RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI MAZISHI YA DADA YAKE RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA LEO

December 21, 2015
  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015
Rais John Pombe Joseph Magufuli akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt JAkaya Kkikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015

 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kkikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Marais Wastaafu Alhaji Ali Hassan  Mwinyi na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakishiriki katika dua wakati wa wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu kt Jakaya Mrisho Kikwete wakiondoka makaburini baada ya mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt JAkaya Kikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015

PICHA NA IKULU

WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKAGUA UJENZI WA MAHAKAMA YA UMOJA WA MATAIFA JIJINI ARUSHA

December 21, 2015

Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akipata maelekezo ya ziada kuhusu ujenzi wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Lakilaki Jijini Arusha. Aneyetoa maelezo ni Afisa Mambo ya Nje na Mwansheria Bw. Elisha Suku. Kushoto kwa Waziri Mahiga ni Nd. Hamdouny Mansour, Katibu Tawala Msaidizi upande wa miundombinu. 
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na ujumbe wake wakiangalia eneo la eka 16 ambapo majengo manne ya Mahakama ya Umoja wa Mataifa yanajengwa. Ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Mwezi Aprili mwaka 2016.
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Mhe. Wilson Nkhambaku baada ya kukagua eneo hilo na kuridhika na kasi ya ujenzi uliozingatia viwango vya kimataifa na vile vya Umoja we Mataifa. 
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akiwa na ujumbe wake baada ya kumaliza ukaguzi wa ujenzi wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa jijini Arusha. 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Serikali imeridhishwa na maendeleo na kasi ya ujenzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (Mechanism for International Criminal Tribunals (MICT) katika eneo la Lakilaki jijini Arusha, uliozinduliwa rasmi Julai mosi mwaka huu.
Akikagua ujenzi huo na kupokea taarifa kutoka kwa wakandarasi na wasimamizi wa ujenzi wa majengo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, amesisitiza kuwa ujenzi huo uzingatie viwango vya kimataifa ili kuhakikisha usalama wa nyaraka na ushahidi utakaohifadhiwa kwenye majengo hayo. 
Alieleza kuwa ahadi ya Serikali iko palepale kushirikiana na Umoja wa Mataifa na kuhakikisha kuwa miundombinu muhimu kama vile barabara, umeme na maji vinapatikana kwenye eneo hilo ambapo ujenzi unaendelea kwa kasi ya kuridhisha.
“Nimefurahishwa na maendeleo ya ujenzi huu kwani hii ilikua kazi yangu ya mwisho nilipokuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kule Umoja wa Mataifa, kutetea mahakama hii ijengwe hapa Arusha. 
Akifafanua miundombinu iliyowekwa na Serikali ya Mkoa wa Arusha, Katibu Tawala Msaidizi upande wa miundombinu Nd. Hamdouny Mansour alisema kuwa kwa upande wa upatikanaji wa maji, mkoa umefanikisha upatikanaji wa bomba maalum linaloleta maji kwenye eneo la ujenzi mojakwamoja bila kuathiri upatikanaji wa maji maeneo mengine pembezoni ili kutimiza azma hiyo ya Serikali. 
Ujenzi huo wa Mahakama unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuwa na majengo makuu manne; jengo la mahakama, jengo la uhifadhi wa nyaraka, jengo la ulinzi na jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa. Msimamizi wa ujenzi wa Umoja wa Mataifa alielezea teknolojia ya kisasa itakayotumika kujenga jengo la kuhifanyia nyaraka haitahitaji kutumia viyoyozi ili kuhifadhi uhasilia wa nyaraka. 
Kwa upande wa wakandarasi wanaojenga ambao ni kampuni kutoka India walielezea changamoto iliyopo kwenye ujenzi huo ni kutekeleza mpango wa kupanda mti aina ya mshita-acacia, utakaomaanisha haki ambayo kihistoria na jadi za kiafrika ilipatikana kwa mazungumzo kwenye mabaraza ya kijiji. Mti huo wa mshita au Tree of Justice utapandwa ndani katikati ya majengo hayo manne. 
Serikali kupitia Hazina ilinunua eneo hilo la Lakilaki lenye ekari 431 na kukabidhiwa Wizara ya Mambo ya Nje ambapo limetengwa mahsusi kwa ajili ya ujenzi wa taasisi mbalimbali za kimataifa. Taasisi nyingine zinazotarajiwa kujengwa kwenye eneo hilo ni African Union Advisory Board on Corruption (AUABC), African Institute of International Law (AIIL) na African Court on Human and Peoples' Rights (ACHPR).
Ujenzi wa majengo haya ya awali kwenye eneo la Lakilaki unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwakani. Ujenzi huo ulizinduliwa rasmi Julai mwaka huu wa 2015 na Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. 
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
20 Desemba, 2015

MSWADA WA SHERIA YA WAZEE KUWASILISHWA BUNGENI

December 21, 2015
Waziri  wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano maalumu na wazee wa Jiji la Tanga leo
Serikali inatarajia kuwasilisha  mswada wa sheria katika bunge la Mwezi wa tisa  kwa ajili ya kuundwa kwa sheria ya wazee ili kuhakikisha sera ya wazee inafanyakazi ipasavyo hapa nchini .
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Alhaj Abdulla Lutavi akitoa neno kwenye mkutano huo

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri  wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea katika mkutano maaluma na wazee wa Jiji la Tanga leo


 Alisema kuwa Mswada huo utakapofikishwa bungeni na wabunge kuuridhia itasaidia kusimamia ufanyaji kazi wa sera ya wazee ambayo ilikuwa imetungwa siku nyingi lakini ilikuwa haifanyiwakazi kwa kukosa muongozo.

“Licha ya serikali kujitahidi kupunguza changamoto za wazee lakinia tunajua kuwa bado  matatizo mengi ya wazee ambayo yanahitaji ufumbuzi na usimamizi wa kisheria hivyo kwa jitihada hizo zitawezesha kumaliza changamoto hizo”alisema Waziri Mwalimu.

Moja kati ya wazee wa mkoa wa Tanga,Alhaji Kassim Kisauji akiuliza swali kwenye mkutano huo
Aidha aliziagiza Halimashauri zote nchini kuhakikisha zinawatambua wazee walioko katika maeneo yao hususani wale waliofikia umri wa miaka 60 na kuendelea.

“Niwaombe katika utambuzi huo muhakikishe unawaainisha wazee wanaojiweza na wale wanaojiweza ilikuhakikisha mnawatengeneza utaratibu maaluma wa kupata mahitaji yao muhimu kama ilivyoainishwa kwenye sera”alisisitiza

Baadhi ya wazee wa mkoa wa Tanga wakifuatilia matokeo mbalimbali kwenye mkutano huo na Waziri Ummy
Hata hivyo Waziri Mwalimu alisema kuwa moja ya mikakati ya wizara yake ni kuhakikisha wamewasajili wazee wapatao laki mbili na kuwaingiza kwenye mpango wa matibabu bure .

Alisema kuwa licha ya idadai hiyo kuwa ni ndogo lakini anaamini mpango huo ukipata usiamamizi mzuri unaweza kuwasaidia wazee kupata huduma bora za matibabu katika ngazi zote za wilaya hadi rufaa.

 
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa asasi ya wazee mkoa wa Tanga TARINGO Fredorin Mbunda aliiomba serikali iangalie uwezekano wa kuongeza kiwango cha fedha za pesheni kwa wazee ili iendane na hali halisi ya mazingira ya sasa.
 

Alisema kuwa peshen iliyopo inawasaidia kupata milo miwili tu kwa siku hali ambayo inasababisha wazee wengi kuishi katika maisha ya tabu na duni kwa kiasi kikubwa.

WAZIRI APIGA MARUFUKUWAHANDISI 'UCHWARA' KUPEWA TENDA ZA UJENZI WA BARABARA

December 21, 2015
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto), akitoa maagizo mbalimbali kwa uongozi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini, alipotembelea bodi hiyo, Dar es Salaam juzi, kujua utendaji wake. Kulia ni Meneja wa bodi hiyo, Joseph Haule. (HABARI,PICHA NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 .Mhandisi Edwin Ngonyani

Na Richard Mwaikenda
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, amepiga marufuku kwa Halmashauri zote nchini, kuwatumia wajenzi wa barabara wasiosajiliwa na Bodi ya Wahandisi nchini (ERB).

Mhandisi Ngonyaji alichukua hatua hiyo alipofanya ziara ya kujua utendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini, Dar es Salaam juzi, ambapo alielezwa na Meneja wa Bodi hiyo, Joseph Haule, kuwa barabara nyingi kwenye halmashauri zinajengwa chini ya viwango kwani wanaopewa tenda hawana utaalam wa ujenzi wa barabara. 

Alisema kuwa, kuanzia sasa halmashauri ziachane kabisa  kuwatumia mafundi wasio na utaalam, bali wawatumie wahandisi waliosajiliwa na Bodi ya Wahandisi nchini, ili barabara zijengwe kwa viwango vinavyotakiwa, na watakaokaidi agizo hilo wanyimwe fedha za mgao kutoka kwenye bodi hiyo.

Pia , Mhandisi Ngonyani, ameitaka bodi hiyo, kutokutuma fedha  za  ujenzi wa barabara kwa halmashauri yoyote ambayo imetumia fedha walizopelekewa na kuzitumia kinyume cha malengo yaliyokusudiwa.

Amemwagiza Meneja wa Bodi hiyo, kuzichukulia hatua halmashauri zote ambazo zimetumia fedha hizo tofauti na malengo yake ikiwa ni pamoja na kutopelekewa fedha  hadi hapo watakapoziresha walizozitumia.

"Ongezeni nguvu zaidi katika kusimamia matumizi ya fedha za mfuko wa barabara kwa halmashauri ambazo fedha hizo zinatumiwa kwa shuguli zisizo za barabara", alisisitiza Mhandisi Ngonyani.

Naye Meneja wa Bodi ya mfuko huo, Joseph Haule, alielezea mafanikio ya mfuko huo tangu ianzishwe  miaka  15 iliyopita kwamba kuwa mapato yameongezeka kutoka sh. bilioni 73 mwaka 2005 hadi sh bilioni 752.

"Kutokana na kupanda kwa mapato mtandao wa barabara umeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwa kuwa barabara nyingi zimejengwa kutokana na kipato hicho", alisema Meneja Haule.


Aidha, Meneja wa Bodi ya mfuko huo, Haule, alisema kuwa  mfuko huo ambao chanzo chake kikubwa ni ukusanyaji wa fedha kutoka sehemu ya mauzo ya mafuta ya petroli na dizeli nchini, Bodi italitia mkazo katika ufuatiliaji wa matumizi ya mfuko kuhakikisha vyanzo vipya vya mapato vinapatikana.

Alisema kuwa, katika kuhakikisha ufuatiliaji wa usimamizi wa fedha hizo unatekelezwa, mfuko tayari umezichukulia hatua halmashauri tatu zikiwemo za Kinondoni, Songea Vijijini na Bukoba Vijinini ambazo zimetumia fedha za mfuko wa barabara kinyume na malengo yaliyokusudiwa.

Alisema Bodi ya Mfuko wa Barabara ilianzishwa kwa lengo la kukusanya mapato, kufuatilia matumizi ya fedha hizo na kugawa kwenye taasisi ambapo asilimia 63 zinapelekwa Wakala wa Barabara wa Serikali (Tanroads) kwa ajili ya matengezo barabar kuu na za mikoa, asilimia 30 katika halmashauri 166 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za halmashauri na asilimia 7 zinapelekwa wizara ya ujenzi



 Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Joseph Haule akijibu baadhi ya hoja.
Naibu Waziri, Mhandisi Ngonyani akisisitiza jambo katika mkutano huo.

MEGATRADE INVESTMENT LTD YA JIJINI ARUSHA YATOA SIKU KUU KWA WATOTO WA KITUO CHA AMANI CENTER.

December 21, 2015
Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade kanda ya Kaskazini,Edmnd Rutaraka akizung4umza kabla ya kukabidhi zawadi kwa watoto waishio katika mazingira magumu wanaolelewa katika kituo cha Amani cha mjini Moshi.
Watoto waish7io katika mazing4ira mag4umu wanaolelewa katika kituo cha Amani Center wakifurahia zawadi zilizotolewa na kampuni ya Megatrade kwa ajili ya siku kuu za Christmas na Mwaka mpya.
Meneja mauzo wa kam-puni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akiwa na wafanyakazi wenzake pamoja na wafanyakazi katika kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira mag4umu cha Aman Center wakati alipofika kituoni hapo kukabidhi zawadi kwa ajili ya siku kuu za Christmas na Mwaka mpya.
Baadhi ya zawadi zilizotolewa na kampuni ya Megatrade kwa watoto wao.
Watoto waishio katika mazingira magumu wanao lelewa katika kituo cha Amani Center wakiweka pozi la picha mara baada ya kukabidhiwa zawadi kutoka Megatrade Investment ya jijini Arusha.
Kituo cha watoto cha Amani Center.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.