*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA WATENDAJI WA WIZARA YA ELIMU ZANZNIBAR

April 18, 2014
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini  Zanzibar jana jioni.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi kwa kipindi cha robo mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana jioni, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

*WAUMINI WA DINI YA KIKRISTU WAHUDHURIA IBADA MAALUM YA IJUMAA KUU LEO KANISA LA KKKT

Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika wa Azania Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya Kuwambwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowasa akiwa katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT la Azania Front Dar es Salaam.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph wakiwa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo kanisani hapo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoriki,Mwadhama Porkap Kadinali Pengo akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo.
Waumuni wa Kanisa la Mtakatif Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa wanaubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mtoto, Vanes Mpupua akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mtakatif Josef Dar es Salaam.

Mmoja wa Watoto waliofika katika Kanisa la Mtakatif Josef akiubusu Msaraba wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliofanyika Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI MJINI UNGUJA KUFUNGUA KONGAMANO LA MUUNGANO KESHO.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort. Wa pili (kulia) ni mkewe Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

*WAUMINI WA DINI YA KIKRISTU WAHUDHURIA IBADA MAALUM YA IJUMAA KUU LEO KANISA LA KKKT

April 18, 2014

Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika wa Azania Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya Kuwambwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowasa akiwa katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT la Azania Front Dar es Salaam.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph wakiwa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo kanisani hapo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoriki,Mwadhama Porkap Kadinali Pengo akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo.
Waumuni wa Kanisa la Mtakatif Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa wanaubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mtoto, Vanes Mpupua akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mtakatif Josef Dar es Salaam.
Mmoja wa Watoto waliofika katika Kanisa la Mtakatif Josef akiubusu Msaraba wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliofanyika Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON

MAMA SALMA APOKEA MBIO ZA PIKIPIKI KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUNGANO-ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI

April 18, 2014

 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani  akikabidhi picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mama Salma Kikwete na picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Aman Karume kuashiria muendelezo wa mbio za uzalendo za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo.
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Said Sinani (mwenye kofia) akifuatana na viongozi wenzake wa Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Vijana kwenda kukabidhi mbio za pikipiki kwa uongozi wa Mkoa wa Lindi kwenye Kijiji cha Madangwa jana.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  wa Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini mtoto Idd Omar kutoka katika Kijiji cha Madangwa , kata ya Sudi huko Lindi Vijijini. Mama Salma alifika kijijini hapo kwa ajili ya kupokea mbio za uzalendo za pikipiki zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana, (UVCCM) kitaifa zikitokea Mkoa wa Mtwara.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara kwa watoto waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya zao kwani wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa ya kuambukizwa.

 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani  akikabidhi picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa na picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Aman Karume kwa Mama Salma Kikwete kuashiria muendelezo wa mbio za uzalendo za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar. KWA MATUKIO ZAID KATIKA PICHA BOFYA READ MORE

 Makabidhiano rasmi yakiendelea huku mamia ya wananchi  waliofurika kushuhudia wakishangilia.
 Baadhi ya Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano.
 Bwana Salum Musa Mtungulu mkazi wa Kijiji cha Madangwa alitumia fursa hiyo ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kurejea Chama Cha Mapinduzi akitokea Chama Cha NCCR- Mageuzi. Katika picha hiyo anatoa maelezo  ya kitendo hicho huku makada wakimvisha mavazi ya Chama Cha Mapinduzi.
 Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mnazi Mmoja kilichoko katika Kata ya Mingoyo walifurika kushuhudia sherehe za mbio za pikipiki za uzalendo kusherehekea miaka 50 ya Mungano .
Wasanii wa Kata ya Mingoyo wakitoa burudani wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele Aprili 26.
 Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Madangwa na wageni waliohudhuria sherehe ya kupokea mbio za pikipiki kwa Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojumuisha Ruvuma, Mtwara na Lindi katika kusherehekea miaka 50 ya Mungano.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Seleman Salum Namputa, miezi 3, aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine. Kulia ni Mama mzazi wa mtoto Seleman ajulikanaye kama Mariam kutoka katika kijiji cha Moka huko Lindi Vijijini. Mama Salma alitembelea hopitalini hapo.
Mama Salma, akizungumza wakati wa mkutano huo. PICHA NA JOHN LUKUWI. 

*RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AWAONDOA HOFU WATANZANIA, MUUNGANO BADO NI IMARA

April 18, 2014

 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea maelezo kutoka kwa Afisa wa Bunge Bwana Patson Sobha, wakati alipowasili kwenye Banda la Bunge la maonesho ya maadhisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yanayoendelea katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Maonesho hayo yatakayofikia kilele siku ya Jumamosi Aprili 19, ikiwa ni maandalizi ya siku kuu ya Muungano ambayo huherekewa Aprili 26 kila mwaka.
Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akikabidhiwa  zawadi ya vitabu na nyaraka mbalimbali za Bunge na Bi. Devotha George alipotembelea banda la Ofisi ya Bunge kwenye Maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
ais Msaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akikabidhiwa nyaraka na Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chach,zenye ujumbe wa shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka katika  Maadhimisho ya Miaka 50 ya sherehe za 
Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
Rais  mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi  akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo  katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.