mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho
ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani
Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike akimuelewesha mkulima jinsi kampuni yao inavyofanya kazi ya kusambaza teknolojia ya umwagiliaji wa Matonye
Washiriki ambao ni wakulima wakifuatilia kwa makini mada ambazo zilikuwa zikiendelea wakati wa ufunguzi
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
sekta
ya kilimo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufugaji holela , ambao hupelekea uharibifu wa mazingira,Teknolojia duni
pamoja na ugumu wa kupata mitaji ya kuboresha miundombinu ya kilimo.
Hayo
yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho
ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani vilivyopo ndani ya jijini Arusha ambapo ni
mara ya kwanza kufanyika .
Alisema
kuwa sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto za ufugaji holela ambao
unasababishwa na wafugaji ,wakulima kutumia teknolojia duni au zazamani katika
ukulima pamoja na wakulima wengi kukosa
mitaji ya kubesha miundo mbinu ya kilimo
Alisema
kuwa hii inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha maendeleo ya sekta hii
kutokana na wananchi wengi kutumia kilimo cha kawaida badala yakutumia kilimo
cha kisasa ambacho kinaleta tija .