BINGWA WA MASOMO YA HISABATI ATANGAZWA

October 20, 2023


Chama Cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) kimetoa orodha ya wanafunzi 233 kati ya 812 waliofanya vizuri katika shindano la hisababti Nchini Tanzania.

Wanafunzi hao kutoka mikoa 11 ya Tanzania bara na visiwani, walipata asilimia 40 na zaidi ya alama zilizohitajika kwenye shindano hilo na wengine 579 wakipata chini ya asilimia 40.

Mtihani huo ulihusisha makundi mawili, kundi la kwanza likiwa ni wanafunzi wa kidato cha tatu hadi cha nne na kundi la pili ni kidato cha tano hadi sita na washindi.

washindi hao wanatoa wanatoa mwanya wa kupatikana kwa washiriki nane katika shindano la hisabati ngazi ya Afrika mashariki, Afrika na Dunia litakalofamyika mapema mwakani

Akisoma matokeo hayo jDar es Salaam, Mwenyekiti wa CHAHITA Betinasia Manyama,alitaja badhi ya wanafunzi wa kundi la wanafunzi 10 bora wa jumla kidato cha tatu na nne akiwemo Stella Maliti wa Shule Marian Girls ya Pwani, Brown Mafuru wa Marian Boys Pwani na Alice Gonza wa Canossa ya Dar es Salaam.

Kuhusu ya idadi ya shule zilizoshirikia, alisema ni 58 wanafunzi wakiwa 540 ambapo waliopata asilimia 40 na kuendelea ni 167 na chini wastani huo ni 373.

Kwa kidato cha tano na sita, Betinasia alisema walioshiriki ni 272 kutoka shule za sekondari 22, wavulana wakiwa 162 na wasichana 110 takwimu zikionyesha waliopata asilimia 40 na zaidi ni 66 pekee na wenye upungufu na wastani huo wakiwa 206.

Baadhi walioshika nafasi 10 za mwanzo ni Amosi Paulo wa Mzumbe mkoani Morogoro,Elia Wambura wa Iyunga Technical Mbeya na Mwanaarab Said wa Lumumba mjini Magharibi.

Betinasia alisema mtihani wa kuwapata washindi ulifanyika Agosti mwaka huu na washindi nane wanasakwa kuiwakilishi nchi kwenye mashindano ya hisabati Afrika Mashariki, Afrika na Duniani.

“Lengo la mashindano haya ni kupata wanafunzi watakaoiwakilisha nchi kushiriki katika mashindano ya kimataifa,pia kujenga ushirikiano wa kitaaluma na mataifa mbalimbali duniani,baada ya matokeo haya washidi 10 kwa kila jundi watapatiwa zawadi siku ya maadhimisho ya Hisabati Duniani Machi14,2024”alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHAHITA Dk Said Sima alisema malengon yao mwakani ni kuhakikisha mikoa yote nchini inashiriki shindano hilo.

Alisema si kila mwanafunzi anashiriki bali ni wale wenye vipaji na uongozi kwenye shule husika ndio huwachagua wahusika kuingia kwenye shindano hilo la mitihani ya hisabati.

“Tunaweka mikakati hawa washindi tuwape elimu ya kutosha ili washiriki kwenye mashindano ya kimataifa vyema,”alisema.

Naye Mkuu wa Idara ya Hisabati Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Sylvester Rugeihyamu alisema lengo la shindano la hisabati ni kutambua na kuibua vipaji kwenye somo hilo,kuchochea na kutambua ubunifu wa uvumbuzi kupitia mitihani

Pia kuwapa motisha wanafunzi kuipenda somo la hisabati akisistiza mitihani hiyo haitumii mitaala inayotumiwa na Baraza l;a Mitihani Tanzania (Necta)

Mikoa ambayo imetoa shule zilizoshiriki kwenye shindano hilo ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Mbeya,Arusha,Dodoma, Iringa,Kilimanjaro, Songwe,Mwanza na mjini Magharibi.
Mwenyekiti wa Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA), Betinasia Manyama, akitangaza matokeo ya mitihani ya mashindano ya hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha tatu, nne, tano na sita, katika Idara ya Hisabati, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Said Sima na kulia ni Mkuu wa Idara ya Hisabati na Mlezi wa CHAHITA, Dk. Sylvester Rugeihyamu. na mpiga picha wetu

Katibu mkuu wa chama cha hisabat Said Sima mara baada ya kutangazwa matokeo ya mitihani ya mashindano ya hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha tatu, nne, tano na sita, katika Idara ya Hisabati, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jana,kulia ni Mkuu wa Idara ya Hisabati na Mlezi wa CHAHITA, Dk. Sylvester Rugeihyamu.

Mkuu wa Idara ya Hisabati na Mlezi wa CHAHITA, Dk. Sylvester Rugeihyamu akizungumza jambo mara baada ya kutangazwa matokeo ya mitihani ya mashindano ya hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha tatu, nne, tano na sita, katika Idara ya Hisabati, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jana,

Picha ya pamoja


ELIMU

WANAFUNZI 56,132 WAPANGIWA MIKOPO YA SH.159.7 BILIONI AWAMU YA KWANZA 2023/2024

October 20, 2023

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza awamu ya kwanza ya Wanafunzi 56,132 wa shahada ya kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 159.7 kwa mwaka wa Masomo 2023/2024.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Bw. Abdul-Razaq Badru amesema kuwa kati ya wanafunzi hao, wa kiume 32,264 sawa na asilimia 57% na wa kike ni 23,868 sawa na asilimia 43% na kuanzia leo wanaweza kuona taarifa za mikopo waliyopangiwa katika akaunti walizotumia kuomba mkopo.

Aidha Bw.Badru amesema kuwa maafisa wa HESLB watakuwa katika taasisi za elimu ya juu nchini kuanzia Jumatatu , Oktoba 23,2023 ili kuratibu usajili wa wanafunzi hao katika mfumo wa malipo.

"Kwa wanafunzi wapya, kama walivyoshauriwa wakati wa kuomba mkopo, wafike vyuoni wakiwa na namba za akaunti zao za benki, namba zao za simu zinazopatikana na watasajiliwa katika mfumo wetu wa malipo wa DiDiS baada ya kusajiliwa na Chuo'. Amesema Bw.Badru

Pamoja na hayo Bw.Badru amesema kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 731 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi 220,376, kati yao, wanafunzi 75,000 watakuwa ni wanufaika wa mwaka wa kwanza wa shahada ya kwanza na wanafunzi zaidi ya 145,376 ni wanaoendelea na masomo baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka.

Vilevile amewasihi waombaji wa mikopo wa shahada ya Kwanza, Stashahada na wanufaika wa 'Samia Scholrship' kwa mwaka 2023/2024 kuwa watulivu wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikipo na ufadhili kwa wanafunzi wenye sifa ukiendelea.

Kwa upande wake rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) Bi.Maria Thomas ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuongeza bajeti ya mikopo ambapo mwanzo ilikuwa Bilioni 654 hadi kufikia Bilioni 731.

Ameipongeza Bodi ya Mikopo kwa kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyiwa kazi.

Hata hivyo amewaomba wanaufaika wa mikopo watakapopata fedha zao, wazielekeze katika malengo mahususi katika kutimiza ndoto za elimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) , Bw. Abdul-Razaq Badru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) , Bw. Abdul-Razaq Badru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) , Bw. Abdul-Razaq Badru akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) , Bw. Abdul-Razaq Badru akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) , Bw. Abdul-Razaq Badru akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) , Bw. Abdul-Razaq Badru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam.
rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) Bi.Maria Thomas (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa upangaji na utoaji mikopo wa HESLB, Dkt. Peter Mmari akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Watumishi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakifuatilia Mkutano wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) , Bw. Abdul-Razaq Badru na Waandishi wa habari leo Oktoba 20,2023 katika Ofisi za HESLB Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

MAJALIWA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA JIMBO LA LOMBARDIA

October 20, 2023

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi Rais wa Jimbo wa Lombardia Mhe. Attilio Fontana baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye kwenye ofisi za jimbo hilo, Milan, Italia Oktoba 20, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Jimbo wa Lombardia Mhe. Attilio Fontana kuhusu ushirikiano kati ya jimbo hilo ambalo ni maarufu kwa ujenzi wa viwanda pamoja na Tanzania, kwenye ofisi za jimbo hilo, Milan, Italia Oktoba 20, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Jimbo wa Lombardia Mhe. Attilio Fontana kuhusu ushirikiano kati ya jimbo hilo ambalo ni maarufu kwa ujenzi wa viwanda pamoja na Tanzania, kwenye ofisi za jimbo hilo, Milan, Italia Oktoba 20, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Jimbo wa Lombardia Mhe. Attilio Fontana kuhusu ushirikiano kati ya jimbo hilo ambalo ni maarufu kwa ujenzi wa viwanda pamoja na Tanzania, kwenye ofisi za jimbo hilo, Milan, Italia Oktoba 20, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jimbo wa Lombardia Mhe. Attilio Fontana alipowasili kwenye ofisi za jimbo hilo, Milan, Italia Oktoba 20, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jimbo wa Lombardia Mhe. Attilio Fontana alipowasili kwenye ofisi za jimbo hilo, Milan, Italia Oktoba 20, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UIMARISHAJI MFUKO WA PSSSF

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UIMARISHAJI MFUKO WA PSSSF

October 20, 2023

 


 

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bungeni , Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bungeni, Jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akichangia jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Hufadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mbarouk Magawa akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni Jijini Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Dkt. Aggrey Mlimuka akizungumza wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakuu wa Idara, Vitengo na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamoja na Watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wakifuatilia maelezo ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo, Bungeni, Jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, imeridhishwa na dhamira ya serikali ya kuimarisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ikiwamo kulipa Sh.Trilioni 2.17 ambazo ni sehemu ya deni la michango ya watumishi wa kabla ya Mwaka 1999.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe.Fatuma Toufiq ameyasema hayo katika kikao cha kamati hiyo cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya PSSSF uliopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Amesema kamati inampongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha mfuko huo ambapo Desemba 15, 2021 serikali ilitoa fedha hizo na kulipa madeni ya uwekezaji sh.Bilioni 500 kati ya Sh.bilioni 731 zilizohakikiwa.

Mhe. Toufiq amehimiza mfuko kutoa elimu ya kujiandaa kustaafu kuanzia kwa waajiriwa wapya ili wafanye maendeleo na kujiwekea akiba mapema badala ya kusubiri hadi wastaafu.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako, amesema serikali itaendelea kuimarisha uhai wa mfuko huo na kuahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa na kamati hiyo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe.Patrobas Katambi, amesema serikali imetengeneza mifumo ya kisheria inayolenga kuleta ustawi kwa watumishi wanapostaafu.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba, amesema hatua zingine zilizochukuliwa na serikali kuboresha mfuko huo ni pamoja na kuzuia uwekezaji kwenye maeneo yasiyo na tija na kuweka ukomo wa uwekezaji ili kuleta ufanisi.

MHANDISI LUHEMEJA ATAKA WCF KUSAJILI WAAJIRI WOTE NCHINI

MHANDISI LUHEMEJA ATAKA WCF KUSAJILI WAAJIRI WOTE NCHINI

October 20, 2023

 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  wilayani Morogoro.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akisisitiza jambo kwenye kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  wilayani Morogoro.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt.John Mduma akizungumza kwenye kikao hicho Oktoba 19, 2023 wilayani Morogoro

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakimsikiliza Katibu Mkuu. Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja kwenye kikao cha Baraza hilo wilayani Morogoro.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wilayani Morogoro.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa maagizo manne kwa Baraza la wafanyakazi la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ikiwamo kuwasajili waajiri wote nchini.

Mhandisi Luhemeja ameyasema hayo  wilayani Morogoro alipokuwa akifungua kikao cha Baraza hilo.

Amesema ni muhimu WCF ikaongeza malengo ya kusajili waajiri wote hasa wa sekta binafsi ambao wanaajiri wafanyakazi wengi wa ngazi ya chini na wanaofanya kazi kwenye mazingira hatarishi.

“Suala jingine ni elimu kwa umma huu mfuko ni muhimu unawagusa watanzania wote kutokana na wapendwa wao kupata madhira kazini, wajue manufaa ya mfuko na majukumu yake,”amesema.

Pia, amehimiza kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu ili watanzania wavutiwe na huduma zinazotolewa.

“Mmbebe jukumu hili kwa pamoja na kazi hii muibebe kwa moyo lakini mkifanyia kwa maslahi hamtafanikiwa, pia suala jingine ni mashirikiano fanyeni kazi kama timu muheshimiane wafanyakazi na viongozi ili kuleta ufanisi wa mfuko,”amesema.

Naye, Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, amesema mfuko upo imara na wajumbe wa baraza hilo wamejadili masuala mbalimbali ikiwamo huduma za utengamao.

WATANZANIA CHANGAMKIENI FURSA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA MAREKANI

October 20, 2023

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa rai kwa Sekta Binafsi kutumia fursa ya makubaliano ya majadiliano ya kibiashara kati ya Tanzania na Marekani kubainisha changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kufanya biashara na Marekani ili zitatuliwe na kukuza biashara na kuongeza mapato ya wananchi na Taifa.


Aidha, amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Marekani kuja Tanzania kufanya biashara na kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa nchini na kwenye masoko ya EAC, SADC na AfCFTA.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo 10/19/2023 wakati wa hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya Majadiliano ya Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani (MoU) yaliyofanyika katika ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.

Pia, Dkt Kijaji amebainisha kuwa Makubaliano hayo yanatarajia kukuza biashara baina ya Tanzania na Marekani hususani uuzaji wa bidhaa kupitia Mpango wa AGOA ambapo mwaka 2022 mauzo ya Tanzania kwenda Marekani yalikuwa na thamani ya Dola Marekani Milioni 74.5 na manunuzi yalikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 93.7.

Aidha. Dkt Kijaji ametaja maeneo ambayo yataanza katika majadiiano hayo kutokana na umuhimu wake ambayo ni Uchumi wa Kidigitali (Digital Economy), Upatikanaji wa Masoko (Market Access), Mifumo ya Kisheria na Mazingira ya biashara (Regulatory and Business Environment Reform), ushirikiano kwenye Maonesho ya Biashara (Trade Mission). Mengine yataongezwa kulingana na pande zote mbili

Vile vile amebainisha kuwa hatua ya makubaliano hayo ni mwendelezo wa Jitihada za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kufungua fursa za biashara na uwekezaji na nchi mbalimbali duniani. MoU hiyo itasaidia katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Marekani.

Aidha Dkt Kijaji ameahidi kuendeleza ushirikiano na Waziri wa Biashara wa Marekani Mhe. Gina Raimondo katika kuhakikisha kuwa biashara baina ya Tanzania na Marekani inaendelea kukua na kuimarika.

Naye Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Michael Battle amesema kupitia makubaliano hayo wafanyabiashara wa Marekani na Tanzania watakuwa wakikutana mara kwa mara hali ambayo itaiwezesha sekta binafsi kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina Tanzania na Marekani.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) (Kulia) akiwa na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe. Michael Battle (kushoto), wakisaini Hati ya Makubaliano ya Majadiliano ya Kibiashara kati ya Marekani na Tanzania Oktoba 19,2023, JNICC, Dar es salaam. Walioko Nyuma ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodegar Tenga(kulia), Afisa Biashara Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Sekela Mwaisela na Afisa Biashara Mwandmizi wa Ubalozi Marekani nchini Bi Aliza Totayo wakishuhudia , hafla iliyofanyika Oktoba 19,2023, JNICC , Dar es salaam






TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUU UKANDA WA NCHI ZA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA

October 20, 2023

 Pamela Mollel, Arusha


Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa jukwaa la majaji wakuu ukanda wa nchi za kusini na Mashariki mwa Afrika(SEAJAA) utakaofanyika oktoba 23 hadi 27 jijini Arusha

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mwenyekiti wa Chama cha hicho, Profesa Elisante ole Gabriel ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, amesema maandalizi ya kikao cha watendaji hao yanaendelea vizur  na kuwa Mkutano huo utakaofunguliwa na Rais Dkt Samia Hassan Suluhu.

Profesa Gabriel amesema katika  kikao hicho tayari nchi 13 zimejiunga na chama hicho huku jitihada za nchi nyingine tatu  kujiunga na chama hicho zikiendelea na badae idadi ya wanachama wengine itaongezeka kufika Afrika nzima

Aliongeza kuwa malengo ya chama hicho ni kubadilishana uzoefu katika nchi wanachama ikiwemo jinsi gani wakuu wa mahakama wanavyoendesha shughuli za mahakama

Amesema kikao kazi hicho kitajadili mambo mbalimbali kwani watendaji wakuu wanawashauri majaji wakuu katika masuala ya miundombinu, rasilimali za watu na masuala ya fedha

Pia kitakuwa na ajenda za marekebisho ya katiba ya chama hicho ikiwemo uboreshaji wa vyanzo vya fedha, uboreshaji wa mtandao wa chama hicho, mikakati ya masuala ya fedha huku nchi 13 za umoja huo zitakazoshiriki mkutano huo ambazo ni Angola, Botswana, Lesotho, Zanzibar, Shelisheli, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Eswatini, Zambia, Namibia na mwenyeji Tanzania.


WAZIRI MKUU ATEMBELEA SHAMBA SHAMBA LA KISASA LA MIFUGO, MILAN, ITALIA

October 20, 2023

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia zoezi la ukamuaji wa maziwa kwa kutumia mashine alipotembelea shamba la kisasa la mifugo la Alessandra (Artificial Intelligence Farm) ambalo ni maarufu kwa teknolojia ya kisasa ya kutunza mifugo, lililopo Milan, Italia Oktoba 19, 2023.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Alessandra Seresina ambaye ni Mmiliki wa shamba la kisasa la mifugo Alessandra (Artificial Intelligence Farm) kuhusu ufugaji wa kisasa, wakati alipotembelea shamba hilo lililopo Milan, Italia Oktoba 19, 2023. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mahmoud Thabiti Kombo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia majani ambayo hutumika kama malisho ya mifugo kwenye shamba ya mifugo la la Alessandra ambalo ni shamba la kisasa la mifugo (Artificial Intelligence Farm) na maarufu kwa teknolojia ya kisasa ya kutunza  mifugo, wakati alipotembelea shamba hilo lililopo Milan, Italia Oktoba 19, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Alessandra Seresina ambaye ni Mmiliki wa shamba la kisasa la mifugo Alessandra (Artificial Intelligence Farm) kuhusu ufugaji wa kisasa, wakati alipotembelea shamba hilo lililopo Milan, Italia Oktoba 19, 2023. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mahmoud Thabiti Kombo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Alessandra Seresina ambaye ni Mmiliki wa shamba la kisasa la mifugo Alessandra (Artificial Intelligence Farm) kuhusu ufugaji wa kisasa, wakati alipotembelea shamba hilo lililopo Milan, Italia Oktoba 19, 2023. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mahmoud Thabiti Kombo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mashine ya kunyonyeshea Ndama iliyopo katika shamba la kisasa la mifugo la Alessandra (Artificial Intelligence Farm) ambalo ni maarufu kwa teknolojia ya kisasa ya kutunza mifugo, lililopo Milan, Italia Oktoba 19, 2023. Wengine pichani kutoka kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mahmoud Thabiti Kombo, Mmiliki wa shamba hilo Alessandra Soresina na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)