MAKAMU WA RAIS KUONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA

March 15, 2018
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kamati ya Harambee hiyo, Hassan Msumari na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamis Mgoda. Imeandaliwa na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog;0715264202,0689425467


Na Mwandishi Wetu

MAKAMU  wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.


Akizungumza katika mkutano na wanahabari, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema kuwa hafla hiyo itakayoanza leo Ijumaa saa 12 jioni  kwenye Hoteli ya Golden Tulip ya Masaki, Dar es Salaam itaambatana na chakula cha usiku kwa wageni waalikwa.

Hivi sasa Wilaya hiyo haina Hospitali ya Wilaya na wananchi wanaohitaji huduma za afya wamekuwa wakitumia hospitali teule ya Kanisa la Anglikana ambayo imeingia mkataba na Serikali na kutokana na idadi ya wananchi wa wilayani hapo hospitali hiyo imezidiwa.

Hayo yamesemwa leo na Mhandisi Tumbo wakati akizungumzia harambee ya kuchangisha fedha inayotarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.

Mhandisi Tumbo amesema kutokana na Wilaya ya Muheza kutokuwa na Hospitali ya Wilaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974, wananchi wamekuwa wakiteseka pindi wanapohitaji huduma za afya na hivyo wakaamua kuchanishana fedha ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo.

Amefafanua tayari wananchi na wadau wa maendeleo wilayani Muheza mkoani Tanga na Watanzania kwa ujumla wameanza kuchingiaa ujenzi huo na hadi kukamilika kwake zinahitajika fedha Sh.bilioni 11.1, hivyo wakati wakisubiri fedha za Serikali Kuu na zile za kwenye bajeti wameamua kuanza kwa kuchangisha fedha hizo.

"Kesho tutakuwa na harambee itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni ambapo wananchi wa Wilaya ya Muheza wanaoishi Dar es Salaam pamoja na watanzania wengine tunaomba wajitokeze kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya.

"Mgeni rasmi kwenye tukio hilo la harembee ya kuchangisha fedha atakuwa Makamu wa Rais ,Mama Samia Suluhu Hassan. Kwa wachangiaji ambao tumewapa kadi ya kuja kwenye harembee hiyo kila mchangiaji atachangia kuanzia Sh.milioni moja kwa walio na kadi.Na wote ambao tumewaalika kesho wana kadi za mualiko,"amsema.

Amefafanua kwa wale ambao wanahitaji kadi ni vema wakawasiliana naye kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi ya 0713 341937 ili wapatiwe kadi huku akifafanua pia mbali ya wale ambao watafika kesho kwenye harambee hiyo pia wameandaaa utaratibu mwingine wa kuchangia ujenzi huo.

Mhandisi Tumbo amesema ili kufanikisha ujenzi huo wanapokea mchango wa kiasi chochote cha fedha na hao wachangie kupitia Tigopesa au M-pesa kwa kutumia namba 395533 ambayo kumbukumbu namba ya kampuni ni 123.

"Tunatambua jitihada za Serikali katika kutatua changamoto kwenye sekta ya afya, na hasa Muheza lakini kwa upande wetu tumeamua kuanza kwa kuchangishana, wapo wanaotoa fedha, wapo wanaochangia kokote, mchanga , saruji na vifaa vingine vya ujenzi.Tumeanza vizuri kwani tayari msingi wa wadi ya akina mama na watoto umejengwa na lengo letu hadi Oktoba mwaka huu tuwe tumekamilisha ili wananchi wapate huduma za afya.

"Tukifanikiwa kuwa na Hospitali ya Wilaya Muheza mwananchi anayehitaji huduma za matibabu ya afya atakuwa na nafasi ya kuchagua aende kwenye Hospitali ya Anglikana au ya Wilaya.Niishukuru Hospitali ya Anglikana kutokana na kutoa huduma za tiba kwa wananchi wa Muheza,"amesema Mhandisi Tumbo.

Pia amesema wakati wanaendelea kutafuta fedha kujenga Hospitali ya Wilaya ya Muheza, wanaendelea na jitihada za kujenga zahanati na ujenzi huo unaendelea kwa kasi kutokana na wananchi kuhamasika kuchangia ili kuondoa changamoto ya uhaba wa zahanati za vituo vya afya.
 Baadhi ya waandishi wa habari walihudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya 
Golden Tulip katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Katikati ni Adam Ngamange Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), ambaye kwa asilimia kubwa alisaidia kuaandaa mkutano huo.
 Sehemu ya wanahabari hao
 Mkuu wa Wilaya, Tumbo akifafanua jambo ambapo aliwaomba wananhi kujitokeza kutoa michango kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo. Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Desderia Haule.
 Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza akijibu maswali ya wanahabari
 Wajumbe wa Kamati ya Harambe hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano na wanahabari kwenye Hoteli ya Golden Tulip, katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Juma Mgazija,  Mwenyekiti wa Kamati, Hamis Mgoda, Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Mwanasha Tumbo, Katibu Tawala wa Wilaya, Desderia Haule na Katibu wa Kamati, Hassan Msumari.

RATIBA YA NAMNA UNAVYOWEZA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA PASAKA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT

March 15, 2018




RC SHINYANGA AKAGUA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA WILAYA YA KISHAPU

March 15, 2018
                                 Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amekagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa miundombinu ya kituo cha afya Songwa pamoja zahanati ya Maganzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Katika ziara hiyo Telack alikagua ujenzi wa chumba cha upasuaji na maabara katika kituo hicho cha afya ambayo unaotekelezwa kwa fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB) sh. milioni 400.
Akiwa Songwa aliwapongeza wananchi kwa akujitolea katika shughuli za maendeleo umoja na kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha wanapata maendeleo katika maeneo yao ikiwa ni kuboresha huduma.
“Niwapongeza wananchi kwa kujitolea kushiriki shughuli za ujenzi na tumekuja hapa tumeona mmejitokeza kwa wingi kujenga kituo chenu siku. Siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu kazi itakwenda haraka na kwa muda mfupi kwa sababu ninyi mmeamua kusema kile kitu ni cha kwenu,” alisema.
Mhe. Telack aliwataka wananchi kuwapa ushirikiano watumishi wa afya ambao wanawahudumia na kutoa taarifa kwa viongozi wao endapo wanaona wanakwenda kinyume cha taratibu za kazi.
Pia aliwataka watumishi wasivunjike moyo kutokana na baadhi ya changamoto zinazojitokeza pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao huku akiwaahidi kuwa Serikali iko nao bega kwa bega.
Awali akiwasilisha taarifa ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba alisema huduma ya upasuaji katika kituo hicho cha afya itaanza baada  kukamilika  kwa majengo ya upasuaji.
Alisema Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi, Serikali Kuu na wadau mbalimbali wa maendeleo wanaendelea kujenga vituo vya afya na zahanati kwa kutenga fedha kwa ajili ya ukamilishaji.
Mhe. Taraba aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri imetenga jumla ya sh. 100,000,000 kwa ajili ya kukamilisha jengo la afya ya baba, mama na mtoto katika hospitali ya wilaya.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na watumishi pamoja na wananchi katika viwanja vya kituo cha afya cha Songwa alipofanya ziara kukagua mradi wa afya. Wengine pichani kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba na diwani wa kata ya Songwa, Abdul Ngoromole.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wananchi wanaojitolea nguvu kazi akiwa katika mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Songwa wilayani Kishapu.
 Sehemu ya watumishi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao viwanja vya kituo cha afya Songwa.
 Mganga mfawidhi wa zahanati ya Maganzo, Sam Phillip akitoa maelezo kuhusu kituo hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alipokitembelea.
 Wananchi wa kata ya Songwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack viwanja vya kituo cha afya Songwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na watumishi pamoja na wananchi katika viwanja vya kituo cha afya cha Songwa alipofanya ziara kukagua mradi wa afya.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akitoa taarifa ya wilaya kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na ujumbe kutoka mkoani alipowasili ofisini kwake tayari kwa kuanza ziara.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Peter Mwita akitoa maelezo kuhusu shughuli za afya katika zahanati ya Maganzo.

BODI YA WADHAMINI HOSPITALI YA MUHIMBILI YAZINDUA KAMATI MBILI, YAJIWEKEA MIKAKATI YA MIAKA MITANO

March 15, 2018


Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini (MNH), Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro wakati akizindua Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (katikati) akitambulisha viongozi na wajumbe wa Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Viongozi wa kamati ya Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu wakijitambulisha.
Viongozi wakifuatilia uzinduzi huo.
Kiongozi kutoka idara ya utawala bora, ofisi ya Rais, Ikulu kwa kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakitoa mafunzo elekezi na wawezeshaji kwa kamati zilizochaguliwa.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Ellen Mkondya-Senkoro (wa tatu toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa kamati mbili zilizochaguliwa.
Picha/Habari: Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.


BODI ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Menejimenti yake imejiwekea mikakati mbalimbali katika mpango mkakati wake wa miaka mitano kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2022 unaolenga kuimarisha utawala bora ambao ni muhimu katika utekelezaji wa mikakakati mingine inayolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Ellen Mkondya-Senkoro wakati akizindua Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Amesema pamoja na ueledi wa kazi, uadilifu katika utumishi wa umma ni pamoja na kutokuomba rushwa au kutoa rushwa wakati watumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao. "Hospitali ya Taifa Muhimbili inau
nga mkono mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa na mpango mkakati wa utekelezaji wa awamu ya tatu (2017-2022).

"Nina imani kwamba kamati hizi zitatekeleza majukumu yake ipasavyo kuhakikisha kwamba mkakati huu unatekelezwa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali," amesema Dk. Mkondya-Senkoro.

Ameongeza utawala bora ni pamoja na kuwepo kwa uadilifu wa hali ya juu katika taasisi ambao kawaida unasimamiwa na Bodi ya wadhamini na pia kuzingatiwa kwa ukaribu na viongozi watendaji na watumishi katika taasisi husika.

"Kwa mantiki hiyo, bodi ya wadhamini na Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na menejimenti yetu tumejiwekea mikakakati yetu ya miaka mitano na lengo kuu ni kuhakikisha tunaboresha huduma kwa wateja wetu ambao ni wagonjwa," amesema.

Amefafanua kamati ambazo wamezizindua leo ni kwamba ya kamati ya kwanza itakuwa ya uratibu ambayo itakuwa kamati ya uongozi itakayosimamia utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kudhibiti uadilifu katika hospitali hiyo.

Amesema kamati ya pili ni kamati ya kudhibiti uadilifu ambayo ndio itahusika na utekelezaji na mikakati ya kudhibiti uadilifu na kuziwasilisha taarifa zake katika kamati ya uongozi kwa hatua zaidi.

"Niwaambie kwamba wajumbe kamati hizi mbili wamepewa mafunzo elekezi na wawezeshaji kutoka idara ya utawala bora, ofisi ya Rais, Ikulu kwa kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

"Nina imani kubwa baada ya ya mafunzo kamati zitaweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo kama yalivyoanishwa kwenye mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa na mpango wa utekelezaji wa awamu ya tatu," amesema.

JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA

March 15, 2018
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ametoa miezi miwili kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuhakikisha linakamilisha uboreshaji wa jengo la abiria lililopo katika kiwanja cha ndege cha Dodoma ili kuwezesha jengo hilo kuhudumia abiria wengi zaidi kwa wakati mmoja.

Ametoa agizo hilo, mkoani Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa jengo baina na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) na NHC na kusema kuwa kukamilika kwake kutawezesha abiria zaidi ya 100 kuhudumiwa kwa wakati mmoja ambapo kwa sasa jengo linahudumia abiria 35.

“Mkataba tunaoshuhudia ukisainiwa leo unaitaka NHC kukamilisha mradi huu ndani ya miezi mitatu lakini niagize mradi huu ukamilike ndani ya miezi miwili kwa sababu fedha zipo na cheti mlichonacho cha daraja la kwanza kinaonyesha namna mnavyoweza kufanya kazi hii kwa haraka’ alisema Mhandisi Nditiye.

Aidha Naibu Waziri Mhandisi Nditiye ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), pamoja na maboresho hayo kuhakikisha inafanya maboresho kwa kujenga maduka ya kubadilishia fedha na bidhaa ili abiria watakaotumia kiwanja hicho hiyo waweze kupata huduma mbalimbali wakati wanaposubiria kupanda ndege.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Dodoma kwa sasa ndio Makao Makuu ya Serikali hivyo miradi yote inayotekelezwa chini ya Wizara lazima izingatie viwango na thamani ya fedha ili kuendana na hadhi ya mji.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Mheshimiwa Antony Mavunde ameipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi huo na kumuomba Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, kuwafikiria wananchi waliopisha upanuzi wa kiwanja hicho kwa kuwalipa fidia mapema.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamuhanga amesema Serikali inaendelea na mipango ya kuboresha viwanja vya ndege mbalimbali hapa nchini ili kurahisisha huduma za usafiri wa anga.

Ameongeza kuwa Serikali imepanga kujenga Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa katika eneo Msalato ambapo kwa sasa wataaalam wanapitia usanifu wa kiwanja hicho na wakati wowote zabuni itatangazwa ambapo kiwanja hicho kitaweza kuhudumia ndege kubwa za kisasa kwani kinatarajiwa kuwa barabara ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa Kilomita 4.5 mpaka 5.

Awali akitoa taarifa yake kabla ya utiaji saini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela, amesema kuwa Fedha zinazotumika kukarabati jengo hilo ni fedha za ndani za mamlaka hivyo jengo hilo litakamilika kwa wakati na viwango.

Uboreshaji wa jengo la abiria lililopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma utagharimu takribani kiasi cha shilingi milioni 600 na utahusisha mifumo ya kisasa ya Tehama, mifumo na maji taka , mifumo ya matangazi ya ratiba za ndege pamoja na mgahawa.

Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia), akioneshwa na Meneja Mradi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mhandisi Focus Kadege, jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Dodoma ambalo litafanyiwa uboreshwaji ili kuweza kuchukua abiria 100 kwa mara moja, Mkoani humo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamuhanga (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa kuboresha jengo la abiria katika kiwanja cha Ndege cha Dodoma.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Mavunde, akitoa hotuba katika hafla ya utiaji saini wa uboreshaji wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege Dodoma, Mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela (kushoto waliokaa) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi (kulia waliokaa), wakisaini mkataba wa uboreshaji wa jengo la abiria uliopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia), Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamuhanga (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (kulia), Felix Maagi wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya uboreshaji wa jengo la abiria uliopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma mara baada ya kusaini, Mkoani humo.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA SIGARA CHA MANSOOR INDUSTRIES LTD KILICHOPO KINGOLWIRA MOROGORO

March 15, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Sigara cha Mansoor Industries ltd kilichopo chini ya leseni ya Phillip Morris Tanzania katika eneo la Kingolwira mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Phillip Morris Tanzania Dagmara Piasecka akipiga makofi, wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe pamoja na Mmiliki wa kiwanda cha Sigara Mansoor Shanif Hirani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tumbaku inayotumika katika utengenezaji wa Sigara hizo za Marlboro mara baada kufungua kiwanda hicho cha Sigara mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mapakiti ya sigara hizo za Marlboro wakati akikagua utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mara baada ya kukifungua

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya hatua katika utengenezaji wa Sigara mara baada ya kufungua kiwanda hicho mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya vifungashio vya Sigara hizo kiwandani hapo mara baada ya kukifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Msanii mkongwe Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kuhutubia wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kutoa burudani ya mziki na kutangaza rasmi kuhamia katika Chama cha Mapinduzi CCM katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Chifu Kingalu Mwanabanzi wa Kabila la Waluguru wa Morogoro mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi waliofika katika kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.



Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akipongezwa na baadhi ya wananchi mara baada ya kuimba wimbo wake wa Mimi ni Msanii katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe mara baada ya kuzindua kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmiliki wa kiwanda hicho cha Sigara Mansoor Shanif Hirani mara baada kufungua kiwanda hicho. PICHA NA IKULU



Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa  Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro.






Mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa  Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro akichangiwa fedha na wadau mbalimbali mara baada ya kero yake kupatiwa ufumbuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.