Wakurugenzi, Waganga Wakuu itangazeni NHIF- Waziri Jaffo

Wakurugenzi, Waganga Wakuu itangazeni NHIF- Waziri Jaffo

April 16, 2016

NH1 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jaffo akizungumza na uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa kupokea msaada wa Magodoro 60 kutoka NHIF, kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Elizabeth Omingo na kushoto ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko NHIF.
NH2 
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Elizabeth Omingo akiongozana na Naibu Waziri (TAMISEMI) Seleman Jaffo wakati wa kupokea msaada kutoka NHIF.
NH3Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Rehani Athumani akitoa maelezo ya awali juu ya misaada ambayo Mfuko umetoa katika maeneo mbalimbali.
NH4 
Naibu Waziri Mh Suleiman Jafo akipata maelezo wodini kutoka kwa mganga mkuu wahospitali  ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Elizabeth Omingo
NH5 
Naibu Waziri Suleiman Jaffo akipokea msaada wa magodoro 60 kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Msoko NHIF Bw. Rehani Athumani.
NH6 
Naibu Waziri Suleiman Jaffo akisikiliza jambo kutoka kwa Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma Grace Michael kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko Bw. Rehani Athumani.
NH7 
Naibu Waziri Suleiman Jafo akielezea mikakati ya Serikali ya awamu ya tano katika uboreshaji wa huduma.
NH8 
Magodoro yakishushwa tayari kwa kupokelewa.
NH9
NH10 
Kazi ikiendelea.
……………………………………………………………………………………………………
Na Grace Michael
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jaffo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Waganga wa Wilaya kuhakikisha wanatoa elimu ya umuhimu na matumizi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watumishi wengine ili waweze kunufaika na huduma hizo.
Mbali na hilo, ameupongeza Mfuko huo kwa jitihada ambazo umekuwa ukifanya katika kushughulikia changamoto mbalimbali hususan za huduma za matibabu katika maeneo yote wanapokutana nazo.
Hayo ameyasema wilayani Kisarawe wakati akipokea msaada wa magodoro 60 kutoka NHIF ambao ambao umekabidhiwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo kwa lengo la kusambazwa katika vituo vya afya ambavyo vina uhitaji mkubwa.
“Katika hili NHIF mmefanya vizuri sana ….na sio hapa tu, nimekuwa nikipita katika maeneo mbalimbali na taarifa zenu nakutana nazo kuwa mmekuwa wepesi sana katika kushughulikia matatizo hasa ya uboreshaji wa huduma za afya pale mnapokutana nayo,”
“Mmeboresha sana huduma zenu kwa wanachama wenu hasa kwa kupanua wigo wa vituo vya kutolea huduma hatua inayowawezesha wanachama kupata huduma mahali popote wanapotaka wao…sasa naomba viongozi wa halmashauri hakikisheni mnawapa elimu watumishi na wananchi kwa ujumla juu ya huduma hizi za Mfuko,” alisisitiza Naibu Waziri Jaffo.
Akitoa maelekezo ya mgao wa magodoro hayo, alimtaka Mganga Mkuu kutoa kipaumbele katika Vituo vya Afya vya Mwanerumango, Masaki na Mzenga kwa kuwa vina uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo.
Kwa upande wa NHIF, akikabidhi magodoro hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani alisema kuwa Mfuko ulibaini changamoto ya ukosefu wa magodoro wilayani humo wakati ilipopita kwa ajili ya ugawaji mashuka hivyo Mfuko ulidhamiria kuondoa tatizo hilo.
“Tulipita katika vituo mbalimbali wilayani hapa wakati tunagawa mashuka siku ya sherehe za Uhuru ambapo Mfuko pia ulishiriki katika kufanya usafi katika vituo hivyo…baada ya kuona tatizo hilo Uongozi wa Mfuko uliona kuna haja kubwa ya kubana matumizi katika maeneo mengine kwa lengo la kuwasaidia wananchi,” alisema Bw. Rehani.
Alisema kuwa jitihada za kubana matumizi zimeuwezesha Mfuko kutoa misaada ya Magodoro 60 wilayani Kisarawe, mabati 400 katika zahanati ya Mpingi, Songea Vijijini, Vitanda 20 na magodoro 20 katika kituo cha afya cha Mjimwema mkoani Ruvuma pamoja na saruji tani tatu katika Shule ya Sekondari ya Kilangalanga.
“Mfuko huu ni wa Watanzania wote sisi tumepewa dhamana ya kuusimamia hivyo ni lazima twende na kasi ambayo Rais wetu anaitaka kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania na niseme tu kwamba Huduma bora za Afya Tanzania inawezekana.

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLYOVER) MAKUTANO YA BARABARA YA MADELA NA NYERERE

April 16, 2016

 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa  alipowasili kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Dkt Norman Sigalla  alipowasili kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani alipowasili kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na balozi wa japan nchini Mhe  Masaharu Yoshida alipowasili  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa kampuni ya SOMITOMO alipowasili  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea saluti toka kwa Afisa Mwandamizi wa Uhamiaji alipowasili  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema alipowasili  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe Raymond Mushi  alipowasili  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Meya wa Temeke Mstahiki Abdallah Chaurembo alipowasili  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulika Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora  alipowasili  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale kabla ya  kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Mbunge wa Segerea  Mhe Bonna Kaluwa kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.

 Msanii akicheza na nyoka
 Wimbo wa Taifa
 Baadhi ya wafanyakazi wa mradi huo
 Brass Band ya Polisi ikiongoza Wimbo wa Taifa

 Wanahabari kazini
Mkuu wa Mkoa wa Dar  es salaam Mhe Paul makonda akiongea wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akisoma muhtasari wa Mradi kabla ya  kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Bi. Tuma Abdallah na Timu yake walikuwepo. Makao Makuu ya shirika hilo lipo jirani na TAZARA
Sehemu ambapo mradi utapita
Mwanahabari akipiga picha sehemu ya maeneo ya Mradi
balozi wa Japan akiongea
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Dkt Norman Sigalla  akiongea wakati wa  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
Meya wa Temeke Mstahiki Abdallah Chaurembo akisalimia wananchi kwenye hafla ya  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akisalimia wananchi
Naibu waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani alipowasili kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa  akiongea wakati wa kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa TANROADS katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa TANROADS katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Balozi wa Japan Nchini Mhe Masaharu Yoshida akifungua pazia kuashiria  kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Balozi wa Japan Nchini Mhe Mashaharu Yoshida wakishangilia kuwekwa jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipena mikono na Balozi wa Japan Nchini Mhe Mashaharu Yoshida huku wakishangiliwa baada ya kuwekwa jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.

YANGA YASHIKA USUKANI WA LIGI KUU, YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0

April 16, 2016

 Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Majaliwa Shaban katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijii Dar es Salaam. Yanga imeshinda 1-0 na kufikisha pointi 59 na kuongoza katika msimamo wa Ligi huku ikifuatiwa na Simba yenye Pointi 57. (Picha na Francis Dande)
 Mshambukiaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar.
 Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Donald Ngoma akipiga kwa kisigino huku akizongwa na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicenti.
 Hapo je utaweza......
Mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu (kulia) akitafuta mbinu za Henry Joseph  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Henry Joseph akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe (kushoto).
 Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akichuana na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicent
 Henry Joseph akipeana mkono na kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi.
 Kocha na wachezaji wa Yanga wakitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo.
 Haruna Niyonzima akibadilishana mawazo na Simon Msuva baada ya mchezo kumalizika.
 Kocha wa Yanga, Mecky Maxime kulia akiwa na msaidizi wake Zuberi Katwila.
 Kikosi cha mtibwa Sugar kilichoanza leo
 Kikosi cha Yanga kilichoanza leo.

 Deus Kaseke akiwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar.
Simon Msuva akimtoka beki wa Mtibwa Sugar.