Rais Dkt. John Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani

Rais Dkt. John Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani

July 25, 2016


index 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani, Umoja na Utulivu uliojengwa na mashujaa hao.
Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Dodoma.
Pamoja na kutoa rai hiyo Rais Magufuli ameahidi kuwa atahakikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma inatekelezwa kabla ya kuisha kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano.
“Tunapoadhimisha siku ya Mashujaa hatuwezi kumsahau Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa alisema makao makuu yawe Dodoma, haiwezekani sisi watoto wake, sisi wajukuu wake tupinge kauli ya Mzee huyu.
“Kwa hiyo nilikwishazungumza na leo narudia hili katika siku ya Mashujaa, mlinichagua ndugu zangu wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano, hadi sasa miezi minane imepita, nimebakiza miaka minne na miezi minne, nataka kuwathibitishia kuwa katika kipindi cha miaka minne na miezi minne iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma bila kukosa” Amesema Rais Magufuli.
Kufuatia maelekezo hayo ya Mhe. Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Mawaziri wote waanze mara moja kuhamia Dodoma na kwamba yeye mwenyewe atakuwa amehamia Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.
Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa vyama vya siasa na dini, maafisa na askari waliopigana vita mbalimbali.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
25 Julai, 2016

MAALIM SEIF KUNGURUMA TENA MAREKANI

July 25, 2016
Na Mwandishi wetu,  Philladelphia
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anatazamiwa kunguruma tena chini Marekani wiki hii.
Maalim Seif Sharif Hamad  akiwasili katika uwanja wa ndege Philladelphia
Gwiji huyo wa siasa ambaye aliwasili jijini Philladelphia hapo jana, anatarajiwa kuwakhutubia Watanzania katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika Jumamosi hii katika jiji la Boston.
Katibu huyo Mkuu wa CUF pamoja na ujumbe anaofuatana nao aliwasili nchini humu akitokea Uingereza baada ya kukamilisha ziara yake ya Ulaya iliyochukua muda wa zaidi ya wiki moja. 
Akiwa Ulaya Maalim Seif alitembelea Uiengerza na kufanya mikutano na Maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Uingereza, Vyama vya kisisasa na Taasisi mbalimbali. Baadaye alielekea nchini Ubelgiji ambako alifanya ziara kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na kufikisha madai ya Wazanzibari ya kurejeshewa haki yao ya Kidemokrasia.
Aidha alitembelea nchini Uholanzi ambako pamoja na mambo mengine, alikutana na maofisa wa Mahakama ya Ukhalifu ya Kimataifa na kufikisha kilio cha Wazanzibari dhidi ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu unaendelea Visiwani Zanzibar.
Ziara hiyo ya Ulaya ilikuja katika kile maofisa wa CUF walichokielezea kuwa ni awamu ya pili ya ziara za nje za mwanasiasa huyo mkongwe katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono wa Kimataifa kwa mgogoro wa Kisiasa Zanzibar.
WHO YATOA MAFUNZO KWA WATAALAM WA AFYA KUTOKA NCHI 14 ZA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

WHO YATOA MAFUNZO KWA WATAALAM WA AFYA KUTOKA NCHI 14 ZA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

July 25, 2016


W1 
Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwajengea uwezo watalaam hao uelewa wa ujazaji wa taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha mgonjwa kwenye cheti cha kifo (Death Certificate) ili wakatoe mafunzo kwa wataalam wengine kwenye nchi zao. Mafunzo hayo ya Siku mbili yanafanyika jijini Dar es salaam.
W2 
Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva, Olau Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo unaotumika kutambua  sababu ya kifo cha mgonjwa utakaowasaidia watalaam hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha kifo.
W3 
Mtakwimu kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Doris MA FAT (Kulia) akigawa machapisho yenye mwongozo kuhusu namna ya kujaza taarifa mbalimbali zinazosababisha vifo wakati wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.
W4 W5 W6 
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania, Zambia na Cameroon wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam.
PICHA/Aron Msigwa -MAELEZO
RAIS DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA LEO,

RAIS DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA LEO,

July 25, 2016


z1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Said Bakar Jecha kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
z2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bibi Septuu Mohamed Nassor kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,
z3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Dk.Juma Yakout Juma kuwa Naibu Katibu Msaidizi wa Baraza la Mapinduzi (Sera,Ufuatiliaji na Tathmini) katika  hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
z4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Ndg.Tahir Mohamed Khamis Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira  katika  hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
z5 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba Sheria,utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika kuapishwa Viongozi mbali mbali leo Ikulu Mjini Zanzibar.
[Picha na Ikulu.] 25/07/2016.
RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MAADHIMISHO KUMBUKUMBU YA MASHUJAA MJINI DODOMA

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MAADHIMISHO KUMBUKUMBU YA MASHUJAA MJINI DODOMA

July 25, 2016

shuj2 
Msafara wa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Mashujaa tayari kwa maadhimisho hayo yaliyofanyika  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa  mjini Dodoma leo Julai 25, 2016 (PICHA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA NA IKULU)
shuj4 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mashujaa tayari kwa kuongoza maadhimisho hayo yaliyofanyika  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa  mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj2A
miri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiielekea kwenye mnara wa kumbukumbu tayari kwa kuongoza maadhimisho ya mashujaa  katika Mnara wa kumbukumbu wa Mashujaa  mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj8 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akitoa heshima mara baada ya kuweka Sime na ngao  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj6 
Baadhi ya askari wa vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama vikiwa vimejiweka tayari kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu  ya mashujaa iliyoadhimishwa leo kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma.
shuj7 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akielekea kwenye mnara tayari kwa  kuweka Sime na ngao  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj1 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akikabidhiwa  Sime ili kuweka  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj9 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj8 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akitoa heshima mara baada ya kuweka Sime na ngao  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj9shuj4 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa wamesimama na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma leo.
shuj1 
Viongozi mbalimbali wa serikali,vyama vya siasa wakiwemo wabunge wakiwa  katika maadhmisho hayo mjini Dodoma leo.
shuj5 
Kutoka kulia ni Mke wa Rais Mama Janet Magufuli, Mwenyekiti wa TLP Bw. Agustino Mrema. Spika mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Amer Pandu Kificho, Waziri wa mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba. Waziri wa Ulinzi Dk. Hussein Mwinyi, Mwanasheria mkuu wa Serikali Mh. George Masaju na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika maadhimisho hayo.
shuj7 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj11 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
1 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
maj1 
Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi katika maadhimisho hayo.
shuj13 
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 20
shuj10 
Baadhi ya wananchi wakishangilia wakati Rais Dk. John Pombe Majaliwa alipokuwa akizungumza katika maadhimisho hayo.
shuj12 
Baadhi ya viongozi waliohudhuria maadhimisho hayo wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wakati alipokuwa akiwasalimia wakazi wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo kutoka kushoto ni Naibu Spika Tulia Akson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar   Mhe Mohammed Said Mohammed Dimwa, Mke wa Rais Mama Janet Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwa katika maadhimisho hayo.
……………………………………………………………………………………………
Na: Immaculate Makilika- Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa watanzania kudumisha amani iliyopo ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa mbalimbali kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.
Akizungumza leo, wakati akihutubia wananchi mara baada ya kumaliza shughuli za maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa  iliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.
Rais Magufuli alisema kuwa maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa  ni muhimu kwa vile watu hao walijotoa kwa ajili ya kulitetea taifa.
“Wakati tunawakumbuka waliotangulia mbele za haki, sisi tuliobaki tudumishe amani hii, kama ambavyo wao waliotutangulia hawakujali dini zao bali taifa hili” alisema Rais Magufuli.
Aliongeza kuwa nchi ya Tanzania imebaki kuwa kisiwa cha amani, na amani hiyo isichezwe  bali ijengwe na kudumishwa kwa umoja na mshikimamano ili kusaidia kuitangaza nchi zaidi.
Aidha, viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Ali Mohamedi Shein, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili  Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa John Samweli Malecela nao wapewa fursa ya kuzungumza na wananchi kuhusu maadhimisho hayo ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
Viongozi hao, wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani iliyopo na kusema kuwa ni jukumu la wananchi  wote kuhakikisha  hawashiriki katika vitendo vitakavyosababisha   uvunjifu wa amani.
Ambapo, waliwataka wananchi kuwaombea Mashujaa wote waliofariki katika vita mbalimbali wakiwa  katika  harakati za kulifanya Taifa la Tanzania kuwa huru.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, alisema kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa agizo la Rais la kuitaka Serikali kuhamia mjini Dodoma.
“Nahamia Dodoma mwezi wa tisa,na nitakapohamia mawaziri wote lazima wanifuate. Katika hili nitasimamia kwa nguvu zote” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Awali, Mheshimiwa Rais Magufuli alisema kuwa atahakikisha katika kipindi cha utawala wake, Serikali inahamia mjini Dodoma, kwa vile Rais wa Awamu ya kwanza Mwl. Julius Nyerere alionesha nia ya kufanya hivyo.
 Aliongeza  kuwa  kwa sasa mji wa Dodoma unaweza kukidhi mahitaji hayo ya Serikali kwa kutumia  miundombinu iliyopo, hata hivyo Serikali inaendelea kujenga miundombinu mipya.
Maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa hufanyika Julai 25, ya kila mwaka, kwa   kufanya  maombolezo ya Mashujaa waliopigana katika vita mbalimbali katika harakati za kutetea uhuru wa nchi ya Tanzania.
Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma, ambapo Rais John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria maadhimisho hayo kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tanzania yasherekea Siku ya Merit kwa kukutanisha vijana kuwapa elimu kuhusu SDGs

Tanzania yasherekea Siku ya Merit kwa kukutanisha vijana kuwapa elimu kuhusu SDGs

July 25, 2016



Katika kusherekea Siku ya Merit ambayo huadhimishwa kila Julai, 24 ya kila mwaka, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja ili kuweza kujadili kuhusu Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na kuweka mipango jambo gani lifanyike ili kuhakikisha kila raia anapata elimu kuhusu SDGs.

Akizungumza na Mo Blog kuhusu siku hiyo, Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga alisema kwa Tanzania mwaka huu wamekutanisha vijana kwa pamoja na kujadili jinsi gani wanaweza kusaidia watu wengine kujiunga katika utekelezaji wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililokutanisha vijana ikiwa ni katika kusherekea Siku ya Merit. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)

Alisema pamoja na kukutanisha vijana pia wamekutanisha mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambayo yataweza kuelezea jinsi gani yanafanya kazi, jinsi ambavyo yanaweza kuwasaidia vijana na jinsi ambavyo wanaweza kusaidiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kutekeleza Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

"Kwa mwaka huu tumekutanisha mashirika ambayo yameungana nasi katika kuadhimisha Siku ya Merit lakini pia tuna vijana ambao wameshamaliza vyuo kwa sasa wanatafuta ajira, vijana waliomaliza kidato cha sita na wengine wamemaliza kidato cha nne," alisema Rose.
Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akizungumza katika kongamano lililokutanisha vijana na kupata elimu kuhusu Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Alisema kuwa wameamua kukutanisha vijana wakiamini kuwa bado wana nguvu na wanauelewa mpana hivyo ni rahisi kwa wao kutumika kutoa elimu kwa watu wengine ambao bado hawajawa na uelewa kuhusu SDGs

Aidha alisema hiyo ni moja ya hatua za awali ambazo wanazifanya kwani wanatambua kuwa kundi kubwa la vijana bado lipo mtaani na hivyo baadhi yao wanataraji kwenda katika mkutano wa kujadili Maendeleo Endelevu (SDGs) utakaofanyika New York, Marekani na baada ya kurejea watarudi na mipango mkakati ambayo wataitumia kufikisha elimu kwa kila mtu ili ajue SDGs ni nini na jinssi gani inaweza mfikia. (Na Rabi Hume - MO Blog)
Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akiendelea kuzungumza na vijana kuhusu SDGs.
Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu (SDGs), Nicolaus Mukasa akiwapa elimu washiriki kuhusu SDGs.
Baadhi ya wawakilishi wa mashirika yaliyoshiriki kongamano hilo wakielezea jinsi mashirika yao yanafanya kazi, jinsi yanavyoweza kuwasaidia vijana na kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kusaidia kusaidia kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).





Baadhi ya washiriki waliohudhuria kongamano hilo.


Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.