BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)LATOA KIBALI KWA TAASISI YA UHASIBU (TIA) MBEYA KUANZISHA KOZI NYINGINE ZA SHAHADA YA MASOKO

November 08, 2015
Kikosi cha brasband cha Magereza kikiongoza Maandamao kuelekea uwanjani kwenye mahafali hayo ya Kumi na Tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa kampasi ya Mbeya .

Baadhi ya wahadhiri wa Taasisi hiyo ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya wakiandamana kuelekea uwanjani tayari kwa mahafali hayo .

Wahitimu wakiwa katika maandamano hayo ya Mahafali ya kumi na Tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa Kampasi ya Mbeya.


Meza kuu wakipokea maandamano ya wahitimu katika mahafali ya kumi na tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa kampasi ya Mbeya yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Chuo hicho jijini Mbeya.

Baadhi ya wahitimu wa Uhasibu  (TIA) kampasi ya Mbeya



Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt .Joseph Kihanda akizungumza kwenye mahafali ya Kumi na tatu ya Taasisi na ya Tatu kufanyika katika Kampasi ya Mbeya .

Mgeni rasmi Ndugu Nyirembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ambaye pia alimwakilisha Waziri wa Fedha katika mahafali hayo ya Taasisi ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya.

Wahitimu wa Masomo ya Uhasibu Katika Taasisi hiyo wakisikiliza kwa umakini nasaha kutoka kwa mgeni rasmi .

Kikundi cha ngoma za asili kutoka Ilemi jijini Mbeya kikitoa burudani katika mahafali hayo .


Mgeni rasmi Nyirembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akitoa zawadi kwa washindi walio fanya vyema katika masomo yao.

Baadhi ya wahitimu wa masomo ya Uhasibu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Kampasi ya Mbeya wakitunukiwa rasmi cheti cha awali,Stashahada na Shahada ya Uzamili katika fani mbalimbali ambapo jumla ya wanafunzi 1689 wamehitimu mafunzo hayo ambapo kati yao wanaume ni 838 na wasichana 851 .





Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi (NACTE)limetoa kibali kwa taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Mbeya ili kuongeza kozi nyingine za shahada ya Masoko na uhusiano kwa umma (Bachelor Degree in Marketing and public Relation kwa mwaka wa masomo wa 2015-16.
        Aidha baraza hilo pia limetoa kibali kwa kuanzishwa kwa kozi nyingine ya shahada ya uhasibu wa fedha za umma (Bachelor Degree in Public Sector Accounting and Finance) kwa mwaka huu wa masomo.
 Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt.Joseph Kihanda kwenye mahafali ya kumi na Tatu ya Taasisi na y a tatu kufanyika katika kampasi ya Mbeya.
        Amesema katika mwaka wa masomo wa 2014-2015 kufuatia maombi ya muda mrefu ya wadau wake kampasi ya mbeya ilianza kutoa kozi za shahada ya uhasibu na shahada ya Ununuzi na Ugavi ambazo mwitikio wake umekuwa mkubwa hivyo kulazimika kuomba kibali cha kuanzisha kozi nyingine ambazo tayari baraza hilo limekwisha toa kibali .
        Amesema kuanzishwa kwa kozi hizo kumeiwezesha kampasi ya Mbeya kuwabakiza wanafunzi wanaohitimu kozi za Stashahada katika fani husika ambao hapo awali walilazimika kuhamia vyuo vingine vinavyotoa kozi hizo kwenye ngazi ya shahada na hivyo kuikosesha Taasisi mapato.
        Aidha Dkt Kihanda amesema kuwa kuanza kwa kozi hizo  pia kutawawezesha wakazi wa mbeya na mikoa mingine ya jirani kupata fursa ya kujiendeleza kitaaluma Katika ngazi ya  shahada kwani masomo yanatolewa katika mfumo wa kutwa na jioni hivyo kukidhi kiu ya wengi.
        Hata hivyo amesema kampasi ya mbeya imejiimarisha sana katika utoaji wa elimu yenye ubora ili kuwawezesha wahitimu kufanya vizuri katika masomo yao ya baadae na katika sehemu zao za kazi.
            Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya wizara ya fedha Profesa Isaya Jairo amesema bodi hiyo itashirikiana na uongozi wa TAASISI  kuishauri wizara ya fedha kuitngea fedha za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu mbalimbali pamoja na vitendea kazi.
Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 1689 wa stashahada na stashahada za udhamili katika fani mbalimbali wanahitimu masomo yao ambapo kati yao wasichana 851 na wanaume 838.
Mwisho.(Imeandaliwa na Emanuel Madafa Jamiimojablogu Mbeya)

POLISI TANGA YAWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU 45

November 08, 2015


Tangakumekuc
Tanga,POLISI Mkoani Tanga, imewakamata wahamiaji haramu 45 wenye asili ya Kiethopia wakiwa katika gari aina ya fuso baada ya  kuwepo kwa taarifa ya  watu hao kusafirishwa kutoka Moshi Mkoani Kilimanjaro kueleka Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 6 usiku katika kizuizi cha polisi cha Mombo Wilayani Korogwe.
Alisema watuhumiwa hao waligundulika wakiwa wamefichwa katika gari aina ya fuso ambalo mlangoni na pembezoni mwa gari iliwekwa  mikungu ya ndizi ili kuwaficha lakini polisi ilitilia shaka baada ya kusikia minong’ono ya sauti za watu ikitokea ndani ya gari.
Kamanda Mombeji aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni, Mlacho Mathias (24) Oleso Bafe (22) Dameke Lodore (20) Damekglo Achore (20), Jose Yosete (25), Tarafa Kajamo (18), Aserat Eleysa (17), Dagu Sumoro (40), Akililu Abeba (22), Aberhame  Tadewose (20), Abara Adese (30) , Ayrno Bekele (20),  Taseme Workicho (20), Adam Ashore (21), Tamasegen Tumoro (19), Baharu Detamo (21), Sekadu Ababea (23), Wondem Wakere (24), Tamerat Dafar (21), Beruke Kelebore (21), Nuruden Tamso (22), Dekebe Abebe (17), Mulegeta Alam (20), Chakebo Muhaba (22), Alamayu Tasama (23), Manegestu Marko  (24), Kayadayn Nourgaba (24), Eleyas Eregano (24), Tasama Herama (18), Adese Kate (22), Daraje Damaka (22), Ramato Atoro (23), Damake Damerati (25), Workicho Kidir (20), Tamasgen Lamango (20), Sambatno Asafa (23), Takatare Tsagaye  (22), Takala Aniko (17), Kabada Tadewose (16), Mide Mhamade (25) Dandem Deledele (23), Dagenet Wolede (25) , Gelachu  Tadese (20), Lere Abdella (18)  na Thomas Kibamo (21).
Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa kituo kikuu cha Polsi cha Chumbageni na wanahojiwa na mara baada kukamilika upelelezi watafikishwa mahakamani kujibu tuhumza za kuingia nchini bila kibali.
Alisema mbali ya wahamiaji hao pia inawashikilia Watanzania watano kwa tuhuma za kuwasafirisha Waethopia hao akiwemo dereva wa Fuso Khamis Ally (31) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam pamoja na utingo na watu waliokuwa ndani ya gari hilo.
Aliwataja watu hao kuwa ni Ally Haruni (17) ambaye ni utingo mkazi wa Tegeta, Mussa Shaban (30) fundi gari mkazi wa Kinondoni MkwajuniYohana Teherera (22) mfanyabiashara wa Dar es Salaam na Fadhilui Hussein  (27) fundi muashi na mkazi wa Muheza Tanga.
“Wale wahamiaji walikuwa wamewekwa katika fuso huku mlangoni walikuwa wameweka mikungu ya ndizi pamoja na pembezoni kwa ubavu wa gari ili kuwalaghai polisi njiani ambapo njama zao ziligonga mwamba” alisema Mombeji na kuongeza
“Wakati gari iliposimamishwa na askari wanalikagua walipoulizwa wakadai kuwa wamepakiza ndizi na kupeleka Dar es Salaam---mara wakasikia watu wanakohowa na minong’onomong’ono na kugundua rundo la watu ndani” alisema
Kamanda alisema watu wote wanashikiliwa na polisi kituo kikuu cha Chumbageni pamoja na gari kwa mahojiano na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhumza za kusafirisha wahamiaji haramu.





 Wahamiaji haramu 45 wenye asili ya Kiethopia wakiwa katika uwanja wa ndani ofisi za Uhamiaji Tanga jana waliokamatwa Mombo Wilayani Korogwe waliokuwa wakisafirishwa kuelekea Dar es Salaam kwa kutumia gari aina ya Fuso.

NJOO WEWE NA YULE KATIKA ‘SKYLIGHT SUNDAY BONANZA’‬ KIOTA CHA ESCAPE ONE LEO JIONI

November 08, 2015


Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha sehemu ya mashabiki wao sambamba na Sony Masamba jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza‬ kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam na hivi leo mwendo ni ule ule na speed 120.(Picha na Geofrey Adroph wa pamoja blog).
Rapa Joniko Flower akichuana na mmoja wa shabiki wa Skylight Band staili mbalimbali za sebene huku mashabiki wengine wakiangalia na kuiga miondoko hiyo.
Msanii Em Evans kutoka bendi ya Wana Njenje akijumuika kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band jumapili iliyopita kwenye kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar…Kwa mbali ni Tophy Bass akicharaza nyuzi kisawa sawa.
Msanii Em Evans kutoka bendi ya Wana Njenje sambamba na Kasongo Junior wa Skylight Band katika kolabo matata sana kuonyesha kipaji chao, njoo leo uwashuhudie Live kiota cha Escape One Mikocheni.
Em Evans na Kasongo Junior wakiendelea kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi kutoka Skylight Band, Joniko Flower katika hisia kali kuwapa raha mashabiki wake kiota cha Escape One, Mikocheni jumapili iliyopita ambapo leo pia mwendo ni ule ule, bila kukosa njoo wewe na yule waambie na wengine pia bila kukosa katika fukwe tulivu kabisa.
Kasongo Junior katika hisia kali sambamba na Joniko Flower kwenye kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Kasongo Junior na Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Bamutu wa Congo wakiburudisha mashabiki wa Skylight Band Joniko Flower na Sony Masamba ni ndani ya kioata cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Sam Mapenzi akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Sony Masamba na Joniko Flower kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

November 08, 2015

  
jpm
   Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli jana asubuhi katika Ikulu ya Dar es Salaam  amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka  mara baada ya  kuapishwa.
     “Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.
     Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.
     Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.
     Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:
Kuanzia mwezi  Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa utekelezaji Suala la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa  na mabalozi wa Tanzania  wanaowakilisha nchi  huko nje.
Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.
     Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa  kufanyiwa  kazi mapema  zaidi.
     Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais  ama Makamu wake.
     Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali  kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.
     “Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya kazi.
Imetolewa na Premi Kibanga, Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi Ikulu, DAR ES SALAAM.