JK KUKABIDHI KIJIKI LEO KWA DKT JOHN POMBE MAGUFULI

July 23, 2016



 Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete,akifafanua jambo wakati akisoma hotuba yake ya Mwisho katika kiti hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete.

Sehemu ya Meza kuu kama ionekanavyo pichani tayari wamekwisha ingia ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Rais Dkt Shein pamoja na Mwenyekiiti mtarajiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.PICHA NA MICHUZI JR -DODOMA.
 Viongozi wakuu wa Wastaafu wa chama cha CCM na Serikali kwa ujumla wakifuatilia yanayojili ukumbini .
 Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mwenyekiti ambaye leo anaachia kiti hicho na kukabidhi kwa Mwenyekiti mpya Dkt John Pombe Magufuli,katika mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC),mkoani Dodoma





Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa ratiba na miongozo mbalimbali kwa Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao tayari wako ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.
Mwanana mahiri wa nyimbo za Taarab kutoka kundi la Tot Plus Khadija Kopa akiimba mbele ya Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao tayari wako ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka vyama mbalimbali vya upinzani pia wanahudhuria mkutano huu Maalum wa CCM.Ambapo vyama vya siasa vipatavyo 12 vilialikwa na vyote vimefika katika mkutano huo isipokuwa chama cha CHADEMA.
Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM wakiwa tayari ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.

MAMBO YAMENOGA MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM MJINI DODOMA

July 23, 2016
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia), akiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Igoma Jijini Mwanza, wakiwa katika Viunga vya Ukumbi mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma wa Dodoma Convetional Centre ambapo Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unafanyika.

Ni Mkutano Maalumu kwa ajili ya Wajumbe hao kumchagua Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa, ambapo jana Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM walipitisha kwa kura zote jina la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa chama hicho. Dkt.Magufuli anapokea kijiti cha uongozi wa chama kutoka kwa Rais Mstaaf wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

Mji wa Dodoma umegubikwa na shamra shamra mitaa yote na tayari wajumbe wa Mkutano Mkuu wameanza kuingia Ukumbini kwa ajili ya Mkutano huo huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa vyema kila kona.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akisalimiana na mjumbe mwenzake wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma hii leo
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (kushoto) akiwa na Katibu wake, Heri James, Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma hii leo
Heri James (kushoto) akiwa na mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, wakisalimiana ukumbini.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (kushoto), akiwa ukumbini na mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM.
Kaimu Katibu wa CCM mkoani Mwanza Elias Mpanda (kulia) akisalimiana na aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Manju Msambya (kushoto).
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka mkoani Mwanza
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM akiwemo Le Mutuz (kulia) wakiperuzi taarifa mbalimbali kuhusiana na Mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akitoa burudani na Bendi ya TOT Pus
Ni burudani kutoka kwa bendi ya TOT Pus Ukumbini
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akitoa mwongozo wa kuanza kwa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma.
Taswira Ukumbini