October 19, 2016
januar1
Kuanzia mwakani kila Mwanafunzi wa darasa la kwanza akiripoti atatakiwa kuja na mche wa mti na ataupanda na kuutunza kwa miaka yote saba na hatapewa cheti cha kumaliza darasa la saba kabla hajaonyesha mti wake. Katika shule zenye maeneo madogo, miti hiyo itapandwa katika maeneo yatakayoelekezwa na Serikali za Vijiji na Mitaa. Kwa wanafunzi wa Sekondari, itakuwa hivyo hivyo lakini itakuwa miti mitatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe January Makamba amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kuanzia mwakani itatoa maagizo kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anayeanza darasa la kwanza katika shule za serikali na zile za binafsi atahitajika kufika shuleni na mche mmoja wa mti siku  ya kuanza masomo ikiwa kama moja ya mahitaji ya msingi na kwa upande wa wanafunzi wa sekondari watapaswa kufika na miche mitatu wakati wa kuanza masomo.
Waziri Makamba ameainisha kwamba maelekezo yatapelekwa Wizara ya Elimu na TAMISEMI na moja ya mahitaji ya kupewa cheti cha kuhitimu ni kukabidhi miti iliyopandwa wakati mwanafunzi anaingia kuanza masomo hivyo atahitajika kutunza na kuhudumia miti hiyo kipindi chote cha masomo.
Waziri Makamba ameyasema hayo wakati akishiriki zoezi la upandaji miti na wanafunzi katika Shule ya Msingi Mlandege iliyopo katika Kata ya Kwakilosa, Manispaa ya Iringa ambapo aliongozana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Iringa. Waziri Makamba ametanabaisha kuwa lengo la kushiriki zoezi la upandaji miti pamoja na wanafunzi  hao ni kutuma ujumbe mahsusi na wa uhakika kabisa kwamba uhifadhi,usimamizi na utunzaji wa Mazingira ni jukumu la msingi kwa manufaa ya kizazi kinachokuja na ndio sababu hasa ya kushiriki na wanafunzi ili waweze kujifunza na kuelewa. 
Waziri Makamba ameainisha kuwa katika shule zenye uhaba wa maeneo yanayoweza kutumika kwa upandaji miti, maeneo mbadala yatakayoelekezwa na serikali za vijiji na mitaa.
Waziri huyo mwenye dhamana ya Mazingira amesema hili linafanyika ikiwa ni moja kati ya hatua mahsusi,  stahiki na za maksudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuendana na mabadiliko ya tabia nchi hasa ikizingatiwa kuwa asilimia 61 ya nchi yetu ipo katika tishio la kuwa  jangwa.
Vilevile Waziri Makamba amesema kuwa kuanzia tarehe 5-6 Novemba Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wenyeviti na Mameya wote watakutana Jijini Arusha Kwaajili ya kupata mafunzo na maelekezo mahsusi yanayohusiana na Hifadhi ya Mazingira, ikiwemo upandaji miti na utunzaji wa vyanzo vya maji

MKOA WA SONGWE WAPIGWA JEKI MIFUKO 125 YA CEMENT KUTOKA TPB

October 19, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Songwe (katikati)  Luteni Mstaafu Chiku Galawa akipokea msaada wa Cement mifuko 125 yenye thamani ya shilingi mil 2 kutoka kwa benki ya Posta Tanzania (TPB) tawi la Mbeya.kulia aliyevalia T.shart Meneja Benki ya Posta Mbeya Humphrey Julias ,kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo na Meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduma Teddy Msanzi aliyshikana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa mifuko ya cement 125 kutoka benki ya Posta Tanzania (TPB)Tawi la Mbeya ,hafla ambayo imenyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Songwe Octobar 18 mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo akishukuru mara baada ya kupata msaada wa Cement1 kutoka benki ya Posta Tanzania (TPB)

Mkuu wa Mkoa Songwe Picha ya Pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Songwe na wadau mbalimbali .


BENKI ya Posta Tanzania(TPB) kupitia tawi lake Mkoani Mbeya, imetoa msaada wa mifuko ya saruji  125  thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa serikali ya Mkoa mpya wa Songwe.

Akikabidhi mifuko hiyo , kwa uongozi wa serikali ya Mkoa wa Songwe, Meneja wa benki ya Posta mkoa wa Mbeya, Humphrey Julius amesema benki hiyo iliguswa na suala la ujenzi wa majengo mapya ya ofisi za Mkoa wa Songwe hivyo kuona umuhimu wa kuchangia ikiwa kama faida wanayoipata kutoka kwa wateja wanaowahudumia.

Amesema, mbali na kutoa msaada huo wa mifuko ya saruji, pia benki hiyo imeshakabidhi madwati 130  kwa baadhi ya shule za msingi za Wilaya ya Tunduma, Ileje zilizopo Mkoani Songwe na dawati 30 kwa shule ya Mbeya Day Mkoani Mbeya.

Amesema, serikali pekee haiwezi kufanya mambo yote ni lazima wadau zikiwemo Taasisi, Mashirika, Asasi na mtu mmoja mmoja kuingiza mikono yao ili kuipungizia serikali mzigo.

Hata hivyo, akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu  Chiku Galawa, aliishukuru benki ya Posta kwa msaada huo, muhimu kwani serikali ya Mkoinahitaji zaidi ya mifuko 50 elfu ya saruji na mabati  laki moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo ya ofisi pamoja na shule na Zahanati.
MAKAMBA AZIPONGEZA KAMATI ZA VIJIJI ZA MAZINGIRA WILAYANI KILOLO

MAKAMBA AZIPONGEZA KAMATI ZA VIJIJI ZA MAZINGIRA WILAYANI KILOLO

October 19, 2016
kih1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akipata maelezo kutoka kwa Bw. Mutagabaya Mtaalamu  kutoka maabara maalumu ya kutunza Vyura ya Kihansi.
kih2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa Kijiji cha Mwantasi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, aliposimama akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua masuala ya mazingira.
kih3
Mjumbe wa Kamati ya Mazingira ya Kijiji cha Mwantasi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa akipokea kiasi cha Shilingi laki moja zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba kuchangia Mfuko wa Mazingira wa Kijiji.
kih4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na ujumbe wake wakikagua mitambo ya kusukuma maji katika Mkoa wa Iringa, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza.
…………………………………………………
Na Lulu Mussa
Kilolo – Iringa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesisitiza umuhimu wa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa shughuli zifanywazo na binadamu kando ya Vyanzo hivyo hupelekea mito hiyo kukauka.
hayo yamebainishwa leo na Waziri Makamba alipofanya ziara ya kikazi Kihansi Wilayani Kilolo kuangalia chanzo cha Mto Kihansi. Waziri Makamba kwa nyakati tofauti amefanya mazungumzo na wanakijiji wa Kijiji cha Mwantasi ambao wamefanya jitihada za dhati kuhifadhi Vyanzo vya Maji.
Waziri Makamba amewapongea na kuchangia kiasi cha shilingi laki mbili kwa vijiji vya Mwantasi kwa ajili ya Mfuko wa Mazingira wa Kijiji wenye lengo la kusimamia masuala za mazingira katika kijiji chao.
“Nawapongeza sana kwa jitihada mlizonazo ikiwa ni pamoja na kuwa na sheria ndogo ndogo za kutunza mazingira, nami nawaunga mkono kwa kuchangia kiasi cha shilingi laki moja kwa kijiji cha Mwantasi na laki moja kwa kijiji cha Wangama ili kuimarisha mfuko huo” Makamba alisisitiza.
Aidha Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Kilolo kuhakikisha fani zinazotozwa za uharibifu wa mazingira sehemu ya pesa hizo zinapelekwa katika vijiji husika ili kukuza mfuko huo na kuwaagiza wajumbe wa Kamati za Mazingira ngazi ya kijiji kuzitunza fedha hizo benki na kuagiza matumizi sahihi.
Waziri Makamba anaendelea na ziara ya kikazi katika Mikoa mbalimbali hapa nchini na leo yuko katika Mkoa wa Morogoro ambapo ametembelea Mto Kihansi na Ruaha Mkuu.

SBL yatoa elimu kuhusu unywaji pombe kistaarabu

October 19, 2016
Meneja wa SBL wa  Uwajibikaji Katika  Jamii, Hawa Ladha  akitoa maelezo katizo kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu katika mkutano na wadau mbali mbali wakiwepo toka vyombo vya usalama na wafanyabiashara wanaofanya kazi na SBL na wafanyakazi wa kiwanda cha SBL moshi katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro

Meneja wa mauzo wa Sbl Mkoani Kilimanjaro Godwin Seleliii akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu iliyofanyika katika mji wa Moshi mkoani kilimanjaro mapema jana.

Mkaguzi wa polisi Mkoa wa kilimanjaro Peter Mizambwa akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa keampeni ya unywaji kistarabu iliyozinduliwa mapema jana na Sbl katika mji wa Moshi


Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini elimu juu ya unywaji wa kistaarabu katika uzinduzi wa kampeni hiyo mapema jana
Waendesha bodaboda wakipata elimu ya unywaji kistaarabu kutoka kwa mfanyakazi wa SBL aliyekuwa anapita mitaani 


Mdau akiwa na zawadi ya kava la gari mara baada ya kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa kuhusu unywaji wa pombe kistaarabu
Moshi, Oktoba 18, 2016. Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu. Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.  
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkaguzi wa polisi Mkoa wa Kilimanjario, Peter Mizambwa , amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia  bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha.
“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Mizambwa .  
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Bi Zauda.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia Mizambwa anasema “ma kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.  
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.
Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.

TAASISI YA ADLG YAANZA KUWANOA WANAHABARI JIJINI MWANZA KUHUSIANA NA SEKTA YA MADINI NCHINI.

October 19, 2016
Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza, wakijadiliana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari zenye tija katika jamii kuhusiana na sekta ya madini nchini. 

Pia wanahabari hao walipata wasaa wa kuwasilisha tathimini yao kuhusiana na ziara mbalimbali ambao wamezifanya kwenye maeneo yenye wawekezaji wa madini Kanda ya Ziwa ikiwemo mkoani Shinyanga.

Wa kwanza kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo, Fredirick Katulanda, ambaye pia ni mhariri wa magazeti ya kampuni ya New Habari (2006) Ltd Kanda ya Ziwa.

Mafunzo hayo yanaandaliwa na Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, yenye makao yake makuu Jijini Mwanza.
Na BMG
Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, Jimmy Luhende, akifuatilia majadiliano hayo.
Baadhi ya Wanahabari/Bloggers Jijini Mwanza
Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza wakiwa kwenye mjadala mzito kuhusu sekta ya madini nchini.

Na George Binagi-GB Pazzo
Waandishi wa Habari mkoani Mwanza, wameanza kupatiwa mafunzo yatakayowasaidia kuandaa habari, makala pamoja na vipindi vyenye tija katika jamii kuhusiana na sekta ya madini nchini.


Mkufunzi wa mafunzo hayo, Fredrick Katulanda, amesema hatua hiyo itasaidia kuibua chachu ya wananchi kutambua haki zao kuhusiana na masuala ya uwekezaji wa madini na hivyo kuondoa migogoro iliyopo baina yao na wawekezaji.

Baadhi ya waandishi wa habari wanaonufaika na mafunzo hayo wamesema yatawasaidia kuandaaji wa habari zenye tija kwa jamii ikiwemo kuondokana na madhara yanayotokana na shughuli za migodini kama vile athari za maji taka.

Mafunzo hayo yanaandaliwa na Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ambapo Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, amesema mafunzo yatawasaidia waandishi wa habari kuibua masuala mbalimbali yenye changamoto katika sekta ya madini ili kutafutiwa ufumbuzi.

MBUNGE VENNANCE MWAMOTO AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA KILOLO

October 19, 2016
 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya wanawake wa  kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo

na fredy mgunda,iringa.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu  za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza vipaji vya wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.

Mwamoto ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Kilolo katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.

Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mwamoto amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni  kutokana na ahadi yake  yeye kama Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku  baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.

“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata.Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mwamoto.
Mwamoto ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
“Mimi nimecheza mpira kwa mafanikio ndio maana hadi saizi,kwa hilo mimi najua kuwa michezo ni ajira rasmi hivyo mtu kama unakipaji kitumie kipaji chako vizuri”. Mwamoto
Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi  na mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
“Leo nimetoa mipira na jezi hizi kwa timu za Bomalang’ombe na vijiji vya jirani kwa timu zote za wanaume na wanawake kwa lengo la kuendeleza vipaji vyenu”alisema Mwamoto
Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.

DOLA 20,000 KUCHUKULIWA NA WABUNIFU WA KIDIGITALI KATIKA TUZO YA TANO YA MWAKA YA TIGO KIDIGITALI YA CHANGE MAKERS

October 19, 2016

Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo Woinde Shisael akizngumza na wanahabari wakati wa Uzindizi wa shindano hilo leo Jijini Dar es salaam 
 Kampuni ya simu ya Tigo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Reach For change wamezindua shindano la Tuzo ya mwaka ya kidigitali ya Tigo Change Makers,shindano linalolenga kuwatambua na kuwasaidia wajasiriamali jamii kwa kutumia zana za kidigitali na Technologia katika kuboresha Jamii pamoja na matokeo yake kwa Vizazi vya Baadae,ambapo kwa mwaka huu Tigo inaangalia ubunifu uliojikita katika mtazamo wa elimu kupanua kujumuisha kidigitali na ambao unalenga kusaidia shiughuli za Ujasiriamali.
 Faraja Nyarandu Pichani  alishinda dola 20,000/- Mwaka 2014 katika shindano la @TigoTanzania #DigitalChangemakers.leo akizungumza mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi na kuwezeshwa na Tigo Tanzania
Jumla ya fedha taslim dola za marekani 20,000 zitatolewa kwa kila wazo litakaloshinda kati ya mawazo mawili yatakayoshinda na hivyo kutoa  nafasi ya kuingia katika malezi ya Reach For change,mafunzo ya kibiashara na mtandao wa dunia wa wajasiriamali wengine wa kijamii.ambapo kipindi cha kutuma maombi kwa ajili ya kushiriki katika shindano hilo kimefunguliwa Rasmi leo hadi November 21,2016.

Akiangumza katika mkutano wa wanahabari wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo Woinde Shisael amesema kuwa Tigo inayo furaha kuendesha Tuzo ya kidigitali ya Tigo change makers mwaka huu ikiwa na mtazamo Mpya,huku akisema kuwa Timu ya tigo ina hamu sana ya kusaidia Ubunifu wa Kidigitali na shughuli za ujasiriamali nchini Tanzania.

Shisael ameongeza kuwa Tuzo ya kidigitali ya Tigo Changemakers ni niia kubwa ya kuwasaidia wabunifu kijamii wazuri walio na weledi ambao wanahitajika nchini katika kuwawezesha kubadilisha maisha ya jamii kupitia masuluhisho ya Kidigitali.
Ikiwa ni mwaka wa Tano ambapo Tigo Reach For change wanaendesha shindano hilo la kutafuta mjasiriamali jamii,Bi Woinde amepongeza kazi za washindi waliotangulia na kuhimiza wengine kushirikiana nao katika mawazo yao.
“Hivi sasa tutawasaidia wajasiriamali 9 kupitia mkakati wa kidigitali wa Tigo Changemakers.wametumia vizuri fedha walizopewa,mafunzo ushauri,na Zaidi ya yote kuleta mabadiliko nchini Tanzania”amesema Meneja huyo wa Huduma za kijamii Tigo.
Carolyne Ekyarisiima Mshindi wa mwaka 2015 akieleza machache mbele ya wanahabari
Akitaja mifano ya washindi ambao wamenufaika na shindano hilo tangu lianzishwe  amesema kuwa Carolyne Ekyarisiima ni mmoja washndi wa tuzo ya Tigo Change makers ambaye amekua akifanya kazi ya kuziba pengo la kijinsia katika Technologia ya Habari na mawasiliano kupitia ujasiriamali kijamii wa Vifaa na watoto wa kike(Apps &girls)
“Mwaka 2015 Carolyne alileta mabadiliko kwa wasichana 1000,kupitia mfumo wa klabu mashuleni, warsha,maonesho,mawasiliano ya simu,kambi za mijadala na mashindano”amesema Shisael na kuongeza kuwa “sio tu kwamba mkakati huu unasaidia kuhakikisha watoto wengi wa kike kuzifikia Teknolojia za kidigitali,hali kadhalika inawezesha kuwa Viongozi wa baadae wa Teknolijia Ya habari na mawasiliano.

Carolyne ni mmoja wa mfano wa wabunifu weledi wa kidigitali ambao Tigo inawatafuta ili iwasaidie kupitia tuzo ya mwaka huu,Shisael amesema anatarajia kupitia Upya ubunifu wa kidigitali wa kuvutia ambao utawasilishwa katika shindano la mwaka huu.
VIJANA WATAKIWA KUACHA KILA MARA KUIHOJI SERIKALI NA BADALA YAKE WAJIKITE ZAIDI KUFANYA KAZI

VIJANA WATAKIWA KUACHA KILA MARA KUIHOJI SERIKALI NA BADALA YAKE WAJIKITE ZAIDI KUFANYA KAZI

October 19, 2016


Kufuatia changamoto ya uhaba wa ajira hususani kwa vijana nchini, wametakiwa kuwa wabunifu na watafutaji wa fursa za kujiajiri badala ya kuilalamikia serikali kuwa haitatui changamoto hiyo kwa muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam kuelekea sherehe za maadhimisho ya wiki ya Umoja Mataifa, amesema vijana inabidi wawajibike katika kuleta maendeleo ya uchumi kwenye jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla.

Pia amesema vijana waache kuhoji serikali kuwa inawafanyia nini badala yake wawe wazalendo kwa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya Taifa lao.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC). (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

"Tuna kazi kubwa ya kujenga fikra za vijana kwamba ili kufanikiwa katika maisha siyo lazima kuajiriwa, vijana wengi ukiwahoji wanakwambia changamoto kubwa wanayoikabili ni ukosefu wa ajira. Lakini wanasahau kuwa changamoto zipo nyingi zinazowakabili," amesema.

Prof. Ole Gabriel amezitaja changamoto nne zinazokabili vijana ambazo zinasababisha washindwe kujiajiri au kushindwa kujiendeleza pindi wanapojiajiri kuwa ni, ukosefu wa fikra kutokana kwamba wengi hawaziruhusu fikra zao kubuni mbinu za kujiajiri. Changamoto nyingine aliyoitaja ni vijana kukosa uelewa, mbinu na ubunifu wa kuongeza thamani ya shughuli wanazofanya.

Changamoto nyingine aliyoitaja ni mfumo mbovu na usio rafiki kwa vijana hasa mifumo duni ya upatikanaji mitaji na masoko, hususani katika kipindi hiki ambacho kuna wimbi kubwa la vijana wasio na ajira.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo kwa vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.

Ameshauri kuwa "Hivi sasa kuna elimu ya ujasiriamali lakini niseme tu haitomsaidia kijana kujikwamua sababu hutoa elimu ya uzalishaji pekee. Ili kijana afanikiwe na ujasiriamali, kwanza inabidi apewe elimu ya kufanya utafiti wa bidhaa inayohitajika kwa kipindi husika, akishajua bidhaa hitajika ndipo afanye uzalishaji kisha hatua ya mwisho kutafuta masoko ambayo tayari ameshayafanyia uchunguzi."

Pia ameshauri vijana kuwekeza katika biashara kilimo kwa kuwa ndiyo sekta pekee yenye fursa ya kutoa ajira kwa wingi kwa kuwa imeajiri asilimia 84 ya vijana.

"Tanzania ina vijana zaidi ya milioni 16.2 ni sawa na asilimia 70 ya watanzania, waliofanikiwa kuajiriwa katika sekta binafsi ni milioni 1, waliojiajiri milioni 1.1 waliopo katika sekta ya umma ni 18,8000 na katika sekta ya kilimo wapo vijana milioni 13.2 na bado nafasi zipo katika sekta hiyo," amesema.
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza machache kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

Hata hivyo, Prof. Gabriel amewaasa vijana kutotumia utandawazi vibaya hasa mitandao ya kijamii kutokana kwamba imekuwa sababu ya vijana wengi kutokuwa na maadili.

"Utandawazi unabomoa uwezo wenu wa kufikiri, zamani vijana walikuwa wanakimbilia kuwekeza katika sekta ya kilimo ila sasa kutokana na utandawazi wanakimbilia kutafuta ajira hata kama fursa hakuna," amesema na kuongeza.

"Msipoangalia miaka michache ijayo tutakuwa watu wa teknolojia na mitandao. Maadili mema tuliyojengewa yatapotea kwa sababu ya kufikiri kwamba mitindo ya kimaisha kutoka nje ndiyo inafaa kuliko ya kwetu, inabidi turudishe yale maadili ya zamani sababu nchi yoyote isiyokuwa na maadili, tamaduni imeparanganyika na haina maendeleo," amesema.

Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza kwa niaba ya UN amesema kuwa shirika hilo litahakikisha linawezesha vijana kushiriki katika maendeleo ya uchumi kwa kuwainua kiuchumi pamoja na kutoa elimu ya namna ya kujiajiri.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza jambo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mbunifu wa mavazi Johari Sadiq akizungumzia jitihada, changamoto, fursa na mafanikio aliyoyapata katika yake ajira binafsi kama mtoto wa kike, kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
MC maarufu nchini ambaye pia ni Mhamasishaji Ujasiriamali, Anthony Luvanda akizungumzia ajira yake binafsi na mafanikio aliyonayo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji ambaye ni Mjasiriamali kijana Stella Imma, akizungumza kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mshauri na Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako (SIYB) akitoa hamasa kwa vijana kutoka shule mbalimbali na vyuo waliohudhuria kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwanafunzi Matilda Moses wa kidato cha pili kutoka shule ya sekondari ya Gerezani akimuuliza swali Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) juu ya kusimamia maadili ya Kitanzania na kuwaelimisha wazazi namna bora ya kusimamia malezi ya watoto wao jijini Dar es salaam wakati wa kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililoandaliwa na Shirika Umoja wa Mataifa linalishughulikia Maendeleo (UNDP).
Pichani juu na chini vijana pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakiuliza maswali kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa tatu kulia) akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana kuelekea wiki ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji MC Anthony Luvanda akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwatambulisha baadhi maafisa wa wizara hiyo waliochini ya idara yake ambao ni vijana na wamepata nafasi ya ajira serikalini na kuwasifia kwamba ni wachapakazi na hodari katika vitengo vyao wakati wa kongamano la vijana kuelekea wiki ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Vijana wakiwa wamejipanga huku wakishikilia mabango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwapiga msasa vijana kuhusiana na Malengo ya Dunia kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Picha ya pamoja.
Pichani juu na chini ni Sehemu ya wanafunzi wa shule mbalimbali na vyuo vikuu walioshiriki kongamano la vijana lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).





Baadhi ya maafisa wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa katika picha ya pamoja wakati wa kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.