RAIS DKT MAGUFULI AELEKEA ADDIS ABABA, ETHIOPIA, KWENYE MKUTANO WA 28 WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA

January 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Comoro nchini   Dk.Ahamada El Badaoui Mohamed  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa  Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan atika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

PICHA NA IKULU

MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA NJOMBE

MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA NJOMBE

January 28, 2017
agaooo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya wanawake wa Njombe kabla ya kuondoka kwenye Ikulu ndogo  baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo  Januari 28, 2017. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri.
agao 11
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri kwenye Ikulu ndogo ya Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo, Januari 28, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

January 28, 2017
SOUPO
  • MTU MMOJA JAMBAZI APIGWA RISASI WAKATI AKIJARIBU KUTOROKA POLISI WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA TARHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 00:30HRS USIKU KATIKA MTAA WA BWIRU KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA JAMBAZI ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA MAARUFU LA MUNGIKI, MWANAMUME, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 30 HADI 35, ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKIJARIBU KUTOROAKA POLISI BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA SILAHA AINA YA BASTOLA YENYE NAMBA ZA USAJILI TZCAR 97076 AMBAYO ALIIPORA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA  MWAKA 2013 MKOANI TABORA.
AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA YUPO KIJANA  ANAYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA MUNGIKI ANAYEMILIKI SILAHA, PIA ANAJIHUSISHA NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA HAPA JIJINI MWANZA NA KATIKA MIKOA YA JIRANI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI KUHUSIANA NA TAARIFA HIZO NA KUFANIKI KUMKAMATA MTUHIMIWA TAREHE 26.01.2017 MAENEO YA GREENVIEW KATA YA NYAMANORO WILAYANI ILEMELA. AIDHA MTUHUMIWA ALIPOHOJIWA NA ASKARI ALIKIRI KUWA NI KWEILI ANAMILIKI BUNDUKI AINA YA BASTOLA AMBAYO AMEIFICHA MAENEO YA SONGAMBELE KATIKA MLIMA WA KABOHORO KWENYE MAPANGO YA MAWE, MTUHUMIWA ALIWAONGOZA ASKARI  HADI ENEO ALIPOLIFICHA BUNDUKI HIYO NA KUIKUTA BUNDUKI AINA YA BASTOLA YENYE NAMBA ZA USAJILI TZCAR 97076 AMBAYO ALIKUWA AMEIFICHA KWENYE PANGO LA JIWE.
MTUHUMIWA ALIPOENDELEA KUHOJIWA NA ASKARI ALIDAI KUWA BUNDUKI HIYO ALIPEWA NA MTU MMOJA JINA TUNALIHIFADHI KWASABAU ZA KIUCHUNGUZI  ANAYEISHI MAENEO YA MEDICAL RESEARCH BWIRU, AMBAYE WALIKUWA WAKISHIRIKIANA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA UNYANG’ANYI  WA KUTUMIA SILAHA HAPA JIJINI MWANZA NA MIKOA YA JIRANI, AMBAPO  ALIKIRI KUWA AKISHIRIKIANA NA MWENZAKE HUYO WALIVAMIA MADUKA MAWILI YA MIHAMALA YA FEDHA (M-PESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY) KATIKA MAENEO YA KILIMAHEWA KWA MSUKA AMBAPO   WALIPORA VITU MBALIMBALI KWA KUTUMIA SILAHA HIYO, AMBAPO ILIFUNGULIWA KESI YENYE NAMBA MZN/IR/632/2017 YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
ASKARI WALIONGOZANA NA MTUHUMIWA HADI ENEO HILO LA MEDICA RESEACH AMBAPO ALIDAI KUWA MWENZAKE  ANAPATIKANA  ILI AWEZE KUKAMATWA. AIDHA WAKATI WAMEFIKA ENEO HILO GHAFLA MTUHUMIWA MUNGIKI ALIKURUPUKA AKIWA NA PINGU MKONONI NA KUANZA KUKIMBIA UPANDE WA PILI WA BARABARA AMBAKO KUNAMSITU MKUBWA WA MEDICAL RESEARCH KWA LENGO LA KUTOROKA, ASKARI WALIFYATUA RISASI KADHAA HEWANI WAKIMUAMURU ASIMAME LAKINI ALIKAIDI, NDIPO ASKARI WALIMFYATULIA RISASI ZA MIGUUNI, LAKINI NYINGINE KWA BAHATI MBAYA ZILIMPATA SEHEMU YA JUU YA KIUNO AMBAPO MTUHUMIWA ALIFARIKI DUNIA NJIANI WAKATI AKIKIMBIZWA HOSPITALI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI.
AIDHA UCHUNGUZI UMEFANYIKA NA KUBAINI KUWA SILAHA HIYO AINA YA BASTOLA ILIYOSAJILIWA NA NAMBA  TZCAR 97076, MMILIKI WAKE NI BWANA JULIAN THADEUS LYIMO MIAKA 40, MENEJA WA MAMLAKA YA TUMBAKU TABORA NA MKAZI WA NYASUBI WILAYA YA KAHAMA MKOA WA SHINYANGA, AMBAYE ANAMILIKI SILAHA HIYO TANGU MWAKA 2011. AIDHA SILAHA HIYO ILIPORWA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KATIKA BARABARA YA SIKONGE TABORA MWAKA 2013, NA KUFUNGULIWA KESI YENYE NAMBA TBR/RB/8345/2013.
KATIKA TUKIO HILO MAJAMBAZI WALIZUIA MAGARI KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO BARABARANI NA KUFANIKIWA KUPORA FEDHA NA VITU MBALIMBALI VYA ABIRIA AMBAPO BWANA JULIAN LYIMO AKIWA MMOJA WAPO ALIPORWA BUNDUKI YAKE AINA YA BASTOLA, KOMPYUTA MPAKATO AINA YA DELL, MIWANI YA MACHO PEA MBILI NA FEDHA KIASI CHA TSH 67,000/=.
ASKARI WANAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA NA MISAKO YA KUWATAFUTA WATU WENGINE WALIOKUWA WAKISHIRIKIANA NA MAREHEMU KATIKA KUFANYA UHALIFU HAPA JIJINI MWANZA NA MIKOA YA JIRANI, ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI WAHALIFU WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, LAKINI PIA ANAWATAKA WANANCHI WOTE WAWAKANYE WATOTO WAO WASIJIHUSISHE NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA NA UHALIFU MWINGINE, ILI KUFANYA MKOA WETU WA MWANZA UWE SALAMA NA TULIVU ILI KUWAVUTIA WAWEKEZAJI AMBAO WAKIWEKEZA WATALETA MAENDELEO YA KIJAMII NA KIUCHUMI.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

KUKOSEKANA UZIO SHULE YA MSINGI MCHANGANYIKO PONGWE KUNA WEZA KUSABABISHA HATARI KWA WANAFUNZI.

January 28, 2017
Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi akiangalia namna wanavyoandika wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi ya Mchanganyika Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake
 Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi wa kwanza kushoto akisikiliza kero za wanafunzi hao.
 Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Msingi Mchanganyiko ya Pongwe ya wanafuzi wasiosikia na wenye matatizo ya ngozi (Albino),Waziri Mfaume kulia akimuonyesha diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi maeneo yenye mapori yaliyozunguka shule hiyo ambayo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi hao wakati wa ziara ya diwani huyo
WATOTO wenye ulemavu wa ngozi na wasioona wanaosoma shule ya msingi ya mchanganyiko ya Pongwe iliyopo Jijini Tanga wapo hatarini kuvamiwa na watu waovu na kuwafanyia vitendo vya kikatili kutokana kukosa uzio na sehemu kubwa kuzungukwa na pori ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Shule hiyo ambayo inapokea watoto wenye matatizo hayo kutokana mikoa mbalimbali Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana uzio huku sehemu kubwa ikipakana na pori jambo ambalo linaweza kusababisha hatari kwa ustawi wao kielimu.

Hayo yalibainishwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Waziri Mfaume wakati wa ziara ya Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi aliyoifanya kuangalia changamoto ambazo zinaikabili na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Waziri alisema licha ya kufanya jitihada kubwa za kuanza ujenzi wa
uzio huo eneo la mbele ya shule hiyo lakini mpaka sasa hakuna msaada wowote ambao wamekuwa wakiupata ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linatishia usalama wa watoto hao.

Alisema awali changamoto hiyo ilikuwa eneo la mbele ya shule hiyo na kuona namna ya kulipatia ufumbuzi haraka ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuwavutia wadau kuweza kusaidia lakini suala hilo mpaka sasa limeshindwa kupatiwa tiba.

 “Awali tuliona tuanze kujenga ujenzi wa fensi mbele ya shule hii
lengo likiwa kuwavuta wadau wengine ili kutusaidia lakini tukashindwa kujenga eneo ambalo ni pori kubwa na hivyo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi “Alisema.

Aidha alisema licha ya jambo hilo lakini lingine ambalo limekuwa
kikwazo kwao kwenye suala la usalama ni walinzi ambao wanalinda shule hiyo ambao ni mgambo wanaotumia virungu  na mapango ambazo ni silaha ndogo kuweza kuwakabili wahalifu.

 “Ukiangalia kwenye shule hii tuna wanafunzi 87 ikiwa ni mchanganyiko wa walemavu wenye ualibinisimu,wasiosikia na wengine hawaoni hivyo ni hatari sana iwapo kutakuwa hakuna uzio na hawa wanatoka mikoa mbalimbali hapa”Alisema .

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uzio kwa sababu ipo kwenye mazingira magumu kwani imezungukwa na pori ambalo ni hatari kwao.

 “Hii changamoto  ni kubwa sana na hatari kwa usalama wa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo hivyo niwaombe wadau wa elimu,viongozi na serikali kuona namna ya kusaidia jambo hilo kwa maendeleo ya taalumu za watoto hao “Alisema.

Hata hivyo alisema pia suala la uhaba wa madarasa kwenye shule hiyo atalichukua na kulifikisha kwenye kikao cha baraza la madiwani ili waweze kuona namna ya kuyashughulikia.

Naye kwa upande wake,Mwenyekiti wa Mtaa wa Pongwe,Hemed Kileo alisema kukosekana kwa uzito kwenye shule hiyo ni jambo la hatari hivyo kuziomba mamlaka husika kuona namna ya kulishughulikia.

Alisema shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1948 ikiwa na darasa la kwanza mpaka la sita ambayo walikuwa wakisoma wakoloni kabla ya mwaka 1957 kubadilishwa matumizi na kuwa shule ya bweni  na baadae ikiwa ni ya mchanganyiko .

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO WA JESHI LA PILISI,NSATO MARIJANI AWAFARIJI ASKARI WALIOPOTEZA MALI ZAO KWA TUKIO LA MOTO MJINI MOSH

January 28, 2017
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari lililoungua moto huku akiongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa.
Jengo la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo..
Kamishna Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za askari hao.
Kamishna Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto.
Kamishna Marijani akita pole kwa PC  Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya jengo hilo.
Kamishna Marijani akimfariji  CPL,Simba baada ya kutembelea jengo hilo kujionea athari iliyotokana na moto huo.
Kamishna Marinaji akimpa pole SGT Hashim baada ya kupoteza vitu vyote vya ndani pamoja na mavazi kufuatia moto ulioteketeza seheumu ya juu ya jengo hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuongoza Kamishna Marijani kukagua maeneo mengine  ya jengo hilo ambalo linakumbwa na tukio la moto kwa mara ya pili sasa.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi ,Nsato Marijani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kutoa pole kwa asakri waliounguliwa vitu katika jengo hilo.
Waliovalia kiraia ni askari Polisi waliofikwa na janga la kuunguliwa moto vitu vya ndani pamoja na mavazi wakionekana wenye huzuni.
Afisa Mnadhimu daraja la kwanza wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani alipotembelea kambi ya polisi mjini Moshi.
Kamnada wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa juu ya tukio la moto katika jengo la makazi ya askari Polisi.
Baadhi ya wanandugu wa familia zilizounguliwa moto wakionekaa wenye huzuni.
Mkuu wa Shule ya Polisi,Kamandanti Matanga Mbushi akizungumza wakati wa kuzifariji familia za askari waliopoteza vitu vyao katika tukio la moto.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisni nchini ,IGP Ernest Mangu kwa askari waliopoteza vitu vyao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa katika makazi ya askari Polisi mjini Moshi.
Mmoja wa wageni waalikwa akizungumza wakati akitoa salamu za pole kwa jeshi la polisi. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

JESHI la Polisi nchini limetangaza kuwahamisha askari tisa wa vikosi mbalimbali vya jeshi hilo waliopoteza mali zao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa vya jengo la ghorofa mbili ambalo ni makazi ya askari.

Mbali na hatua hiyo jeshi hilo pia limetoa kiasi cha Sh Milioni tisa kwa familia za askari hao kwa ajili ya kuanza kununua vitu vidogo yakiwemo mavazi baada ya kutoambulia chochote wakati wa tukio hilo zikiwemo sare za jeshi hilo.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani ametoa kauli hiyo jana kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisi ,Inspekta Jenerali,Ernest Mangu wakati akizifariji familia za askari hao pamoja na kutembelea jengo lililoteketea kujionea athari za moto huo uliotokea usiku wa kuamkia juzi.

Akiwasilisha salamu za Pole kwa niaba ya IGP Mangu,Kamishna Marijani alisema jeshi la Polisi litaendelea kutoa msaada kwa askari hao hadi pale maisha yao yatakaporejea huku akivishukuru vikosi vya jeshi la zima moto vya uwanja wa ndege wa KIA,kiwanda cha sukari cha TPC na Halmashauri kwa kazi waliyofanya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa amemwelea kamishna Nsato kuwa thamani ya mali za askari zilizoteketea kwa moto imefikia sh Mil 93.9 huku akiomba wadau kujitokeza kusaidia familia hizo.

Tukio la moto katika jengo hilo lililopo jirani na ofisi za kikosi cha kutuliza ghasia lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 2:30 usiku ,ukianzia katika chumba kimojawapo cha ghorofa ya pili na kuenea katika vyumba vingine nane wakati huo umeme ukiwa umekatika.

Kufuatia moto huo familia tisa za askari hao zenye jumla ya watu 40, ambao 23 ni watu wazima na 17 ni watoto tayari zimepatiwa malazi ya muda katika chuo cha Polisi Moshi wakati taratibu nyingine za kuwasaidia zikiendelea.

Tayari jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limeunda timu ya wataalamu kutoka katika jeshi hilo wakisaidiana na wale wa kikosi cha zimamoto pamoja na shirika la umeme (TANESCO) kufanya uchunguzi wa matukio ya moto katika jengo hilo.

Mwisho.
 

SITAKI TENA KUSIKIA MSAMIATI “MRADI UKO CHINI YA KIWANGO”, RC NCHIMBI AAGIZA.

January 28, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi au “mama Nchimbi” kama anavyojulikana jana amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mkalama na kuagiza watendaji kusimamia miradi kwa umakini kwakuwa hataki kusikia mradi wowote uko chini ya kiwango.

Dkt. Nchimbi amesema msamiati chini ya kiwango hataki kuusikia kwakuwa umekua ukifanya watendaji kuwa wazembe na kuongeza kuwa hatua kali zitachukulkiwa kwa viongozi wote ambao hawatasimamia ipasavyo utekelezaji wa maelekezo hayo.

Ameongeza kuwa watendaji wamekuwa wakiilalamikia serikali na kuirudisha nyuma kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kupelekea wananchi kuona serikali haifanyi chochote wakati inaleta pesa nyingi za miradi mbalimbali ambapo jukumu la watumishi ni kusimamia miradi ili ifanye kazi ipasavyo.

Dkt. Nchimbi amesema viongozi wote kabla ya kusaini mikataba yoyote ya halmashauri wanapaswa kukiri thamani ya mali zao zinazohamishika na zisizohamishika ili kama mradi utatekelezwa chini ya kiwango, mali zao zitumike kufidia pesa ya serikali iliyopotea.

“Mradi wakati unajengwa Mkurugenzi, Mwenyekiti wa halmashauri na wataalam wanauangalia bila kusema chochote, ukikamilika ndio wanakuambia umejengwa chini ya kiwango, kuanzia sasa sitaki kusikia msamiati wa ‘chini ya kiwango’ na endapo ikitokea chini ya kiwango tutahakikisha fedha ya serikali inarudi”, amesema Dkt. Nchimbi.

Aidha katika kikao hicho na watumishi wote wa halmashauri hiyo amewaagiza wakuu wote wa shule za msingi na sekondari kuwaruhusu wanafunzi ambao hawana sare kuanza masomo huku utaratibu wa kuwafuatilia wazazi watimize majukumu yao ukiendelea.

“ Baada ya elimu kuanza kutolewa bure, changamoto nyingine iliyobakia kwa baadhi ya wazazi ni uwezo wa kuwashonea watoto wao sare za shule, sasa ninaagiza wakuu wa shule za sekondari na Msingi wote Wilayani hapa kuwaruhusu watoto hao waingine madarasani hata kama hawajavaa sare za shule ili wasikose haki yao ya msingi kwa sababu ya sare tu”, ameagiza Dkt. Nchimbi.

Awali kabla ya kuzungumza na watumishi Dkt. Nchimbi alifanya ziara katika mashamba ya wakulima ili kujionea na kushiriki na wananchi shughuli za kilimo hasa mashamba ya viazi katika kijiji cha Nkungi na mashamba ya mtama katika kijiji cha Ilunda wilayani humo.

Dkt. Nchimbi akiwa katika shamba la mkulima wa viazi lishe katika kijiji cha Nkungi alipanda viazi na kuhamasisha wananchi wengine walime mazao ambayo yanatumia maji kwa ufanisi kama vile viazi, mihogo, matama na uwele kutoka na mabadilike ya tabia nchini ili kujihakikishia uwepo wa chakula.

Amewataka watendaji hasa wa kada za kilimo na ufugaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea hasa kuandaa taarifa za makaratasi bali wawatembelee wakulima na wafugaji katika maeneo wanayofanya shughuli zao ili waweze kutoa ushauri kwa kupata picha halisi.“Sipendi kiongozi anayesema yupo karibu na wananchi kwa sababu hatuwezi kupima ukaribu uliopo hivyo ni vyema kuanzia sasa tuache kuwa karibu na badala yake tuwe pamoja nao”, amesema Dkt. Nchimbi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama katika ziara yake wilayani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Jakson Masaka akishiri kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima katika kijiji cha Nkungi Wilayani humo.

MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI WATOA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPTALI YA RUFAA YA MKOA WA KILIMANJARO,MAWENZI

January 28, 2017
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Maawenzi wakiwa  wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo
Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi ,Boniface Lyimo akizungumza mara baada ya kuwapokea Madiwani hao na kutoa maelekezo ya namna ya kutoa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,wakielekea katika wodi walimolazwa wagonjwa kwa ajili ya kutoa zawadi.
Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema na Diwani wa kata ya Kiusa,Stephen Ngasa akikabidhi zawadi ya sabuni ya unga kwa wagonjwa waliolazwa katika Hopstali ya Mawenzi.
Diwani wa kata ya Mawenzi,Hawa Mushi akitoa zawadi kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
Diwani wa kata Pasua ,Charles Mkalakala akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wagonjwa katika Hospitali hiyo.
Madiwani wakiongojea kuingia katika wodi nyingine kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wagonjwa katika hospitali hiyo.
Madiwani wakitoa zawadi katika wodi ya wanawake Hospitali ya Mawenzi
Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema,Stephen Ngasa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,awenzi mara baada ya kuhitimisha zoezi la kutoa zawadi kwa wagonjwa pamoja na kusafisha mazingira katika Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema,Stephen Ngasa akiagana na katibu wa Hosptali ya Mawenzi ,Boniface Lyimo mara baada ya kuhitimisha zoezi la kutoa zawadi na kusafisha mazingira ya hosptali hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.