MATATIZO YA KIUFUNDI YAKWAMISHA SUPER WEEK ‘LIVE’

MATATIZO YA KIUFUNDI YAKWAMISHA SUPER WEEK ‘LIVE’

April 13, 2013
Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Mechi tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.

Kwa mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.

Mechi hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini Tanga.

 Tatizo hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya.

 Tshunungwa amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.

 Pia TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport watakuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa.

 MWISHO.

JK azindua barabara ya Tanga-Horohoro.

April 13, 2013
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho Kikwete akikapa utepe wa barabara ya Tanga-Horohoro leo wanaoshuhudia ni mkuu wa mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa,Mbunge wa Jimbo la Mkinga,Dastani Kitandula.Picha na Mwandishi Wetu,Mkinga.

Uzinduzi wa barabara ya Tanga-Horohoro

April 13, 2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dokta Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiriana uzinduzi wa barabara ya Tanga-Horohoro halfa hiyo iliyofanyika Kasera wilayani Mkinga,anayepo kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa,Picha na Mwandishi Wetu,Tanga.
JK awapiga vijembe wapinzani uzinduzi wa barabara

JK awapiga vijembe wapinzani uzinduzi wa barabara

April 13, 2013
Na Mwandishi Wetu,Mkinga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema licha ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi licha ya kuleta maendeleo kwa wananchi ikiwemoujenzi wa barabara bora ambazo wanazitumia lakini bado wanaibeze serikali iliyoko madarakani.

Hayo aliyeasema wakati akizindua mradi wa barabara ya lami ya Tanga Horohoro yenye urefu wa Km 65 katika eneo la Kasera kwenye wilayani Mkinga Mkoani Tanga, alisema wapinzani kazi yao ni kubeza maendeleo yanayofanywa katika nchi .

Alisema mwaka 2010 alipokuaja mkoani hapa kuomba kura aliwahakikishia wanachi kuwa mradi huo barabara utakamilika kabla ya kuondoka madarakani ambapo kwa wapinnzani ilikuwa ni vijembe kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa ni ndoto ujenzi huo kukamilika.

“Leo nazindua ujenzi wa barabara ambao umeshirikisha serikali ya Tanzania na na Marekani kupitia mfuko wake wa Changamoto za Milenia MCC,lakini yote haya wapinzani hawataona kuwa ni maendeleo bali mwenye nyoyo za korosho hawewezi kutusifia na kutupongeza”alisema Kikwete.

Hata hivyo alisema ujenzi huo uligharimu kiasi cha dola Bil 75.75 hadi kukamilika kwake kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa madaraja 11 na alama za barabara ikiwemo kingo na maenero ya waendakwa miguu .

Rais Kikwete alisema lengo la serikali ni kuunganisha mtandao wa barabara kuu nchi nzima kuwa za kiwango cha lami na zinazopitika katika maira yote ya mwaka ili kurahisisha usafirishaji pamoja na kuchangia kasi ya maendeleo katika nchi.

Nae Balozi wa Marekani Nchini Alfonso Lenhardts alisema kukamilika na kuzinduliwa kwa barabara hiyo kutasaidia fursa za biashara kati ya Tanzania na nchi za Kenya ,Msumbiji na Nchia ya Malawi na kuleta maendeleo kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hizo na taifa kwa ujumla.

Alisema serikali ya Marekani imetenga kiasi cha Dol Mil 698 kwa ajili ya kusaidia miradi ya barabara,nishati na mifumo ya maji ikiwemo kukarabati Km 435 za barabara nchi ili kuweza kuwa na mtandao wa barabara za lami.

“Watu wa Marekani kupitia Rais Barack Obama tunaifuvunia ufadhili huu kwqa ushirikiano na serikali ya Tanzania Kuchangia kuboresha mtandao wa barabara nchini Tanzania utakaovutua wawekezaji na kuchangia pato la taifa la nchi hii”alisema Balozi wa Marekani.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa alisema wananchi wa Tanga wataitunza barabara hiyo kwa kuhakikisha wanazingatia matumizi sahihi ya barabara ikiwemo kutoruhusu magari yenye uzito mkubwa pamoja kuchoma  moto kando ya barabara.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Patrick Mfugale alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua milango ya biashara katika nchi za Afrika ya Mashariki na kutawezesha wafanyabiashara kutumia bandari ya Tanga kwa ukamilifu.
Mwisho.