RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WAKAZI WA MANYONI NA IKUNGI AKIWA NJIANI AKIELEKEA MKOANI SINGIDA

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WAKAZI WA MANYONI NA IKUNGI AKIWA NJIANI AKIELEKEA MKOANI SINGIDA

July 29, 2016

mny1 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
mny2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Manyoni Mkoani Singida mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Singida.
mny5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Manyoni Mkoani Singida mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Singida.
mny7
mny9 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wakazi wa Singida mara baada ya kuwasili.
mny10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Manyoni mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
mny12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Manyoni mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
mny13 
Mbunge wa manyoni Magharibi Yahya Masare akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za asili cha Manyoni kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli kuhutubia mkutano katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
mny14 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ikungi waliomsimamisha wakati akielekea Mkoani Singida. PICHA NA IKULU
KATIBU MKUU TFF ATOA SABABU ZA AIRTEL KUIBUA VIPAJI

KATIBU MKUU TFF ATOA SABABU ZA AIRTEL KUIBUA VIPAJI

July 29, 2016
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amesema kutimia kwa malengo ya Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel imesukuma kampuni hiyo kuendelea kudhamini mashindano ya soka kwa vijana - wavulana na wasichana.
Selestine alisema hayo kwenye hafla ya kukabidhiana vifaa kwa Airtel kwenda TFF kabla ya kwenda kwa klabu shiriki iliyofanyika Ukumbi wa TFF, Dar es Salaam. Vifaa vilivyotolewa kwa timu jezi kamili ikiwa ni pamoja na jezi za waamuzi, viatu, mipira na vizuia ugoko kutopata madhara.

Alisema sababu hizo ni uhusiano mzuri kati ya TFF na Airtel inayotoa bora za mawasiliano kwa miaka sita sasa sambamba na kuendeleza vipaji kwani nusu ya wachezaji wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, wanatoka katika michuano hiyo ya mwaka jana.
Wachezaji hao ni  Ramadhani Awm Kabwili, Nickson Clement Kibabage, Dickson Nickson Job, Ally Hamisi Ng’anzi, Syprian Benedictor Mtesigwa, Mohammed Abdallah Rashid na Muhsin Malima Makame na Katibu Mkuu alisema: “Hawa wamepita Airtel. Tunashukuru Airtel kwa kuingia katika zonal (ukanda) ambao wengi hawapendi kuingia.”
Selestine alisifu Airtel akisema imejitofautisha na taasisi nyingine na kuamua kwenda shambani au jikoni kulima au kupika chakula ambacho leo tunajivunia kuwa na kikosi bora na imara cha Serengeti Boys ambayo wiki ijayo itakuwa na mtihani dhidi ya Afrika Kusini.
Rai wa Karibu Mkuu, Selestine ni kwa viongozi kuratibu vema mashindano ya Aitel msimu huu kwa kufuata kanuni ambazo zilijadiliwa na kupitishwa mara baada ya kuzindua mashindano hayo. “Kama viongozi mmeingia kwenye mashindano haya na hujafuata au hujui kanuni ujue tu umejiandaliwa kushindwa.”
Kadhalika aliwataka wazazi na walezi kuwatia shime wachezaji ili wafanye vema kwenye michuano hii ili siku moja waingie kwenye ajira ya soka wakitokea mashindano ya kuibua vipaji ya Airtel. Pia alitaka wajitokeze kwa wingi kwenye mashindano hayo yatayosimamiwa na kuendeshwa na TFF katika mikoa mbalimbali.
Mikoa ambayo itazindua Mashindano hayo ni pamoja na Mbeya, Mwanza, Morogoro, Ilala, Kinondoni na Temeke kwa upande wa wavulana wakati wasichana mikoa iliyoteuliwa ni Lindi, Zanzibar, Arusha na Ilala, Kinondoni na Temeke.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

July 29, 2016


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhan Feruzi (katikati) ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Said Mohamed mkazi wa Mafia ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Mkazi huyo wa Mafia alimueleza Makamu wa Rais juu ya ugumu wa upatikanaji wa Dawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Bi. Maria Maliseli Boniface wa Kilosa Morogoro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Calist P. Mushi mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo (kulia) wakati wa kutembelea Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na wananchi waliokuja kuwaona ndugu na jamaa zao ambao wamelazwa  katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Wananchi hao walimueleza Makamu wa Rais haja ya kuongezwa kwa mashine za mionzi suala ambalo Makamu wa Rais aliwajibu kuwa zitafungwa mashine mpya mbili katika mwaka huu wa fedha 2016-2017 ilikurahisisha matibabu.

...................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa serikali  itanunua mashine mbili za kisasa za mionzi kwa ajili ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kupata matibabu katika Taasisi hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulu Hassan ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara fupi ya kutembelea Taasisi ya Saratani ya Ocean Road pamoja na Kumtembelea na kumpa pole Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhani Feruzi ambaye anapatiwa matibabu kwenye Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa mkakati uliopo wa serikali unalenga kuhakikisha kuwa hali ya utoaji wa huduma za afya na dawa kote nchini unaimarika maradufu ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwenye maeneo yao kwa ubora unatakiwa.
Kuhusu uhaba wa wahudumu wa afya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameuahidi uongozi wa Taasisi hiyo kuwa serikali itahakikisha wahudumu hao wanapatikana katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

 Baadhi ya wagonjwa na wananchi wamepongeza utoaji wa tiba katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na wameomba serikali iendelee kuipatia taasisi hiyo vifaa vya kisasa vya kutolea tiba kama hatua ya kuboresha utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu ya saratani.
MAKONDA, MALINZI KUPAMBA UZINDUZI AIRTEL RISING STARS KESHO

MAKONDA, MALINZI KUPAMBA UZINDUZI AIRTEL RISING STARS KESHO

July 29, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho Jumamosi Julai 30, 2016 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya kuibua na kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya Barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
Sambamba na Makonda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi naye amethibitisha kuwako kwenye hafla hiyo ambayo mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za Ilala Boys dhidi ya Bombom Ilala, Dar es Salaam. Inawakilishwa na mikoa yote mitatu kisoka ambayo ni Ilala, Kinondoni na Temeke kwa pande zote mbili za wavulana na wasichana.

Kadhalika, wakuu wa mikoa mingine ambayo mashindano hayo yatafanyika nao watakuwa wageni rasmi katika mikoa yao ambayo ni Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana pia Arusha, Lindi na Zanzibar kwa upande wa wasichana.

MAALIM SEIF KUONGEA NA WATANZANIA BOSTON

July 29, 2016
Zanzibar Diaspora Association inapenda kuwaalika kwenye mkutano wa hadhara utakao fanyika Siku ya Jumamosi July 30th -
MAHALI: 42 Charles St Boston
MA 02122.
MDA: Kuanzia 5:pm mpaka 7:pm
Mgeni rasmi ni Katibu mkuu wa CUF. 
Maalim Seif Shariff Hamad
Nyote mnakaribishwa

Ratiba ya Usaili Maisha Plus East Africa 2016

July 29, 2016
Baada ya Usaili kufanyika kwa kishindo katika mikoa ya Mtwara na Dar es salaam usaili wa Maisha Plus unaendelea katika mikoa mingine ndani ya Tanzania. 
30/07/2016 - MBEYA - Ukumbi wa City Pub 
31/07/2016 - IRINGA - Savanna Garden 
02/08/2016 - DODOMA - Matei Lounge 
04/08/2016 - MWANZA - Rock Garden 
06/08/2016 - ARUSHA - Via Via
 13/08/2016 - ZANZIBAR - Ngome Kongwe 


Vijana wote wenye umri wa miaka 18 - 26 wanakaribishwa kujitokeza kwa wingi. Elimu na ujuzi ni kiwango chochote. Zawadi kwa mshindi ni Tzshs. Milioni 30. Fomu zinapatikana BURE kabisa kupitia www.maishaplus.tv na katika maeneo tajwa hapo juu. 

 Maisha Plus East Africa 2016 | #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
   

 Bofya hapa chini kuona video 33 fupi za usaili wa Maisha Plus Dar es salaam.

Tigo yadhamini mkutano wa wadau wa simu duniani (GSMA)

July 29, 2016
Mkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Diego Gutierrez (kushoto) akijibu swali wakati wa mahojiano kwenye mkutano wa wadau wa Makampuni ya simu Duniani (GSMA) wanaokutana jijini Dar es Salaam.


  1. Mkuu wa kitendo cha masoko wa kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo Tanzania Olivier Prentout (kulia), akizungumza na Emmanuel De Dinechin ambaye ni mshiriki mwenzake wa mkutano wa wadau wa Makampuni ya simu Duniani (GSMA) wanaokutana jijini Dar es Salaam.


  1. Head of B2B wa Kampuni ya Tigo Tanzania Rene Bascope (kulia), akizungumza na washiriki wenzake  wa mkutano wa wadau wa Makampuni ya simu Duniani (GSMA) wanaokutana jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Peter Maver na katikati ni Riyaz Shak.

Afisa Biashara mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Shavkat Berdiev akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuhutubia mkutano wa wadau wa makampuni ya simu duniani (GSMA) unaofanyika nchini.

Wadau wa habari wakiwa katika banda la Millicom ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania.

photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com