ASASI YA TREE OF HOPE YAENDESHA MDAHALO WA WADAU WA ELIMU HANDENI

October 19, 2017
 Mratibu wa Mradi wa kuhamasisha Uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha huduma za elimu katika Jamii ambao unatekelezwa na Asasi ya Tree of Hope chini ya Ufadhili wa Shirika la Foundation for Civili Society,Goodluck Malilo akisisitiza jambo kwenye mdahalo wa wadau wa Elimu Kijiji cha Michungwani na Kwedizinga wilayani Handeni Mkoani Tanga
 Mratibu wa Mradi wa kuhamasisha Uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha huduma za elimu katika Jamii ambao unatekelezwa na Asasi ya Tree of Hope chini ya Ufadhili wa Shirika la Foundation for Civili Society,Goodluck Malilo akisisitiza jambo kwenye mdahalo wa wadau wa Elimu Kijiji cha Michungwani na Kwedizinga wilayani Handeni Mkoani Tanga
 Mwanasheria na Wakili Richard Vicent akisisitiza jambo kwenye mdahalo huo uliohusidha viongozi mbalimbali na walimu Kijiji cha Michungwani na Kwedizinga wilayani Handeni mkoani Tanga
 Afisa Mradi huo,Abdul Kihange akisisitiza jambo wakati wa mdahalo huo
 Diwani wa Kata ya Segera (CCM) wilayani Handeni,Yassin Tamimu  akizungumza katika mdahalo huo
 Afisa Mradi huo,Abdul Kihange akigawa makabrasha kwa washiriki wa mdahalokuhamasisha Uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha huduma za elimu katika Jamii ambao unatekelezwa na Asasi ya Tree of Hope chini ya Ufadhili wa Shirika la Foundation for Civili Society,Goodluck Malilo akisisitiza jambo kwenye mdahalo wa wadau wa Elimu Kijiji cha Michungwani na Kwedizinga wilayani Handeni Mkoani Tanga
 Sehemu ya washiriki katika mdahalo huo wakiufuatilia
 Sehemu ya washiriki katika mdahalo huo wakiufuatilia
 Sehemu ya washiriki katika mdahalo huo wakiufuatilia
Baadhi ya washiriki wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo

MBUNGE RITTA KABATI AMEKERWA NA MIMBA ZA UTOTONI KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KWAKILOSA

October 19, 2017
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea na wanafunzi,wazazi na walimu wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka huu 2017 katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo katika manispaa ya Iringa 
Baadhi ya wanafunzi na wazazi walihudhuria sherehe za kuhitimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo kata ya Mwangata.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi cheti mmoja ya wanafunzi wa kike aliyehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwakilosa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekerwa na uwepo wa mimba za utotoni katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo kata ya Mwangata manispaa ya Iringa kwa kuwa kitendo hicho kinachosababisha kushuka kwa elimu katika shule hii.

Akizungumza wakati wa shererhe za kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka huu Kabati alisema kuwa amesikitishwa kusikia kila mwaka kuna wanafunzi wanakatisha masomo kwa ajili ya kupata ujauzito.
“Jamani tumekuwa tukitoa elimu kila mara juu ya madhara yanayotoka na upatikanaji wa mimba za utoto za hiii shule imekuaje kila mwaka wanafunzi wanapata mimba hii haikubariki katika jamii kabisa maana hawa wanafunzi ndio tegemeo la taifa kwa sasa” alisema Kabati

Kabati aliwataka wazazi na walimu kuwalinda wanafunzi wa kike ili wasikumbane na ardha ya kupata mimba wakiwa watoto wadogo kwani kunapoteza muelekeo wa maisha yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

“Haiwezekani kila mara wazazi mnakuwa wa kwanza kuwa chanzo cha kuwaharibu watoto na kwanini wazazi mnafanya hivyo maana watoto hawa ndio watakao wasaidia hapo baadae ndio maana mkiwa mmezeeka kwa hiyo ndio watakuwa msaada katika maisha yenu naombeni muwatunze watoto wenu” alisema Kabati

Aidha Kabati aliwataka wanafunzi wote mkoani Iringa na Tanzania kwa ujumla kuacha kufanya mapenzi wakiwa na umri kama wao hivyo wanapaswa kujilinda ili kufikia malengo yao waliojiwekea na walidhike na kipato walicho nacho wazazi wao.

“Hivi kaka mimi ningeanza mapenzi nikiwa na umri kama wenu unafikiri ningefikia malengo haya niliyonayo hivyo nawaomba msifanye mapenzi mkiwa na umri mdogo ili baadae mje kufikia malengo yenu” alisema Kabati

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Hudson Luhwago aliwatupia lawama wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo kwa kutowalea katika malezi mazuri wanafunzi hao.

“Yaani kabisa mzazi anakuja na wanafunzi anamuombea ruhusa kuwa walikuwa fiesta wote hivyo mtoto amechoka hawezi kuja shule hii ni aibu na ukweli unaoendelea kwa baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule hii” alisema Luhwago

 Luhwago alisema kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanawanaume zaidi ya watano na wazazi wanayajua hayo lakini wanashindwa kuwakemea watoto wao na ndio maana wanakuja shule wakiwa na kiburi hata kwa walimu.

“Wanafunzi hawa wanaomaliza hitimu shule leo walikuwa wanakiburi kwa sisi walimu hadi ikabidi tukae kama wanalimu tuwajadili lakini chanzo chote ni malenzi mabaya wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya wazazi au walezi wao” alisema Luhwago

Akisoma risala kwa mgeni rasmi makamu mkuu wa shule Praygod Makongwa alisema kuwa hadi sasa kuna mwanafunzi ameachishwa shule akiwa kidato cha kwanza kwa sasbabu ya kuwa mujamzito na hata hawa wanaohitimu hii leo mwenzao mmoja alikatisha masomo akiwa kidato cha pili kwa kuwa na ujauzito.

“Sisi kama walimu wa shule hii tushazoe kuona wanafunzi wanakatisha masomo kwa ajili ya kupata mimba na ukiangalia kwa umakini walimu tunawalea wanafunzi kwa maadili yanayotakiwa tatizo lipo kwa wazazi hao unakuta mtoto na mzazi wapo disco pamoja wanakunywa pombe pamoja sasa hapo utapata matokeo gani?” alisema Makongwa


Lakini Makongwa alisema kuwa shule imejiwekea mikakati ya kuhakikisha inajenga majengo ya mabweni kwa wanafunzi ili kumaliza tatizo la mimba za utoto na kuboresha elimu ya shule ya sekondari ya Kwakilosa.
Ziara ya Waziri Makamba visiwani Zanzibar yaingia siku ya pili

Ziara ya Waziri Makamba visiwani Zanzibar yaingia siku ya pili

October 19, 2017
1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (kushoto) akimsikiliza Kapteni Abdallah Juma Abdallah Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Zanzibar alipokuwa akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi za bandari mara baada ya Waziri Makamba kupata fursa ya kuwatembelea.
2
Viongozi waandamizi wa Bandari – Zanzibar wakifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba alipotembelea bandari hiyo hii leo kujionea utendaji kazi wao na kuwapa fursa ya kuianisha changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kukabiliana nazo.
3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar  wa (pili kulia). Waziri Makamba amefanya ziara ya kutembelea ofisi zao na kupata fursa ya kufanya majadiliano kwa manufaa na ustawi wa Muungano wetu.
4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akiwa katika kikao na Menejimenti ya Bodi ya Mapato Zanzibar. Wa pili kushoto ni Kamishna wa Bodi Bw. Amour Hamil Bakari na Bi. Khadija Shamte  Naibu Kamishna. Waziri Makamba yuko ziarani Zanzibar kutembelea Taasisi za Muungano na zile zisizo za Muungano.
…………………………………………………………………….
Imebainika kuwa Bandari ya Zanzibar ni miongoni mwa Vyanzo vya Mapato vinavyopelekea ukuaji wa uchumi baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na fursa zilizopo katika nyanza za biashara.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Captain Abdallah Juma Abdallah katika siku ya pili ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ambapo amepata fursa ya kutembelea Bandari ya Zanzibar.
Katika siku ya pili ya ziara yake ya siku saba Visiwani Zanzibar Waziri Makamba amebainisha kuwa lengo la ziara yake ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa masuala waliyokubaliana katika vikao baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar katika vikao vya mashirikiano.
“Niko Zanzibar kwa ziara ya kikazi na nimejikita zaidi katika kushughukikia masuala ya uchumi ikiwa ni pamoja na masuala ya Bandari, Forodha, Kodi na kubaini changamoto zilipo, utekezaji wa maazimio yaliyokubaliwa katika vikao vya majadiliano na kuangalia maeneo mapya yanayohitaji kuingizwa katika mfumo wa utatuzi,” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba amesema kuwa kuwepo kwa bandari ni ufanisi kwa uchumi na ni namna bora ya kuimarisha  Muungano  na ustawi wa Zanzibar na pande zote mbili za Muungano hazina budi kuondoa changamoto zilizopo kwa manufaa ya wote.
Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Mapato Zanzibar na kuwafahamisha kuwa lengo la Serikali zote mbili ni kuhakikisha kuwa pande zote mbili za Muungano zinanufaika na fursa za uchumi zilizopo, na kila upande unufaike na fursa zilizopo katika mambo ya Muungano na yale yasiyo ya Muungano.
Katika ziara hiyo Waziri Makamba amewataka  watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania upande wa Zanzibar kuzifanyia kazi changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza kwa haraka, kupunguza urasimu na kuongeza elimu kwa umma ili kujenga uelewa kwa wananchi  juu ya mambo yanayopaswa kuzingatiwa na yale yasiyopasa ili kuondoa vikwazo vinavyojitokeza katika bandari ili kuondoa malalamiko ya wananchi.
Nae Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  kwa upande wa Zanzibar Bw. Mcha Hassan Mcha amesema kuwa ni vema wananchi wazingitae kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ikiwa pamoja na kupata risiti halali kwa kila bidhaa wanazonunua ili kuepuka usumbufu pindi wasafirishapo bidhaa baina ya Tanzania bara na Zanzibar.
Ziara ya Waziri Makamba visiwani Zanzibar itaendelea kesho kwa kutembelea miradi mbalimbali ya Mazingira.

Barclays launches 'TwendeKazi & BaloziMwanafunzi' scholarships programs

October 19, 2017
 Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), is convoyed by Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left), University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo (right), some Barclays senior officials and invited dignitaries before the launching ceremony of  Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
 Barclays Bank Head of Marketing and Corporate Relations Aron Luhanga (third left), and University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo, sign contract documents to officiate the launching  of Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday. Looking on from left are Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji, Barclays Head of Human Resources, Patrick Foya, UDSM  Deputy Corporate Counsel, Dr. Saudin Mwakaje and Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako.
 Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), addresses participants during the official launching of Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
 A cross section of partakers during the launching ceremony of Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
RAIS DKT MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MAKUBALIANO YA KAMATI ZA TANZANIA NA KAMPUNI YA BARRICK GOLD KUHUSU MAKINIKIA

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MAKUBALIANO YA KAMATI ZA TANZANIA NA KAMPUNI YA BARRICK GOLD KUHUSU MAKINIKIA

October 19, 2017
ma2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp.Profesa John L. Thornton alipokutana nae wakati wa kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
ma3a
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John L. Thornton akiwa na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold  Richardc William huku Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Florens Luoga nao pia wakiweka saini ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
ma12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold  Richardc William na maafisa waandamizi wa kampuni hiyo baada ya kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
ma8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John L. Thornton wakimsikiliza Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba akitoa muhtasari wa  ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
ma9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea  ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
PICHA NA IKULU
TANZANIA NA OMAN KUANZISHA UTALII WA PAMOJA WA KIHISTORIA NA UTAMADUNI

TANZANIA NA OMAN KUANZISHA UTALII WA PAMOJA WA KIHISTORIA NA UTAMADUNI

October 19, 2017


1J8A7639
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
1J8A7650
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, Kulia ni Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
1J8A7652
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
1J8A7659
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akiteta jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, wakati akishuhudia tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
1J8A7663
Bendi ya Jeshi la Taifa la Oman wakipiga nyimbo za Taifa hilo zinazofanyika wakati wa vita na ukombozi
1J8A7672
Baadhi ya wananchi wakiwa na bendera za Taifa la Oman na Tanzania wakishuhudia tukio hilo
1J8A7679
Baadhi ya Askari Maji wa kikosi cha Oman wakiwa katika tukio hilo.

MBIO ZA TIGO DODOMA HALF MARATHON ZAZINDULIWA RASMI

October 19, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma -  Jordan Rugimbana akizungumza na waandishi wa habari anayefuatia ni Kaimu Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini - Henry Kinabo na mwisho ni Mkurungenzi Mtendaji wa Vision Investment, Ally Nchahaga wakizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika uzinduzi rasmi wa mbio ndefu za Dodoma almaarufu Dodoma Marathon. Mbio hizo zimethaminiwa na Tigo Tanzania na zinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma mwezi  Novemba mwaka huu.
(Kutoka kushoto)  Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dodoma - Robert Mabonye , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma -  Jordan Rugimbana ,Kaimu Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini - Henry Kinabo na Mkurungenzi Mtendaji wa Vision Investment, Ally Nchahaga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa mbio ndefu za Dodoma almaarufu Dodoma Marathon. Mbio hizo zimethaminiwa na Tigo Tanzania na zinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma  mwezi Novemba mwaka huu.  
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika atika uzinduzi rasmi wa mbio ndefu za Dodoma almaarufu Dodoma Marathon. Mbio hizo zimethaminiwa na Tigo Tanzania na zinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma  mwezi Novemba mwaka huu.   .

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akutana na Wafanyabiashara Jijini Mwanza

October 19, 2017
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji jana amekutana na wafanyabiashara Jijini Mwanza kwa ajili ya kusikiliza na kutatua baadhi ya kero za kibiashara kutoka kwa wafanyabiashara hao chini ya chama chao cha TCCIA.

Dkt.Kijaji aliwahakikishia wafanyabiashara hao kwamba serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara huku akibainisha kwamba mashine za kutolea stakabadhi EFD's sasa zinatolewa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA na hivyo wafanyabiashara hao wataondokana na baadhi ya kero walizokuwa wakikumbana nazo kutoka kwa mawakala wa mashine hizo ikiwemo kuzinunua kwa bei kubwa.

Awali wafanyabiashara hao walilalamikia suala la machinga kupanga bidhaa zao kando ya milango ya maduka yao ambapo Naibu Waziri Kijaji aliwasihi kuwa na subira wakati serikali utaratibu wa kuwasajili na kuwapatia machinga vitambulisho kama ilivyoelezwa kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 na hatimaye kuwaboreshea maeneo yao ya kufanyia biashara.
Na Binagi Media Group
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (kushoto), akizungumza na wafanyabiashara Jijini Mwanza jana. Wengine ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari (katikati) pamoja na Naibu Kamishina wa Kodi za Ndani TRA Makao Makuu, Beatus Nchota.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (aliyesimama), akizungumza na wafanyabiashara Jijini Mwanza jana. Wengine ni Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee (wa kwanza kushoto), Injinia Boniphace Nyambele aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari (kulia).
Naibu Kamishina wa Kodi za Ndani TRA Makao Makuu, Beatus Nchota, akizungumza kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari, akizungumza kwenye kikao hicho

Mawakala wa benki ya CRDB watakiwa kuendeleza uadilifu

October 19, 2017
Mawakala wa benki ya CRDB kupitia huduma ya Fahari Huduma kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza, wakiwa kwenye semina iliyoyandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kuwajengea weledi na uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja.

Mawakala kutoka wila ya za Nyamagana, Ilemela, Magu, Misungwi, Kwimba, Sengerema pamoja na Ukerewe walihudhuria kwenye semina hiyo iliyofanyika alhamisi iliyopita Oktoba 12,2017 Jijini Mwanza.

Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Wambura Calystus aliwasihi mawakala hao kuwa waaminifu katika kuwahudumia wateja ikiwemo kutunza siri za mihamara ya pesa za wateja wao huku wakitoa huduma bora kama ilivyo ada ya benki ya CRDB wanayoiwakilisha katika maeneo yao.

Mawakala hao walieleza kwamba semina hiyo itawasaidia kuboresha huduma zao kwa wateja na hivyo kuwahimiza wateja wa benki ya CRDB kuendelea kutumia huduma za benki hiyo kwani zinapatikana kwa urahisi katika maeneo yote nchini.
Na Binagi Media Group

Mkurugenzi wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Wambura Calystus, akifungua semina hiyo
Meneja wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Mafwimbo Mulungu akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa wa CRDB, Danford Muyango akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa BIMA kutoka benki ya CRDB tawi la Nyanza, Jackline Jubilate akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Meneja biashara wa CRDB tawi la Nyanda, Eugenius Mashishanga (kushoto), akizungumza kwenye semina hiyo
Baadhi ya wakala wa CRDB wakichangia mada kwenye semina hiyo
Baadhi ya mawakala wa benki ya CRDB wakiwa kwenye semina hiyo
Bonyeza HAPA CRDB ilivyoadhimisha Wiku ya Huduma kwa Wateja Geita