RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI PAMOJA NA JAJI KIONGOZI, PIA AAGANA NA BALOZI WA OMAN ANAYEMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI.

June 10, 2016

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Shaaban Ali Lila mara baada ya kumuapisha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali mara baada ya kumuapisha kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji Kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali (kulia)mara baada ya tukio la uapisho lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani mara baada ya tukio la uapisho wa Majaji hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani pamoja na Majaji mbalimbali wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwa furaha huku akiwa amemshika mkono Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila huku viongozi wengine wakishuhudia ikulu jijini Dar es Salaa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanyakazi hapa nchini.

NAIBU WAZIRI AKUTANA NA UJUMBE WA UNDP

June 10, 2016
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina akimkaribisha Bi. Awa Dabo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa. Mazungumzo baina yao yamefanyika leo Mtaa wa Luthuli, jijini Dar es Salaam.
 Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, kutoka kushoto ni Bw. Nehemia Murusuri, Bi. Getrude Lyatuu na Bi. Awa Dabo, walipomtembelea Naibu Waziri Mh. Luhaga Mpina hii leo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya mazungumzo baina yao.

Na Lulu Mussa
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina hii leo amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo pamoja na ujumbe aliombatana nao, Ofisini kwake Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao ujumbe huo umeonyesha nia ya kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Makamu wa Rais hususan katika nyanja ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na nishati mbadala.
Awali Naibu Waziri Mpina aliwafahamisha kuwa Ofisi yake imeandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kupanda miti nchi nzima na kuwataka wadau wa maendeleo kuwaunga mkono. "Tunaendelea na jitihada za kupanda Miti mingi iwezekanavyo na katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kazi hiyo" alisisitiza Naibu Waziri Mpina.
Aidha, Naibu Waziri Mpina ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuunga mkono kampeni hii kubwa ya upandaji miti nchi nzima na kusisitiza kuwa uhai wa viumbe vyote unategema Mazingira hivyo ni vema kuyahifadhi na kuyalinda kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mheshimiwa Mpina pia amesema Ofisi yake kwa sasa inafanya marekebisho ya Sera ya Mazingira na kujenga uwezo kwa watendaji wa ngazi zote juu ya kusimamia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 pamoja na kuelimisha Umma juu ya kampeni ya Usafi ya kila mwisho mwa mwezi.
kwa upande wake Bi. Dabo amesema kuwa shirika lake limeweka vipaumbele vya kutekeleza ndani ya miaka mitano ambavyo vinaendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa, sambamba na kusaidia vikundi mbalimbali katika ngazi za vijiji juu ya kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira.
Bi Dabo ameahidi kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais katika jitihada za  kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi.

USAJILI WANANCHI VITAMBULISHO VYA TAIFA KUKAMILIKA NCHI NZIMA DESEMBA 31 MWAKA HUU

June 10, 2016

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bi. Rose Mdami, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Saalam. Katika kikao hicho NIDA iliwasilisha mpango usajili kufikia 31 Desemba 2016 ambapo usajili utakamilika nchini nzima na wananchi kuanza kutumia namba ya utambulisho kupata huduma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Mifumo ya Komputa (TEHAMA) Ndugu Mohamed Khamis, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho Ndugu Alphonce Malibiche
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Mifumo ya Komputa (TEHAMA) Ndugu Mohamed Khamis, akifafanua namna mwananchi anaweza kutumia tovuti salama kujua taarifa zake wakati wa kikao na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa NIDA Bi Rose Mdami.

Serikali imekusudia kukamilisha Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wote kufikia Desemba 31 mwaka huu.

Akuzungumza na vyombo vya habari leo, msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Rose Mdami, amesema NIDA imepanga kutumia taarifa za NEC kukamilisha usajili wa awali na kutoa namba ya Utambulisho kwa wananchi wote ambao hawakusajiliwa katika mfumo wa NIDA.

Akifafanua, Bi Rose amesema baada ya kuhakikisha kila mwananchi ana Nambari ya Utambulisho, kila mwananchi atalazimika kukamilisha usajili wake ikiwa ni hatua ya kujaza vipengele vya maswali vilivyobakia katika fomu ya maombi ya vitambulisho kabla ya kupata utambulisho kamili.

“kama mnavyofahamu, katika usajili wa NEC fomu ilikuwa na vipengele 32 vya kujaza kulinganisha na fomu ya NIDA ambayo ina vipengele 74, hivyo ni lazima kila mwananchi kutambua, ili kuwa na utambulisho kamili lazima kujaza vipengele vilivyobaki pamoja na kuambatanisha nakala ya viambata vyake muhimu kuthibitisha taarifa za umri, uraia na makazi” alisisitiza.

Amesema lengo la kuanza kutoa namba ya utambulisho ni kuwawezesha wananchi kuanza kufaidi huduma zinazotolewa, wakati uzalishaji Vitambulisho ukiendelea. Uwezo wa mashine za NIDA ni kuzalisha vitambulisho 24,000 kwa siku hivyo itachukua muda kukamilisha uchapishaji wa vitambulisho kulingana na idadi ya Watanzania, Wageni na Wakimbizi watakao andikishwa.

Akifafanua namna NIDA ilivyojipanga kuhakikisha zoezi la usajili linakamilika kwa wakati iliyojiwekea, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho Ndugu Alphonce Malibiche, amesema NIDA imeshapokea BVR Kit 5000 na kwakuwa NIDA tayari ilishakuwa na MEU (Mobile Enrolment Unit) 1500, vifaa hivi vitasambazwa nchi nzima mpaka ngazi ya Kata ambapo wananchi watasajiliwa kwa hatua zote; lengo ni kuwafikia wananchi ambao hawakujisajili kupiga kura na vijana wanaotimiza umri wa miaka 18.

“NIDA imejipanga kuchakata taarifa za NEC na kuingiza taarifa hizo katika mfumo wa NIDA utakaoondoa durufu ili kuruhusu majina kupelekwa kwenye Kamati za Ulinzi na Usalama kwa uhakiki pamoja na kuruhusu wananchi kuweka mapingamizi kwa wale wote watakaotiliwa shaka ya uraia”.

Amesema NIDA itatumia mbinu zote katika kusambaza namba za Utambulisho mpaka vijijini, pamoja na kutumia ofisi za NIDA zitakazofunguliwa katika Wilaya zote nchini, kuwezesha kuanza kwa matumizi ya utambulisho yatakayojikita katika huduma mbalimbali zitolewazo nchini.

Akipambanua namna mfumo wa Utambulisho wa Taifa utakavyotumika katika kutoa huduma mbalimbali, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi Mifumo ya Kompyuta ndugu Mohamed Khamis amesema tayari NIDA imeshabuni mifumo mbalimbali itakayotumika kusoma taarifa katika mfumo Mama (Kanzidata) ya NIDA ikiwemo tovuti salama ambayo itamwezesha mtoa huduma kusoma taarifa za mteja wake mahali alipo kwa idhini itakayotolewa na mteja mwenyewe.

Amesema mfumo huu wa kitaalamu umebuniwa katika kumrahisishia mwananchi kupata huduma pamoja na kufuatilia hatua ya usajili wake ilipofikia. Mbali na tovuti salama pia njia ya SMS itatumika kusoma taarifa za mwombaji.

Katika hatua zote hizi suala la usalama wa taarifa limezingatiwa na hakutakuwa na taarifa za mwananchi zitakazosomwa bila idhini ya mhusika ambaye ni mmiliki wa Utambulisho/kitambulisho.

“kupitia mfumo huu wa NIDA Serikali itaweza kubaini na kuondokana kabisa na tatizo la wafanyakazi hewa kwani namba ya utambulisho niya kipekee na hivyo hakutakuwepo durufu ya taarifa” alisema.

Tayari NIDA imeshaanza mazungumzo na Utumishi kufanya usajili wa watumishi Nchi nzima ili mfumo wa mishahara kuunganishwa na mfumo mama wa taarifa (Kanzidata) NIDA.

Mpaka sasa NIDA imekamilisha ujenzi wa miundombinu na kusajili wananchi katika mikoa ya Dar-es- salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga, Morogoro na Zanzibar.

Zaidi ya vitambulisho mil 2.7 vimeshagawanywa kwa wananchi na kuanza matumizi katika baadhi ya huduma zikiwemo za kibenki katika baadhi ya mabenki nchini.

TANZANIA NA ZAMBIA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA MAZAO YA MISITU NA MAGOGO KUPITIA MIPAKA YA NCHI HIZO

June 10, 2016

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Zambia,  jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususan magogo katika mipaka ya nchi hizo mbili. Wanaoshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili, Gladynes Mkamba na Kaimu Mtendaji Mkuu TFS, Richard Kamwenda (kushoto). Waliosimama kulia ni Mwanasheria wa TFS, David Mung’ong’o na Mwanasheria wa Wizara ya Maliasili, Stephen Mwamasenjele. 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda akisaini  makubaliano hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakibadilishana hati ya makubaliano waliyosaini kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi hizo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza katika hafla fupi ya kuweka makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Zambia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi hizo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda. Maj. Gen. Milanzi alisema kuwa ushirikiano huo utaleta tija katika udhibiti wa biashara haramu ya uvunaji na usafirishaji wa magogo kutoka katika nchi hizo kwenda nchi nyingine kupitia mipaka ya nchi hizo na bandari ya Dar es Salaam. Aliwataka watanzania wanaojihusisha na biashara haramu ya uvunaji na usafirishaji wa magogo nje ya nchi waache mara moja kwani Serikali imejipanga kuhakikisha wanakamatwa na sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiteta jambo wakati wakikagua Makontena 103 ya magogo (nyuma pichani) yaliyokamatwa hivi karibuni katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao wamesaini makubaliano ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo kwenye mipaka wa nchi hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiangalia sehemu ya magogo yaliyokamatwa hivi karibuni katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao wamesaini makubaliano ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo kwenye mipaka wa nchi hizo. (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)