KAGERA SUGAR YAIBUKA MSHINDI WA 1-0

September 13, 2015


Kikosi kazi cha Timu ya Mbeya City fc kikiongwozwa na Gorikipa mahiri Juma Kaseja katika picha waki mwomba Mwenyezi munu kabla ya kuanza Mtanange, ambapo Kagera Sugar iliibuka mshindi kwa kuitundika Mbeya City fc Gori Moja kwa bila (1,0) Dakika ya 41, Mchezaji Poul Ngaiyoma Jezi Nambari 8, Mgongoni kuipatia ushindi Timu ya Kagera Sugar katika Mechi ya Kwanza Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mtanange ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mtanange ukiendelea katika Uwanja wa Kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya ambapo Kagera Sugar iliibuka kidedea kwa Gori moja kwa Sifuri (1,0) Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.
Juma Kaseja Jezi Nambari Moja Mgongoni akiwa makini Lango la Mbeya City katika Mtanange wa Mbeya City fc na Kagera Sugar, ambapo Kagera Sugar iliibuka kidedea kwa Gori moja kwa Sifuli (1,0).
Mashabiki wa Mbeya City fc wakishangilia katika Mtanange uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kagera moja huku Mbeya City fc Mama kajabwela Tumbo kamsokota Tumbaku Bilaaa..

WATENDAJI WA SEKTA YA AFYA WATAKIWA KUBUNI VYANZO VYA MAPATO

September 13, 2015


Na Beatrice Lyimo – Maelezo
12/09/2015
 SERIKALI imewataka Serikali imetoa  changamoto kwa watendaji wote  afya  wa halmashauri ,mikoa wilaya kuhakikisha wanabuni mbinu mpya na  kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza kuendelea kuboresha huduma za sekta ya afya nchini.
 
Aidha Serikali pia imewataka watendaji wa Idara ya Ustawi wa Jamii, kujumuisha suala la kutatua tatizo la watoto yatima kwa kuweka  katika mipango  ya sekta hiyo.
 
 Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati akifunga mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.  
 
“Kila mmoja  anapaswa kusimamia vyanzo vya mapato, misaada na bajeti ya Serikali haikidhi mahitaji kwa asilimia 100. Tunapaswa kusimamia kwa ukamini na ukamilifu suala la mapato katika vituo vya afya. Tusipotekeleza wajibu wetu ipasavyo tutawajibika kwa hili tutawajibika kwa Watanzania na hata kwa Mwenyezi Mungu,” alisema Dkt. Mmbando.
 
 Aliongeza kwamba hili kuweza kufanikiwa   vema katika masuala hayo wanapaswa kuwa makini katika kutoa maelekezo kwa kuzingatia sera, taratibu, miongozo na mikakati rasmi  ya Sera ya Afya ya mwaka 2007.
 Aliwataka watendaji hao, kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kuwasiliana na uongozi wa wizara.Pia kutumia uzoefu walioupta katika mkutano huo.  
   
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dkt. Deo Mutasiwa alisema watendaji hao kuongeza kasi ya utendaji kazi ili kuweza kukabiliana na matatizo ya sekta ya afya nchinina kufanikisha malengo ya milinea(MDG’s), mkakati wa awamu ya nne wa afya, kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na mamawajawazito, kutoa elimu juu ya masuala ya lishe kwa jamii.

TPA YASIFU BENKI KUONGEZA MUDA WA KAZI

September 13, 2015


 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo Benki Kuu, Bw. Bernard Dadi (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza rasmi mabenki kufanya kazi kwa muda wa nyongeza kuwawezesha wateja wa bandari na wadau wengine kufanya malipo hadi saa 2 usiku kwa siku za kazi na saa 8 kwa siku za mwisho wa wiki na sikukuu.  Wengine ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (wa pili kushoto), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire (wa pili kulia) na Kamishna wa Forodha wa TRA, Bw. Tiagi Kabisi (kulia). Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ufanisi bandari hiyo.
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akielezea jambo kwa kundi la waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo kuona maendeleo ya utekelezwaji wa miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa Matokeo Makubwa Sasa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Inatarajiwa kuwa baada ya kukamilika, miradi hiyo itaongeza uwezo na ufanisi wa bandari hiyo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo Benki Kuu, Bw. Bernard Dadi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza rasmi mabenki kufanya kazi kwa muda wa nyongeza kuwawezesha wateja wa bandari na wadau wengine kufanya malipo hadi saa 2 usiku kwa siku za kazi na saa 8 kwa siku za mwisho wa wiki na sikukuu.  Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ufanisi bandari hiyo.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeelezea kuridhishwa kwake na uamuzi wa serikali kuruhusu rasmi nyongeza ya muda wa kufanya kazi kwa benki hapa nchini na kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam.

Hatua hii inakuja baada ya serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuruhusu kutumika kwa mfumo wa huduma baina ya taasisi za kibenki (TISS) hadi saa 2 usiku na hivyo kuwezesha wateja kufanya malipo na kuendelea na taratibu nyingine katika bandari hiyo bila tatizo.

Mfumo huo umeunganishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara ya Fedha ili kuwezesha malipo mbalimbali kama kodi kuweza kulipwa katika muda huo wa nyongeza.

Kaimu Meneja wa bandari hiyo, Bw. Hebel Mhango amesema jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa mfumo huo utaisaidia mamlaka hiyo na wadau wengine kwa kiwango kikubwa kwa kuwa utasaidia kuendana na mpango ulioanzishwa bandarini wa kufanya kazi kwa saa 24.  

Aliwakumbusha watumiaji wa bandari hasa wakala wa mizigo kuwa mfumo huo mpya unalenga kuwasaidia kuokoa muda, gharama na hivyo kuongeza ufanisi katika biashara zao.

“Tunaomba sasa wadau wengine wajitahidi kuendana na kasi ya bandari kwa kufanya pia kazi kwa muda wa saa 24. Tutaendelea kuhamasisha wadau wetu kuhusiana na mfumo huu mpya,” alisema.

Akizungumza awali, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire alisema serikali imeamua kuongezamuda wa utendaji kazi kwa mabenki ili kuruhusu wateja na wadau kulipia kodi zao hadi saa 2 usiku.

Alisema mbali na utekelezaji wa mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya uchukuzi, hatua hiyo pia itarahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali na huduma ya mizigo.

Kwa mujibu wa takwimu, muda wa miezi sita ya majaribio iliyopita, mfumo huo umeonyesha mafanikio makubwa.

“Miezi 6 ya kipindi cha majaribio ya mfumo huu, jumla ya miamala 7,727 yenye thamani ya Tshs 382 bilioni ilifanyika,” alisema.

Alisema serikali itaendelea kutekeleza miradi ya BRN katika kuifanya bandari kuwa kivutio cha nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

“Wadau wote wa bandari watumie fursa hii kuleta ufanisi katika kazi zao,” alisema.

Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo BoT, Bw. Bernard Dadi alisema benki hiyo imeruhusu malipo kufanyika hadi saa 2 usiku kwa siku za kazi na kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana mwisho wa wiki na siku za sikukuu.

“Ni vyema benki zikazingatia muda huu mpya badala ya ule zamani ambapo malipo kama hayo yalirusiwa kufanyika hadi saa 7 mchana,” alisema.

Kamishna wa Forodha wa TRA, Bw. Tiagi Kabisi alisema mamlaka hiyo inakubaliana na muda huo wa nyongeza kwani utasaidia katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.

“TRA pia imeongeza masaa ya kuhudumia wateja wake ili kuendana na kasi ya maboresho ya bandari yanayoendelea,” alisema.
NAPE AKUTANA NA MAMA SAMIA LINDI

NAPE AKUTANA NA MAMA SAMIA LINDI

September 13, 2015

7
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipowasili mpakani mwa mkoa wa Pwani na Lindi wakti akiwasili wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Septemba 12, 2015. Nape pia ni Mgombea wa Ubunge jimbo la Mtama mkoani Lindi.
8
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijadiliana jambo ma Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hasaan alipowasili kufanya mkutano wa kampeni jimbo la Kilwa Kaskazini Septemba 12, 2015. Nape pia ni Mgombea wa Ubunge jimbo la Mtama mkoa wa Lindi.
1
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgombea Ubunge jimbo la Rufiji Mohammed Mchengerwa wakati wa mkutan wa kampeni uliofanyika Sepemba 12, 2015 katika jimbo hilo.
2
Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Rufiji Dk. Seleman Rashid akiteta jambo na aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga Adam Malima, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mama Samia katika jimbo la Rufiji septemba 12, 2015.
6
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 12, 2015, Ikwiriri, Rufiji mkoa wa Pwani.
4
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akionyesha kadi za CUF na Chadema, alizopokea kutoka kwa wanachama wa vyama hivyo waliohamia CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika Ikwiriri, Rufiji mkoa wa Pwani, Septemba 12, 2015.
3 
Bibi Mwanahawa Saidi akitangaza kuhama CUF kurejea CCM, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika septemba 12, 2015, Ikwiriri Rufiji mkoawa Pwani.
5  
Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa CCM, uliofanyika septemba 12, 2015, Ikwiriri, Rufiji mkoa wa Pwani.
(Picha zote na Bashir Nkoromo)
Rais Kikwete akimkabidhi zawadi ya gari Jenerali Sarakikya

Rais Kikwete akimkabidhi zawadi ya gari Jenerali Sarakikya

September 13, 2015

unnamed 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi ya gari Mkuu wa Majeshi wa kwanza Mzalendo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa jeshi katika chuo cha Momduli Septemba 12, 2015.  Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.Jenerali Sarakikya amekabidhiwa zawadi hiyo kwa kutambua mchango wake mkubwa kwa kujenga misingi imara ya jeshi la Wananchi wa Tanzania lenye weledi na nidhamu ya hali ya juu.
(Picha na Freddy Maro)

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA Edward Lowassa- MJINI SINGIDA

September 13, 2015

 
Wananchi wa Mji wa Singida wakiishangilia Chopa iliyombeba  Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya M,uungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, akiwakilisha vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, , Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015 ambapo maelfu ya wananchi walifurika kumsikiliza mgombea huyo ambaye anasisitiza Mabadiliko ni lazima kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2mwaka huu.
(Picha na Othman Michuzi)
Wadau wa Singida wakitafuta namna ya kupata taswira ya Mgombea wao, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye wakiwapungua wananchi wa mji wa Singida, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mabango yenye jumbe mbali mbali kwenye Mkutano huo.
Mkali wa Propaganda, Tambwe Hizza akisema yake kwenye Mkutano huo.
Mke wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia wananchi wa mji wa Singida leo.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akimuonyesha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, mfano wa funguo wenye ujumbe, aliopewa na wananchi wa Singida, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa UKAWA kupitia CHADEMA wa Jimbo la Singida Mjini, Mgana Msindai “CRDB”, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
 
 
 
JK AWATAKA WANASAYANSI WA DUNIA KUTAFUTA SULUISHO LA NYAYO ZA LAETOLI

JK AWATAKA WANASAYANSI WA DUNIA KUTAFUTA SULUISHO LA NYAYO ZA LAETOLI

September 13, 2015

188 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikiwete akiweka jiwe la msingi katika jengo la kitega uchumi linalomilikiwa na Mamlaka ya hifadhi ya Bonde la Ngorongoro lililopo mjini Arusha.
………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Raisi Jakaya Kikwete amewataka wanasayansi wa dunia kutafuta suluhisho la nyayo za Laetoli kwani ni ufumbuzi pekee utakosaidia kuweka kumbukumbu sahihi ya mwanadam wa kale na si kufukia eneo hilo bali kuliendeleza ndio jawabu la msingi kwa kuwa hawajashindwa kufanya utafiti juu ya eneo hilo.
Kauli hiyo  aliitoa wakati akiweka jiwe la msingi la jengo la jakaya kikwete ngorongoro tower lililopo katikati ya jija la arusha litakalo kuwa kichocheo cha uchumi linalomilikiwa na mamlaka ya hifadhi za ngorongoro.
Raisi alisema kuwa ili uhifadhi wa mwanadam wa kale uendelee kuweza kuipatia mamlaka mapato lazimaWabuni njia ya kutolitegemea shimo la kreta pekee na waangalie namna watalii watangalia wanyama wakiwa nje ya shimo la kreta kwani shimo hilo pekee ni kivutio na bila kusahau historia ya mwanadam wa kale.
 Pia aliwataka kuangali suala la kuwapa changamoto wanasayansi wa dunia ni jinsi gani ya kuhifadhi nyayo za Laetoli zitakazosaidia kuweka sawa histori ya mahali hapo na ya mwanadam kwa eneo hilo ni urithi wa dunia na kila mkazi wa eneo hilo anatakiwa kujivunia na kutunza uhifadhi wake kwa historia ya baadae.
Aidha aliitaka mamlaka ya hifadhi za ngorongoro kuangalia ni namna gani wataweza kuisaidia jamii ya eneo hilo kufanya maisha mengine bila ya kutegemea kilimo kwani jicho la ulimwengu linaangalia eneo hilo kama eneo la urithi wa dunia unaosaidia uhifadhi.
“Ongezeni maeneo ya vivutio katika hifadhi yenu kama mgeni kuangalia wanyama akiwa nje ya kreta hii itasaidia kuvuta watalii wengi watakao kuja kutembelea hifadhi na kuongeza mapato”alisema Dk kikwete
Alisema kuwa pamoja na kuangalia eneo hilo alimuagiza mkurugenzi wa mambo ya kale kukaa na wanasayansi wa dunia kulipatia majawabu suala la laitolya kwani ufumbuzi wa kufukia eneo hilo si jawabu sahihi la kutunza historia ya eneo hilo.
Awali akimkaribisha Mh.Raisi, Naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud mgimwa alisema kuwa jengo hilo ni adhma ya mda mrefu ya mamlaka hiyo kuwa na kipato nje ya biashara ya utalii na kuwa jengo hilo limepewa jina la jk ngorongoro tower kwa kujua kuwa yeye ni Raisi ni mhamasishaji wa utalii kwa kuutangaza duniani kote alipotembelea
Alibainisha kuwa usanifu wa jengo hilo umeangalia wanyama kwani mbele na juu kuna pua ya tembo na juu pembe za nyati ikiwa ni ishara ya kutangaza utalii na kuipatia mamlaka hiyo mapato nje ya biashara ya utalii.
Naye  mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka balozi Mwanaid maajar alisema kuwa 
 jengo hilo litakalo kuwa na ghorofa15 litakapokamilika litagharim bilioni 42 za kitanzania na linajengwa na kampuni ya kichina ya Catic International Engineering na kuweza kutoa ajira kwa wakazi wa jiji la arusha na ni kichocheo cha maendeleo kwa wakazi hao.alisema kuwa jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwakani mwezi november nalitasaidia kuongeza mapato mamlaka hiyo na kuwa wazo hilo lilibuniwa na bodi iliyopita mwaka 2010 na ujenzi wake kuanza miezi miwili iliyopita na hadi sasa ujenzi upo ghorofa ya tatu.

Rais Kikwete atunuku kamisheni kwa maafisa wapya WA JWTZ

September 13, 2015
2
Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Jakaya Mrisho akiwa katika gari maalum la wazi na Mkuu wa Chuo cha maafisa wa Jeshi(TMA) Monduli akiingia katika uwanja wa paredi tayari kwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi Septemba 12, 2015.
(Picha zote na Freddy Maro)
1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride muda mfupi kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa wapya wa Jeshi katika Chuo cha Jeshi Monduli Septemba 12, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipoka heshima katika uwanja wa paredi.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange(kushoto) na Mkuu wa Chuo Meja Jenerali Paul Masao wakiangalia gwaride rasmi la kuhutimu maafisa wapya waliopatiwa kamisheni zao. 
6
Maafisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe za kutunukiwa kamisheni kwa maafisa hao wahitimu kwenye Chuo Cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi, (TMA) Monduli mkoani Arusha Septemba 12, 2015.
5
Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika Cho cha Jeshi(TMA) Monduli Mkoani Arusha Septemba 12, 2015.
11
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiiangalia picha ya kuchora ya Mkewe Mama Salma Kikwete aliyoipokea kwa niaba yake.
9
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkabidhi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya picha akiwa katika gari la wazi katika sherehe za awali chuoni hapo, na kitara pamoja na nembo maalum ya jeshi kwa kutambua mchango wake katika kuliboresha na kulifanya la kisasa Jeshi la Wananachi wa Tanzania wakati wa Sherehe za kutunuku l\kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli Septemba 12, 2015.
10
8    4
Amiri Jeshi Mkuu Rasi Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa akimpa zawadi afisa mwanafunzi bora wa kike Luteni Usu Martina James Shija  wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo hca jeshi Monduli.
3 
4-D92A3192

WATENDAJI WA SEKTA YA AFYA WAASWA KUKABILIANA NA KIPINDUPINDU

September 13, 2015


  Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Deo Mutasiwa asisitiza jambo jana jioni  wakati wa ufungaji wa mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando na  wakipongezana mara baada ya kumaliza   jana jioni mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.
Picha namba 3367 ni Baadhi ya wanganga wakuu wa mikoa na wilaya wakiwa katika  huo.
Na Magreth Kinabo
 SERIKALI imewataka watendaji wote  afya  wa halmashauri ,mikoa wilaya  kusimamia suala la usafi wa mazingira ilikuizesha jamii kuepukana na matatizo ya milipuko ya magonjwa likiwemo suala la ugonjwa wa kipindupindu.
 
 Aidha Serikali pia imewataka watendaji hao, kuanzisha siku maalum ya usafi katika maeneo wanayotoka.
 
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati akifunga mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.  
 
“Ni lazima tuwe na utaratibu huu mpya kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)  vyombo vya habari ili kuweza kutatua tatizo hilo,” alisema Dkt. Mmbando.
 
 Aliongeza kwamba watendaji hao watakiwa kutoendelea kuruhusu vyakula kusafirishwa katika maeneo ya wazi, madimbwi ya maji machafu, usimamizi wa huduma za afya ufanyike ipasavyo.
 
“ Tusimamie mpango wa utekelezaji wa elimu ya afya mashuleni, likiwemo suala la vyoo ambalo limepewa walimu maalum wa kusimamia ,hivyo zamani tulikuwa tunakaguliwa kuhusiana na usafi wa mwili mashule mafano kuoga nna kuchana nyewele pia  kuweka  yanayotunguzuka kuwa safi mazingira. Turudi katika misingi hiyo tuaondokana na matatizo ya afya,” alisisitiza.
 
 Dkt. Mmbando alisema kanuni na miongozi ipi ya kutosha hivyo, watendaji hao wanapaswa kuongeza kasi ya utendaji kazi na kushirikiana kwa pamoja katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza na kuambukiza ili kuweza kuiwezesha sekta ya afya kupata mafanikio makubwea zaidi katika kufikia malengo ya milinea(MDG’s ).
 
  Aliongeza kwamba Mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu umetokea katika mikoa ya Dares Salaam, Morogoro na Pwani  na unatokana na tatizo la kutozingatia , misingi ya usafi wa mazingira   husasan kwenye vinywaji, vyakula na mazingira yasiyosafi.