RAIS SAMIA AZINDUA MAJENGO MAPYA YA IKULU YA CHAMWINO DODOMA

May 21, 2023

 

Taaswira ya Jengo jipya la Ikulu ya Chamwino kama linavyoonekana pichani ambalo limezinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 20 Mei, 2023.
***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Mei 20, 2023 ameandika historia mpya ya Tanzania kwa kuzindua Majengo mapya ya Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma akishuhudiwa na mamia ya watanzania pamoja na wageni mbalimbali kutoka nje ya Tanzania.



Katika hafla za uzinduzi huo Rais, Dkt. Samia alisema jambo hilo ni la kihistoria kwa watanzania kwani kwa mara ya kwanza, wameweza kujenga Ikulu yao kwa kutumia rasilimali zao pamoja na wataalamu wa ndani ambapo alisema kukamilika kwa mradi huo ni jitihada za Serikali za Awamu zote Sita za uongozi aidha, Rais Samia alisema aliahidi kukamilisha miradi aliyoipokea kutoka kwa mtangulizi wake Hayati Dkt. John Magufuli, hivyo kukamilika kwa mradi huu ni utekelezaji wa kauli yake.

“Nilipokabidhiwa hatamu za kuiongoza nchi yetu, niliahidi nitaendeleza mema yaliyopo, nitaboresha inapobidi na nitaleta mema mapya, ujenzi wa Ikulu hii ni moja ya miradi niliyorithi kutoka kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na ni mradi wa pili kuukamilisha, mradi wa kwanza ulikua daraja la Tanzanite – Dar es Salaam, namuomba Mungu anipe uwezo niikamilishe yote,” alisema Rais, Mhe. Dkt. Samia.

Rais Samia alisema ni takribani miaka 50 toka mchakato wa Serikali kuhamishia Makao Makuu ya nchi Dodoma kutangazwa rasmi mwaka 1973, ambapo Serikali ilianza utekelezaji kwa kujenga taasisi zake mbalimbali ikiwemo Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ofisi za Bunge, Wizara ya TAMISEMI, Chuo Kikuu cha Dodoma, Hospitali ya Benjamini Mkapa na Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete pamoja na kupanua eneo ilipojengwa Ikulu hiyo kutoka heka 66 mpaka 8473.

“Katika utekelezaji wa wazo la kuhamisha Makao Makuu ya Serikali Dodoma, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ameandika historia yake, hatutoweza kuandika historia ya shughuli hii bila ya kuwepo kwa tahariri ya mchango wake mkubwa, tuendelee kumuombea Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani,” alisema Rais Samia.

Akiongelea hatua inayofuata baada ya kukamilika kwa majengo ya Ikulu hiyo Rais Samia alisema ni ujenzi wa jengo la kisasa litakaloitwa ‘Samia Complex’ ambapo litajumuisha ukumbi mkubwa wa mikutano utakaoweza kuchukua idadi ya watu 2000 – 3000, nyumba za viongozi, Zanzibar lounge, East Afrika lounge, njia ya ndege, sehemu ya historia ya viongozi pamoja na viwanja vya michezo mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino huku viongozi mbalimbali wakishuhudia katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Ali Hassan Mwinyi, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuzindua Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla pamoja na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla pamoja na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wakipiga ngoma kabla ya kuingia Rasmi katika Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Rasmi la Ukaguzi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
 Viongozi wa Serikali, Viongozi wastaafu, watu mashuhuri pamoja na wananchi wengine wakiwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kwa ajili ya Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu Chamwino tarehe 20 Mei, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Mama Maria Nyerere wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Hayati Rais wa Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa Mama Janeth Magufuli wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson pamoja na Spika wa Baraza la Waakilishi Mhe. Zubeir Ally Maulid mara baada ya kufungua Jengo la Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na viongozi wengine wakati wakiangalia juu wakati Bendera ya Taifa, ya Rais na ile ya Afrika Mashariki ikipandishwa mara baada ya ufunguzi wa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.

WIZARA YA ARDHI BARA NA ZANZIBAR ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA ARDHI

May 21, 2023

 

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akibadilishana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na Dkt. Mngereza Mzee Miraji, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023.

*************

Na Munir Shemweta, WANMM

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na ile ya Makaazi Zanzibar pamoja na Taasisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na lile la Zanzibar (ZHC) zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi na Nyumba.

MWENYEKITI WA UVCCM UBUNGO ANOGESHA NUSU FAINALI KIMWANGA CUP, HAWA ABDUL REDE CUP KWA KISHIND0

May 21, 2023







Na Mwandishi Wetu -Dar es Salaam


Hekaheka za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu katika ligi ya Kimwanga CUP na mashindano ya Hawa Abdul Rede CUP yamepamba moto huku Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Ubungo, Shadrack Makangula, akiwataka vijana kutumia fursa hiyo kama sehemu ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Katika mtanange huo kwa upande wa mpira wa miguu umezikutanisha timu za Ting Wayland ambapo ilifanikiwa kuvuka hatua ya fainali kwa kuchambana timu cha kituo cha kulea vipaji Lamasia FC kwa bao 2-0 huku upande wa Rede timu ya Kanuni ikifanikiwa nayo kwenda fainali kwa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manzese Princes.


Hayo ameyasema kabla ya kuanza kwa michuano hiyo inayopigwa katika Uwanja wa Bubu Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo, katika mashindano hayo ya kuwania ng’ombe aliyoandaliwa na Diwani wa Kata hiyo, Bakari Kimwanga pamoja na Diwani wa Viti Maalumu Manispaa ya Ubungo, Hawa Abdulraman ambaye amekutanisha mabinti nao kuwania ng’ombe katika michuano hiyo.


“Kwanza, nitumie nafasi hii kuwashukuru madiwani wetu kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuanzisha michuano ya mpira wa miguu na rede ambayo yote kwa ujumla wake yanawasaidia vijana wetu kuonyesha vipaji vyao walivyonavyo, lakini pia inasaidia kupata exposure (fursa) na kubwa zaidi kutengeneza mahusiano mazuri baina ya viongozi na wananchi.


“Hivyo ni vema kwa mashabiki, wakeleketwa na wananchi kwa ujumla ambao timu zao wanazozishabikia zimefuzu kucheza nusu fainali kuhakikisha kuwa wakati wa michezo hiyo inapoendelea wawe na utulivu wawapo uwanjani kwa sababu tutakapoanzisha vurugu uwanjani hapa tutawakatisha tamaa wadau, wahisani na viongozi katika kuanzisha ligi mbalimbali kwa ujumla wake,” amesema Makangula


Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa UVCCM amewataka wananchi kwa ujumla kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya aliwashukuru viongozi mbalimbali aliombatana nao na kuwaomba madiwani hao michezo hiyo iwe endelevu.


Mwisho