MCHECHU AONGOZA HAFLA YA KUCHANGIA VITABU 2500 KWA SHULE ZA SEKONDARI NA ZA MSINGI ILIYOANDALIWA NA TAASISI ISIYO YA KISERIKALI YA NKWAMIRA

October 11, 2014



 Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akihutubia wakati wa hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam  ya Shirika Lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Nkwamira Sustainable Life Trust
, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jana usiku Oktoba 10, 2014 jijini Dar es Salaam. 
NHC imechangia kiasi cha shilingi milioni 12, na imeahidi kujenga madarasa mawili katika shule ya msingi Saku iliyopo Mbagala. 
Azim Jamal ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc kampuni inayojishughulisha na kusaidia wadau  na makampuni kupata stahiki katika kazi zao,na ni mwandishi wa vitabu mbalimbali vilivyotafsiriwa katika lugha 10, akizungumza katika hafla hiyo jana.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Madini nchini, Richard Kasesela akizungumza wakati wa hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,  ya Shirika Lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Nkwamira Sustainable Life Trust
 Wadau waliofika katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo
Muongozaji wa sherehe hiyo maarufu kama MC Luvanda, Anthony Luvanda akiinua picha juu kuinadi kwenye hafla hiyo ya uchangiaji kwaajili ya kuwezesha watoto kupata vitabu vya kusoma.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari akifuatilia jambo katika hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Omari Mjenga kwenye hafla hiyo.
 Wadau waliofika katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo
 Wadau Abdul Njaidi na mwenzie wakifuatilia jambo katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Saku wakitoa ushuhuda wao wa namna wanavyopata shida kupata elimu katika shule yao hiyo ambapo walisema wengi wao wanakaa chini na vitabu na madarasa hayatoshi.
 Kikundi cha burudani cha Dar Choral Society wakitumbuiza muziki laini katika hafla hiyo jioni ya jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Kikundi cha burudani cha Dar Choral Society wakitumbuiza katika hafla hiyo jioni ya jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Kikundi cha burudani cha Dar Choral Society wakitumbuiza katika hafla hiyo jioni ya jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), William Genya, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari na Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu, Veronica Mtemi wakifuatilia hafla hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Nehemia Kyando Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla wakifuatilia hafla hiyo
Wadau waliofika katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo.
 Mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akipokea hundi ya Shilingi milioni saba iliyotolewa na Benki ya KCB jana jioni.
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akipokea hundi ya Shilingi milioni saba iliyotolewa na Benki ya KCB jana jioni.

KINANA,NAPE WASHIRIKI UCHUMAJI WA MAJANI YA CHAI MUFINDI

October 11, 2014
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia0 na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakichuma majani ya chai katika shamba la Unilver, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi katika Jimbo la Mufindi Kusini, mkoani Iringa leo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu (katikati) wakisaidia kuchuma majani ya chai katika shamba hilo la Unilve akiwa na viongozi wengine wa chama hicho 
 Kinana akijumuika na wananchi kucheza wimbo wa Ilani ya Chama ya Bendi ya CCM Mufindi, wakati wa mkutano huo.
 Kinana akisaidia kumwagilia maji miche ya miti alipokwenda kukagua bustani ya Vijana mjini, Kigamboni mjini Mafinga
 Mfuasi wa CCM, Keneth Mwangosi, akiwa mbele ya gari lake  alilolifanyia ukarabati na mbele yake kuandika jina la Kinana
 Kinana akikagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Nyololo, Kata ya Igowole
 Kinana akiwasalimia wananchi alipokuwasili kwenye mkutano huo.
 Sehemu ya umati wa watu katika mkutano huo ulihutubiwa na Kinana katika mji wa Nyololo, Mufindi.
 Wananchi wakishangilia kuonesha wanamkubali Kinana na Nape
 Ni furaha tele, iliyojaa nderemo na vifijo baada ya kumuana Kinana
 Wananchi wakiitikia CCM Oyeeeeeeee
 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa hadhara ambapo alisema kuwa kitendo cha Katibu iliyopendekezwa kupita katika Bunge Maalum la Katiba, ni kifo cha vyama vya upinzani.
 Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, akihutubia na kuelezea kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010.
 Vijana wa Green Guard wa CCM wakishangilia baada ya kunogewa na hotuba ya Kinana wakati wa mkutano huo wa hadhara.
 Bendi ya CCM Mufinndi, wakionesha umahiri wao wa kuimba wimbo wa Ilani ya  CCM mbele ya Kinana.
 Kinana akicheza na wananchi wimbo wa Ilani ya CCM baada ya mkutano kumalizika
 Nape na Katibu wa CCM, Mufindi, Mtaturu waiwa na furaha walipokuwa wakicheza wimbo huo
Kinana na Nape wakiangalia CD yenye nyimbo za bendi ya CCM

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC) CHAENDELEA KUIPINGA ADHABU YA KIFO

October 11, 2014


  Mkurugenzi Mtendaji  wa Kituo cha Sheria na Haki za 
Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba.
 Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio (kulia) akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Dawati la Katiba, Anna Henga. 
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo Duniani. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Dawati la Katiba wa LHRC, Anna Henga na Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urrio.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

ADHA YA UKEKETAJI TANZANIA KUJADILIWA NA WABUNGE UINGEREZA

October 11, 2014


                                               Na Freddy Macha

Jumatano ijayo tarehe 15 Oktoba, 2014...kundi la kina mama watatu akiwemo Mtanzania litashiriki jopo la ukeketaji na Wabunge, London, Uingereza.

Mtanzania, Rhobi Samwelly, mama wa watoto wanne, ni mzawa wa Butiama, Mara. Wenzake ni Comfort Momoh, toka Nigeria, anayetibu wanawake waliokeketwa hospitali mbili za Guy’s na St Thomas, London na Ann-Marie Wilson mkurugenzi wa “28 Too Many.” Shirika hili lenye tovuti yenye ni maktaba kubwa yenye habari, picha, utafiti na uchunguzi wa ukeketaji duniani.
Bango linalotumika kuchangia makutano na hafla mbalimbali za fedha za ujenzi wa nyumba ya hifadhi ya wasichana Mugumu, Mara

Mwaka1997 Comfort Momoh alianzisha msururu wa shughuli za kuwasaidia akina mama waliokeketwa likiwemo shirika la African Well Women’s Clinic. Bi Momoh mwenye shahada ya uzamili (MA) ni mshauri wa shirika la Afya duniani (WHO) kuhusu adha ya ukeketaji.

Mtanzania Rhobi na Ann-Marie walikuwa baadhi ya wazungumzaji kwenye hafla iliyofanywa Alhamisi na Jumamosi iliyopita kuchanga fedha za kujenga nyumba ya hifadhi kwa wasichana wanaokimbia ukeketaji, Mugumu, Mara.

Hafla hiyo iliendeshwa na shirika la urafiki baina ya Tanzania na Uingereza (British Tanzania Society) na Shirika la Misaada ya Kimaendeleo Tanzania (Tanzania Development Trust Fund). Fedha zilizokusanywa zinaendelea kusaidia ujenzi wa nyumba ya kuwahifadhi wasichana wanaokimbia ukeketaji jimbo la Mara.
Mwanasaikolojia, mtafiti na mtetezi wa haki za waliokeketwa, Anne-Marie Wilson(kulia kabisa) akijadiliana na wanachama wengine wa Jumuiya ya Uingereza na Tanzania (BTs), ukumbi wa Central Hall, Westminster baada ya hotuba yake. Alisisitiza kila sekunde kumi , msichana fulani hukeketwa ulimwenguni. Kati kati ni mweka hazina wa BTs, Bw. Robert Gibson na Jonathan Cape, mwendeshaji wa hafla.

Nilimuuliza Dada Rhobi je hawa wasichana hawatadhurika? Je, wazazi husika hawatawafuata? Akajibu kwa sasa kuna vyombo vingi husika kikiwepo polisi, serikali na kanisa la Anglican ambalo yeye ni mjumbe pia.

Rhobi ni mratibu wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo ya akina mama vijiji vya Mara. Mbali na ukeketaji anaangalia pia maslahi ya unyanyasaji wa kijinsia. Baada ya Bi Neema Wambura kupigwa na mumewe majuma kadhaa yaliyopita, Bi Rhobi alikuwa mmoja wa waliomhudumia kwa kuhakikisha anapata matibabu. Neema alimwagiwa maji moto na kuunguzwa kifuani na mkononi.

MAPENDEKEZO YAWASILISHWA KWA UONGOZI WA BENKI YA DUNIA

October 11, 2014

Ujumbe kutoka Tanzania ukimsikiliza kwa makini  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose Mkurugenzi Mtendaji mpya anayeachiwa kiti.

KATIKA mkutano muhimu uliofanyika jioni hii hapa mjini Washington DC. Kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile na Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika pamoja na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo ulimpatia nafasi nzuri sana Dr. Likwelile kuweza kueleza mambo muhimu ambayo Benki ya Dunia ingepaswa kuyafahamu. 
Katika mawasilisho yake katibu Mkuu huyo aliwaeleza viongozi wa Benki ya Dunia kuwa anashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao ameupata kutoka Benki ya Dunia na kusema kuwa hii imeisaidia sana Tanzania katika kupiga hatua kiuchumi. Akiendelea kuzungumza Dr. Likwelile alisema kuwa pamoja na kufanikiwa katika ushirikiano huo kumekuwa na tatizo ambalo lina sababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa Bajeti. Hili amelieleza kuwa linatokana na masharti ya wafadhili kutaka kwanza mambo yanayohusu IPTL kupatiwa ufumbuzi , kitu ambacho hakikuweko kwenye makubaliano. “ IPTL haina uhusiano na makubaliano ya awali suala hili limeingia katikati hii inaathiri utekelezaji wa kibajeti.”alisema. Aidha aliendela kueleza kuwa sera ya Benki ya Dunia inadai kuwa kabila la Kimasai limetengwa na hivyo kutaka baadhi ya miradi isiende sehemu nyingine zaidi ya umasaini, hii nayo ni changamoto nyingine”. Katika mazungumzo hayo ilionekana kweli kuwa kwa kuchelewesha kutoa fedha kwa ajili ya miradi kunachangia sana kurudisha nyuma maendeleo. 
Kwa mapendekezo haya mawili makubwa kama yatafikishwa kwenye ngazi ya juu na yakafanyiwa kazi basi nchi yetu itapiga hatua kama ilivyojipangia. Wakurugenzi hao waliyapokea mapendekezo hayo kwa mikono miwili na wakaahidi kuyafikisha na kuyafanyia kazi.
Hali ya hewa mjini hapa ni ya baridi na manyunyu ya hapa na pale.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha
Washington D.C
10/10/2014
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakiwaangalia kwa mshangao wakurugenzi hao wawili walipokuwa wakiingia hawapo kwenye picha.

PSPF YATOA MSAADA WA KOMPYUTA 12 KWA VYUO VIWILI BAGAMOYO

October 11, 2014


 Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani kushoto Akimkabidhi Msaada wa Kompyuta Mkuu wa Chuo Kikuu teule cha Marian Father Luke Mbefo  ambapo Kompyuta hizo zitatumika katika Kuhifadhi Nyaraka mbalimbali za Maktaba
 
 Mkuu wa Chuo Kikuu teule cha Marian Father Luke Mbefo  kulia akimshukuru Afisa Mahusiano wa PSPF Bi. Coleta Mnyamani kwa msaada huo
 Mwakirishi wa Shirika la Roho Mtakatifu Father Nicetas Kyara akitoa neno la Shukurani Baada ya kukabidhiwa msaada wa Kompyuta Mbili za kisasa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF
 Afisa Mahusiano wa PSPF Bi. Coleta Mnyamani akizungumza neno Baada ya kukabidhi Msaada huo
Afisa wa Fedha kutoka PSPF Bwana Samwel Haule Akizungumza Jambo wakati wa Makabidhiano wa Kompyuta hizo katika Chuo Kikuu teule cha Marian
 Mkuu wa Chuo teule cha Marian Father Luke Mbefo wakiteta Jambo na Afisa Mahusiano wa Pspf Bi Coleta Haule Baada ya Kukabidhi Msaada huo
 Picha ya Pamoja ya Viongozi wa PSPF na Chuo  Kikuu teule cha Marian
Kulia ni Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka akimkabidhi Kompyuta 10 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt. Ally S. Mcharazo kwa niaba ya chuo hicho
Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka  akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu pamoja na wagani waalikwa wakati wa kukabidhi msaada huo wa kompyuta 10 za kisasa
Rais wa Chuo cha Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu Daudi Joho akitoa neno la Asante Baadhi ya Kukabidhiwa Msaada huo 
Mbele ni Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt. Ally S. Mcharazo  akitoa neno la Shukurani
 Baadhi ya wanafunzi wakisoma Vipeperushi vya PSPF
Wanafunzi wakiwa wanafuatilia kwa makini
Kila mtu anachukua Kumbukumbu