RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA HOSPITALI YA TAALUMA NA TIBA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI KAMPASI YA MLOGANZILA

November 25, 2017
...AWATAKA WAFANYABIASHARA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA VYA MADAWA

Na Jonas Kamaleki - MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara kuweza katika viwanda vya madawa ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa bidhaa hiyo nchini.
Rais Magufuli ameto wito huo leo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wakati akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Syansi Shirikishi Muhimbili.
“Wafanyabiashara tumieni fursa hii ili muweze kuwekeza katika viwanda vya madawa kwani Tanzania imepewa nafasi ya kuuza dawa katika nchi za SADC na tumetenga zaidi ya bilioni miambili kwa ajili ya kununulia madawa,”amesema Rais Magufuli.
Ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kujenga kiwanda cha madawa Mloganzila badala ya kukkopesha fedha hizo kwa watu wanaojenga nmajumba.
Magufuli amesema kuwa Serikali imedhamira kuwekeza katika masuala ya Afya ili kuwa na Taifa lenye watu wenye afya ili wawezekushiriki katika ujenzi wa viwanda. Bila afya njema hakuna ambacho kitafanyika, alisisitiza Rais Magufuli.
Katika Chuo kitakachojengwa Mloganzila kikitumika apmoja na hospitali hiyo, Rais Magufuli amesema kitatola wataalaam wenye ubora ambao utaendana na hadhi ya chuo hicho.
Ili kuongeza ufanisi katika hospitali za mikoa, Rais ameshauri zisimamiwe na wizara ya afya kuliko ilivyo sasa ambapo zilikuwa zikisimamiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
“Hospitali hizo haziwezikusimamiwa na watu ambao sio wataalaamu wa tiba, hivyo hospitali zote za mikoa ziwe chini ya wizara ya Afya ambayo ndiyo inasimamia Sera ya Afya, na hizo nyingine za wilaya, kata na vijiji ndizo zisimamiwe na TAMISEMI, alisema Rais Magufuli.
Amesema kwa usimamizi huo sekta ya Afya itaimarika kuanzia ngazi ya mikoa hadi Taifa.
Rais Magufuli amewataka madaktari na wahudu wa afya hapo katika Hospitali ya Mloganzila kutunza vifaa na miundombinu ya hospitali hiyo ili kuhakikisha ubora uliopo sasa hivi uweze kudumu.
Amewataka kutoharibu vifaa hivyo vya kisasa ambavyo Rais amesema kuwa Hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa na ina hadhi kama hospitali za Ulaya.
Kwa upande wa Bima za Afya, Rais magufuli amewataka wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ambayo itawahakikishia upatikanaji wa matibabu.
“Msiendekeze ununuzi wa nguo, starehe bali changieni katika mifuko hiyo ambayo itawasaidia watoto wenu kupata matibabu ya uhakika, ukiuza majogoo wawili utaweza kumlipia mwanao gharama za matibabu kwa mwaka,”alisisitiza Rais Magufuli.
Aidha, Rais amewataka mawaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana katika kuendesha hospitali za Muhimbili na Mloganzila.
Amewambia kuwa umimi hauhitajiki katika masuala ya kitaifa hivyo wizara hizo zishirikiane katika kuhakikisha ufanisi wa Hospitali ya Mloganzila.
Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya ya Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Apolinary Kamuhabwa amesema kuwa Hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa ambavyo vitatumika katika kutoa huduma za tiba ya dhararula kwa watu wazima na watoto, huduma za magonjwa ya akina mama na mfumo wa uzazi, magonjwa ya macho, mfumo wa pua, koo na masikio na magonjwa ya akili.
Kwa mujibu wa Prof. Kamuhabwa huduma nyingine zitakazotolewa na hospitali hiyo ni pamoja na hmatibabu ya magonjwa ya mifupa na majeruhi, upasuaji mkubwa na mdogo, huduma za kusafisha damu kwa magonjwa ya figo na tiba za magonjwa mbalimbali zikiwemo za kinywa.

Hospitali ya Mloganzila imejengwa na Serikali ya Tanzania na Korea ya Kusini ambayo imetoa mkopo wa masharti nafuu. Ujenzi wa Hospitali umegharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 94.5 (USD) ambapo Serikali ya Tanzania imetoa jumla ya dola za Kimarekani milioni 18.4.                                        
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akielekea sehemu ya sherehe wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole OCS wa Kibamba Mrakibu wa Polisi (SSP)  Pius  Lutumo akipata matibabu wakati akitembelea  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole OCS wa Kibamba Mrakibu wa Polisi (SSP)  Pius  Lutumo akipata matibabu wakati akitembelea  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Leornad Akwilapo, na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba wakielekea sehemu inakofanyika sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017

UMEME MEGAWATI 30 KUINGIZWA KWENYE GRIDI YA TAIFA DESEMBA 7, 2017, NI KUTOKANA NA KASI YA UJEZNI WA MITAMBO KINYEREZI II

November 25, 2017
 WAKANDARASI wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) na wale wa kigeni, wakiendelea kuchapa kazi leo Novemba 25, 2017 ili kukamilisha hatua ya kwanza ya ujenzi wa mitambo Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambapo kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, kasi ya ujenzi inaridhisha na kwamba katika hatua hiyo ya kwanza TANESCO inatarajia kuingiza kiasi cha umeme Megawati 30 kwenye Gridi ya Taifa ifikapo Desemba 7, 2017 na hivyo kuongeza kiasi cha umeme katika safari ya kupata umeme wa uhakika na wakutosha kwenye ujezni wa uchumi wa Viwanda.

UAMUZI WA KAMATI KUHUSU USAJILI LIGI YA WANAWAKE

November 25, 2017
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyokutana Novemba 22, 2017, katika ofisi za TFF Karume, pamoja na mambo mengine ilijadili shauri la mapingamizi mbalimbali yaliyowekwa na timu za Ligi ya Wanawake.

Timu ya Mburahati Queens iliweka pingamizi kwa mchezaji Ever Kombo ikipinga timu ya Baobab kumtumia kwa kuwa hakulipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake.

Kamati imeiruhusu timu ya Baobab kumtumia mchezaji huyo baada ya Mburahati Queens kuondoa pingamizi hilo.

Aidha Kamati imeiruhusu timu ya Fair Play ya Tanga kumtumia mchezaji Anastazia Mmwacha baada ya timu ya Mburahati Queens kuondoa pingamizi iliyomuwekea kwa kutolipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake.

Kamati imeiruhusu timu ya Panama kumtumia mchezaji Sabina Mbuta aliyewekewa pingamizi na Mburahati Queens kwa kutolipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake,Panama wameruhusiwa kumtumia baada ya kulipa ada hiyo ya shilingi laki moja(100,000).

Timu ya Marsh Academy imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Asfaty Kasindo,Janeth Simba ,Rose Mpoma na Arafa Ramadhan wa Mlandizi Queens,Monica Conrad,Christer J Bahera na Niwael  Makuluta wa Mburahati Queens, Neema Kiniga wa Kigoma Sisters baada ya kukubali kuzilipa timu zao ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake na timu hizo kukubali kuondoa pingamizi.

Nayo, timu ya JKT Queens imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Najiat Abassi,Fumu Ally,Hamisa Athuman wa Ever Green Queens,Fatuma Makusanya na Elizabeth Kadonya wa Mburahati Queens baada ya timu zao kuondoa mapingamizi waliyoweka kwa wachezaji hao kutolipiwa ada ya uhamisho.

Timu ya Simba Queens imezuiwa kuwatumia wachezaji Zainab Rashid wa Ever Green Queens, Grace T Mbelayi, Jackline Kulsanga, Dinna Omary wa Mlandizi Queens, na Halima Hamdani Mchen wa Kigoma Sisters mpaka pale watakapolipa ada ya uhamisho wa shilingi laki moja (100,000) kwa kila mchezaji kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya wanawake.

Mapingamizi yaliyowekwa na timu ya Makongo High School kwa timu mbalimbali ikipinga timu hizo kuwatumia wachezaji wake bila kulipa ada,mapingamizi hayo yametupwa baada ya timu hiyo kushindwa kufika kutetea hoja za mapingamizi hayo.

Timu ya Marsh Academy ya Mwanza imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Zainab Hassan Kienje na Silva Daud waliowekewa pingamizi na timu ya Kigoma Sisters ambayo ilishindwa kufika kwenye kikao cha kujadili pingamizi lake.

Wachezaji Asia Juma,Betista Othuman Abdala na Josephine Julius Nyirenda wameruhusiwa kucheza timu ya Baobab baada ya timu ya Kigoma Sisters iliyowawekea pingamizi kuamua kuyaondoa mapingamizi hayo.

KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA GAMA

November 25, 2017
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (Pichani Juu)  amepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama.

Kutokana na msiba huo, Rais Karia ametua salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Kadhalika Rais Karia ametuma salamu za salamu rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Ruvuma (FARU), Golden Sanga pamoja na Mwenyekiti wa Majimaji ya Songea, Steven Ngonyani na wanafamilia wote wa mpira wa miguu na wananchi wote wa mjini Songea.

“Songea ina historia ya mpira na akina Gama ni chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu Songea. Tumepoteza hazina nyingine, lakini niombe tu familia ya Gama, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao,” amesema.

“Nawapa pole nyingi sana na kupitia viongozi wa FARU, Majimaji, Mlale JKT na wanafamilia wengine wa soka katika Mkoa wa Ruvuma, naomba mfikishe salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu,” amesema Rais Karia.

Rais Karia amesema anamkumbuka Gama kwa uhodari wake katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo ukuu wa wilaya, mkoa na ubunge kwani alifanya kazi kwa kujiamini na kupenda kupigania maendeleo hususani mpira wa miguu bila kuchoka.

WAZIRI MWAKYEMBE KUZINDUA LIGI YA WANAWAKE ARUSHA

November 25, 2017


Ligi ya wanawake inatarajia kuanza Jumapili Novemba 26, 2017 kwenye vituo viwili vya Dar Es Salaam na Arusha ambapo kundi A litakuwa Dar es Salaam likitumia Uwanja wa Karume wakati kundi B litakuwa Arusha likitumia Uwanja wa General Tyre.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  katika mchezo wa uzinduzi wa Ligi Kuu soka ya Wanawake, imefahamika.

Mbali ya Dk. Mwakyembe, wageni wengine wanaotarajiwa kuwa katika uzinduzi huo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred pamoja na viongozi wengine wakiwamo Wakuu wa Wilaya mbalimbali za Arusha na mikoa ya jirani.

Kundi A lina timu za Mlandizi Queens ya Pwani, JKT Queens ya Dar es Salaam, Fair Play ya Tanga, Simba Queens ya Dar es Salaam, Ever Green Queens ya Dar es Salaam na Mburahati Queens ya Dar Es Salaam.

Kundi B lenyewe linajumuisha timu za Marsh FC ya Mwanza, Kigoma Sisters ya Kigoma, Panama FC ya Iringa, Baobab Queens ya Dodoma, Alliance Queens ya Mwanza na Majengo Queens ya Singida.

Ufunguzi rasmi wa ligi hiyo utafanyika mkoani Arusha Jumapili Novemba 26, 2017 na mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya Panama FC itakayocheza na Alliance Queens mchezo utakaotanguliwa na hafla ya ufunguzi.

Katika siku hiyo kituo cha Dar Es Salaam kinachotumia Uwanja wa Karume nako kutakuwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha Mlandizi Queens dhidi ya JKT Queens.

DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017

November 25, 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe, (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, wakiwaonyesha waandishi wa habari, tuzo ambayo PSPF ilinyakua katika mashindano ya kimataifa wakati wa mkutano wa taasisi ya hifadhi ya jamii Duniani, International social security association, taasisi tanzu ya ILO, tuzo ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017 mjini Adis Ababa Ethiopia mwezi uliopita. Tukio hili limefanyika pembezoni mwa mkutano wa kampeni ya uzalendo na utaifa iliyoongozwa na waziri Mwakyembe kwenye ukumbi wa mikutano wa PSPF jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umenyakua tuzo ya kimataifa ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017, baada ya kuwa Mfuko unaotoa huduma bora kupitia ubunifu wa mafao ya muda mfupi, yaani service quality in short-term products.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuonyesha tuzo hiyo iliyokwenda sambamba na kampeni ya uzalendo na utaifa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu alisema, Mfuko huo unajivunia kwa kuwa Mfuko wa kwanza miongoni mwa Mifuko mitano ya Hifadhi ya Jamii nchini, kuanzisha bidhaa na huduma za muda mfupi ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na hivyo kuvutia mifuko mingine ambayo kwa sasa nayo imeanza kutoa huduma hizo.
“Mwaka huu katika mkutano wake wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani yaani International Social Security Association, taasisi tanzu ya Shirika la Kazi Duniani,(ILO) imeipatia PSPF tuzo baada ya kuwa Mfuko bora barani Afrika katika utoaji huduma bora kupitia ubunifu wa Mafao ya muda mfupi yaani service quality kwenye short-term products.” Alifafanua Bw. Mayingu.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliipongeza PSPF kwa kujinyakulia tuzo hiyo na kuliletea taifa heshima kubwa kimataifa.
“Kupambanishwa katika bara la Afrika na kushinda vigezo kadhaa ndipo unaambiwa bwana wewe unapata hii tuzo na tuzo hii imetolewa na taasisi yenye ushirikiano wa karibu sana na ILO hongereni sana.” Alipongeza Dkt. Mwakyembe.
Alisema ushirikiano wa karibu miongoni mwa wafanyakazi wa PSPF ndio umepelekea mafanikio hayo.
“Niwapongeze viongozi wote wa PSPF, Wafanyakazi wote wa PSPF, kwa kazi nzuri mnayoifanya mpaka mnatambuliwa na jumuiya ya Kimataifa.” Alisema.
Aidha kabla ya tukio hilo, Waziri aliwahamasisha watanzania kujenga moyo wa uzalendo na kujivunia utaifa wao kwani mambo hayo ni muhimu katika ujenzi wa taifa.
“Sisi tuliokuwepo kabla ya uhuru, niwaombe sana, tuwasaidie vijana wetu wa sasa kutambua tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi, kwa kujenga uzalendo wa kuipenda nchi yetu kama ambavyo ilikuwa hapo awali.” Alisema.
Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muunganmo wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli baadaye mwezi ujao mjini Dodoma, na Waziri aliwahamasisha wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia fedha ili kufanikisha swala hilo muhimu kwa taifa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyemba, akizungumza kuhusu umuhimu wa jamii kiujenga uzalendo wa taifa lao la Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa, Leah Kilimbi, akizungumzia maudhui ya hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. ASdam Mayingu, akizunhgumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza wakayti wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw.Sami Khalfan, wakifuatilia hafla hiyo.
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Nelly Msuya akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa vipindi wa Azam TV, Bw. Charles Hillary, (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Bw. Mayingu akizungumza huku akipongezwa kwa makofi na waziri Mwakyembe na Bi.Joyce Fisso, Katibu Mtendaji bodi ya Filamu Tanzania.
Naibu Waziri Mavunde agawa mashine 31 kwa wananchi wa Dodoma Mjini

Naibu Waziri Mavunde agawa mashine 31 kwa wananchi wa Dodoma Mjini

November 25, 2017
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amegawa mashine 31 za aina mbalimbali kutoka kampuni ya HiTECH International kwa vikundi 31 katika jimbo lake la Dodoma Mjini. Mashine alizozitoa Naibu Waziri ni pamoja na mashine za kutotolea vifaranga (incubators- mayai 1056 na mayai 528) mashine za matofali (umeme na manual), mashine za Popcorn zenye matairi, vyerehani, mashine za kutengeneza chaki (chaki 50,000-80,000 kwa siku), mashine za kunyonyolea kuku mpaka kuku 500 kwa siku. Mavunde ametoa mashine hizo zenye thamani ya milioni 55.8 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake katika uvhaguzi wa mwaka 2015 kuwezesha wananchi ili wajikomboe kiuchumi lakini pia kuunga mkono mpango wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa vikundi mbalimbali vya Dodoma Mjini. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akizungumza jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde wakati wa hafla ya kukabidhi mashine 31 kwa wananchi wa Dodoma Mjini.

NDEMLA AFUZU MAJARIBIO SWEDEN

November 25, 2017
 
TAARIFA KWA UMMA
     _____________________________

Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya. 

Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko.anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja. 

Na mara baada ya kurejea. klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko. 

Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla. 

Wakati huo huo kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi.

Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017.

Mwisho

Uongozi wenu unawaomba Wanachama na washabiki wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli ya Iringa. 

Imetolewa na..... 

HAJI S. MANARA
Mkuu wa Habari  na mawasiliano Simba  Sports Club.

WAHITIMU IFM WAASWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA NA UFISADI

November 25, 2017
Meza Kuu wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) wakiimba Wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika Nyanja za Fedha, Uhasibu, Bima, TEHAMA na Hifadhi ya Jamii. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof. Lettice Rutashobya na wa Pili kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tadeo Satta.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Prof. Tadeo Satta, akihutubia wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
Mwenyekii wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Prof. Lettice Rutashobya, akihutubia wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa mahafali hayo ambayo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, Dkt. Philip Isdor Mpango Mb), akihutubia Jumuiya ya wanachuo hicho ambapo aliwatunuku vyeti wanafunzi 2692 waliohitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao wakipokea zawadi ya hundi kifani yenye thamani ya shilingi 1,200,000 ambayo ni sehemu ya zawadi lukuki walizopewa wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo hicho, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam.
Mhitimu Bi. Elizabeth Mnzava akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) baada ya kufanya vizuri katika masomo yake.

WANAFUNZI ZAIDI YA 700 WAHITIMU MAFUNZO YAO CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MNMA

November 25, 2017
 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  ZanzibarMashavu Ahmad Fakir akihutubia wakati wa kutunuku vyeti kwa wahitimu wa Ngazi ya Shahada na Astashahada wa chuo hicho kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Prof . Shadrack Mwakalila  akizungumza juu ya mipango ya chuo hicho wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika katika jengo la utamaduni la MNMA Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  ZanzibarMashavu Ahmad Fakir akikabidhi zawadi kwa Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mwaka wa masomo 2017
 Baadhi ya wahitmu wa Shahada ya Maendeleo ya Jinsia ya MNMA Wakiwa wanasubiri kutunukiwa shahada zao wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dare s Salaam
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  ZanzibarMashavu Ahmad Fakir  akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi waliofanya Vizuri
--

PSPF YAUNGA MKONO JUHUDI ZA DC IKUNGI MHE MTATURU, YACHANGIA MABATI 100

November 25, 2017
Na Mathias Canal, Singida

Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari (PSS) umeendelea kuyafikia makundi mbalimbali kujiunga na mpango huo ambapo pamoja na mambo mengine umeendelea kusaidia jamii ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali.

Mapema Leo asubuhi Novemba 25, 2017 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekabidhiwa mabati 100 na Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Penseni (PSPF) Mkoani Singida Bi Hafsa Ally kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo.

Mabati hayo yametolewa na PSPF Kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Uongozi wa Wilaya ya Ikungi inayoongozwa na Mhe Mtaturu katika kuimarisha mfuko wa elimu kwa muktadha wa kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuhimiza utatuzi wa Changamoto mbalimbali katika Wilaya ya Ikungi ikiwemo Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.

Akizungumza katika dhifa ya makabidhiano ya mabati hayo iliyofanyika katika eneo la shule ya sekondari Ikungi Mhe Mtaturu ambaye pia ni mlezi wa mfuko wa Elimu amewasihi wananchi na wadau kuchangia fedha au thamani zozote kadri wawezavyo ili kufanikisha kuboresha miundombinu ya elimu katika wilaya hiyo. 

Sambamba na hayo pia ameushukuru Uongozi wa Mfuko wa Penseni PSPF kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kuboresha elimu kwa manufaa ya watanzania wote.

Aidha, ameupongeza mfuko huo wa PSPF kwa mpango wao wa uchangiaji wa  hiari ambapo  mwanachama hutakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 , ili kuwa huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake ambapo kiwango cha chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Mkoani Singida Bi Hafsa Ally Ameeleza kuwa PSPF ipo karibu na watumishi lakini pia ipo karibu na jamii hivyo wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuwashirikisha kwenye jambo hilo muhimu la kuboresha elimu katika wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla wake.

MAJI MAREFU ASIFU JUHUDI ZA SERIKALI YA JPM KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

November 25, 2017

 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mombo mashuka  kwa niaba ya Vituo vya Afya vyengine kwenye halfa iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Korogwe Vijijini kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dkt Frank Chiduo na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mombo mashuka  kwa niaba ya Vituo vya Afya vyengine kwenye halfa iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Korogwe Vijijini kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dkt Frank Chiduo na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu kulia akiteta jambo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo kuhusu umuhimu wa vifaa hivyo kutunza ili kuweza kuwahudumia wananchi.
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiingia kwenye hospitali ya wilaya ya Korogwe Magunga kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Serikali kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,John Nyarongo
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,John Nyarongo
 Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dkt Frank Chiduo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea vifaa hivyo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,John Nyarongo naye akizungumza katika halfa hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini akizungumza na waandishi wa habari
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Nyong’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu alisifu juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto za afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili wananchi kupata huduma bora
Proffesa Maji Marefu aliyasema hayo wakati akikabidhi vifaa tiba kwa Halmashauri ya Korogwe Vijijini vilivyotolewa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kupitia Bohari ya Madawa MSD wamewapatia vitanda vya kulalia wagonjwa,magodoro na mashuka vikiwa na thamani zaidi ya sh.milioni 17.
Vifaa tiba hiyo kwa upande wa vitanda vya wagonjwa vitasambazwa kwa baadhi ya vituo vya Afya na Zahanati zilizopo wilayani humo ambavyo ni Magoma, Mombo, Bungu,Mazinde,Manka,Hale,Mashewa,Vugiri na Makumba
Kwa upande wa vitanda vya kuzalishia vitapelekwa kwenye zahanati za Mandera,Kwemazandu,Lwengera,Mkomazi  na Makumba ambavyo vitasaidia kuondoa changamoto zilizokuwepo hapo awali.
“Niwaambieni tu serikali yenu chini ya Rais Dkt John Magufuli imejipanga vema kuhakikisha inatatua kwa vitendo changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ya huduma za afya na ndio maana leo hii tunakabidhi vifaa hivi kwa lengo la kuboresha huduma hizo “Alisema.
Alisema vifaa hivyo vimefika wakati muafaka ambapo vitasaidia kuondoa changamoto mbalimbali ambazo zilikuwepo ikiwemo mashuka,magodoro na vitanda vitakavyosaidia kuhakikisha huduma zinazotolewa vinakuwa bora.
“Ndugu zangu wananchi serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imefanya mambo mengi makubwa likiwemo la kuhakikisha wanaboresha huduma za Afya katika maeneo mbalimbali nchini  hivyo tuendelea kumuombea mungu na kumuunga mkono katika juhudi hizo “Alisema.
Awali akizungumza katika makabidhiano hayo,Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe (DMO) Dkt Frank Chiduo aliishukuru serikali kwa kuwapatia msaada huo ambao umekuwa chachu ya ya kupunguza changamoto za upungufu wa vifaa tiba kwenye wilaya hiyo kwa kuwapatia vifaa hivyo
Alisema halmashauri ya wilaya ina jumla ya hospitali moja ,Vituo vya Afya vitatu na Zahanati arobaini na mbili zote zikiwa zinamiliki wa na serikali .
“Lakini pia Halmashauri ina jumla ya vitanda 330 vya kulala wagonjwa pamoja na magodoro,shuka 624 kati ya shuka hizo 1320 zinahitajika ,vitanda 61 vya kujifungulia katika vituo vyote hivyo kukidhi mahitaji yaliyopo kwa sasa “Alisema.
“Pia kati ya magodoro yaliyopo 80 yemachakaa na yanahitaji kubadilishwa hivyo kuwa na upungufu wa shuka 690 na godoro 80 “Alisema.