TGGA YAZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA

May 16, 2017
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi, Thomas Safari akizindua rasmi Kampeni ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani itakayofikia kilele Mei 28. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi leo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TGGA, Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Lindi wakiingia kwa maandamano kwenye Uwanja wa Ilulu, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

Na Richard Mwaikenda-Lindi
SERIKALI ya Mkoa wa Lindi imekubali ombi la Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), kwa kila shule kutenga chumba kimoja kwa ajili ya kujistiri wasichana wakati wa hedhi.

Ombi hilo lilitolewa na Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi, ambapo aliiomba serikali na walimu wakuu wa shule kutenga vyumba mashuleni vya wasichana kujihifadhi wakati hedhi.

Shaba ambaye ni mwalimu mstaafu, alisema kuwa wakati akitumikia ualimu katika shule mbalimbali alikuwa anatenga vyumba kwa ajili ya kazi hiyo na kwamba viliwasaidia sana wanafunzi wasichana.

Akihutubia wakati wa hafla hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya, Thomas Safari alisema vyumba vya siri kwa ajili ya wasichana wakati wa hedhi ni muhimu sana kwani vinawafanya wawe salama kiafya na wasafi wakati wote.

Alisema watahakikisha kwa kila shule katika mkoa huo inakuwa na chumba cha siri kwa wasichana, iliwe mfano hata kwa mikoa mingine na taifa kwa ujumla.

Pia aliwaasa wazazi, walezi na waalimu kueneza elimu hiyo ili watoto waelewe vizuri umuhimu wa usafi wakati wa hedhi, jambo ambalo litawafanya wawe na furaha, afya na usafi, hivyo kuondokana na mazoea ya kujinynyapaa na kulifanya la siri.

"Tuondokane na baadhi ya mila zetu potofu zinazolifanya suala la hedhi kuwa la siri, inatakiwa kuanzia sasa watoto wa kike wabebe begi lenye vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia wakati wa hedhi, ikiwemo khanga, pedi, vitambaa na mtandio.
"alisema Safari.


"Inabidi sote tuwe mabalozi kwa kuongea na watoto, tutunze afya na usafi wao, kwani hao ndiyo viongozi wa taifa letu la kesho
. Bila kuwa na afya njema hatutakuwa na viongozi imara wa  Taifa letu."Alisisitiza Safari.

Dhima na lengo la TGGA ambayo ina wanachama zaidi 100,000 nchininni kuwajengea wasichana nafasi ya kujithamini, ari ya maendeleo, uzalendo kwa nchi na kujiamini.







 Wanafunzi wakiimba wimbo wa hamasa ya kampeni hiyo
 Mmoja wa wanafunzi akielezea jinsi ya kutumia pedi

 Maandamano ya wanafunzi kwenye Uwanja wa Ilulu
 Wanafunzi wa kike wakiwa na furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
 Rehema Kijazi wa TGGA Makao Makuu akiwahamasisha wanafunzi wakati wa maandamano
 Wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kuhamasisha matumizi salama ya vihifadhi yaani Pedi


 Viongozi wa TGGA Mkoa wa Lindi wakiwa eneo la uzinduzi wa kampeni hiyo
 Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Saharifa Mkwango akisherehesha 
hafla hiyo

 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa kuwaeleza  dhima na lengo la chama hicho kuwaelimisha wasichana kuhusu maadili mema na matumizi sahihi ya pedi wakati wa hedhi.
 Baadhi ya wazazi miongoni mwao wakiwemo walimu wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi

 Girl Guids kutoka Rwanda, Uganda na Madagascar wakihamasisha matumizi ya pedi wakati wa hedhi

 Mgeni rasmi, Thomas Safari akihutubia
 Safari akizindua rasmi kampeni hiyo kwa kufungua kasha lenye pedi
 Mgeni rasmi akikabidhi makasha yenye pedi yaani vihifadhi kwa wanafunzi wa shule mbalimbali



 Wanafunzi wakisakata muziki wakati wa kampeni hiyo

 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliokabidhiwa makasha ya pedi zitakazogawiwa shuleni kwao

 Girl Guids wakiwa katika picha ya pamoja

 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akisaidiana na mwanafunzi Caren Seki kumwagilia mti alioupanda katika shule ya Msingi Mtuleni
Mgeni rasmi, Thomas Safari akipanda mti wa kumbukumbu katika Shule ya Msingi Mtuleni
Girl Guids kutoka Rwanda, Madagascar na Uganda ambao wapo nchini kwa mpango wa kubadilishana uzoefu wakipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya msingi Mtuleni, Lindi
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF) ALIYEAMBATANA NA UJUMBE WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF) ALIYEAMBATANA NA UJUMBE WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

May 16, 2017
tot1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
tot2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
tot3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
tot4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
tot5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang wanne kutoka (kushoto) Gavana wa Benki Kuu (BOT) Profesa Beno Ndulu, wapili kutoka kulia, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango watatu kutoka kushoto pamoja na ujumbe wa Mkurugenzi huyo wa IMF.
tot6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

VIONGOZI WA KIJIJI CHA KIBADA WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA KIJIJI KUONGOZA WANANCHI

May 16, 2017
Kushoto ni Jamali Juma afisa mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira kwa vitendo (LEAT) akifuatiwa na Afisa habari wa LEAT Edina Tibaijuka pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili wakati wa mkutamo wa hadhara wa kijiji cha kibada ukiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha kibada 
Hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo wa hadhara wenye lengo la kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na Maliasili za kijiji

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Ili kuongoza au kusimamia jamii ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuondoa migogoro mbalimbali inajitokeza na itakayo kujitokeza kwa sababu ya kuzivunja sheria na taratibu hizo.

Hayo yamesemwa na Afisa mradi wa Mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira Jamali Juma wakati wa mkutano wa kijiji cha kibada kilichopo kata ya sadani wilayani Mufindi Mkoani Iringa kwa kuwataka viongozi na wananchi kutimiza wajibu na haki ili kukifanya kijiji kiwe na maendeleo.

Juma alisema kuwa sheria na taratibu zilizopo hapa kijiji zitanatakiwa kufuatwa kwa ajili ya manufaa ya sasa na ya kizazi kichacho lakini pia inajenga imani na amani ya kijiji.

"Leo hii usipofuata sheria na taratibu za kijiji lakina utakwazana na viongozi au wananchi na kupelekea migogoro ndani ya kijiji kwa kuwa sheria zinakuwa zimekiukwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977" alisema Juma

Aidha Juma aliwataka viongozi wa kijiji cha kibada kuitisha mikutano ya hadhara na kuwasomea mapato na matumizi ili wananchi wajue wapi kijiji kimetoka kimaendeleo na ipi mikakati ya kimaendeleo kijiji.

"Ukipita vijiji vingi unakuta migogoro mingi inayotokana na kutosomewa mapato na matumizi kwa sababu binafsi za viongozi husika hivyo ni lazima viongozi wa vijiji kuongoza vijiji kwa kufuata sheria na taratibu za kijiji"alisema Juma

Lakini Juma aliwataka wananchi wa kijiji cha kibada kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na Maliasili walizonazo na kuacha kuishi kwa mazoea ili kuboresha Mazingira ili yarudi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kulima kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia.

"Jamani kuna njia nyingi za kulima mboga mboga kwa njia ya kisasa kwa mfano unaweza kuchukua gunia au sarufeti na kuuweka mchanga kisha kupanda mbegu za mboga na kumwagilia maji machafu unayokuwa unayatumia nyumbani kwao na kuvifanya vyanzo vya maji kuwa salama" alisema Juma

Fadinard yilikwipande,Shauri na Stephano waliitaka serikali kuanga upya sheria za kilimo cha mboga mboga kilinacholimwa kwenye utongo mnyevumnye au karibu na vyanzo vya maji kwa akili ya kilimo changu kwa ajili ya kujiongezea kipato chao.

"Sisi tunalima kwenye vijaruba vidogo vidogo tu maarufu kama vinyungu wala hatuleti madhara yoyote ya uharibifu wa vyanzo vya maji na mbona miaka yote tulikuwa tunalima bila kuharibu Mazingira na serikali itambue kuwa Kilimo hiki ni cha kitamaduni sasa inatakiwa kutofautisha sheria za mambo ya asili au ya kitammaduni"walisema wananchi wa kibada

Kwa upande wake Afisa habari wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira kwa vitendo (LEAT) Edina Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha kibada kuzifuata sheria walizoletewa za kulinda Mazingira na vyanzo vya maji hadi pale serikali itakapoa tamko liingine kuhusu hiyo sheria.

"Jamani sheria ni msumeno hivyo mnapaswa kuzifuata kwa kuwa msipozifuta mtatiwa nguvuni na kupelekwa mahakama hivyo itakuwa inawapunguzia nguvu kazi yenu na kupelekea Msumbufu kwa familia zenu,Mimi nawaomba tiini sheria bila shuruti ili kuepukana na hayo matatizo" alisema Tibaijuka

Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha kibada kupelekea malalamiko yao kwa viongozi wa serikali, madiwani na wabunge wao ili kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo la sheria hiyo mpya iliyokuja baada makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu la kukataza Kilimo chochote kile kwenye vyanzo vya maji.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili aliwaomba viongozi wa serikali kuifikiria upya sheria waliyoitunga juu ya matumizi ya vyanzo vya maji kwa kuangalia utamaduni wa watu Vijijini hasa kwenye swala la Kilimo cha kipindi cha kiangazi maeneo ya mabondeni kwa kuwa wananchi wa Vijijini wantegemea kilimo hicho.

"Hivi kama huku wilaya ya Mufindi wakulima wanategemea Kilimo cha kulima kwenye mabonde maarufu kama Kilimo cha kwenye vinyungu kwa kupanda mboga mboga pamoja na mahindi ya msimu wa kiangazi"alisema Nyavili

UKWELI KUHUSU MTI ULIOGOMA KUNG'OLEWA JIJINI MWANZA

May 16, 2017
George Binagi-GB Pazzo @BMG
Wakazi wa Jiji la Mwanza wameingia katika taharuki baada ya kutokea uvumi wa taarifa za mti kugoma kung’olewa katika eneo la Pasiansi ambapo kuna shughuli ya upanuzi wa barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa Mwanza.

Taharuki hiyo ilianza tangu jana majira ya jioni ambapo mamia ya wananchi walijazana katika eneo hilo ili kushuhudia mgomo wa mti huo ambao inasadikika ulikuwa ukitoa sauti za kulalama mithiri ya binadamu.

Zoezi la kuung’oa mti huo aina ya mwembe limefanikiwa hii leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya shughuli pevu ya kuung’oa kwa kutumia mashine aina ya burudoza huku baadhi wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina na wengine wakisema ni upotoshaji tu ulifanyika juu ya tukio hilo.

Kasim Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works inayojenga barabara ya Pasiansi, amesema taarifa za mti huo kuzungumza ni za upotoshaji na kwamba zoezi la kuung’oa lilichukua muda mrefu tangu juzi ili kupisha hatua za upimaji wa ukubwa wake na kusubiri mashine aina ya“skaveta” iliyofanikiwa kuung’oa.

Katibu wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman, amesema tukio la mti kuzungumza ama kugoma kung’olewa halina ukweli wowote kwa karne hii ya 21 japo matukio ya aina hiyo yalikuwepo enzi za kale kabla ya ujio wa dini barani Afrika ambapo amewatahadharisha watumiaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kujiepusha na usambazaji wa taarifa za upotoshaji.
Zoezi la kuung'oa mti likiendelea
Hapa msumeno ulikata ila mti ukagoma kuangua licha ya kuvutwa
Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa
Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa
Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limezaa matunda
Katibu wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman, akizungumzia tukio hilo
Kasim Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works akizungumzia tukio hilo
Mkazi wa jiji la Mwanza akizungumzia tukio hilo
Wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia tukio hilo
Wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
Wanahabari na wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
Wanahabari na wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
Kushoto ni dereva aliyekuwa akiendesha mtambo uliong'oa mti huo