Internews Tanzania yawakutanisha wanahabari kujadili Sheria ya Mtandao na Takwimu

Internews Tanzania yawakutanisha wanahabari kujadili Sheria ya Mtandao na Takwimu

January 18, 2017
Mkurugenzi wa Miradi wa Internews Tanzania, Wenceslaus Mushi akizungumza na washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika majadiliano ya Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Miradi wa Internews Tanzania, Wenceslaus Mushi akizungumza na washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika majadiliano ya Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam.Mmoja wa wadau wa habari (kulia) akiwasilisha mada katika mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania. Mmoja wa wadau wa habari (kulia) akiwasilisha mada katika mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania.Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania. Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania.Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania. Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews TanzaniaSehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Wamiliki na Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (TBN-Bloga ) akiwa katika mjadala huo. Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Wamiliki na Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (TBN-Bloga ) akiwa katika mjadala huo.Mmoja wa wadau wa habari (katikati) akiwasilisha mada katika mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi wa Internews Tanzania, Wenceslaus Mushi. Mmoja wa wadau wa habari (katikati) akiwasilisha mada katika mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi wa Internews Tanzania, Wenceslaus Mushi.Mwanasheria na Mwanahabari, James Marenga akiwasilisha mada kwa washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika majadiliano ya Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mwanasheria na Mwanahabari, James Marenga akiwasilisha mada kwa washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika majadiliano ya Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu leo jijini Dar es Salaam.
___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

MADAKTARI BINGWA KITUO CHA MOYO CHA JKCI WAFANIKIWA KUPANDIKIZA MISHIPA YA DAMU KWENYE MOYO BILA KUTUMIA MASHINE YA MAPAFU NA MOYO

January 18, 2017
 Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kituo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Evarist Nyawawa (kushoto) na  Dk Hussein Hassanali wakimfanyia upasuaji mmoja wa wagonjwa ambapo wengine huwapandikiza mishipa ya damu kwenye moyo juzi katika kituo hicho kilichopo Muhimbili, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Madaktari mbalimbali wakiendelea na kazi katika chumba cha upasuaji moyo
 Mmiliki wa Blog hii ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda (katikati) akiwa na wanahabari wenzie wakijiandaa kufanya coverage kwenye chumba cha upasuaji
 wakiendelea na upasuaji
 Mtaalamu wa Usingizi wa Kituo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Edwin Lugazia akitumia kompyuta kuhakikisha hakuna hitilafu yoyote inatokea kwa mgonjwa aliyekuwa anapandikizwa mishipa ya damu kwenye moyo  katika kituo hicho kilichopo Muhimbili, Dar es Salaam.

 Watalaaamu wa mashine ya mapafu na moyo Sophia Lukonge na Sylvester Mbunda wakiwa makini kuhakikisha mashine hizo hazipati hitilafu



 Wasaidizi wa chumba cha upasuaji wakiwa wamejipanga tayari kwa kazi. Kutoka kulia ni Hildegard Karau, Hania Bwahama na Faustina Mwapingo



HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 300 ZILIZOKUWA ZIENDE KWA KWA WAKANDARASI

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 300 ZILIZOKUWA ZIENDE KWA KWA WAKANDARASI

January 18, 2017

 Image may contain: 1
person, phone and indoor


Na Woinde Shizza,Arusha
Halmashauri ya jiji la Arusha imeokoa zaidi ya shilingi  milioni mia tatu sitini na nne  zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kuwapa wakandarasi  kwa jili ya kujenga madarasa  baada yake  kamati za shule kupewa jukumu la kusimamia ujenzi wa madarasa hayo badala ya mkandarasi

Hayo yamebainishwa na meya wa halmashaur i ya jiji la Arusha Kalist Lazarowakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa halmashauri yake wamekaa chini na kuona kuliko fedha hizo zipewe wakandasi ili wajengee madarasa ni bora fedha  za ujenzi wa madarasa zipelekwe katika kamati za
shule pamoja na bodi za shule ili wasimamie ujenzi huo

Alisema kuwa  sasa ivi halmashauri imetoa shilingi bilioni moja laki nne kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 56 ya shule za msingi na fedha zote zilishapelekwa  katika kamati za shule  ili waweze kusimamia ujenzi  mpaka ukamilike.

“zamani tulikuwa tunatumia wakandarasi kwa kutangaza tenda kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule za  msingi  ,lakini tangu tuanze kujenga madarasa kwa kupitia kamati za shule na sio  wakandarasi tumekuwa tunaokoa milioni mia tatu sitini nne  ambazo tumeziokoa tungetumia wakandarasi zote zingeingia katika mfuko wa mkandasi sasa ndio maana tumeamua kumtumia  kamati za shule kwa shule za msingii “alisema Kalist

Aidha alisema kuwa jiji la Arusha kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto ambao wanaandikishwa darasa la kwanza tuofauti na mwaka huliopita kwani tangu zoenzi limeanza adi kufikia sasa wameshaandikisha wanafunzi wa darasa la kwaza zaidi ya elfu 12000 tofauti na mwaka uliopita 2016 ambapo watoto  elfu
tisa mia sita na mia waliandikishwa kuingia darasa la kwanza , ambapo alisema bado wanaendelea kuandikisha watoto adi mwezi march ili watoto wote waweze kwenda shule

Alisema kuwa kutokana na kuwepo na watoto wengi  waliojiandikisha kumekuwa na upungufu wa madarasa  hivyo halmashauri imejenga madarasa 56 kwa ajili ya watoto hao wapya na kukarabati madarasa manne ya shule ya msingi  ambayo yatasaidia kabisa kumaliza tatizo hili,ambapo alisema kuwa pia madarasa hayo yanaitaji madawati na hadi sasa halmashauri imeshatoa fedha kwa ajili
ya madawati 1380 ambayo watoto hao watakalia katika madarasa hayo mapya hivyo wanaimani kuwa watoto wote wanaoanza darasa la kwanza wataingia madarasani na kukaa katika madawati  na kusoma vizuri kama vile
inavyotakiwa.

Akifafanua kuhusu wanafunzi wa shule za sekondari alisema kuwa jiji la Arusha lilifaulisha kwa asilimia 92% wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza na kukakuwepo na upun gufu wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi hao lakini jiji limeshajipanga vyema na imeanza kujenga madarasa 25 kwa ajili ya shule
za sekondari na kiasi cha shilingi milioni 700 zimeshatumwa katika bodi za shule hizo na wanaimani adi ifike mwisho wa mwezi huu wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza wataingia  madarasani na kuendelea na
masomo kama kawaida.

“napenda ku sema kuwa hakuna mtoto ambaye amefaulu kuingia kidato cha kwanza ataacha kuingia darasani  ifikapo mwisho wa mwezi huu madarasa yatakuwa tayari na wanafunzi wote waliofaulu wataenda shule “alisema kalist

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA ELIMU KWA WADAU KUHUSU UALIBINO JIJINI MWANZA

January 18, 2017
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ufunguzi wa semina kwa wadau wanaosaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watu wenye ualibino, inayofanyika kwa siku nne kuanzia leo Jijini Mwanza. 

Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun ambapo imelenga kupanua uelewa kwa wanajamii/ wadau  kuhusu ualibino ili kusaidia kupambana na ukatili kwa watu wenye hali hiyo.
Binagi Media Group
Mwasisi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun, lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, akizungumza na wanahabari kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun nchini Tanzania, Bi.Vicky Ntetema, akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
Mkufunzi Dr.George Rhoades kutoka nchini Marekani, akitoa 
 Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino duniani, Under The Same Sun, limebainisha kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualibino nchini vinaendelea kupungua.

Mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Vicky Ntetema, ameyasema hayo leo Jijini Mwanza kwenye semna kwa wadau wanaofanya kazi kwa ukaribu na watu wenye uaribino kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo za kijamii, elimu na afya.

Ntetema amesema elimu inayoendelea kutolewa kwa wanajamii imesaidia kupunguza ukatili kwa watu wenye ualibino ikiwemo kukatwa viungo na mauaji licha ya kwamba kumekuwepo taarifa za makaburi ya watu wenye ualibino waliofariki kufukuliwa katika mikoa ya Kagera, Mbeya na Morogoro.

Mwasisi wa shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya wanafunzi zaidi ya 300 wenye ualibino wanaosomeshwa na shirika hilo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo amewasihi wanajamii kuondokana imani potofu juu ya watu wenye ualibino ili kutokomeza ukatili dhidi yao.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, amesema serikali imelenga kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualibino vinatokomezwa ambapo amesisitiza elimu zaidi kuendelea kutolewa kwa wananchi ili kufanikisha lengo hilo.

MADIWANI WA MANISPAA YA MOSHI WATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA)

January 18, 2017
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa ukaribisho wa Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi walipotembelea ofisi za mamlaka hiyo.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakifuatilia maelezo ya awali ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na  Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) alipokuwa akitoa neno la ukaribisho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond  Mboya akizungumza wakati wa utamburisho wa Madiwani waliotembelea ofisi za MUWSA.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi aliyeongozana na Madiwani wa Halmashauri hiyo akizungumza wakati wa  ziara ya madiwani katika ofisi za MUWSA.
Baadhi ya Madiwani wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa za Mamlaka hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Mipango na Huduma za Biashara Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Tumaini Marandu akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Madiwani waliofanya ziara katika ofsi za MUWSA.
Diwani wa kata ya Miembeni ,Mbonea Mshana akichangia jambo katika taarifa ya Mamlaka hiyo.
Diwani wa kata ya Kilimanjaro,Priscus Tarimo akichangia jambo mara baada ya kusikiliza taarifa ya Mamlaka hiyo katika utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka kwa wakazi wa manispaa ya Moshi.
Diwani wa kata ya Mabogini,Emanuel Mzava akichangia jambo katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Njoro ,Jomba Khoi akichangia jambo katika kikao hicho.
Diwani wa viti maalumu ,Mama Kowelo  akichangia katika kikao hicho.
Mkurugenzi ,Joyce Msiru akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizoibuliwa na madiwani katika kikao hicho.
Meneja Ufundi wa MUWSA ,Patrick Kibasa akitoa ufafanuz juu ya hoja zilizohusu masuala ya ufundi .
Kaimu Meneja Fedha wa MUWSA ,Rehema Minja akiteleza jambo katika kikao hicho.
Kaimu Meneja rasilimali watu wa MUWSA,Laurian Kessy akichangia jambo katika kikao hicho.
Mkaguzi wa ndani wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Benson Maro akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia maelezo wakati a mjadla katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi.(kushoto).
Madiwani wakitembelea chanzo cha maji cha Shiri.
Chanzo cha Maji cha Shiri kilichopo wilaya ya Hai.
Madiwani wakiwa katika chanzo cha maji cha Shiri walipofanya ziara kutembelea vyanzo hicho na kupata maelezo.
Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Ufundi wa Mamlaka hiyo ,Patrick Kibasa namna maji yanavyotibiwa.
Madiwani wakiwa katika chanzo kipya  cha maji cha Mkashiringi .
Meneja Ufundi wa MUWSA,Patrick Kibasa akitoa maelezo kwa madiwani mara baada ya kutembelea chanzo cha maji cha Njoro ya Goha.
Madiwani wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) mara baada ya kuhitimisha ziara ya kutembea ofisi hizo pamoja na vyanzo vya maji.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.