Timu ya uendeshaji wa huduma za afya wilayani Korogwe, mkoani Tanga
Meneja
wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akitoa
maelezo ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa kikao cha Timu ya Uendeshaji
wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa
kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika
Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha
kwanza kilifanyika jana Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya
Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni mgeni rasmi aliyekaribishwa kufungua
kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis
Kalinjuna (katikati) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry
Mwakanyamale (kulia).
Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale (Kulia)
akiongea wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (Katikati) katika ufunguzi wa kikao
cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT)
kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi
(TIKA). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika
ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni Meneja wa
Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).