

April 24, 2016
 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akiwapokea waliokuwa viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama chama ambao ni  Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi  Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi mbele ya waandishi wa habari.
 Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK. 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam, Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya aliyehamia chama hicho.


Na Dotto Mwaibale


CHAMA cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa, John Momose Cheyo, kimepata pigo baada ya wenyeviti wawili wa mikoa ya Mtwara na Dar es 
Salaam kukihama na kujiunga na Chama Cha Kijamii (CCK).

Viongozi waliokihama chama hicho ni  Salum Makunganya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara,  Mkurugenzi wa Uchaguzi  Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmshauri Kuu, Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa 
habari.

Wenyeviti hao baada ya kujitoa walikabidhi kadi zao za UDP kwa Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi ambaye naye aliwakabidi kadi ya CCK na kuwatangaza rasmi  kuwa wanachama wa chama hicho.

Makunganya alikabidi kadi yake ya UDP yenye namba 4544 na kukabidhiwa ya CCK namba 1597 huku Mwakitiga akibidhi kadi yake ya UDP namba 2852 na kukabidhi ya CCK yenye namba 01599 katika tukio lililofanyika ofisi za CCK.

Wakizungumzia sababu zilizowafanya wajitoe UDP walisema ni kutokana na chama hicho kutokuwa na mwelekeo wa kimaendeleo ambacho kwa zaidi ya miaka sita viongozi wake wa kitaifa hawajaitisha mikutano ukiwamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.

Walisema sababu nyingine ni kwamba viongozi wa kitaifa wa UDP wamekigeuza chama hicho kama kampuni binafsi ambapo wamekuwa wakitoa maamuzi mbalimbali ambayo hayajaamuliwa na wanachama kwenye vikao .

“Nyie waandishi si mnaishi Dar es Salaam tangu lini mlishaona Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo akiitisha hata mkutano wa hadhara hapa Dar es Salaam kuzungumzia mambo mbalimbali ya chama na taifa kwa ujumla kama vinavyofanya vyama vingine…jibu ni hakuna, UDP inabuka tu wakati wa uchaguzi na tena kwenye eneo moja tu,”alisema Mwakitiga.

Muabhi akizungumza baadhi baada ya kuwakabidhi kadi wenyeviti hao alisema CCK inawapokea kwa mikono miwili viongozi hao na kwamba wakiwa ndani ya chama hicho wataona utofauti na vyama vingine kwa kuwa chama kimejiwekea misingi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Muabhi aliitaka serikali kulitazama upya suala la vikao vya Bunge kutotangazwa kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo kunawanyima haki wananchi ya kupata habari na hivyo kushindwa kujua nini kinaendelea Bungeni.

“Serikali ijitathimini, wananchi wasipojua nini kinaendelea Bungeni kuna haja gani kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenda Bungeni, wananchi watajuaje kama wawakilishi wao wamezifikisha kero zao serikalini,”alisema.

Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma, alisema ujio wa wanachama hao wapya ambao ni wakongwe katika siasa na hivyo CCK itajifunza mambo mengi kutoka kwao.

MATUKIO YA PICHA BAINA YA COASTAL NA YANGA KOMBE LA FA

April 24, 2016


 Wachezaji wa Coastal Union wakiruka juu kuondoa hatari langoni mwao wakati wa mchezo wa FA uwanja wa Mkwakwani leo.
 Kiungo wa Coastal Union ya Tanga, Abdulhalimu Humuod, akiruka juu kugombea mpira wakati wa mchezo wa FA uwanja wa Mkwakwani Leo.

 Washabi wa Yanga wakiishangilia timu yao jana wakati ikimenyana na Coastal Union kombe la FA uwanja wa Mkwakwani Leo.

WAZIRI MUHONGO ATUA JIJINI DAR JIONI HII AKITOKEA NCHINI UGANDA KUKAMILISHA DILI LA BOMBA LA MAFUTA

April 24, 2016


 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kati) akiwasili jijini Dar es salaam jioni hii, akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akionyesha kwa wanahabari, mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda mpaka Jijini Tanga, mara tu baada ya kuwasili nchini akitokea jijini Kampala. Mbali na kunufaika kwa Watanzania kupitia Mpango huo, pia utazinufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio walipokuwa wakimsubiria Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alierejea jijini Dar es salaam leo akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga. 

RC . MONGELLA ATOA SAA 24 KOMPUTA ILIYO IBWA IPATIKANE

RC . MONGELLA ATOA SAA 24 KOMPUTA ILIYO IBWA IPATIKANE

April 24, 2016



Na Mwandishi wetu Mwanza
Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa,kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyo ibwa usiku wa kuamkia April 22,2016 kwenye chumba kinacho tumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)
Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilicho fanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.
“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana,amesema Mongella na kuongeza ,sisi tunajua Nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo komputa hiyo.
Akizungumza kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri,kaimu mhazini wa halmashauri hiyo Baraka Munuo,alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe akimuelezea upotevu huo.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe,, kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo mkuu wa mkoa amedai linachangiawatumishi kufanyakazi kwa mazoea,”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu, haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana, alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.
Awali akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema wilaya imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa kimepiga kambi katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.
Mkuu wa mkoa wa yupo katika ziara yakujitambulisha na hii ikiwa ni wilaya yake ya saba,Mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe inakuwa wilaya ya saba huku akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye halmashauri za Buchosa na Sengerema yenyewe.(P.T)

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA CHUO CHA KILIMO FAFU CHINA

April 24, 2016

Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwa pamoja na uongozi na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma chuo cha Kilimo na Misitu FAFU.
Dkt Kikwete akiwa katika chuo cha Kilimo FAFU ambapo  alialikwa kutembea leo hii.
Waziri Mhe. Kairuki afungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi

Waziri Mhe. Kairuki afungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi

April 24, 2016

SONY DSC
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kufungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi uliofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Dkt.  Ndumbaro ni Mwenyekiti wa Baraza hilo.
SONY DSC
SONY DSC 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifungua  mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi uliofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
K3 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Mstari wa mbele katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe  wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi uliofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Picha na mpiga picha wetu