Msanii kutoka (NTT) amwaga mistari yake kwa uchungu!

August 23, 2017
Msanii wa Muziki wa Bongo Flava kutoka New Talents Tanzania (NTT)  Helton Dickson akiwa katika harakati za kutafuta njia ya kutokea kupitia Muziki, amefunguka na kumwaga Mistari yake huku akiwa na hisia kali kwenye mashahiri yake.

MWENYEKITI WA BODI IKUNGI SEKONDARI AMSHUKURU DC IKUNGI

August 23, 2017
BMG Habari
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu ameendelea kupokea pongezi baada ya kuanzisha ligi soka ya "Ikungi Elimu Cup 2017" ili kuhamasisha wananchi wa wadau mbalimbali ili kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu wilayani humo.

Kwenye uzinduzi wa ligi hiyo uliofanyika jumamosi Agosti 19,2017 uwanja wa shule ya sekondari Ikungi, Mhe.Mtaturu alikabidhi mifuko 100 ya simenti na kuungwa mkono na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali waliochangia mifuko 194 na hivyo kusaidia upatikanaji wa mifuko 294 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ikungi ambao ulikwama tangu mwaka 2009.


Siku hiyo pia ulifanyika uzinduzi wa zoezi la kufyatua matofali ambapo Kata zote wilayani Ikungi zimedhamiria kufyatua matofali 10,000 kila Kata ili kusaidia ujenzi wa madarasa, nyumba za waalimu, maabara pamoja na vyoo.
Tazama video hapo chini

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu (wa pili kushoto) akikabidhi mifuko 100 ya simenti ya kwa ajili ya ujenzi wa maabara shule ya sekondari Ikungi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu akishiriki zoezi la uzinduzi wa ufyatuaji matofali kwenye Kata zote wilayani Ikungi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, maabara, vyoo na nyumba za waalimu ambapo kila Kata itaanza kwa kufyatua matofali elfu kumi
Mgeni Rasmi, Katibu Tawala mkoani Singida, Dkt.Angeline Lutambi akizindua zoezi la ufyatuaji matofali wilayani Ikungi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dkt.Rehema Nchimbi.
Mgeni Rasmi, Katibu Tawala mkoani Singida, Dkt.Angeline Lutambi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu (kulia), wakisogeza tofali wakati wa uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji matofali wilayani Ikungi

KODI YA PANGO LA ARDHI SASA KIDIGITALI

August 23, 2017

1.MtaalamuwamfumowaGePG (Government electronic Payment Gateway)kutokaWizarayafedhaakielezeafaidazamfumokwawatumiajipamojanajinsiyakuutumiakatikakutoahuduma bora.

Mafunzojuuyamatumiziyamfumowa Ge PG yakitolewa kwa maofisa wa ofisi zaArdhi Nyandaza Juu Kusini
   Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi pamoja na maofisa kutoka ofisiza Ardhi Nyanda zaJuu Kusini wakifuatilia mafunzo kwa umakini
MtaalamukutokaWizarayaArdhi (aliyesimama nyuma)akitoa msaada jinsi ya kutumia mfumo kwa maofisa wa ofisi za Ardhi Nyanda zaJuuKusini
 
1.      MtaalamukutokaWizarayaFedhaakioneshamfanowafomuzabenkiya NMB ambazo mwananchi atapaswa kujaza akienda kulipia kodi ya pango la Ardhi katika benki hiyo.

NA: ELIAFILE SOLLA.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekusudia kuboresha huduma zake pamoja kuzisogeza karibu zaidi na wananchi ambao ndio wateja wakubwa wa Sekta hiyo. Hii ni katika kuboresha utoaji huduma na kuongeza ufanisi wa huduma za Ardhi.

Katika kuhakikisha hili linafanikiwa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaanzisha mifumo ambayo itakuwa inatumika kama njia rahisi ya utoaji huduma kwa wananchi. Mifumo yote hiyo ni kwa lengo la kuboresha huduma, kurahisisha huduma na pia kuondoa urasimu ambao ungeweza kujitokeza katika utoaji wa huduma kwa mwananchi. 

Mfumo wa GePG (Government electronic Payment Gateway) ni mfumo wa Serikali ambao umetengenezwa kwa lengo la kukusanya na kusimamia mapato ya Serikali. Mfumo huu pia utakuwa unatumiwa na Wizara kuu za Serikali, Taasisi za kifedha, Makampuni ya simu, Serikali za mitaa na Idara zote za Serikali ambazo zina vyanzo vya mapato. 

Malipo yote yatakuwa yanalipwa kwa kutumia namba maalumu ya malipo inayojulikana kama “control number” ambayo itamuwezesha mwananchi kulipia katika benki za NMB, CRDB au kwenye Mpesa na Tigo pesa mahali popote.
Mwananchi anaweza kupata makadirio yake ya kodi ya pango la Ardhi kwa kutumia mfumo huu wa GePG. Hii ndiyo maana halisi ya kusema sasa huduma za sekta ya Ardhi zinaboreshwa kwa kuondoa usumbufu wa kutembelea vituo vya makusanyo.

Njia mojawapo ya kupata makadirio ni kwa kutumia tovuti ya Wizara ya Ardhi (www.ardhi.go.tz).  Utachagua ‘kadiria kodi ya Ardhi’ na kisha utafuata maelekezo ya namna ya kuingiza taarifa za kiwanja chako. Baada ya kuingiza taarifa sahihi utabonyeza kitufe cha kadiria na hapo utapata taarifa za deni la kodi ya pango la ardhi pamoja na namba ya kulipia inayoanzia 99117…..

Pia unaweza kupata makadirio ya kodi ya pango la ardhi kupitia simu ya mkononi kwa kuingiza menyu kuu ya taifa ambayo ni *152*00# , kisha unachagua namba 4 malipo ya Serikali. Baada ya hapo utachagua namba 2 kadiria kodi ya kiwanja ambapo, utachagua nmba 1 kwa viwanja vya Dar es Salaam au namba 2 kwa viwanja vya mikoa mingine. 

Utachagua 1 kama unajua namba ya kiwanja au 2 kama unajua Lot ID na hapo hapo utapokea ujumbe wa malipo ukiwa na kumbukumbu namba inayoanzia na namba 991177….. Ukishapokea huo ujumbe utakuwa na uwezo wa kulipia katika beki za CRDB, NMB na kwa Mpesa au Tigo pesa. 

Malipo yoyote yakifanyika kupitia simu ya mkoni, mwananchi atapokea uthibitishpo wa malipo ambao ni risiti namba. Nakala ngumu ya risiti (hard copy) inapatikana katika kituo chochote cha makusanyo, mwananchi atapaswa kwenda na uthibitisho wake wa malipo tuu ili kupatiwa nakala ngumu ya stakabadhi.