Fastjet yatoa zawadi shindano la Pasaka

April 04, 2016














Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

JUMLA ya washindi 12 wamepewa tiketi za bure za safari ya ndege katika shindano lililodhaminiwa na Festjet Tanzania.

Tiketi hizo ambazo zitawawezesha kusafiri katika ndege ya garama nafuu ndani ya ndani na nje ya nchi ambako Fastjet husafiri, ni sehemu ya zawadi zilizotolewa na kampuni ya Fastjet wakati wa msimu wa sherehe za Pasaka ziliyomalizika wiki iliyopita.

Akizungumza wakati wa sherehe ya kutoa zawadi hizo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro alisema kuwa shirika la Fastjet limechukua hatua ya kudhamini wateja wake kwa kuwapa zawadi hizo za tiketi za bure ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kurudisha shukrani kwa wateja wake ambao wamekuwa watiifu kwa shirika hilo.

“Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kampuni ya fastjet imekuwa ikitoa huduma bora za safari ya anga ambazo ni salama, zenye uhakika na kuaminika kwa wateja wake ambao hadi sasa wamefikia abiria milioni 1.8”, alisema Mbogoro.

Aliongeza na kusema kuwa, “tunaimani kubwa na wateja wetu kwa ushirikiano wao waliouonyesha pamoja na sisi katika kipindi hicho chote na kutokana na hali hiyo, fastjet imeamua kutoa zawadi ya tiketi za bure kwa baadhi yao ili wasafiri kwenda kokote kule ndani na nje ya nchi”, Mbogoro aliongeza.

Alisema kuwa tiketi hizo zitawawezesha washindi wao kusafiri na wenzi wao ili kufurahia msimu huu wa sikukuuu ya pasaka na wapendwa wao wakiwemo marafiki na jamaa zao.
Aliongeza kuwa, washindi hao walichaguliwa baada ya kutoa majibu sahihi wakati wa maswali yaliyofanyika kwa njia ya mahojiano ya vyombo vya habari nchini.


“Washiriki katika shindano hili walikuwa wengi mno, na kati yao 12 pekee ndio waliofaulu na jopo la majaji kuwachagua kama washindi”, Mbogoro alifafanua.

Katika mahojiano, mmoja wa washindi wa zawadi hii, Ally Sangawe, alisema: “ Naishukuru fastjet kwa kuandaa shindalo hili kwa kuwa sasa nitaweza kusafiri kwa kutumia tiketi hii ya bure na kufurahia wikiendi njema na mpenzi wangu. Hii ni fursa ya kipekee na ambayo ni muhimu kwangu”.

Karim Lungu, ambaye pia ni miongoni mwa washindi, alitoa rai ya furaha kwa waandaaji wa shindano hilo na kusema kuwa, “sasa kwa kuwa nilikuwa na hamu ya kusafiri kwenda Mwanza ambapo hapo awali sikuwa na uwezo wa kukata tiketi, na sasa nashukuru kupata tiketi ya bure ambayo sasa imeniwezesha kutimiza ndoto yangu ya kufika huko”.


Mbali na kusafiri ndani ya nchi kila siku katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya na Zanzibar, Mbogioro alisema kuwa Fastjet husafiri na kutua katika mji wa Johannesburg-Afrika ya Kusini, na pia kampuni ilizindua safari ya moja kwa moja kwenda Nairobi-Kenya na sasa imeongeza maradufu safari za kila siku, kutoka mara moja kwa wiki na kwenda mara mbili kwa wiki ndani ya miji hii miwili iliyo mikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

HEKTA 5000 ZA ARDHI YA KIJIJI CHA LUHANGA WILAYANI MBARALI ZARUDISHWA KWA WANANCHI KUTOKA WAWEKEZAJ

April 04, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya kwa lengo la kutoa tamko la serikali juu ya ulejeshwaji wa ardhi ya wananchi hao hekta 5000 ambazo zilichukuliwa na wawekezaji.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akisisitiza jambo katika Mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu huyo wa Mkoa kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Luhanga (Hawapo Pichani)Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya .

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Luhanga Mbarali Mkoani Mbeya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kulejeshewa ardhi yao iliyochukuliwa na wawekezaji .

Mkutano ukiendelea katika kijiji cha Luhanga Mbarali katika ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Wananchi wa kijiji hicho ambao walikuwa katika mgogoro mkubwa wa ardhi na wawekezaji.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mbeya Guram Shekifu akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya kumaliza mgogoro huo.

Wananchi wakifuatilia Mkutano.

Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali Mbeya wakichukua kumbukumbu za Mkutano huo.

SERIKALI Mkoni Mbeya, imezirejesha hekta 5000 za ardhi ya kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali, zilizokuwa zimetolewa kwa wakulima zaidi ya 200 wa chama cha Luhanga (Luhanga AMCOS), huku ikiuagiza uongozi wa halmashauri kuwachukulia hatua watendaji wote walihusika na mchakato wa ugawaji wa ardhi hiyo.

Akikabidhi ardhi hiyo leo, kwa wananchi wa Kata ya Luhanga, Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala, alisema serikali imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kwamba zoezi hilo lilifanyika kinyume  na sheria na kanuni za ardhi za vijiji zinavyoelekeza.

Amesema, sheria  mama namba 5 ya ardhi ya mwaka 1999, imebainisha kwamba halmashauri ya kijiji haina mamlaka ya kugawa ardhi zaidi ya ekali 20 au 50 lakini wao wamegawa ardhi zaidi ya hekta 5000.

Mkuu huyo ameongeza kuwa mbali na zoezi hilo kughubikwa na ukiukwaji wa sheria lakini pia, wawekezaji hao wameonekana ni wababaishaji  kutokana na kushindwa kutimiza ahadi za maendeleo walizokuwa wamezitoa kwa wananchi wa eneo hilo.

 Aidha, Makala, aliwatahadharisha wananchi hao, kujiepusha na walaghai wa ardhi na kuacha kugawa ardhi ovyo kwani rasilimali hiyo haiongezeki ukilinganisha na mahitaji ya watu, ambao kila siku wanaongezeka idadi.

Amesema serikali inaweza kufanya uparesheni ya kuwataka vijana wafanye kazi lakini kama wananchi au viongozi wanauza ardhi zoezi hilo haliwezi kufanikiwa . 

Amesema mkoa wa mbeya unajulikana kwa kuongoza kwa migogoro ya ardhi hususani wilaya ya mbarali hivyo yeye kama mkuu wa mkoa  atahakikisha anashughulika vyema na suala hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka jamii za wafugaji wa kimasai kuhakikisha wanaachana na tabia ya kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo badala yake wawalitihishe katika elimu ambayo ndio mkombozi kwao.
Mwisho.
Habari hii imeandaliwa na mtandao wa kijamii wa www.jamiimoja.blogspot.com-0759406070 Mbeya.

WATU WASIOJULIKANA WATUMIA NAMBA YA SIMU YA MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI MJINI KUTAPELI.

April 04, 2016
TANGAZO KWA UMMA.

Mbunge wa Jimbo  la Moshi mjini Jafary Michael (Chadema) anatoa tahadhari kwa umma ya kuwa kuna baadhi ya watu wenye nia mbaya wanatumia namba yake ya simu ya mkononi  ya mtandao wa Vodacom kufanya utapeli .

Watu hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi (SMS) kwa watu mbalimbali kwa lengo la kutapeli wakiomba kutumiwa fedha .

Wakati akishughulikia suala hilo katika vyombo vya dola ametoa ombi kwa yeyote atakayepata ujumbe huo kuupuza na kutoa taarifa kwa yeyote atakaye fikwa na kadhia hiyo.

Ukipata ujumbe huu mfahamishe na mwenzako.

Imetolewa na :
Japhary Michael
Mbunge wa Moshi mjini
 

SHIRIKA LA EfG LAFANYA TAMASHA LA KUPINGA UKATILI WA JINSIA AWAMU YA PILI KATIKA SOKO LA MCHIKICHINI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

April 04, 2016
 Ofisa Ufutiliaji na Tathmini wa Shirika la Eguality for Growth (EfG), Shabani Lulimbeye, akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu vitendendo vya ukatili wa kijinsia katika Tamasha lililofanyika leo asubuhi viwanja vya Soko la Mchikichini Ilala jijini Dar es Salaam.
 Mfanyabiashara katika soko hilo, Suleiman Azizi akichangia jambo kuhusu ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
 Kikundi cha Sanaa cha Machozi cha Temeke jijini Dar es Salaam kikihamasisha wananchi kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia masokoni katika Tamasha hilo.
 Wafanyabiashara ndogo ndogo katika soko hilo wakifuatilia tamasha hilo.
 Wasaidizi wa kisheria katika soko hilo wakiwa kwenye tamasha hilo. Kulia ni Zainab Namajojo na Mechi Mtindi.
 Wasanii wa kundi la Machozi wakila wakati wakiigiza igizo la kupinga ukatili wa kijinsia.
 Raia wa kigeni ambao wanafanyakazi ya kujitolea katika Shirika la EfG wakiwa kwenye tamasha hilo.
 Taswira katika tamasha hilo.
Wasanii wa Kundi la Machozi wakionesha igizo la ukatili wa jinsia masokoni.

ELFU MBILI TU KUZIONA SERENGETI BOYS v THE PHARAOHS

ELFU MBILI TU KUZIONA SERENGETI BOYS v THE PHARAOHS

April 04, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kiingilio cha shilingi elfu mbili tu (2,000) kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kirafiki wa kimataifa kati ya Serengeti Boys (Tanzania U17) dhidi ya The Pharaohs (Misri U17).
Mchezo kati ya timu hizo za vijana utachezwa kesho Jumanne saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati, katika uwanja wa Azam Complex uliopo eneo la Chamazi jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa kirafiki wa awali uliochezwa Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Serengeti Boys waliibuka na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya The Pharaos, mabao ya Serengeti yakifungwa na kiungo Cyprian Bennedictor na Ally Hussein.
Kikosi cha Serengeti Boys kinachonolewa na makocha Bakari Shime na Sebastian Mkomwa wakishauriwa na Kim Paulsen, baada ya mchezo wa awali kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo huo wa kesho.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maaandalizi kwa timu zote Tanzania (U17) na Misri (U17) zinazojiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar.
Serengeti Boys itaanza kutupa karata yake dhidi ya Shelisheli Juni 25, 2016 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na marudiano kuchezwa baada ya wiki moja nchini Shelisheli.
WAZIRI PROF. MBARAWA AKAGUA BARABARA YA TABORA-KOGA-MPANDA KM 356

WAZIRI PROF. MBARAWA AKAGUA BARABARA YA TABORA-KOGA-MPANDA KM 356

April 04, 2016


Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi akimuonesha athari za mvua Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia kwake) wakati akikagua daraja la Koga lililoathirika. Daraja hilo linaunganisha mkoa wa Katavi na Tabora.
Muonekano wa Daraja la Koga baada ya kufanyiwa ukarabati kufuatia kuathiriwa na mvua kubwa zilizonyesha katika mkoa wa Katavi. Daraja hilo kwa sasa linaruhusu magari kupita ya tani 1 hadi 3.
Muonekano wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa Km 356 inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa katika hatua za awali za ujenzi wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya CICO anayejenga barabara ya Tabora-Koga- Mpanda yenye urefu wa Km 356, sehemu ya Tabora-Sikonge kumaliza mradi huo kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Bi. Hanifa Sirengu akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hali ya miundombinu katika wilaya yake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakati alipotembelea kiwanja cha ndege cha Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maelezo ya namna vifaa vya kuongozea ndege vinavyofanya kazi kutoka kwa mtaalamu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Uwanja wa ndege wa Tabora Bw. Yahya Nassoro akitoa maelezo ya namna gari la kuzimia moto linavyofanya kazi katika uwanja huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa Km. 356 kwa kiwango cha lami ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Awamu ya Tano aliyoitoa kwa wananchi wa Mikoa ya Katavi na Tabora.

Ametoa kauli hiyo wilayani Sikonge mkoani Tabora, mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesema ujenzi huo unatarajia kuanza rasmi hivi karibuni.

‘Ujenzi wa barabara hii tumeugawa katika sehemu tatu ili kuharakisha utekelezaji wake, tutahakikisha ifikapo mwisho wa mwaka huu, makandarasi wote watatu watakuwa katika maeneo yao ya kazi’, amesema Prof. Mbarawa.

Amesisitiza kuwa wananchi wanaostahili kulipwa fidia watalipwa kwa wakati kwa kuwa takribani shilingi bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Prof. Mbarawa pia amekagua daraja la Koga linalounganisha Mkoa wa Katavi na Tabora na kuwataka viongozi wa mikoa hiyo kuhakikisha kuwa magari yasiyozidi tani tatu ndio yanayopita katika daraja hilo ili kuepusha ajali hadi ukarabati mkubwa utakapofanyika.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Kanali Mstaafu Issa Nziku amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupandisha hadhi baadhi ya barabara katika Wilaya hiyo ili zihudumiwe na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kutokana na uwezo mdogo wa Halmashauri hiyo kuzikarabati kila wakati.

Katika Hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua uwanja wa Ndege wa Tabora na kuwataka viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kuangalia namna bora ya ukarabati wa kiwanja hicho ili uruhusu ndege kubwa kutua na kuongeza biashara.

Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya siku saba ya kukagua miundombinu ya taasisi zilizo chini ya Wizara yake katika mikoa ya Magharibi ili kuifungua kanda hiyo kimiundombinu na hivyo kufufua fursa za kiuchumi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

KAMANDA SIRO AZUNGUMZIA MIKAKATI YA OPERESHINI YA KUPAMBANA NA UHALIFU PAMOJA NA BODA BODA

April 04, 2016

.....UPDATES......
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata Marobota 10 ya vitenge na Katoni 17 za Pampers  pamoja na Gari lililotumika kubebea hitu hivyo katika eneo ya Gezaulole lililopo pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa kukamatwa kwa gari lenye vitu hivyo ni mara baada ya kupewa taarifa na Raia wema kwa kuwa katika eneo hilo kunapitishiwa mali zisizotolewa ushuru.

Siro amesema kuwa Gari lililo kamatwa na Vitenge na Pampers ni aina ya Suzuki Carry lenye namba za usajili T490 CQB ambalo nalo linashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam.

Pia Sirro amesema kuwa mwananchi anaeona kuwa alitelekeza gari hilo lililo na vitu hivyo ajisalimishe Polisi ili apelekwe Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) akalipie ushuru wa vitu hivyo.

Katika Operesheni nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilifanikiwa kukamata gari moja la wizi aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 314 DFH  ambapo kabla ya kuibwa lilikuwa na namba za usajili T 622 DDR  ikiwa gari hilo ni Mali ya Hellen Michael liliibwa maeneo ya Kitunda Kivule ambapo lililuwa limeegeshwa nyumbani kwake. Pia Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limkamata watu wawili wakiwa na Pikipiki mbili zenye namba za usajili MC343 ASL aina ya Boxer na MC 606 ex aina ya Fercon ambazo ni za wizi na watuhumiwa hao kukuli kuwa wameziiba Pikipiki hizo.

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kwa kipindi cha wiki moja limefanikiwa kukamata Pikipiki 519 katika Operesheni ya ukamataji wa Pikipiki kwa makosa mbalimbali operesheni hiyo ilifanywa katika mikoa ya Ilala piki[iki 183,Kinondoni pikipiki 139 na Temeke pikipiki 197.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusina na Operesheni ya kukamata Pikipiki519 pamoja na gari lililokuwa na Vitenge marobota 10 na Pampers katoni17 katika eneo la Gezaulole pemeni mwa ufukwe wa bahari ya hindi ambapo eneo hilo linatumika kupitisha mali zisizolipiwa ushuru.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akionyesha Baadhi ya Vitenge na Pempers zilizokamatwa katika operesheni ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akionyesha gari lilokamatwa na vitenge na Pampers.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akionesha pikipiki 519 ambazo zimekamatwa ja jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Kamanda Sirro akionesha mali zilizokamatwa katika Operesheni hiyo ya kupambana na Uhalifu,mbele ya Waandishi wa Habari,leo jijini Dar.


Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kuhusiana na suala zima la Operesheni ya kupambana na Uhalifu pamoja na Bodaboda.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamisi Kigwangalla afungua ofisi mpya za shirika la T-Marc Tanzania.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamisi Kigwangalla afungua ofisi mpya za shirika la T-Marc Tanzania.

April 04, 2016

1T
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla Charles Singili Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la T. Marc Tanzania pamoja na Diana Kisaka Mkurugenzi wa Shirika la T.Marc Tanzania wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi za shirika hilo zilizoko Kunduchi jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki , Shirika hilo linajihusisha na shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu katika masuala ya ukimwi, Malaria na Elimu ya Uzazi.
2T
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitembelea mabanda yaliyokuwa yakionyesha vitu mbalimbali pamoja na vijarida vinavyota elimu katika masuala mbalimbali kama vile Ukimwi na Malaria.
3T
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mkurugenzi wa kampuni ya Montage Bi Teddy Mapunda wakati alipowasili katika ofisi hizo tayari kwa uzinduzi kutoka kulia ni Diana Kisaka Mkurugenzi wa shirika la T-Marc Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya T-Marc Tanzania Bw. Charles Singili.
4T
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya T-Marc Tanzania Bw. Charles Singili alipowasili katika uzinduzi huo.
5T
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
6T 7T
Kikundi cha ngoma cha Msanii Wanne Star kikitumbuiza katika uzinduzi huo.
8T
Kikundi cha ngoma cha Msanii Wanne Star kikitumbuiza katika uzinduzi huo.
9T
Kikundi cha ngoma cha Msanii Wanne Star kikitumbuiza katika uzinduzi huo.
11T
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya T-Marc Tanzania Bw. Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi huo kufanyika kutoka kushoto ni Doris Chalambo Meneja wa Mipango na Diana Kisaka Mkurugenzi wa T- Marc Tanzania.
12T
Diana Kisaka Mkurugenzi wa T- Marc Tanzania akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo kutoka kulia ni Mjumbe wa bodi ya T-Marc Tanzania Mwanasheria Alex Mgongolwa na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya T-Marc Tanzania Bw. Charles Singili.
13T
Doris Chalambo Meneja wa Mipango wa T-Marc akifafanua jambo wakati akizungumza nawaandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo  katika picha kutoka kulia ni Mjumbe wa bodi ya T-Marc Tanzania Mwanasheria Alex Mgongolwa, Mwenyekiti wa Bodi ya T-Marc Tanzania Bw. Charles Singili na Diana Kisaka Mkurugenzi wa T- Marc Tanzania.
14T
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya shirika la T-Marc Tanzania.
15T
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi Bw. Charles Singili Mkurugenzi wa T-Marc Tanzania Diana Kisaka na Mwanasheria Alex Mgongolwa  na baadhi ya wafanyakazi wa shirika  la T-Marc Tanzania.