RC SIMIYU ATOA UFAFANUZI SAHIHI WA TAARIFA KUHUSU WALIMU WAKUU KUVULIWA MADARAKA

August 24, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka,
Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema(kulia)  akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka. 
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani)  wa kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.

Dixon Busagaga wa Michuzi blog Kanda ya Kaskazini.
TAIFA STARS YA KUIVAA NIGERIA HII HAPA

TAIFA STARS YA KUIVAA NIGERIA HII HAPA

August 24, 2016
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.

“Tanzania hatuwezi kupuumza mchezo huu, tumeuchukulia serious (kwa umakini) kabisa kwa sababu tunacheza ugenini ambako matokeo mazuri yanaweza kutusongesha mbele na kuingia ndani ya timu 99 bora katika viwango vya FIFA,” amesema Mkwasa.
Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
“Timu itaingia kambini Agosti 28, itakaa kambini kwa siku tano kabla ya kusafiri kucheza mchezo huo wa kukamilisha ratiba ambao Misri tayari wameshafuzu fainali za Afrika,” amesema Mkwasa na kuongeza kuwa kuna mchezaji wa Tanzania, Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana baadaye amwite kuchezea timu ya taifa. Anakipiga Klabu ya Brencia Calcio ya Italia.
Wachezaji walioitwa:
Makipa-
Deogratius Munishi – Young Africans
Aishi Manula – Azam FC

Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC

Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania

Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC

Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
Watanzania warahisishiwa upatikanaji wa huduma za teknolojia

Watanzania warahisishiwa upatikanaji wa huduma za teknolojia

August 24, 2016

Pamoja na kuwepo kwa maendeleo ya kasi katika nyanja mbalimbali lakini sekta ya teknolojia inabaki kuwa moja ya njia ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo kwa kurahisisha kazi nyingi kufanyika kwa haraka.

Kwa kutambua hilo, kampuni inayohusika na utoaji wa huduma zinazohusiana na teknolojia ya EnGenius imeingia katika makubaliano na kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia ya Red Dot ili iweze kusambaziwa vifaa na huduma mbalimbali ambazo zinafanywa na Red Dot katika nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao akizungumzia kazi ambazo wanazifanya na mipango ya kutoa bidhaa bora kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kampuni ya EnGenius ambayo inatoa huduma kama za internet wireless, radio frequency (RF) technology na kusambaza bidhaa mbalimbali kama kompyuta imesema kuwa imefanya maamuzi ya kuingi katika makubaliano na Red Dot ikiamini kuwa ni moja ya njia sahihi ambayo itawawezesha kuwafikia wateja kwa karibu zaidi.

Akizungumzia makubaliano hayo, Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao alisema kampuni ao kwa sasa inahitaji kujitanua katika nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia hivyo wameungana na Red Dot ili waweze kukuza biashara yao zaidi.

"Tumeingia makubaliano na moja ya wasambazaji wakubwa wa Red Dot na tunaamini watatusaidia EnGenius kufikia malengo yetu ya kuwa wauzaji wakubwa wa bidhaa za kiteknolojia kwa Afrika Mashariki, tunafahamu kuwa ni wasambazaji wakubwa na atatusaidia kukuza biashara yetu," alisema Hsiao.


Na Rabi Hume, modewjiblog.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution akielezea jinsi ambavyo wamejipanga kufanya kazi na EnGenius. (Picha zote na Na Rabi Hume, modewjiblog.com)

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani alisema kuwa ni ushirikiano mzuri ambao wameanza kuufanya na EnGenious na wana mipango mingi kuhakikisha malengo ambayo yamewekwa yanafikiwa.

"Tuna taraji mafanikio makubwa, Red Dot ni kampuni ya kitanzania ambayo inafanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki kwahiyo tunatazamia ushirikiano huu utakuwa na faida," alisema Bharwani.
Meneja Mkuu wa Red Dot Distribution Tanzania, Rajesh Adiani akifungua halfa ya uzinduzi wa makubaliano kati ya Red Dot na EnGenius kwa kuelezea shughuli ambazo wanazifanya.
Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa EnGenius, Alishan Zaidi akilelezea huduma ambazo wanazitoa za kiteknolojia na usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia kama kompyuta na kamera za usalama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani na Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao wakipongezana baada ya kuingia rasmi katika makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia bidhaa ambazo zinatolewa na EnGenius.
Baadhi ya wageni waaliakwa waliohudhuria halfa ya makubaliano ya Red Dot Distribution na EnGenius.

Tigo yakabidhi madawati ndani ya msimu wa fiesta wilayani Kahama

August 24, 2016
Mkurugenzi  wa Tigo kanda ya Ziwa Ally Maswanya (kushoto) akimkabidhi madawati Mkuu wa wilaya ya Kahama  Fadhili Nkulu kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Kahama Mjini. Jumla ya madawati 235 yalitolewa kwa shule za wilayani humo ndani ya msimu huu wa fiesta.


Wanafunzi  wa shule ya Msingi Mungula wakiwa wamekaa kwenye madawati baada ya kuyapokea madawati 235 kutoka kwa Kampuni ya Tigo Wilayani Kahama mkoani Shinyanga

Mkurugenzi  wa Tigo kanda ya Ziwa Ally Maswanya (wa kwanza kulia ) akiwa amekaa kwenye madawati baada ya makabadhiano anayefuatia ni  Mkuu wa wilaya ya Kahama  Fadhili Nkulu kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Kahama Mjini. Jumla ya madawati 235 yalitolewa kwa shule za wilayani humo ndani ya msimu huu wa fiesta.



photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.tz Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com

WALIMU WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI WATAKAOKUTWA NA WANAFUNZI HEWA KUKIONA

August 24, 2016
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS),Faidha Salim amesema wilaya hiyo itawachukulia hatua kali za kisheria walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari ambao watabainika shule zao kuwa na wanafunzi hewa wanaoingizwa kwenye bajeti ya mgao wa fedha zinazotolewa kutoka serikali .

Faidha aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Tanga Raha blog katika mahojiano maalumu kuhusu hatua ambazo watazichukua kwa shule ambazo zitabainika kuwa na wanafunzi hewa kutokana na agizo la Rais Magufuli la kutaka kuwepo uhakiki huo ili kuona fedha zinazotumika kihalali.

Alisema kuwa kwa wilaya ya Tanga tayari walikwisha kuanza mchakato huo wa uhakiki kwa kutoa fomu ambazo zitapelekwa kwenye shule zote ili kuweza kubainika uwepo wa wanafunzi hewa ambao waliingizwa kwenye mgao wa fedha zinazotolewa na serikali.

  “Unajua hivi sasa tunachokifanya sisi kama wilaya ya Tanga kwa kushirikiana tumeanza mchakato huo wa uhakiki hivyo tunachokifanya hivi sasa ni kupata idadi kamili ya wanafunzi na fedha kiasi gani ambacho kilipelekwa ili kujua hatua za kuchukua”Alisema.

  “Kama ujuavyo katika wilaya ya Tanga tuna shule za serikali za sekondari 26 na za msingi 79 hivyo tunachokifanya ni kutoa fomu hizo na baadae watapata maelezo kutoka kwa walimu wakuu ambao watabainika kuna wanafunzi hewa kwanini wanawapokea wanafunzi hewa wakati wanajua kufanya hivyo ni kosa kisheria “Alisema.

Aidha alisema kuwa shule ambazo zitabainika kuwepo kwa wanafunzi hewa walimu wakuu watashughuliwa kwa mujibu wa sheria zilizopo kutokana na kuisababishia hasara serikali kwa kutoa fedha ambazo zinapotea.

Katika hatua nyengine,Katibu Tawala huyo alisema kuwa hivi sasa wilaya ya Tanga inaendelea na mchakato wa uhakiki wa watumishi hewa na wamekwisha kufikia asilimia 50 hivyo wanatarajia kukamilisha kazi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.