NAIBU SPIKA DK. TULIA AKSON AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA “MBEYA TULIA MARATHON 2018”

NAIBU SPIKA DK. TULIA AKSON AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA “MBEYA TULIA MARATHON 2018”

May 06, 2018
 



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mbio za Mbeya Tulia Marathon 2018 zilizofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo, Mbio hizo Zimeshirikisha wanariadha mbalimbali wakiwemo wakenya na watanzania pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi wa mkoa wa Mbeya , kumekuwepo na washiriki wa mbio mbalimbali zikiwemo za Kilomita 41, kilomita 21, Kilomita 5, Kilomita 2, Mita 100, Mita 400 na Mita 800.

Dk. Tulia Akson Naibu Spika wa Bunge amewashukuru wadhamini mbalimbali ambao wamewezesha kufanyika kwa mbio hizo kwa mafanikio makubwa mbali ya changamoto ndogondogo ambazo zitaendelea kuboreshwa katika maandalizi ya mbio zingine zitakazofanyika mwakani jijini Mbeya.



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akihojiwa na Mtangazaji wa Kituo Cha Luninga cha Clouds TV Hassan Ngoma kuhusu mafanikio ya mbio hizo za Mbeya Tulia Marathon 2018.




Mmoja wa wananchi waliohudhuria ili kushuhudia mbio hizo akisoma kipeperushi cha Bahati nasibu ya Mzuka huku akifurahia jambo katika kipeperushi hicho.



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akianzisha Mbio za mita 100 katika mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 zilizowahusisha viongozi wa serikali , Wabunge na Madiwani kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo,




Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku pamoja na baadhi ya wabunge wakishiriki mbio za mita 100 kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati wa mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 jijini Mbeya.



Watoto wakishiriki mbio za mita 1500.



Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio hayo.



Washiriki wa mbio za Baiskeli Kilomita 150 wakiingia uwanja wa Sokoine mara baada ya kumaliza mbio hizo.



Wananchi wakifuatilia matukio.



Afisa Mkuu wa Masoko, wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi wa Tatu Mzuka na maofisa wa Tatu Mzuka Kulia ni Barbara Hassan Matangazaji wa Clouds Radio na Mwanamuziki wa Bongo Fleva Fid Q.



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akicheza Muziki wa Kwaito pamoja na baadhi ya wabunge na viongozi wa Serikali.



Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande akikabidhi king’amuzi na Dishi kwa washindi mbio za Kilomita 21. wanawake.



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akifurahia jambo wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande akizungumza kwenye uwanja wa Sokoine mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo.



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akifurahia jambo wakati Afisa Mkuu wa Masoko, wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza kwenye uwanja wa Sokoine mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo.



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akisikiliza wakati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania RT Mh. Anthony Mtaka akizungumza .

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala akielezea jambo wakati alipokuwa akisifu umakini wa Naibu Spika Tulia Akson na kazi kubwa anayoifanya kusaidia jamii kupitia mfuko wa Dk. Tulia Trust.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala na Naibu Spika Dk.Tulia Akson wakipiga picha ya pamoja na washindi wa mbio za kilomita 21.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande akiwavisha medali washindi wa mbio za kilomita 41.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande na Naibu Spika Dk. Tulia Akson pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala wakipiga picha ya pamoja na washindi mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

Baadhi ya washindi wa mbio hizo wakipiga picha huku wakiwa wameshika zawadi zao za ving’amuzi.

SERIKALI KUTUMIA BILIONI 131.47 KUTEKELELEZA MIRADI YA KIMKAKATI

May 06, 2018

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susan Mkapa (kushoto) na Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Mgonya Benedicto, wakifuatilia tukio la Uzinduzi wa Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akitia saini moja ya mikataba Serikali kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
Wadau kutoka Sekta mbalimbali wakiwemo wabunge, wakurugenzi wa TAMISEMI na viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango waliohudhuria Uzinduzi wa Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo (Mb).


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo (Mb) wakinyanyua vitabu vya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa-TAMISEMI, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusaini mikataba ya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, Serikali imezindua Mkakati wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea.

Mkakati huo umezinduliwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambapo amesema kiasi cha shilingi bilioni 131.47 kitatumika kutoa ruzuku ya utekelezaji wa miradi 22 kwa halmashari 17 zilizoko katika mikoa 10 nchini, katika mwaka wa fedha 2018/19.

Ameitaja mikoa hiyo ambayo Halmashauri zake zimekidhi vigezo vya kunufaika na miradi ya kimkakati katika awamu ya kwanza ya mpango huo kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Morogoro, Mtwara, Pwani, Simiyu na Songwe.

Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa Halmashuri zinajenga uwezo wa kujitegemea kwa takribani asilimia 80 hadi 100 ifikapo mwaka 2025, badala ya hali ya sasa ambapo halmashauri hizo zinategemea ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa zaidi ya asilimia 88.

Amezitaka halmashuri zitakazopata fedha za miradi hiyo kuhakikisha fedha hizo zinawekezwa kwenye miradi yenye tija, inayokuza ajira kwa wananchi na kuongeza mapato ya halmashauri.

Ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri kubuni miradi ya kibiashara kwa ajili ya wananchi wanaowaongoza kwa kutengeneza ajira kwa kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Alionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watendaji wanaosimamia miradi hiyo ikiwa watatumia fedha hizo kwa malengo tofauti na yaliyokusudiwa na kurejea kauli ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwamba kufuja fedha za Serikali katika kipindi hiki ni sawa na kunywa sumu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, amesema kuwa Serikali inazo fedha za kutosha kufanikisha mkakati huo na kutoa wito kwa viongozi wa Mikoa husika kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanisha miradi yenye tija ili ipatiwe fedha.

Alifafanua kuwa tayari Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati katika mkoa wa Dar es Salaam katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwa kujenga Kituo cha Mabasi cha Mbezi Luis, Ujenzi wa Soko la Mburahati katika Manispaa ya Ubungo, Ujenzi wa Soko la Kisasa la Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni na Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu, Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti katika Manispaa ya Ilala.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Selemani Jaffo (Mb) amesema kuwa Ofisi yake itaanza kufuatilia na kupima utendaji kazi wa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini ili kuona kama wanaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliwapongeza Wakurugenzi walioonesha mfano katika kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kubuni miradi yenye tija na ya kimkakati iliyopewa Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango na kuwataka watendaji wengine waige mfano huo.

Baadhi ya miradi itakaotekelezwa na Halmashauri zilizokidhi vigezo ni pamoja na Ujenzi wa Masoko ya Kisasa, Ujenzi wa Maegesho ya Malori, Ujenzi wa stendi za kisasa, Maghala ya kuhifadhi mazao, Masoko ya Kisasa, Machinjio na Ujenzi wa Viwanda.
RAIS DK.SHEIN AONGOZA MKUTANO WA MABALOZI WA WILAYA YA KASKAZINI “A’ UNGUJA

RAIS DK.SHEIN AONGOZA MKUTANO WA MABALOZI WA WILAYA YA KASKAZINI “A’ UNGUJA

May 06, 2018

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini “A” Bw.Ali Makame alipowasili katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A” CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo –Mahonda
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT Taifa Mhe.Thuwaiba Edington Kisasi alipowasili katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A” CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo –Mahonda
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT Taifa Mhe.Thuwaiba Edington Kisasi (kushoto) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Iddi Ali Ameir,Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Mohamed (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanziar Dk.Abdalla Juma Saadala (Mabodi) wakisimama wakati ulipoimbwa Wimbo wa “Sisi Sote Tumegomboka” katika Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A” CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo katika Ukumbi wa CCM–Mahonda
Baadhi ya Mabalozi wakiimba Wimbo wa “Sisi Sote Tumegomboka” katika Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A” CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo katika Ukumbi wa CCM–Mahonda mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na katika Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A” CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja–Mahonda(kushoto) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Iddi Ali Ameir,
Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar (NEC),Washauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine wakiwa katika Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A” CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja–Mahonda
Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A”Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao leo katika Mkutano wa Kuimarisha Chama cha Mapinduzi katiika Mkoa huo katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja-Mahonda
Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A”Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao leo katika Mkutano wa Kuimarisha Chama cha Mapinduzi katiika Mkoa huo katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja-Mahonda,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wazee wa Wilaya ya Kaskazini “A” leo Bi,Siti Ali Haji jimbo la Kijini (kulia) na Mzee Makame Haji –Chaani (katikati) baada ya Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Kaskazini “ A” CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika katika Ukumbi wa Jengo la CCM Mkoa wa Kaskazini –Mahonda

Picha na Ikulu

WAINGEREZA WAVUTIWA KUWEKEZA SELOUS, DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUWEKWA MAKUBALIANO YA AWALI (MOU)

May 06, 2018


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara (hayuko pichani) kushirikiana na wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuandaa mkataba wa makubaliano ya awali (MoU) ya uwekezaji katika sekta ya utalii kwenye Pori la Akiba Selous, ofisini kwake Jijini Dodoma juzi. Wawekezaji hao pichani ni Eva Sanchez na Nicholas Negre.


Na Hamza Temba-WMU-Dodoma
..............................................................


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza uandaliwe mkataba wa makubaliano ya awali (MoU) ya utekelezaji wa mradi wa kuendeleza utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.


Mkataba huo wa makubaliano utahusisha wawekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na utakapokamilika utasainiwa na pande zote mbili.


Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi ofisini kwake Jijini Dodoma kufuatia maombi yaliyowasilishwa kwake na wawekezaji hao, Eva Sanchez na Nicholas Negre.


Akiwasilisha maombi hayo, Sanchez amesema mradi huo utakuwa wa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA ambao ndio wasimamizi wakuu wa Pori la Akiba Selous utakapoanzishwa mradi huo.


Amesema pamoja na mambo mengine mradi huo wa utalii wa picha pia utasaidia kupiga vita ujangili na kukuza uchumi wa jamii zinazozunguka pori hilo.


Dk. Kigwangalla amewataka wawekezaji hao kuwasilisha andiko la mradi huo, kufanya utafiti wa kina na tathmini ya athari za kimazingira zitakazoweza kujitokeza kutokana na uanzishwaji wa mradi huo.


Amesema kwa sasa Serikali inafanya marekebisho ya Sheria mbalimbali zitakazoiwezesha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kutekelezaji majukumu yake ipasavyo ikiwemo uwekezaji wa aina hiyo kwenye sekta ya Utalii wa Picha na Uwindaji wa Kitalii.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara amesema mamlaka hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji hao ili kutimiza azma ya Serikali ya kushirikisha wadau, watu binafsi na wawekezaji katika kukuza sekta ya utalii nchini.


Pori la akiba Selous ndio hifadhi kubwa kuliko zote nchini ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba takriban 50,000 katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Mwaka 1982, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Uneso) lilitangaza eneo hilo kuwa moja ya eneo la Urithi wa Dunia na kuanza kuhifadhiwa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na muwekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza, Eva Sanchez ofisini kwake Jijini Dodoma juzi alipowasilisha ombi lake la kuwekeza kwenye sekta ya utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara (kulia) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji huo.

Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Imani Nkuwi (aliyesimama) akifafanua jambo kuhusiana na uwekezaji huo.

Waziri Kigwangalla akisisitiza jambo katika kikao hicho.

Waziri Kigwangalla akitoa maelekezo katika kikao hicho.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na muwekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza, Eva Sanchez ofisini kwake Jijini Dodoma juzi baada ya kupokea ombi lake la kuwekeza kwenye sekta ya utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.

Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous Eva Sanchez na Nicholas Negre, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara (kushoto) na Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Imani Nkuwi (kulia).
CANACO YAPEWA SIKU SABA KUWASILISHA MKATABA SERIKALINI

CANACO YAPEWA SIKU SABA KUWASILISHA MKATABA SERIKALINI

May 06, 2018

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya mkoa wa Tanga yenye lengo la kukagua shughuli za madini pamoja na kuzungumza na wananchi tarehe 05 Mei, 2018. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.



Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika eneo la kampuni inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited.



Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( wa pili kutoka kulia) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kampuni inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited.



Mmoja wa watendaji wa kampuni ya Tanzania Gold Field Limited, Robert Slavik (kulia) akielezea namna kampuni yake ilivyoingia makubaliano na kampuni ya CANACO Tanzania Limited kwenye shughuli za uchimbaji madini kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( wa pili kutoka kulia)



Sehemu wa wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.



Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga, Mhina Kaoneka akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko(hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.



Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga, Michael Andrea akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko(hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.



Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akifafanua jambo mbele ya wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.



Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe (kushoto) akielezea mchango wa sekta ya madini kwenye wilaya yake mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia).

…………………..

Na Greyson Mwase, Tanga

Mei 05, 2018

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameipa siku saba kampuni inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited, kuwasilisha mikataba na nyaraka zote kati yake na kampuni ya Tanzania Gold Field Limited ili kubaini namna makubaliano ya mkataba yalivyofanyika ikiwa ni pamoja na ulipaji kodi serikalini,

Biteko aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga mara baada ya kufanya ziara katika kampuni ya CANACO Tanzania Limited na kutoridhishwa na utendaji wa kampuni hiyo.

Waziri Biteko yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua shughuli za madini pamoja na kuzungumza na wananchi na kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika shughuli za madini.

Alisema mara baada ya kufanya ziara katika kampuni ya CANACO Tanzania Limited, amebaini kuwa kampuni hiyo mara baada ya kukamilisha shughuli zake za utafiti wa madini ya dhahabu, kampuni hiyo iliikaribisha kampuni nyingine ijulikanayo kama Tanzania Gold Field Limited ya Canada kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo la Magambasi wilayani Handeni mkoani Tanga pasipo kufuata taratibu za kisheria.

Aliendelea kusema kuwa, kampuni ya Tanzania Gold Field Limited iliwataka wachimbaji wadogo waliokuwa wanaendelea na shughuli za uchimbaji madini katika eneo hilo kuondoka ili waanze uchimbaji madini jambo ambalo lilitekelezwa.

Alieleza kuwa, kampuni ya Tanzania Gold Field Limited ilianza shughuli zake bila kuwasilisha makubaliano ya kimaandishi kati yake na kampuni ya CANACO Tanzania Limited Serikalini pamoja na kodi jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.

Biteko aliendelea kusema kuwa kampuni inayotambulika mpaka sasa kisheria ni ya CANACO Tanzania Limited ambapo shughuli za madini katika eneo la Magambasi zimekuwa zikifanyika bila kufuata sheria na kanuni za mazingira.

“Haiwezekani wachimbaji wadogo ambao ndio wamiliki wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wakaondolewa halafu akapewa mwekezaji mkubwa ambaye mpaka sasa hakuna kilichofanyika zaidi ya kuchejua mabaki wa udongo wenye dhahabu na kuuza na kuharibu mazingira huku wachimbaji wadogo wenye uwezo wa kuchimba dhahabu wakihangaika na kuishi katika lindi la umaskini,” alisema Biteko.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko alimtaka Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Handeni, Idrissa Yahya kuanza kazi mara moja ya uchambuzi wa vipengele vyote vya sheria na kanuni za madini ili kuangalia namna vilivyokiukwa na kuwasilisha ripoti ofisini kwake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alimpongeza Naibu Waziri Biteko kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na kuahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Madini ili kuimarisha sekta ya madini katika wilaya yake.(Chanzo Fullshangwe Blog)