DJ LUKE RAIS WA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV 2018

March 25, 2018
Matokeo ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Lucas Mukami (DJ Luke) ibuka mshindi wa Urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV kwa kura 315, dhidi ya Liberatus Mwang'ombe, aliepata kura 262. akifuatiwa na Rebeca 24.
VICE PRESIDENT Joha 352 Joyce 248. SECRETARY Cleopatra 311 Omby 214 Dotto 70. ASST SECRETARY Saria 360 DMK 23. ASST. TREASURY Magret 263 Mikidadi 329.... BOARD Mashaka 413 Zena 296 Jabil 330. Pius 454 Asha 386 Hamza 295 Ruth 250.

WAZIRI UMMY AMTAKA DED TANGA KUTENGA ENEO KWA AJILI YA TAASISI YA GIFT OF HOPE INAYOSIMAMIA KITUO CHA SOBBER HOUSE

March 25, 2018


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akimkabidhi pikipiki Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House cha Gift of Hope kilichopo Kange Jijini Tanga Saidi Bandawe kwa ajili ya kuitumia kwenye matumizi yao


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi ambao waliambatana nae ikiwemo vijana matibabu ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutenga eneo la hekari 10 kwa ajili ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Gift of Hope Foundation ambayo inasimamia kituo cha Sober House.

Hayo ameyazungumza alipotembelea kituo hicho kinachow asaidiawaat hirika wa madawa ya kulevya kilichopo eneo la Kange kata ya Maweniambapo alikabidhi pikipiki 1 kwa ajili ya kituo hicho.

Waziri Ummy alisema jambo linalofanywa na taasisi hi yo lazima liungwe mkono na Serikali kutokana na jitihada zao za kukabiliana na mapambanoya matumizi ya madawa ya kulevya hasa kwa waathirika.

Alisema nguvu kubwa inatumiwa na waanzishaji wa nyumba hizo kwa lengola kusaidia vijana huku wakikosa msaada wa kudumu wa kuwawezeshawaweze kujitegemea tofauti na ilivyo sasa wanavyoishi kwa kuomba misaada.

“Jambo linalofanywa hapa sobber house ni juhudi kubwa na lazima sis ikama serikali tuwaunge mkono hawa watu wakishindwa makundi haya kama yatarudi mitaani hali inaweza kuwa mbaya zaidi”Alisema.

Aidha alisema kufuatia taarifa ya taasisi hiyo ya kuhitaji eneo la
kutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,shughuli za mikono ikiwamou fugaji,kilimo cha mbogamboga na hata ufundi ni jambo la msingi naviongozi wote wanatakiwa walione kwa jicho la tatu.

“Jamani hawa watu wasiishi kw a kuombaomba lazima wapatiwe eneo lao na waanzishe miradi yao itakayowasaidia kujikimu na mahitaji ya kila sikuna tukifanya hivi tutaokoa kundi kubwa la vijana linaloangamia sikihadi siku”Alisema Waziri Ummy.

Mbali na hilo alisema akiwa kama Waziri mwenye dhamana atahakikisha dawa za Methadol zinafika Moani hapa kama ilivyo katika mikoa mingine ili kuweza kuwasaidia vijana hao kupunguza makali ya madawa.

“Kwanza nashangaa kama tanga haipati dawa hizi za methadol ikiwa ni mkoa wa pili baada ya dare s salaam kwa wingi wa watumiaji wa mada ninayo dhaama na dawa hazi zitafika sasa kwa ajili ya vijanawetu”Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi hiyo Said Bandawe alisema kwasasa wanaishi katika nyumba ya kupanga na wamepewa eneo na wamepewa eneo la mtu kwa kuazimwa kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga nashughuli za ufugaji.

Alisema maisha ya vijana  bado magumu hasa swala la chakula,malazi,dawa za Methadol, na namna ya kupata mahitaji ya kila siku kwa ujumla huku akijaribu kutafuta mahitaji kwa kuomba misaada kuwasaidia vijana haowanaokadiriwa kufikia 68.

WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO

March 25, 2018

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Na Hamza Temba, Dodoma
..........................................................

Wizara ya Maliasili na Utalii imeendesha warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Akifungua warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini hapa jana, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na nchi ya Uswizi kupitia shirika la kiuchumi la State Secretariat for Economic Affairs-SECO.

Alisema mradi huo pia unalenga kuongeza ununuzi wa mazao na bidhaa za mbogamboga na matunda zinazozalishwa Tanzania, kuongeza  ajira kwa Watanzania waliojifunza vema masuala ya utalii, na kuongeza nafasi ya kujadili dhana ya Utalii Wenye Manufaa kwa jamii.

"Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Umoja wa Mataifa zinazohusika na eneo la  Maendeleo ya Biashara (UN Trade Cluster Organizations) - UNIDO, UNCTAD, ITC na ILO, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, na sekta binafsi" alisema Dk. Kigwangalla.

Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ilitekelezwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2016 ambapo jumla ya Dola za Kimarekani milioni 3.5 zilitumika.

"Awamu ya pili ya mradi ilianza kutekelezwa mwaka 2017 na utarajiwa kukamilika mwaka huu 2018. Jumla ya Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimetumika katika awamu hii ya mradi" alisema.

Alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuhifadhi mazingira, na kufanya utafiti wa mazao mbalimbali ya utalii ambao utawezesha kuandaa Sera na Mikakati mipya ya kukuza Utalii hapa nchini.

Warsha hiyo ya siku moja imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wiazara hiyo, Degracious Mdamu muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja  iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Ernest Mwamaja ambaye aliwasilisha mada katika warsha hiyo.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.
Naibu Waziri wa Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii akichangia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo na kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsious Mdamu akitambulisha wajumbe wa meza kuu wakati wa warsha hiyo.
 Wajumbe wa Meza Kuu.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
 Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
Warsha ikiwa inaendelea.
Baadhi ya washiriki na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

KINANA AZINDUA SEMINA ELEKEZI KWA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA LEO JIJINI DODOMA.

March 25, 2018
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James (MCC) Kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Kufungua Semina Elekezi kwa Wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana Wa Chama cha Mapinduzi leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kutoa maelezo na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo Maalum kwa Wajumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa leo katika Ukumbi wa NEC katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia semina elekezi ,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni Ndg.Steven Kazidi akiwasilisha Mada katika Semina Elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana CCM Taifa,leo katika Ukumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Meza kuu ikifuatilia Semina
(Picha zote na Fahadi Siraji wa UVCCM)

Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu

March 25, 2018
 Waziri wa Haki na Katiba, Prof Palamaganda Kabudi akionesha kitabu cha vyeti vya kuzaliwa pamoja na simu ya kisasa alipozindua zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu. Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill. Kulia ni Mwenyekiti was Bodi ya RITA, Prof. Hamisi Dihenga.


MARA, tarehe 20 Machi, 2018 – Mkoa wa Mara na Simiyu imezindua kuanza kwa mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi ambao unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watoto 700,000 walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo.


Uzinduzi huo uliofanyika katika mji wa Musoma, ulihudhuriwa na Mheshimiwa Waziwa wa Katiba na  Kisheria Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, UNICEF na Mwakilishi wa Serikali ya Canada na wageni wengine mashuhuri.  Mfumo huo wa usajili uliorahisishwa utasaidia usajili wa watoto wote wachanga na kupunguza idadi kubwa ya watoto ambao hawajasajiliwa walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo miwili.


Mfumo huu ambao unajitegemea usio ratibiwa kutoka serikali kuu unasogeza  huduma ya usajili karibu na jamii. Inaanzisha vituo vya usajili katika vituo vya afya, ambavyo vinatoa huduma ya afya ya uzazi na watoto, na kwenye jamii katika ofisi za mtendaji wa kata kuendana na sera ya serikali ya ugawaji wa madaraka kwa serikali mitaa.  


Zoezi hili limeziba pengo la mijini na vijijini, kwa kuzipa jamii za pembezoni nafasi ya kusajili watoto wao.  Inatatua suala la msingi la upatikanaji na uwezo wa kumudu jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa katika usajili wa vizazi nchini Tanzania.


Kwa kuanza kwa mfumo huo katika mikoa miwili, wazazi wanaweza kufikia kwa urahisi zaidi ya vituo 790  vya usajili kulinganisha na vituo 11 vya usajili vilivyokuwepo awali. Zaidi ya Maafisa Usajili 1,700 wameshapewa mafunzo kwaajili ya kusaidia mchakato wa usajili.


Pamoja na mfumo mpya serikali pia imefuta ada ya usajili na nakala ya kwanza ya cheti cha usajili kinatolewa bure, jambo linalofanya ‘hatua fupi za mchakato wa usajili kwawazazi kupata cheti cha kuzaliwa.  Kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi taarifa husafirishwa mara moja kwa njia ya ujumbe mfupi SMS, karahisisha ufuatiliaji wa maendeleo ya usajili hapo kwa hapo .


Mfumo huu wa kujitegemea unarahisisha kwa kiasi kikubwa usajili wa vizazi kwa eneo la Tanzania bara, baada ya kudorora kwa miaka mingi. “Tunabadilisha mfumo kurahisisha watoto na familia kuweza kupata haki yao ya kuwa na cheti cha kuzaliwa," alisema Emmy Hudson Kaimu  Mkurugenzi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA), anayewajibika katika usajili wa matukio muhimu ikiwemo kuzaliwa. Aliongeza kwamba; “Sasa wazazi wanaweza kupokea vyeti vya kuzaliwa kutoka katika kituo husika cha kutolea huduma za afya au kupitia ofisi za mtendaji wa kata kwa wakati.  Mfumo huu umewasaidia maelfu ya watoto katika mikoa hiyo ambako mfumo huu unafanyakazi na tunapanga kusambaza mfumo huu katika mikoa yote ya Tanzania bara ndani ya muda mfupi kadri iwezekanavyo.” Aliendelea kuongeza zaidi kwamba, “Serikali ya Tanzania inatambua mchango wa Serikali yaCanada, UNICEF na TIGO kwa mchango wao katika suala hili”.


Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Ms Maniza Zaman alisema kwamba "Kila mtoto ana haki ya kupata utambulisho. Mfumo huu mpya unarekebisha kiwango kidogo cha usajili wa uzazi na matokeo yake mamilioni ya watoto wa chini ya miaka mitano ambao walikuwa hawaonekani katika takwimu za taifa sasa watakuwa wanaonekana.   Hii itasaidia watoto wengi wa kitanzania kudai haki yao na kulindwa, na serikali itakuwa na takwimu bora zaidi kwaajli ya sera na mipango."


Serikali inatekeleza mfumo mpya tangu 2012 kwa kushirikiana na UNICEF, TIGO na Serikali ya Canada, ambayo inatoa fedha. Kuanza kwa mfumo huu mkoani Mara na Simiyu, utaongeza mikoa 2 ambayo itakuwa ikiongezeka kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Geita, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Mwanza, Iringa and Njombe ambayo tayari imeshaanza na kufikia watoto milioni 2 walioko chini ya umri wa miaka mitano.


Serikali ya Canada wanaamini katika haki za watoto, wakiwa wanashikilia kwamba kila mtoto anahitaji ushahidi wa kudumu wa kuzaliwa kwake kwani inatengeneza utambulisho wa mtoto kitaifa na haki zao.


"Usajili wa kuzaliwa unasaidia kuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma za kiafya na za kijamii walizonazo kwa kisheria", alisema Ian Myles, Kamishina Mkuu wa Canada nchini Tanzania.   “Canada wanajivunia kuunga mkono juhuduza tanzania katika kukuza usajili wa uzazi, kuwasaidia watoto na familia zao kujipatia haki zao za msingi kama wananchi wa Tanzania . Tunafuraha kuona uzinduzi wa mfumo huu mkoani Mara na Simiyu, ikiwa ni mwenyelezo wa mafanikio ya uzinduzi wa mfumo huu katika mikoa ya Iringa, Njombe, Geita na Shinyanga, Lindi, na Mtwara.” Mpaka sasa mfumo huu umezifikia  Halmashauri za wilaya 58 katika mikoa 9 ya Tanzania bara.


Msaada wa kifedha kutoka serikali ya Canada umewezesha uanzishwaji wa mfumo endelevu wa usajili wa vizazi yenye lengo la kufikia mamilioni ya wasichana na wavulana walioko chini ya umri wa miaka mitano.  Mfumo huu utachangia katika Usajili wa Raia wenye ufanisi na Mfumo wa Takwimu Muhimu katika nchi, ambao unaanzishwa.


TiGO inaunga mkono juhudu hizo kupitia teknolojia ya simu, ambayo inahakikisha kwamba taarifa za usajili ya vizazi unaingizwa na kutumwa kwenye database kuu iliyoko RITA wakati huo huo.   TIGO pia inatumia vyombo vya habari kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa usajili wa uzazi nchini Tanzania.

Akiongea katika sherehe za uzinduzi,  Mkurugenza wa TIGOKanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa amesema “kwa pamoja tuna dhamana ya kuhakikisha ustawi wa nchi na wananchi wake. Maamuzi yaTIGO kuunga mkono juhudu hizi inasisitizia jitihada zetu za kujenga mfumo imara wa kijamii ambao uleta ahadi ya teknolojia katika jamii tunakofanyia kazi.    Kwa uvumbuzi huu, TIGO inatoa mchango mzuri na mkubwa kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu na kulinda haki za watoto. Kwa kuongezea, ushirikiano huu unadhihirisha nafasi ya kampuni za simu katika kutatua mahitaji ya kijamii kupitia matumizi ya teknolojia yako na ujuzi wao.’

MKURUGENZI WA SBL AFANYA MAZUNGUMZO MAOFISA IDARA YA UHAMIAJI

March 25, 2018


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie,



Dar es Salaam, Machi 23 2018- Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, jana alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa ni sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
“Tukiwa kama kampuni inayoheshimu sheria na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla, tumekuwa tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha  haki na maslahi ya wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie
SBL imeajiri wafanyakazi zaidi ya 700 katika viwanda vyake vilivyopo Moshi, Mwanza na Dar es Salaam. Bia yake mama ya Serengeti Premium Lager ilizalishwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia kimea kwa aslimia 100 na imeweza kushinda zaidi ya tuzo kumi za dhahabu za kitaifa na kimataifa.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, SBL imekuwa huku ikiongeza idadi ya bidhaa inazozalisha. Baada ya kisisi iikubwa cha hisa kuchukuliwa na Kampuni ya Bia ya AFRIKA Mashariki (EABL)/Diageo mwaka 2010 kumekuwepo uwekezaji mkubwa amboa umefanikisha uzalishaji w3a bidhaa zenye ubora wa kimataifa na kutengeza fursa kwa Watanzania. Moja kati ya nguzo za Diageo ambayo ni kampuni mama YA sbl ni kujenga na kuwawezesha wafanyakazi wake sehemu yoyote inapofanya kazi ikiwamo Tanzania. Kutokana na hili idadi ya wataalamu wageni imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka zaidi ya 30 hadi sita kufikia mwezi Machi 2018 ikiwa ni chini ya asilimia 1 ya nguvu kazi katika kampuni


“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuimarisha mahusiano  na wafanyakazi wetu. Tutaendelea kukidhi mahitaji yao kwa kuwahakikishia bidhaa bora ikiwa ni sehemu muhimu kwa biashara yetu,”anasema mkurugenzi huyo.

MWISHO//

ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES,AWATAKA WAWE JASIRI

March 25, 2018
 Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Zakia Meghji akitoa maneno ya hamasa kwa vijana wa Girl Guides katika semina iliyofanyika Makao Makuu ya TGGA, Mtaa wa Kibasila, Upanga Dar es Salaam.

Meghji ambaye aliwaelezea historia ya maisha yake tokea utotoni, shuleni, chuoni na ya kisiasa, aliwataka Girl Guides kuwa jasiri, waadilifu, wazalendo na wachapakazi pamoja na kuwa na vision..

Aliwafundisha jinsi ya kupambana na wanaume walaghai wanaowataka kimapenzi na kuwaharibia ndoto yao ya kielimu na maisha kwa ujumla.

Pia aliwataka kuheshimu mila nzuri, desturi na utamaduni mzuri pamoja na kuwaheshimu wazazi na jamii bila kusahau kushirikiana nao katika masuala mbalimbali.

Aliwaambia kuwa baadhi ya mambo muhimu ni kuwa na tabia ya kushirikiana na watu mbalimbali kwa lengo la kubadilisha uzoefu, mawasiliano na kwamba unatakiwa kuanza uongozi ukiwa kijana siyo ukiwa mzee.

Anawaeleza kuwa ushupavu wake ulimfanya kwa mara ya kwanza awe mbunge mwaka 1985, amekuwa Mkuu wa wilaya na waziri kwa muda mrefu mpaka alipoamua kustaafu.

 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0754264203,0689425467
 Girl Guides wakiimba wimbo wa hamasa
 Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema akisalimiana na Girl Guides kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam na mikoani.
 Mkufunzi wa TGGA Makao Makuu ya TGGA,  akielezea historia ya chama hicho
 Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa TGGA, Grace Makenya akitoa maneno ya hamasa kwamba daima hastaafu na kwamba yeye hivi sasa ana miaka 70 lakini bado ni Girl Guides

 Girl Guides wakiimba wimbo wa hamasa
 Yess Girl, Nadine Ratovoson kutoka Madagascar akijitambulisha. Yupo nchini kwa ziara ya mafunzo ya miezi sita ya kubadilishana mafunzo.
 Yss Girl kutoka Zambia ambaye yupo nchini kwa ziara yamiezi sita ya  kubadilisha mafunzo
 Miryam Mjema na Grace Makenya
 Kamishna wa TGGA, Temeke, Komba akijitambulisha
 Sophia Simon (kulia) Mkufunzi wa TGGA Temeke, akijitambulisha
 Kamishna wa TGGA Ilala, Stellah Kasisika akijitambulisha
 Girl Guide wakiwa na furaha
 Meghji akisisitiza jambo
 Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi (kulia) akiwa na Mdau wa TGGA, Asiah Abdul Azizi na Candida Bahame.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Zanaki, Winhope Mgalega, akimmuliza Zakhia Meghji ni nini siri ya mafanikio yake.

UBALOZI WA KUWAIT NA TAASISI YA DORIS MOLLEL WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WATOTO NJITI, HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA, DODOMA

March 25, 2018
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika, sehemu ya vifaa tiba kwa ajili ya Watoto Njiti, vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma. Wengine pichani ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Hospitali hiyo, Neema Tawale (wa pili kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Huduma za Uuguzi, Salome Kasanga.

The Ambassador of Kuwait in Tanzania His Excellency Hon. Jaseem Al Najem (L) Handing Over Equipments to support Premature babies at Benjamin Mkapa Hospital to the Executive Director of the Hospital, Dr. Alphonce Chandika, A support from the Embassy of Kuwait in Collaboration with Doris Mollel Foundation end of this week in Dodoma. second from left is Ms. Doris Mollel Founder of Doris Mollel Foundation and Ambassador to Preterm babies in Tanzania , Neema Tawale(second from right) together with Acting Director of Nursing at Benjamin Mkapa Hospital Sr Salome Kasanga.
 Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akieleza jambo kwa waandishi wa habari juu ya vifaa hivyo vilivyogharimu dola za Marekani elfu ishirini (20,000 USD) huku Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (kulia) wakimsikiliza, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem,  Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Januarius Hingi wakati akitoa maelezo ya namna vifaa hivyo vitakavyosaidia wakina mama wanaojifungua watoto wanaozaliwa kawaida na wale wanaozaliwa kabla ya wakati. 
Sehemu ya vifaa hivyo.
-- Othman Michuzi Editorial Director & Chief Photographer CELL: +255 713 775869 /+255 789 103610 WEB: issamichuzi.blogspot.com mtaakwamtaa.co.tz michuzijr.blogspot.com EMAIL: othmanmichuzi@gmail.com Dar Es Salaam. Tanzania. East Africa.

ONGEZEKO LA WATU, WATUMIAJI WA SIMU KUKUZA BIASHARA ZA MTANDAONI AFRIKA

March 25, 2018


Na Jumia Tanzania


Kuendelea kukua kwa ongezeko la idadi ya watu na watumiaji wa simu za mkononi barani Afrika kuna mchango kwenye ukuaji wa biashara kwa njia ya mtandao. Hilo linaenda sambamba na ueneaji wa huduma za mtandao wa intaneti ambao umebadili namna waafrika wanavyotumia simu zao za mkononi hivi sasa. 

Hivi karibuni Jumia, mtandao unaojihusisha na uuzaji na manunuzi ya bidhaa mtandaoni, ulizindua ripoti kuhusu sekta ya bidhaa za simu kwa mara ya kwanza nchini Tanzania. Ripoti hiyo imeangazia masuala mbalimbali kwenye setka hii pamoja na mchango wake katika shughuli za kijamii na kiuchumi nchini. Ripoti hiyo pia imeangazia namna watanzania wanavyotumia simu na teknolojia ilizoambatana nazo kama vile huduma za fedha na biashara za mtandaoni. 

Akizungumzia juu ya ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Zadok Prescott amebainisha kuwa uwasilishwaji huo umekuja katika kipindi ambacho wanaendesha kampeni ya ‘Wiki ya Simu’ itakayohusisha uuzaji wa simu kwenye mtandao wao kwa kushirikiana na makampuni tofauti ya simu nchini.

“Jumia inaamini kwamba soko la simu ni miongoni mwa sekta kubwa kwenye nchi zinazoendelea barani Afrika, na ina mchango mkubwa kwenye kuziwezesha sekta zingine. Wiki ya Simu itafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kuanzia Machi 24 mpaka 30, kampeni ambayo ni kubwa kabisa ndani ya mwaka ikiwa imejikita kwenye bidhaa moja pekee. ‘Jumia Mobile Week’ itawawezesha watanzania kujipatia mapunguzo na ofa mbalimbali kwenye bidhaa za kutoka kampuni tofauti za simu,” alisema Prescott.

Sekta ya bidhaa za simu Afrika ina thamani ya bilioni $110 

Hivi sasa, idadi ya watu barani Afrika imefikia bilioni 1.27 ambapo takribani watu bilioni 1.04 wanatumia simu za mkononi, sawa na ueneaji kwa asilimia 82. Kuongezeka kwa idadi ya watu na mtandao wa intaneti kwenye maeneo mbalimbali kumeendelea kuifanya sekta hiyo kuwa na tija zaidi. Sekta hii ina mchango mkubwa kwenye maisha ya kila siku ya watu kama vile huduma za fedha kwa njia ya simu. Ambapo nchini Tanzania pekee, zaidi ya watu milioni 40 waliripotiwa kuunganishwa na huduma za simu za mkononi wakati kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 50 zikitumwa kwa njia ya simu. 

Mwaka 2016, huduma za teknolojia ya simu zilizalisha kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 110 katika uchumi wa nchi za Kiafrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, sawa na asilimia 7.7 ya pato la ndani la taifa. Mchango wa sekta ya simu kwenye pato la taifa unatarajiwa kukua na kufikia dola za Kimarekani bilioni 142, sawa na asilimia 8.6 ya pato la ndani la taifa, kufikia mwaka 2020, kwani nchi nyingi zitakuwa zikinufaika na maendeleo katika uzalishaji na ufanisi utakaoletwa na kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi. 


Ueneaji wa watumiaji wa simu Tanzania unakaribiana na wa Afrika

Hivi karibuni, Tanzania ilitangaza kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa simu na kufikia zaidi ya milioni 40, ambayo ni sawa na ueneaji kwa asilimia 72, asilimia 10 pungufu ya ueneaji wa bara zima la Afrika ambao umefikia asilimia 82. 


Uwepo wa ushindani wa bei na motisha kwa wateja kwenye soko la simu umekuwa na mchango mkubwa katika unafuu wa upatikanaji wa bidhaa hizo. Kitu kingine cha muhimu, ni uwepo wa huduma mpya zinazotambulishwa na kampuni tofauti za mitandao ya simu zimekuwa ni kichocheo kikubwa kwa watanzania wengi kumiliki simu za mkononi.

Simu kutoka bara la Asia zatawala kwenye mtandao wa Jumia

Bidhaa za simu kutoka bara la Asia zinaongoza kwa kuwa miongoni mwa simu zinazonunuliwa zaidi kwenye mtandao wa Jumia. Kampuni zinazofanya vizuri ni pamoja na Tecno, Samsung, Lenovo, na Infinix, ukilinganisha na simu kutoka nchi za Magharibi (Ulaya na Marekani). Infinix ni simu inayoongoza kwa mauzo katika nchi 10 ambazo Jumia inaendesha shughuli zake, wakati Tecno ikiwa ni kinara katika mtandao huo nchini Tanzania.  

Simu kutoka bara hilo zimefanikiwa kulitawala soko la Afrika kwa sababu zimeweza kuendana na mahitaji yake. Nchi nyingi za Kiafrika bado zinaendelea, ni dhahiri kwamba nguvu ya manunuzi bado ni ndogo. Kikubwa zaidi, simu zao ni za gharama nafuu na zinapatikana kwa urahisi, karibuni kila mji ukilinganisha na simu kama vile iPhone ambazo hupatikana kwenye miji mikubwa na ya kibiashara pekee. 


Zaidi ya watu bilioni 4 duniani wanatumia intaneti

Idadi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti duniani imevuka bilioni 4, idadi ambayo ni sawa na zaidi ya nusu ya watu wote duniani. 


Tanzania nayo inakua kwa kasi kwa upande wa idadi ya watumiaji wa simu na mtandao wa intaneti katika ukanda wa Mashariki na Afrika kwa ujumla. Mapema mwaka huu, TCRA iliripoti juu ya kuongezeka kwa idadi ya watumiaji na ueneaji wa intaneti kufikia milioni 23 sawa na asilimia 45 mwaka 2017, kutoka watumiaji milioni 7.5 sawa na asilimia 17 mwaka 2012. 


Simu ni mkombozi kwa watanzania kiuchumi na kijamii

Idadi ya watumiaji wa simu za mkononi inatarajiwa kuvuka bilioni 5 kufikia mwaka 2019. 

Nchini Tanzania, idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi wameonekana kukitumia kifaa hiki kwa manufaa mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. Ukiachana na kuzungumza, kutumiana jumbe za maandishi au kuingia kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya watanzania wameanza kufanya shughuli zao za manunuzi mtandaoni, tena kwa kutumia simu zao za mkononi. 


Mwaka 2017, asilimia 83 ya wateja wa Jumia walifanya manunuzi kwa kutumia simu za mkononi. Hii ni ishara kwamba idadi ya watanzania inazidi kuongezeka katika kutumia simu za mkononi kurahasisha shughuli zao za kila siku. 

“Biashara kwa njia ya mtandao bado ni sekta mpya Tanzania, ambayo ipo kwenye hatua za awali za ukuaji. Naamini kwamba ueneaji wa huduma ya mtandao wa intaneti utachochea ukuaji wa sekta hii. Barani Afrika hivi sasa, ni idadi ndogo sana ya manunuzi yanafanyika mtandaoni, yaani kununua bidhaa kwa kutumia intaneti,” alielezea na kuhitimisha, “kuna ukuaji mkubwa wa idadi ya watu wanaomiliki simu za mkononi, hususani simu janja. Hii ni hatua muhimu kwenye sekta. Lakini bado idadi ya wamilikaji wa simu janja ni ndogo, changamoto ambayo Jumia tumeiona na tungependa kuitatua kwa kuhakikisha kwamba zinapatikana kwa gharama nafuu na urahisi. Na hilo ndilo dhumuni la kampeni ya ‘Wiki ya Simu’.’”