ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI MHE.INJINIA MANYANYA MKOANI TANGA

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI MHE.INJINIA MANYANYA MKOANI TANGA

February 15, 2018

1
Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya akikagua maabara ya Vipimo vya sampuli ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Kiwanda cha Tanga Fresh.
2
Magari maalumu ya kusafirishia bidhaa za kiwanda cha Tanga Fresh katika mikoa mbalimbali,
3
Muonekano wa Kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Mkoani Tanga.
5
Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya akizungumza na ndugu Amour Alli meneja wa kampuni ya GBP iliyopo mkoani Tanga.
6
Meneja wa Kampuni ya Mafuta ya GBP ndugu Amour Alli akimuonesha Mhe. Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya sehemu ya upanuzi wa bohari hiyo ya mafuta na jinsi itakavyochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
7
Ziara ya Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya kutembelea kampuni ya GBP inayojihusisha na usambazaji wa mafuta, Mhe. Waziri ataendelea na Ziara yake mkoani Tanga kukagua Viwanda vilivyobinafsishwa kuona utendaji wake na kutoa maagizo ya kuanza uzalishaji mara moja.
8
Ziara ya Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya alipotembelea kampuni ya usambazaji wa mafuta ya GBP iliyopo Mkoani Tanga.
9
Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Viwanda vilivyobinafsishwa mkoani Tanga leo tarehe 15/2/2018.
10
Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya akiwa katika kiwanda cha saruji cha Kilimanjaro kilichopo mkoani Tanga, lengo la ziara hii ni kuona uzalishaji wa Viwanda mbalimbali mkoani Tanga na pia kujua changamoto na kuzifanyia kazi.

WAFANYAKAZI WA TBL GROUP WAADHIMISHA VALENTINE DAY KWA STAILI YA NAMNA YAKE

February 15, 2018
Wafanyakazi wa TBL wakipata mafunzo sambamba na burudani za vinywaji baada ya saa za kazi. Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakifuatilia mafunzo ya mahusiano na afya.
Wafanyakazi wa TBL Arusha wakifutilia mafunzo. TBL Moshi hawakubaki nyuma katika mafunzo hayo.
TBL Mbeya nao walishiriki mafunzo na mijadala ya mahusiano Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBev, imeitumia Siku ya Wapendanao kuandaa semina za wafanyakazi wake kuhusiana na masuala ya mahusiano katika familia, zilizoendeshwa na wataalamu wa masuala ya Saikolojia na ushauri nasaha kutoka taasisi mbalimbali za mafunzo nchini. Semina hizo zilifanyika katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha. Kwa kutumia kauli mbiu ya ‘Nogesha Upendo Valentine hii’ wafanyakazi walipata fursa ya kupata mafunzo,na kushiriki mijadala kuhusiana na mahusiano bora katika ndoa na familia sambamba na changamoto mbalimbali zilizopo, pia waliweza kupata majibu na ushauri wa changamoto hizo waliokuwa wakiendesha mafunzo. -- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

MSD YATUNUKIWA ITHIBATI YA JUU YA UBORA

February 15, 2018


Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imeendelea kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi, utunzaji na usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara (Supply Chain Management) na kupata Ithibati ya Kimataifa ya ubora ya daraja la juu inayojulikana kama ISO 9001:2015 ambayo itadumu kwa miaka mitatu (2018 - 2020).

Hatua hiyo imekuja baada ya ukaguzi wa ubora wa huduma zinazotolewa na MSD uliofanywa na kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED mweziAgosti 2017, na kudhihirisha kuwa huduma zake zinafuata miongozoya ya juu ya kimataifa katika utoaji wa huduma za mnyororo wa ugavi.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema kuwa hatua hiyo ya kupata ithibati ya juu ya Ubora ya Kimataifa imethibitisha umahiri wa MSD na imeongeza chachu ya utendaji, ubunifu na kuboresha masuala yote yanayo husiana na mnyororo wa ugavi ilikuwapa wananchi huduma bora, zenye viwango, bei nafuu na kuwafikishia kwa wakati.

Bwanakunu ameongeza kuwa Ithibati hiyo inaonesha dhahiri ubora wa mfumo wa ugaviwa MSD  kwa wateja na wananchi kwa ujumla, na kueleza kuwa huduma za MSD zinaendelea kuboreshwa zaidi kwani taasisi hiyo iko katika kipindi cha maboresho ya kiutendaji kupitia mpango mkakati wake wamwaka 2017 - 2020. 

Mara ya kwanza MSD ilipataIthibatiya kimataifa mwaka 2013 (ISO 9001:2008) baada ya kukidhi matakwa ya ubora kwa huduma zake za Ununuzi, tunzaji na Usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na iliweza kuishikilia  ithibati hiyo kwa miaka yote bila kunyanganywa, kutokana na kuonekana kuendelea kukidhi viwango vya ubora kila walipokaguliwa. 

MSD imekuwa  miongoni mwa taasisi za kwanza nchinikupataithibatiyauborayakiwango cha ISO 9001:2015 kutokakiwango cha ISO 9001:2008 na imethibitisha umahiri wa utendaji wake.



RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA LUTENI JENERALI YAKUBU HASSAN MOHAMED KUWA MNADHIMU MKUU WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA LUTENI JENERALI YAKUBU HASSAN MOHAMED KUWA MNADHIMU MKUU WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

February 15, 2018
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha cheo kipya Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ambapo awali alikuwa na cheo cha Meja Jenerali kabla hajamuapisha kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu jijini Dar es Salaam.
3-4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu jijini Dar es Salaam.
5
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati Maafisa Mbalimbali wastaafu wa (JWTZ) walipokuwa wakizungumza mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
9 10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi mbalimbali wa habari waliofika kuripoti habari za Uapisho wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed Ikulu jijini Dar es Salaam.
11
Maafisa Mbalimbali wa Jeshi waliopandishwa vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wakipiga makofi wakati wa hotuba za Maafisa mbalimbali wastaafu wa JWTZ walipokuwa wakizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam.
12
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwavalisha vyeo vipya vya Meja Jenerali kutoka Cheo cha Brigedia Jenerali maafisa mbalimbali wa Jeshi hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
13 14
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed mara baada ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
15
Maafisa Mbalimbali wa Jeshi la Wananchi akiwemo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed watano kutoka kulia wakiwa wamepiga Saluti wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
16 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi ambao wamepandhishwa vyeo kutoka Cheo cha Brigedia Jenerali na kupewa cheo kipya cha Meja Jenerali Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MPANGO WA WEZI MRADI WA E-IMMIGRATION NI WALE WALE

February 15, 2018
-- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

MAHUSIANO YA KIMAPENZI BILA KUPIMA AFYA YADAIWA KUWA CHANZO KIKUBWA CHA MAAMBUKIZI YA VVU

February 15, 2018
Imeelezwa kuwa watu wengi wanaendelea kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutokana na kuanza mahusiano ya kimapenzi bila kutambua afya zao hali inayosababisha waanze kuishi kama mume na mke bila kujua hali zao za kiafya. 

HIFADHI YA MIKUMI YAIOMBA SERIKALI KUCHEPUSHA BARABARA YA LAMI INAYOPITA NDANI YA HIFADHI HIYO

February 15, 2018

Na Hamza Temba-WMU-Morogoro
................................................................
Serikali inafikiria namna bora ya kubadilisha uelekeo wa eneo la kilometa hamsini za barabara ya lami inayopita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi au kutoza kodi ya utalii kwa watu wanaotumia barabara hiyo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazosabishwa na barabara hiyo kwenye uhifadhi.

Hayo yamesemwa mkoani Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kufuatia ombi la uongozi wa hifadhi hiyo la kuiomba Serikali kuchepusha barabara hiyo kutokana na athari mbalimbali za kimazingira zinazosabishwa na uwepo wa barabara hiyo ndani ya hifadhi hususan vifo vya mara kwa mara vya wanyamapori, ujangili na ukosefu wa mapato ya Serikali.

Awali akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo mbele ya Waziri Kigwangalla, Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Gerald Mono alisema licha ya barabara hiyo kuwa na fursa nyingi za kimaendeleo imekuwa na changamoto nyingi kwenye uendeshaji wa shughuli za uhifadhi.

Alisema wastani wa mnyamapori mmoja hugongwa na gari kila siku katika barabara hiyo ambapo takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2014 idadi ya wanyamapori waliogongwa walikuwa 351, mwaka 2015 walikuwa 361 na mwaka 2016 walikuwa 218.

Alisema changamoto nyingine ni uchafuzi wa mazingira ambapo wastani wa taka ngumu zisizopungua kilo 138.3 huzalishwa kila siku na watumiaji wa barabara hiyo.

Mbali na changamoto hizo alisema nyingine ni ukosefu wa mapato ya Serikali kufuatia kukosekana kwa mageti ya kulipia tozo za utalii kwa watumiaji wa barabara hiyo ambao hufaidi utalii wa bure na kuikosesha Serikali mapato.

Alisema Changamoto nyingine ni ujangili ambao huchochewa na uwepo wa barabara hiyo ambayo hutoa fursa kwa majangili kuingia katika hifadhi hiyo kiurahisi kwa njia mbalimbali ikiwemo magari na pikipiki.

“Hifadhi inaiomba Serikali kuchepusha barabara hii ili kupunguza changamoto hizi zinazotokana na uwepo wa barabara husika na kuongeza mapato ya Hifadhi kwa kuzuia utalii a bure unaofanywa na watumiaji wa barabara wa ndani na nje,”. Alisema Kaimu Mhifadhi Mkuu huyo wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema changamoto kubwa aliyoiona katika hifadhi hiyo ni namna ya watalii kufika na kufanya shughuli za utalii katika hifadhi hiyo.

Alisema licha ya uwepo wa barabara ya lami inayokatiza hifadhini hapo, barabara hiyo sio rafiki kwenye uhifadhi. “Kuna hiyo barabara ambayo inaleta watalii hapa, ni barabara ambayo iko bize sana, ni barabara ya kitaifa na kwa vyovyote vile hii sio barabara mahsusi kwa ajili ya shughuli za utalii.

“Sisi (Serikali) tunatafakari namna ya aidha kuiondoa hiyo barabara au namna ya kuwachaji watu wanaokatiza hizi kilometa hamsini ambazo zipo ndani ya hifadhi ya Mikumi,” alisema Dk. Kigwangalla.

Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla amemtaka muwekezaji aliyepewa hoteli ya kitalii ya Mikumi Wildlife Lodge iliyopo ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ukarabati na uendelezaji kuhakikisha anakamilisha makubaliano hayo ndani ya muda aliyopewa kwa mujibu wa mkataba aliosaini na TANAPA ama sivyo atanyang’anywa kibali hicho.

Akizungumzia jitihada za kuimarisha ulinzi wa hifadhi hiyo, Dk. Kigwangalla amesema Serikali inakusudia kuharakisha mchakato wa kuanzishwa kwa jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Kidoma itakayojumuisha vijiji vya Kilangali, Doma na Maharaka ili kutengeneza buffer na hatimaye kuimarisha uhifadhi shirikishi.

Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ilianzishwa mwaka 1964 kwa Tangazo la Serikali Na. 465 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 1,070. Mwaka 1975 Serikali iliona umuhimu wa kuongeza eneo upande wa kusini na kaskazini mwa Hifadhi na kufikia ukubwa wa kilometa za mraba 3,230 kwa tangazo la Serikali Na. 121.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongea na Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Gerald Mono wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro. Uongozi wa hifadhi hiyo umeiomba Serikali kuchepusha barabara ya lami inayopita ndani ya hifadhi hiyo kutokana na athari mbalimbali za kimazingira zinazosabishwa na barabara hiyo ikiwemo vifo vya wanyamapori, ujangili na ukosefu wa mapato ya Serikali unaotokana na watu kufaidi utalii wa bure. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maziringira ya jengo lililoungua moto la Mikumi Wildlife Lodge ambalo linalofanyiwa ukarabati wakati wa ziara yake ya kikazi katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi jana mkoani Morogoro ambapo amemtaka muwekezaji aliyepewa hoteli hiyo kuikarabati ndani ya muda aliopewa ama sivyo atanyang’anywa kibali alichepewa. Kushoto kwake ni Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Gerald Mono. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa  na Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Gerald Mono kukagua mazingira ya hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo  kutoka kwa Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Gerald Mono wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mazingira mwanana ya  Hifadhi ya Taifa ya Mikumi wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro.
Picha ya pamoja.