January 26, 2014
 Mgombea wa Chadema Ndg. Hashim Issa Juma akiomba Kura kwa Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki. katika mkutano wake wa Kampeni.
 
 Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha Chadema Ndg. Hashim Issa Juma akijinadi kwa Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakati wa kampeni zake kuomba kura kwa Wananchi wa Jimbo hilo katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika viwanja vya kiembesamaki Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chadame Zanzibar Hassan Mussa Yussuf, akitowa Sera za Chama chake katika mkutano wa kumnadi Mgombea wao kuwania Jimbo la Kiembesamaki, katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya kiembesamaki Zanzibar.
January 26, 2014
 Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013.
 Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake tayari kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji Mkuu wan chi hiyo Jean –Michael Rasolonjatovo (kushoto) wakati wa sherehe za kumuapisha rais huyo zilizofanyika mjini Antananarivo.
 Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akizungumza na wananchi wa Madagascar  waliofurika ndani ya uwanja wa Antananarivo mara baada ya kuapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo mjini.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumuapisha rais mpya wa Madagascar akiwa kwenye jukwaa kuu pamoja na viongozi wengine wa nchi za Afrika waliohudhuria sherehe hizo mjini Antananarivo.Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano, Rais wa Zambia Ipikefunye Pohamba na aliyekuwa rais wa Madagascar Andry Raojolina.

SIMBA YAICHAPA RHINO RANGERS 1-0

January 26, 2014
 
 Ramadhani Singano 'Mess' (kulia), akishangilia bao pekee aliloifungia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam..
 Ramadhani Singano akishangilia kwa staili ya aina yake baada kuifungia Simba bao pekee.

 
 Ramadhani Singano akiipangua ngome ya Rhino Rangers ya Tabora.
January 26, 2014


MKUTANO WA CHADEMA ULIVYOFANYIKA JIJINI MBEYA


Silinde kuhutubia Mbeya

Mbunge wa Mbozi Mashariki, Davi Silinde (Chadema), akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe mjini Mbeya jana.
Slaa kuhutubia Mbeya 1
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akihutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe

MKUTANO WA UZINDUZI WA MAADHIMISHOYA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA KUZALIWA KWA CCM

January 26, 2014


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na vijana Chipukizi  alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa Uwakilishi  Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akivalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma   baada  ya kuvalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanaCCM waliohuduria katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,mara alipowasili katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimnadi na kumuombea kura kwa wanaCCM na Wananchi, Mgombea wa  CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM katika viwanja vya mpira Kiembesamaki.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo 
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,alipkuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa uwakilishi wa  CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
January 26, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO WA KANISA LA MTAKATIFU PETER.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kikristu wakati wa Ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter Oysterbay, leo asubuhi kwa ajili ya kushiriki katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa hilo. ambapo zaidi ya Sh. milioni 65 zilipatikana kati ya Sh. milioni 600, zinazohitajika hadi ifikapo mwezi Julai. Kati ya hizo Cash ni Sh. milioni 5 na zilizobakia zikiwa ni ahadi.
***************************************
Zaidi ya shilingi milioni 65 zimekusanywa katika harambee iliyoongozwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililoko jijini Dar es salaam.
Kati ya fedha hizo zilizokusanywa katika ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa jengo la ukumbi huo ilyoongozwa na Mhadhama Kadinali Polycap Pengo kiasi cha shilingi milioni 60.5 zilikuwa ni ahadi na  shilingi milioni 5 zikiwa ni fedha taslimu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais aliwahakikishia Watanzania kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi za kidini katika kudumisha amani na upendo ndani ya jamii bila ya kujali tofauti za aina yo yote ile.
Alisema kuwepo kwake katika hafla hiyo ni ishara ya uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi mbali mbali za dini  nchini.
“Sisi Watanzania tumefika hapa kutokana na uongozi thabiti wa waasisi wa Taifa letu. Hivyo, tunataka nchi ya watu wanaomwogopa Mungu, watu wanaopendana, watu wanaovumiliana na watu wanaotakiana mema katika shughuli zao.”
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Bibi Rose Rupia kamati yake inahitaji shilingi milioni 600 zaidi kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi wa jengo la ukumbi huo na kwamba tayari wameshatumia kiasi cha shilingi bilioni moja katika ujenzi huo.
Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa pia na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwadhama Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akisalimiana na Mwadhama Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
 Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akiongoza na na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya ibada hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, wakati wa harambee ya kuchangia ujnenzi wa Ukumbi huo iliyofanyika leo asubuhi.
 Picha ya pamoja......
 Akitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter, baada ya ibada maalum ya harambee ya kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika leo asubuhi, Jan 26, 2014. Kushoto ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe.
 
Chanzo Suffianimafoto.com