WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA ARIPOTI OFISINI DODOMA, LEO

October 01, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wakuu wa Ofisi yake  baada ya kuwasili Ofisini kwake mjini Dodoma Oktoba 1, 2016. Kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Ajira, Erick Shitindi, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, Dkt. Hamisi Mwinyimvua na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Makao Makuu, Dodoma baada ya kuwasili Ofisini hapo Oktoba 1, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni,  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Ajira, Eick Shitindi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera na Uratibu, Dkt. Hamisi  Mwinyimvua, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Antony Mavunde.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu, Makao Makuu, Dodoma baada ya kuwasili Ofisini hapo Oktoba 1, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu, Makao Makuu, Dodoma baada ya kuwasili Ofisini hapo Oktoba 1, 2016.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

October 01, 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la JKT Mgulani ambapo shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam zilifanyika.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo katika mti alioupanda eneo la JKT Mgulani Barabara ya kilwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiunga na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
                                           ....................................................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 Oktoba 2016 ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam.
Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya Kilwa – Kurasini katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais  ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora katika utunzaji wa Manzingira.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.
Amesema kuwa jitihada za kupanda miti nchini zinatakiwa kuimarishwa maradufu kwani zitasaidia katika uhifadhi wa mazingira hususani katika suala zima la kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Makamu wa Rais katika hotuba yake ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuongezeka hewa ya ukaa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi kuwa ya watu hivyo jitihada za pamoja kati ya serikali,taasisi binafsi,asasi za kiraia na wananchi zinahitajika katika kutunza mazingira na kupanda miti.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia amepongeza jitihada za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji na uimarishaji wa mifumo ya maji katika barabara itakayosaidia kurahisisha umwagiliaji wa miti iliyopandwa.

Amesema anafaraja na matumaini makubwa kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.

Baada ya kuzindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ambaye aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan Mwinyi itakayotumika kumwagilia miti iliyopandwa pamoja na kuongeza na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Gymkana.

KATIBU MKUU WA CCM, ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CNDD-FDD

October 01, 2016


 Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD cha Burundi Evariste NdayishimIye akimzawadia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kihifadhio cha vitu mbalimbali cha jadi ya Burundi, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Oktoba Mosi 2016, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka. 
  Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD cha Burundi Evariste NdayishimIye akimzawadia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kihifadhio cha vitu mbalimbali cha jadi ya Burundi, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Oktoba Mosi 2016, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mnadhimu Mkuu wa CNDD-FDD, Gerase Ndabirabe na Wapili ni Kaimu Balozi wa Burundi hapa ncini, Prefere Ndayishimiye na Kushoto ni Balozi David Kapya na  Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka. 
 Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD cha Burundi Evariste NdayishimIye akimzawadia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kihifadhio cha vitu mbalimbali cha jadi ya Burundi, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Oktoba Mosi 2016, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mnadhimu Mkuu wa CNDD-FDD, Gerase Ndabirabe na Wapili ni Kaimu Balozi wa Burundi hapa ncini, Prefere Ndayishimiye na Kushoto ni Balozi David Kapya, Katibu wa Habari na Mawasiliano CNDD-FDD Nancy Mutoni,  na  Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka. 
  Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD cha Burundi Evariste NdayishimIye akimzawadia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ngoma ya Burundi inayotambulika Kimataifa,Burundi, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Oktoba Mosi 2016, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mnadhimu Mkuu wa CNDD-FDD, Gerase Ndabirabe na Wapili ni Kaimu Balozi wa Burundi hapa ncini, Prefere Ndayishimiye na Kushoto ni Balozi David Kapya, Katibu wa Habari na Mawasiliano CNDD-FDD Nancy Mutoni,  na  Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka.

 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akimshukuru Katibu wa Habari na Mawasiliano wa CNDD-FDD, Nancy Mutoni baada ya mazungumzo ya Katibu Mkuu wa CCM na Katibu Mkuu wa CNDD-FDD
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsindikiza mgeni wake Katibu Mkuu wa CNDD-FDD, Evariste Ndayishimiye, baada ya mazungumzo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimtoa katika jengo, kwenda kupanda gari Kaibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye, baada ya mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam leo 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiagana na Kaibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye, baada ya mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam leo 
 Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akiagana na Mnadhimu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD, Gerase Ndabirabe baada ya mazungumzo ya Katibu Mkuu wa CCM na Katibu Mkuu wa CNDD-FDD leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam. Kulia ni Balozi David Kapya
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiagana na Kaimu Balozi wa Tanzania hapa nchini Prefere Ndayishimiye baada ya Mazungumzo baina ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) na Katibu Mkuu wa CNDD-FDD, leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
Gari lililombeba Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye, likiondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam, baada ya mazungumzobaina ya Katibu Mkuu huyo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (Kulia). PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

MASAUNI AZITAKA TAASISI ZA KIDINI NCHINI KUPAMBANA NA MAOVU, AFUNGUA MKUTANO WA 47 WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA.

October 01, 2016

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakiwapungia waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanawasili katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masaunia ambaye alikuwa mgeni maalum katika mkutano huo wa 47 wa jumuiya hiyo nchini, aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya katika Mkutano wa 47 wa jumuiya hiyo nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, anayefuata ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia meza kuu) akimsikiliza Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa 47 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia meza kuu) akimsikiliza Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa 47 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokea zawadi ya vitabu vya dini kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry wakati Naibu Waziri huyo alipomaliza kuufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo wa 47 unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 47 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

RC MONGELLA AFUNGUA MKUTANO WA ROBO MWAKA WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU MIKOA MWANZA NA GEITA.

October 01, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita, unaofanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini Mwanza.

Mongella amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa uwazi masuala ya maadili kwa watumishi wa umma na kwamba yawe ajenda ya kudumu katika ngazi mbalimbali za utendaji serikalini hususani katika ngazi ya mahakama.

Amesisitiza mkutano huo kutoka na maadhimio yanayohimiza mahakama kutenda haki na kuleta manufaa kwa wananchi na kuondokana na malalamiko kwamba mahakama hazitendi haki katika maamuzi yake.

Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, chama hicho kinahakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kutenda haki na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa chombo hicho katika utoaji wa haki.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma. 
Na BMG
Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe.Robert Makaramba, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, akizungumza na wanahabari nje ya mkutano huo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi mkoani Mwanza, Mhe.Wilbert Martin Chuma, akizungumza kwenye mkutano wa robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu mikoa ya Mwanza na Geita, unaofanyika leo Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii NSSF mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa mkuatno huo
Katibu wa JMAT ambaye pia ni Hakimu Mkazi mkoani Mwanza, Bittony Mwakisu (kulia) akiwa pamoja na Domician Mlashani, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo wilayani Sengerema na mjumbe wa Kamati tendaji JMAT (kushoto).
Picha ya pamoja
Viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.