SEMA NA TANGA WAKOSHWA NA UWEKEZAJI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA-BOMBO WAHAIDI KUWA MABALOZI
Kundi la Sema na Tanga leo wamefanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo huku wakifurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji na kuimarisha huduma za Afya hapa nchini na kuhaidi kuwa mabalozi wa kuisemea vizuri.
Wametembelea na wamejionea uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kitengo cha dharura (EMD), kitengo cha uangalizi maalumu (ICU), Kitendo cha radiolojia (CT-scan), Kitengo cha uangalizi maalumu kwa watoto wachanga (NICU), Wodi ya upasuaji, Kitengo cha kusafisha figo (Dialysis Unit)
Akizungumza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Japhet Simeo alisema kwamba kundi hilo ambalo ni wadau wa maendeleo walialikwa ili kuweza kuona huduma nzuri ambazo zinatolewa katika Hospitali hiyo na wamethibitisha kuwa uwekezaji ni mkubwa sana na wengi wao walikuwa na picha tofauti na waliyokuwa nayo awali na hawakuamini kama Hospitali hiyo ingeweza kuwa na vifaa kama hivyo na watu wanatibiwa na kupona.
“Ambao waliokuwa na hisia za zamani kwa sasa zitafutika maana wengine wanaamini yale mambo ya miaka 10 iliyopita bado, kwa hiyo Sema na Tanga wanaenda kufuta hayo mambo kwenye fikra za wananchi na tunaamini mtakuwa mabalozi wazuri wa kulisemea hili”Alisema
Hata hivyo alisema hivi sasa wanaendelea kuboresha huduma huku akiishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilivyosimamia kuhakikisha rasimali zinazoletwa zinasimamiwa kikamilifu akianza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba na Katibu Tawala Pili Mnyema namna wanavyompa ushirikiano mkubwa na hivyo kufanya kazi kwa kujiamini
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Kundi la Sema na Tanga alisema wana haja ya kuja kukuunga mkono kama wadau wa maendeleo kutembelea kutokana kujionea maboresho ya huduma yaliyosaidia kuondoa makelele yaliyokuwa yakisikika.
Alisema wametembelea wameona maboresho makubwa ,vifaa mbalimbali, nyenzo nzuri za kisasa.“Tuwaheshimu madaktari na wauguzi hapa nchini na tuache kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalamu maana tutakuwa tunawavunja moyo kama kuna mtu atawahujumu sisi tupo tayari kuwasemea na kusimamia na nyie”Alisema
“Tunamshukuru Waziri Ummy kwa kuteletea Mganga Mfawidhi Mpya Dkt Frank Shega na zile kelele zilizokuwepo kwa sasa hazipo zimeondoka ameonyesha waledi mkubwa, tutakutetea kwa kazi yako nzuri unayoifanya bila kupepesa macho”Alisema
QATAR CHARITY YATOA MSAADA TANI 90 KWA WANANCHI WA HANANG
Ubalozi wa Qatar Tanzania kwa kushirikiana na Tasisi ya Qatar Charity, kwa niaba ya Serikali ya Qatar, imewasilisha misaada muhimu ya kibinadamu kwa waathirika wa Maporomoko ya Udongo yaliyotokea Hanang mkoani Manyara.
Shehena ya misaada hiyo iliyotolewa leo tarehe 18 Februari 2024 kwa kutumia ndege mbili za mizigo kutoka Qatar inalenga kugusa maisha ya wananchi wa Hanang walioathirika na maafa hayo ambayo madhara yake yalikuwa makubwa.
Serikali ya Qatar imetoa kwa ukarimu misaada hiyo ya kibinadamu inayojumuisha chakula kikavu katika vifungashio 1,440 (Dry food basket), chakula kilicho tayari kuliwa katika vifungashio 3,024 (Ready to Eat canned food) na vifaa vya usafi wa wanawake jumla 4,200 (women’s dignity kit) na hivyo kufanya jumla ya tani 90 za shehena.
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amesema kuwa Serikali imepokea kwa moyo wa upendo misaada hiyo itakayoleta faraja kwa Waathirika na kuahidi kufikishwa kwa Walengwa kama ilivyokusudiwa.
Vilevile Mhe. Nderiananga ameeleza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau wote ikiwemo wananchi, sekta binafsi, asasi za kiraia na kidini, mashirika ya kimataifa na umoja wa mataifa kwa ushiriki wao katika kusaidia wananchi walioathirika na maporomoko ya tope katika wilaya ya Hanang'
Akipokea Misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Queen Cuthbert Sendiga ameishukuru Serikali ya Qatar kupitia Qatar Charity kwa misaada hiyo ya kibinadamu ambayo itakwenda kuwasaidia wananchi wa Hanang kurejea kwenye hali yao ya Kawaida.
Aidha, Mhe Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kupatikana kwa Misaada hiyo ni matokeo ya mahusiano mazuri ya nchi ya Tanzania na nchi za jirani ambayo yameimarishwa na serikali ya awamu ya sita Chini Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ndege ya mizigo iliyosheheni misaada hiyoMkuu wa Mkoa wa Manyara akishuka kwenye ndege hiyo mara baada ya kufanya makabidhiano ya msaada.
Viongozi waliohudhuria hafla hiyo fupi iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa KIA.