MHE MWANJELWA AWAAGIZA WAFANYABIASHARA WA MBOLEA NCHINI KUACHA HARAKA KUUZA MBOLEA KWA ZAIDI YA BEI ELEKEZI

November 22, 2017
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza kwa makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi, Jana Novemba 21, 2017. Picha Zote Na Mathias CanalNaibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza kwa makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi, Jana Novemba 21, 2017. Makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini wakifatilia hotuba ya Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi, Jana Novemba 21, 2017. Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia mada mbalimbali kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi Mara baada ya kufungua Mkutano wa Kwanza kwa Makatibu Tawala na washauri wa Kilimo wa Mikoa ya nyanda za juu kusini, Jana Novemba 21, 2017.Makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini wakifatilia hotuba ya Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi, Jana Novemba 21, 2017. 
Na Mathias Canal, Mbeya
Makatibu tawala kote nchini wametakiwa kutafiti na kubaini wafanyabiashara wadogo wa mbolea wanaokiuka bei elekezi kutokana na wafanyabiashara wakubwa kuwauzia wafanyabiashara hao wadogo kwa bei elekezi ya rejereja badala ya bei ya jumla.
Mwito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza kati ya mikutano saba (7) katika Kanda saba (7) za kilimo nchini inayotegemewa kufanyika ambao ni muhimu kwa makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini wa kuelimishana kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi.
Mhe Naibu Waziri wa Kilimo aliwasihi Makatibu Tawala hao wa Mikoa na wataalamu wa kilimo kuhakikisha kwamba wanasimamia bei elekezi ya mbolea, Wanatoa Elimu kwa Wakulima ili wanunue mbolea bora na pia kuimarisha vikundi vya wakulima ili waweze kutumia nguvu ya umoja katika kuboresha kilimo kwa ajili ya utoshelevu wa mahitaji ya kaya zao na kuuza ziada hapa nchini na nchi za nje.
Alisema kuwa wafanyabiashara licha ya kufahamu kuwa wanatakiwa kugawana faida na wauzaji wa rejareja lakini bado wanakiuka taratibu za kisheria hivyo aliwaagiza kuacha tabia hiyo ili mawakala wauze kwa rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao.
Alisema Katika Sekta ya Kilimo mbolea ni moja ya pembejeo zinazohitaji ushirikiano mkubwa kutokana na ukweli kwamba inahitajika kwa wingi na ina gharama kubwa, inahitaji utaalamu katika matumizi yake na kwamba ni bidhaa inayoharibika kwa haraka endapo viwango vya utunzaji wake havizingatiwi.
Mhe Mwanjelwa aliwaagiza wakaguzi wote wa mbolea nchini kufuatilia na kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara wa mbolea ana leseni ya kufanya biashara ya mbolea ambayo itatolewa bure na TFRA na pia wahakikishe kwamba wote wamepata mafunzo haraka iwezekanavyo.
“Mbolea ni moja ya vichocheo vikubwa sana katika suala hili na hivyo, mwisho wa mkutano huu tunategemea kupata taarifa ya mikakati ya namna Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zitakavyosimamia ubora na bei elekezi ya mbolea ili Mkulima aweze kuipata na kuitumia kwa lengo linalokusudiwa” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Naibu Waziri huyo alisema kuwa Wizara ya kilimo ilitunga Kanuni ya Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (Fertilizer Bulk Procurement Regulations) na kuzitangaza kwenye Gazeti la Serikali kupitia tangazo G.N. 49/2017. Pamoja na kuunda kanuni hizo, Wizara ya kilimo  ilirekebisha Kanuni ya Mbolea ya mwaka 2011 kwa Kanuni zilizotangazwa katika Gazeti la Serikali kwa tangazo G.N. Na. 50/2017 ili kuipa nguvu TFRA kukokotoa, kutangaza na kusimamia bei elekezi ya mbolea.
Aliwaagiza pia wafanyabiashara wanaotunza mbolea bila kuzingatia viwango vilivyowekwa na TFRA kuacha haraka tabia hiyo kwani kwani wanasababisha mbolea kumfikia mkulima ikiwa imepungua ubora au kuharibika kabisa na hivyo kumfanya mkulima asipate tija inayotokana na matumizi ya mbolea.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amewataka wataalamu hao Kutenda haki katika uwajibikaji wao, Kufanya kazi kwa weledi, uaminifu, uwajibikaji uliotukuka, na nidhamu ya hali ya juu.
Aliongeza kuwa kwa yeyote atakaye kwenda kinyume na matakwa ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli itamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. JAPHET HASUNGA AAGIZA KUUNDWA KWA CHOMBO CHA KUDHIBITI UBORA WA MAZAO YA MISITU NCHINI

November 22, 2017


Na Hamza Temba – WMU
..........................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kubuni utaratibu mpya ikiwemo kuanzishwa kwa chombo kitakachosimamia upangaji wa madaraja ya ubora wa mbao zinazozalishwa hapa nchini ziweze kukidhi viwango vya mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo jana kwenye kikao cha majumuisho na watumishi wa Shamba la Miti la Serikali la Kiwira ambalo linasimamiwa na wakala huyo wakati anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

“Kuna changamoto kubwa kwenye soko la mbao, kwa kiwango kikubwa mbao zetu nyingi tunaziuza hapa nchini, Lazima tufike mahali hizi mbao tuwe tunaziexport (uza nje) kwa kiwango kikubwa. Lakini ili tufikie malengo hayo mbao zetu lazima ziwe kwenye kiwango kinachokubaliwa.

“Mbao zinazokuwepo kwenye soko letu la ndani huwezi kuzitenganisha kwamba hizi ni za TFS au za mwananchi wa kawaida, nyingine zina ubora nyingine hazina, agizo langu kwenu kaeni chini kama watendaji tuje na utaratibu utakaotuwezesha kuzipanga kwenye madaraja, daraja la kwanza, la pili, la tatu au la nne ili mnunuzi ajue ananunua mbao ya ubora wa aina gani,” alisema Hasunga.

Alisema amepata taarifa kuwa baadhi ya wananchi wanavuna miti ambayo haijakomaa jambo ambalo linaathiri ubora wa mbao kwenye soko kwa kutokidhi mahitaji ya wateja, hivyo akaagiza Wakala huyo kubuni mbinu mpya za kuwalinda wateja ikiwemo kuanzishwa kwa chombo maalum cha udhibiti wa ubora wake.

"Kwa maeneo mengine tuna TBS, kwenye chakuka tuna TFDA, kwenye mbao je? Nani anaregulate?(dhibiti), ni lazima tufike mahali tuwe na mdhibiti atakayetusaidia kuhakikisha kwamba ubora unakuwepo,” alisema Hasunga.

Aidha alitoa wito kwa taasisi hiyo kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuvuna miti ikiwa imeshakomaa ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa miche ya miti na kuhamasisha wananchi wapande miti zaidi kwa faida yao na taifa kwa ujumla.

Akizungumzia nidhamu kwenye Utumishi wa Umma, Naibu Waziri Hasunga alisema Serikali ya awamu ya tano haitomvumilia mtumishi yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa, uzembe au uvivu kwenye kutekeleza majukumu ya Serikali kwa kua sifa hizo ni chanzo kimojawapo kikubwa cha umasikini nchini.

Kwa upande wa kampeni ya upandaji miti kitaifa, alisema Serikali itafuatilia nchi nzima kuona utekelezaji wa agizo hilo ambalo linaitaka kila Wilaya kupanda miti milioni moja na laki tano kwa mwaka ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha miti mingi zaidi inapandwa kwa kuwashirikisha zaidi wananchi.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Zawadi Mbwambo alisema taasisi hiyo imewahi kupokea malalamiko juu ya ubora hafifu wa baadhi ya mbao zinazopatikana kwenye soko ambazo baadhi ya wananchi hutumia jina la Shamba la Miti Sao Hill kuziuza na hivyo kuharibu sifa ya shamba hilo.

Alisema maagizo yote aliyoyatoa Naibu Waziri Hasunga yatafanyiwa kazi kupitia vikao halali vya kiutendaji vya taasisi hiyo ikiwemo vile vya kuandaa mikakati ya utekelezaji wa majukumu yake ya uhifadhi.

Awali Meneja wa Shamba la Miti Kiwira, William Dafa akiwasilisha taarifa yake kwa Naibu Waziri Hasunga, alisema shamba hilo ambalo lilianzishwa mwaka 1964 likiwa na hekta 2,713 limekuwa na maendeleo mazuri ambapo mwaka 2016/2017 lilivuka malengo ya makusanyo ya mapato ya Serikali kutoka bilioni 1.3 hadi bilioni 1.7.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja (wa pili kushoto) alipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo akiongozana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (wa pili kulia) kwa ajili ya kujitambulisha wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Meneja wa Shamba la Miti Kiwira, William Dafa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika shamba hilo jana katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Meneja wa Shamba la Miti Kiwira, William Dafa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika shamba hilo jana katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Zawadi Mbwambo (kushoto) wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi kwenye Shamba la Miti Kiwira lililopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya jana.

STANDARD CHARTERED BANK MWENYEJI WA ‘ONE BELT- ONE ROAD’ (OBOR) AFRICA-CHINA ROADSHOW

November 22, 2017
   Mgeni Rasmi Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akihutubia waalikwa mbalimbali kuhusu fursa zinazopatikana katika uwekezaji. (OBOR Initiative) katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Stanchart bank jana,
    Sanjay Rughani akizungumza na wageni waalikwa katika hafla fupi ya chakula cha jioni ambayo Standard Chartered Bank iliwaandalia wateja wake ambao ni wenyeji kutoka China.
   Bw. Sun Chengfeng, Mkuu wa kitengo cha uchumi na biashara ambaye ni mwakilishi wa China nchini Tanzania akizungumza na waalikwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam
   Mgeni rasmi Mh. Charles Mwijage Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji akibadilishana mawazo na Bw, Chengfeng , Mkuu wa kitengo cha uchumi na biashara ambaye ni mwakilishi wa China nchini Tanzania katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na standard charterd bank
  Wawakilishi kutoka standard chartered bank china, pamoja na afisa mtendaji mkuu wa standard chartered bank Tanzania wakimsikiliza kwa makini Mh. Waziri Mwijage.
     Wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi,Bw Sanjay Rughani, Bw.Sun Chengfeng na wawakilishi mbalimbali katika kitengo cha uchumi na biashara wanaoiwakilisha China nchini Tanzania

  Waalikwa mbalimbali wakimsikiliza bi. Maggie Li alipokuwa akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni ambayo standard chartered iliwaandalia wateja wake wenyeji kutoka nchini China
 Afisa mtendaji mkuu wa benki ya Standard Chartered Tanzania Bw. Sanjay Rughani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu OBOR initiative katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency
  Afisa mtendaji mkuu wa Standard Chartered Bank Tanzania Bw. Sanjay Rughani (kushoto), Bi. Maggie Li Mkuu wa kitengo cha biashara na mauzo katika benki ya Standard chartered China(katikati), pamoja na Bw. Cleophas Ruhumbika ambae ni mwakilishi wa katibu mkuu wa viwanda na uwekezaji (kulia). Wakizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika jana.


  Vijana kutoka kundi la Tanzania House of Talent (THT) wakitoa burudani kwa wageni na waalikwa wa standard chartered bank katika hafla iliyoandaliwa katika hoteli ya Hyatt Regency.
  Burudani kutoka kundi la THT ikiendelea