WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya Cuba kwa kutambua na
kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa wa ukombozi wa Bara la
Afrika, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuwajengea mnara
wa kumbukumbu.
Mnara
huo umejengwa katika Manispaa ya Playa jijini Havana kwenye eneo
maalumu la makumbusho ya mashujaa hao walioshiriki katika ukombozi wa
Afrika, ambapo zimewekwa sanamu zao pamoja na maelezo mafupi ya historia
zao na nchi wanazotoka.
Waziri Mkuu alifanya ziara katika eneo
hilo jana (Ijumaa, Agosti 25, 2017) na kuweka shada la maua katika
mnara huo uliozungukwa na sanamu za mashajuaa wa Bara la Afrika na
kuoneshwa sehemu itakayowekwa sanamu ya Mwl. Nyerere.
Akiwa
katika eneo hilo, Waziri Mkuu aliishukuru Serikali ya Cuba kwa kujenga
makumbusho ya mashujaa hao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana
na Cuba kuhakikisha kuwa sanamu ya Mwl. Nyerere inawekwa katika sehemu
iliyotengwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Instuto Cubano De
Amistad Con El Pueblo (Taasisi ya Ushirikiano wa Cuba na Nchi Marafiki),
Bw. Jose’ Prieto Cintado alisema mnara huo umejengwa kwa lengo la
kutambua thamani na umuhimu wa viongozi hao.
Mkurugenzi huyo
alisema Serikali ya Cuba inathamini mchango mkubwa uliotolewa na
mashujaa hao katika vita ya ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo iliamua
kujenga mnara wa kumbukumbu katika nchi yao.
Alisema wananchi wa
Cuba pamoja na watu kutoka mataifa mbalimbali ndani na nje ya Bara la
Afrika wanakwenda katika eneo hilo la makumbusho na kujifunza historia
za viongozi hao. Pia eneo hilo linatumiwa na watafiti wa masuala ya
kihistoria.
Mashujaa ambao tayari sanamu zao zimekwishawekwa
kwenye eneo la kuzunguka mnara huo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Rais wa
kwanza wa Kenya), Modibo Keita (Rais wa Mali), Amilcar Cabral (Rais wa
kwanza wa Guinea Bissau).
Wengine ni Dkt. Kwame Nkrumah (Rais wa
kwanza Ghana), Oliver Thambo (Kiongozi Mwandamizi wa Chama cha Ukombozi
cha ANC cha Afrika Kusini), Eduardo Chivambo Mondlane (Kiongozi wa
ukombozi nchini Msumbuji).
Wengine ni Samora Moises Machel (Rais
wa kwanza wa Msumbuji), Sekou Toure (Rais wa kwanza wa Senegal), Seretse
Khama (Rais wa kwanza wa Botswana), Alhaji Aboubakar Tafawa Balewa na
Obafemi Jeremiah Awolowo (Mawaziri Wakuu wa zamani wa Nigeria) na Chifu
Jeremia Azikiwe (Rais wa zamani wa Nigeria) .
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa. kushoto , akiwa na mwenyeji wake kulia ambaye ni
Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado
.August 25/2017 wakiangalia Sanamu ya aliyekuwa Raisi wa Msumbiji
Hayati Samora Masheli ambayo ipo katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa
yaliopo Havana Cuba Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu .
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa .kulia pamoja na Mama Mary Majaliwa ,kushoto
pamoja na mwenyeji wao katikati ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya
Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .wakiweka Shada la Maua
August 25/2017 katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliyopo Havana
Cuba .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu