WANAVYUO MKOANI TABORA WATAKIWA KUTUMIA NAFASI ZAO KULINDA NA KUHIFADHI MAZINGIRA.

January 23, 2018
Na Tiganya Vincent

WANAVYUO Mkoani Tabora wameagizwa kuhakikisha kuwa wanatumia elimu wanayopata kuwa mabalozi watakaosaidia katika kuzuia uharibufu wa mazingira na kuwahimiza jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti mipya na kulinda iliyopo kwa ajili ya manufaa yao ya sasa na baadae.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati alipowaongoza wanavyuo kutoka Vyuo mbalimbali katika upandaji miti ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhakikisha kila mtu anashiriki katika zoezi hilo.

Alisema kuwa wasomi kama wanavyuo wakiwa mstari wa mbele katika utoaji wa elimu katika maeneo yao yanayowazunguka na sehemu za baadae watakazopangiwa kazi ipo nafasi ya kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo mistu kuendelea kuharibiwa.

Mwanri alisema kuwa jamii inawategemea sana wasomi katika kutoa elimu katika hatua ya awali ya kuzuia uharibifu kabla ya masuala mengine kama matumizi ya nguvu za dola hayafanyika katika kuzuia uharibifu usiendelee.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kitendo cha wanachuo hao kuomba kuweka alama katika Mkoa wa Tabora kinapaswa kuwa mwanzo kwao katika katika kupeleka elimu hiyo katika maeneo mbalimbali ya jamii inayowazunguka ili wananchi wengi waweze kutambua umuhimu wa kutoharibu mazingira na vyanzo vya maji.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tabora Idd Moshi aliwataka Wanachuo kuunga mkono juhudi za Mkuu huyo wa Mkoa wa kutaka kuigeuza sehemu ya kijana kwa kupanda miti miti na kurudisha uoto wa asili.

Alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora anafanyakazi nzuri ya kuhakikisha anasimamia agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha mikoa yote hapa nchini inapanda miti mingi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Moshi alisema kuwa wanachuo na jamii kwa ujumla wanalojukumu la kuhakikisha kuwa wanaunga mkono viongozi kwa kupanda miti sio katika maeneo ya umma katika maeneo wanayoishi.

Alisema kuwa wao wakiwa vijana wa CCM mkoa wa Tabora wameshapanda miti katika Wilaya ya Igunga , Nzega, Sikonge na Urambo katika kuunga mkono juhudi za viongozi wa Mkoa na Kitaifa.
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AKUTANA NA WATENDAJI WA ASASI YA INTERNATIONAL YOUTH FELLOWSHIP JIJINI DAR

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AKUTANA NA WATENDAJI WA ASASI YA INTERNATIONAL YOUTH FELLOWSHIP JIJINI DAR

January 23, 2018

PIX 1
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiteta jambo Ofsini kwake  na Maafisa Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship(IYF), leo Januari 23, 2018 walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza ambapo Watendaji wa Asasi hiyo wamewalisha mada kuhusu mafunzo yanayolenga mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu mara wamalizapo vifungo magerezani
PIX 2
Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF),  Jeon Hee yong akitoa mada mbele ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kuhusiana na mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu mara wamalizapo vifungo vyao magerezani
PIX 3
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mada kutoka kwa Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF) katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kushoto) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila..
PIX 4
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa taarifa fupi kabla ya  Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF) kuwasilisha mada yao katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 23, 2018.
PIX 5
Kikundi cha Kwaya cha Asasi ya International Youth Fellowship ambacho kinaundwa raia kutoka nchini Korea kikitumbuiza kabla ya uwasilishaji wa mada kama inavyoonekana katika picha.
????????????????????????????????????
Wataalam wa Jeshi la Magereza wakifuatilia Mada kuhusu mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu.
PIX 7
Kamishna Jenaerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship walioketi(wa kwanza kushoto) ni  Mkurugenzi Mkazi wa Asasi hiyo Bw. Jeon Hee yong(wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila. Wengine waliosimama mstari wa nyuma ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, leo Januari 23, 2018 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

Wanafunzi saba wafanya mtihani na kufaulu kupandishwa madaraja ya mkanda mweusi wa Goju Ryu karate

January 23, 2018
 Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Wanafunzi waandamizi saba wa  shule za Karate (dojo) mtindo wa Okinawa Goju Ryu  za  Kaizen na Hekalu la Kujilinda  za jijini Dar es salaam na Dodoma wamefanya mitihani na kufaulu kupandishwa madaraja ya mkanda mweusi chini ya Sensei Rumadha Fundi  (BOFYA HAPA KUMJUA) usiku wa Jumatatu Januari 22, 2018.
Wanafunzi hao kutoka Kaizen dojo  iliyopo Shule ya Sekondari ya Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda iliyopo katika shule ya msingi ya Zanaki ni pamoja na ma-Senpai Yusuf Kimvuli, Abdulwahud Aghfoul, Bilali Mtenga na Seif Soud ambao wamepanda kutoka mkanda mweusi daraja la kwanza (1st Dan)  kwenda la daraja la pili (2nd Dan) lijulikanalo kama "Nidan".
Wakati ma-Senpai Kimvuli, Maghfoul na Mtenga wanatoka dojo la Kaizen, Senpai Seif Soud anatoka Hekalu la Kujilinda.
Wanafunzi wengine watatu waliofaulu na kupanda daraja la kwanza (1st Dan) ama "Shodan" kutoka mkanda wa kahawia ni ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo.
Hii ni mara ya kwanza kwa  Sensei Rumadha Fundi  mwenye Dan 4,“Yondan” na  mwenye uzoefu mkubwa wa  mafunzo ya Goju Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan, kuwafanyia mitihani na kuwapandisha madaraja wanafunzi wa Tanzania.
Sensei Rumadha, ambaye alianza mafunzo ya Okinawa Goju Ryu miaka 38 iliyopita  katika Hekalu la Kujilinda la Zanaki amesema anajisikia furaha na fahari kutimiza hilo jukumu lake kwa mara ya kwanza, na kwamba hajutii kufunga safari hii kutoka Houston, Marekani, anakoishi na kuja kuwasaidia ndugu zake.
Na hilo liliwezakana baada ya mwaka jana huko  nchini Poland  Sensei Rumadha kufanya  na kufaulu vizuri mitihani wake wa kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan"  chini ya waamuzi (masters) toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do huko Okinawa.
Tokea hapo Sensei  Rumadha amekuwa na mamlaka ya kuwasaidia wanafunzi wake wa Tanzania na kuwafanyia mitihani na kuwapa wanafunzi  "Dan" hadi ngazi ya pili " Nidan" sababu katika Goju Ryu Karate  kuanzia Dan ya 3 na kuendelea hutolewa na Master Miyazato pekee.
"Hawa waliofaulu na kupanda daraja la pili hivi sasa wana mamlaka ya kufungua shule zao chini ya uangalizi wangu na wakiendelea kufanya vyema nitatoa idhini ya wao kuwa waalimu ("Sensei") wanaotambulika Okinawa  baada ya muda si mrefu ujao" amesema Sensei Rumadha.
Hakusita kutoa shukran zake nyingi kwa mlezi wake wa mafunzo tokea utotoni,  "Sensei Magoma Nyamuko Sarya akisema chini ya uongozi wake kitengo cha watoto kilichoitwa "Bomani Brigade"  kilichobuniwa  na mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu nchini Tanzania mwaka 1973,  hayati Sensei Nantambu Camara Bomani. 
Alitoa shukurani za pekee kwa viongozi wa sasa wa Hekalu la Kujilinda - Sensei Mohamed Murudker, Sensei Wilfred Melkia, Sensei Geofrey Sawayael “Shoo” na Sensei Rashid Almasi ambao amesema moyo wao wa  kuendeleza Goju Ryu bila kutetereka pale Zanaki ni wa kusifika, na kwamba anawapongeza sana.
Sensei Rumadha pia ameeleza kuwa kabahatika mwaka huu kualikwa kuiwakilisha Tanzania ambayo pamoja na na Angola ni nchi pekee za Afrika zilizoalikwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa chama cha "Jundokan" na Master Eiichi Miyazato Sensei huko Naha City, Okinawa, mwezi wa Novemba 1918. 
Chama hicho kwa sasa kinaongozwa na mwanawe Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye pia ni Mwenyekiti mkuu dunia wa chama hicho na mwanae Master Eiichi Miyazato, ambaye amewafanyia mitihani ya mkanda mweusi zaidi ya walimu 15 toka ngazi ya pili" Nidan" hadi ngazi ya saba "Nandan". 
Kwa mujibu wa Sensei Rumadha, ngazi hizo zote kwa utamaduni wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu Karate huchukua miaka mingi sana kupandishwa ngazi  tofauti na mitindo mingine. 
 Sensei Rumadha Fundi akiwafanyisha mazoezi wanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Viongozi wakuu wa  Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam  wakishuhudia  wanafunzi saba wakifanya mazoezi kabla ya mtihani Jumatatu usiku Januari 22, 2018. Kutoka kulia ni Sensei Wilfred Malekia, Sensei Mohamed Murudker na Sensei Rashid Almasi
  Sensei Rumadha Fundi akiendelea kuwafanyisha  mazoezi wanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Sensei Rumadha Fundi akiendelea kuwafanyisha  mazoezi kwa vitendowanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
 Sensei Rumadha Fundi akitoa mwongozo akiwa na uongozi wa dojo kabla ya  mtihani  wa kupanda daraja wa wanafunzi saba  katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
 Kutoka kushoto Ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo wakifuatiwa na ma-Senpai Yusuf Kimvuli wa Kaizen dojo na Senpai Seif Soud wa Hekalu la Kujilinda.
Wanafunzi watatu waliofaulu na kupanda daraja la kwanza (1st Dan) ama "Shodan" kutoka mkanda wa kahawia ni  kutoka kushoto ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo.

WAGOMBE 27 WATEULIWA MAJIMBO 2 KATA 4

January 23, 2018
Hussein Makame-NEC

WAGOMBEA 27 wa ubunge na udiwani wameteuliwa kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Februari 17, mwaka huu katika majimbo mawili ya ubunge na kata nne.

Katika uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki,  mgombea udiwani kupitita CCM katika kata ya Kimagai iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya  Mpwapwa mkoani Dodoma, amepita bila kupingwa.

Mbali na uteuzi huo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika kata sita za Tanzania Bara wanatarajia kuteua wagombea wa udiwani wa kata hizo siku ya Jumatano ya tarehe 24 Januari, 2018 kukamilisha kata 10 zilizopangwa kushiriki Uchaguzi Mdogo wa Februari 17, 2018.

Akizungumzi uteuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Hamis Mkunga amesema mgombea huyo wa CCMa amepita bila kupingwa baada ya mgombea wa CHADEMA kushindwa kurejesha fomu za uteuzi.

Amesema katika uteuzi wa wagombea Jimbo la Kinondoni, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo amewateua wagombea 12 ambao ni ambao ni Godfrey Maliza  kutoka chama cha TLP, Johnson Mwangosya  (SAU) na  Mwajuma Milambo kutoka UMD.
Mkunga amewataja wagombea wengine walioteuliwa kuwa ni John January Mboya  (Demokrasia Makini), Maulidi Mtulia (CCM), na Mary Mpangala wa DP.
Wengine ni Salim Mwalimu  (CHADEMA), Rajabu Salum (CUF), Mohamed Majaliwa (NRA), George Christian (CCK),  Ally Omari Abdallah (ADA THADEA) na Ashiri Kiwendu wa AFP 

Kuhusu uteuzi wa wagombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, Mkunga amewataja wagombea wanne walioteuliwa kuwa ni Dk Godwin Mollel (CCM) Mdoe Azania Yambazi (SAU), Tumsifuheri Mwanry (CUF) naElvis Christopher MosiwaCHADEMA.

Katika kata tatu zilizobaki, Mkunga amevitaja vyama vya siasa vilivyopitisha wagombea ambao waliteuliwa katika kata ya Isamilo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza kuwa ni Chama cha CUF, DP, UDP, CCM, na CHADEMA.

Katika kata ya Manzase iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, wagombea walioteuliwa wametoka kwenye vyama vitatu vya CCM,CHADEMA na CHAUMA wakati wagombea watatu waliteuliwa kutoka vyama vya ACT-Wazalendo, CCM na CUF kugombea udiwani katika kata ya Madanga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Panganimkoa wa Tanga.

Kuhusu pingamizi kwa wagombea, Mkunga amesema hadi saa 10:00 jioni ya Januari 21, 2018, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walipokea mapingamizi 10 kutoka Jimbo la Kinondoni mapingamizi manne na Kata ya Isamilo mapingamizi 6.

“Hakuna mapingamizi yaliyoripotiwa kutoka Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro na kata za Madanga na Manzase” amesema Mkunga na kuongeza:
“Mapingamizi ya Kinondoni, pingamizi moja limetolewa na CCM dhidi ya mgombea wa SAU, moja linatoka chama cha Dp kwa mgombea wake, lingine limewekwa na mgombea wa CUF na  wa CCM dhidi ya mgombea wa CHADEMA na la nne limewekwa na mgombea wa CHADEMA dhidi ya mgombea wa CCM”

Amefafanua kuwa katika kata ya Isamilo kulikuwa na mapingamizi sita mapingamizi manne ni ya mgombea wa CCM aliyewawekea pingamizi wagombea wa CHADEMA, CUF, DP na mgombea wa UDP.

Mapingamizi mengine ni kutoka kwa mgombea CHADEMA dhidi ya mgombea wa CCM na pingamizi lililowekwa na mgombea wa CUF dhidi ya mgombea wa CCM.

“Kinachofuata kwa sasa ni hawa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wanayapitia haya mapingamizi na kuyatolea maamuzi” ameeleza Mkunga na kufafanua kuwa:

Amesema kwa kuzingatia kifungu cha  44 (5) Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 na kifungu cha 40 (6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,wagombea waliokatiwa rufaa wana haki ya kukata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kata sita zinazotarajia kufanya uteuzi tarehe 24 Januari, 2018 ni kata Buhangazaya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera, na kata ya Kanyeleleiliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza.

Nyigine ni  kata ya Mitunduruni yaHalmashauri ya Manispaa ya Singida mkoani Singida, kata za Kashashi, Gararagua na Donyomuruak zilizopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya  Siha  mkoa wa Kilimanjaro.

Kutokana na mgombea wa udiwani kata ya Kimagai kupitia CCM, kupita bila kupingwa, Mkunga amesema Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani unaofanyika Februari 17, 2018 utahusisha majimbo ya Siha na Kinondoni na kata tisa badala ya kata 10 za Tanzania Bara.

Katika uchaguzi huo jumla ya vituo 869 vya kupigia kura vitatumika na wapiga kura 349,211 wanatarajia kushiriki katika uchaguzi huo mdogo.

Mkunga amewaasa wagombea na vyama kuzingatie ratiba za kampeni kwa sababu kila chama na mgombea wake kimewasilisha ratiba yake ya kampeni lakini pia tufanye kampeni za kistaarabu kwani hilo ni suala la msingi sana.

Amevikumbusha vyama na wagombea kuheshimu maadili ya uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni kwani vyama vyote vimekubaliana kuheshimu maadili hayo na kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingisiku ya kupiga tarehe 17 Febraur mwaka 2018.

NHIF kuimarisha na kuboresha huduma za matibabu nchini

January 23, 2018
Na Grace Michael, Geita
MKUU wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa namna ulivyojipanga na unavyoshirikiana na Uongozi wa Mikoa mbalimbali kwa lengo la kuimarisha na kuboresha huduma za matibabu nchini.
Pongezi hizo amezitoa leo wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Mfuko katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu. 
“NHIF nawapongeza sana kwa namna ambavyo mmekuwa tayari wakati wote kuhakikisha huduma za matibabu zinakuwa bora zaidi na niwahakikishie tu kwamba Mkoa umejipanga kutoa huduma kwa wananchi ambazo ni za kiwango cha juu kwani kama viongozi tuna deni la kuwatumikia Watanzania,” anasema.
Injinia Gabriel aliutaka Mfuko kutochoka kutoa misaada kama hiyo ambayo inalenga kuwanufaisha wananchi moja kwa moja.
Alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. Pombe John Magufuli imedhamiria kusogeza huduma kwa wananchi hivyo Mkoa unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za matibabu ili kuondokana na changamoto za huduma za afya.
Akikabidhi msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Bi. Anjela Mziray alisema jukumu kubwa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa Watanzania kupitia mfumo wa bima ya afya.
“NHIF inayo mipango mbalimbali ya kuhakikisha huduma za matibabu zinawafikia wanachama na wananchi kwa ujumla katika mazingira ambayo ni bora zaidi, mipango hiyo ni pamoja na mpango wa Mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ya vituo vya kutolea huduma ambayo ni mikopo nafuu inayosaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha huduma za matibabu,” anasema.
Alisema kuwa NHIF pia imekuwa na mipango mingine ikiwemo ya kupeleka Madaktari Bingwa katika mikoa mbalimbali kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa huduma za kitalaam katika maeneo yote ambapo Mkoa wa Geita ni moja ya Mikoa ambayo imeshanufaika na mpango huo.
Alitumia fursa hiyo kuuomba uongozi wa Mkoa hususani wa Hospitali kuhakikisha unaunga juhudi za Mfuko kwa kuhakikisha unatoa huduma bora kwa wanachama wake na kutatua kero ambazo wamekuwa wakizipata wakati wa kupata huduma hizo.
Bi. Mziray kwa niaba ya Uongozi wa Mfuko alikabidhi Vitanda 20, Magodoro 20 pamoja na mashuka 80 kwa hospitali hiyo ambayo ilikuwa na uhitaji wa vifaa hivyo.
Wakizungumza kwa nyati tofauti wanachama wa Mfuko waliokuwa hospitalini hapo walisema kuwa, huduma wanazopata kupitia kadi za matibabu za NHIF ni nzuri ambazo zimewaondolea usumbufu wa kutafuta fedha wakati wanapopatwa na magojwa.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bi. Anjela Mziray akionesha vifaa vya msaada vilivyotolewa na Mfuko huo katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akipokea vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 80 msada ambao umetolewa na NHIF.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akikalia kitanda kwa lengo la kukagua ubora wake.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akichunguza kitanda hicho na kuangalia ubora wa mashuka yaliyokabidhiwa.
 Baadhi ya Watumishi wa Hospitali hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa katika hafla ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo.
 Meneja wa Mkoa wa Geita wa NHIF, Dk. Mathias Sweya akielezea shughuli zinazofanywa na Mfuko mkoani humo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bi. Anjela Mziray akizungumza na Mama ambaye ni mmoja wa wanachama wa Mfuko.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel wakiwa na Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

RC MASENZA AZIPIGA JEKI SHULE TANO MKOANI IRINGA

January 23, 2018
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu mkoani Iringa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari na akiuliza kitu kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyanzwa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari akielekea kukagua vyoo vya shule ya sekondari ya Nyanzwa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo katika sekondari ya Ibumu
 Na hili ni moja ya jengo ambalo linajengwa kwa ajili ya maabara za shule ya sekondari ya Ibumu

Na Fredy Mgunda,Kilolo

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa jumla ya shilingi milioni nne (4,000,000) kwa ajili ya kuchochea manendeleo ya ujenzi  majengo kwenye shule nne za sekondari  ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule hizo wanasoma bila kuwa na usumbufu wowote ule.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya za sekondari zilizopo tarafa ya Mazombe mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kulipia kitu mchango wowote ule utakaochangishwa na walimu.

“Mimi nimetumwa na Rais kusisimamia ila ya chama cha mapinduzi kuhakikisha inatendewa haki katika kuleta maendeleo hivyo ni lazima nihakikishe wanafunzi wanakwenda shule na sio vinginevyo maana bila wanafunzi kwenda shule Rais hawezi kunielewa nitakuwa sijatimiza malengo ya kutoa elimu bila malipo” alisema Masenza

Masenza alisema kuwa atachangia shilingi milioni moja kwa kila shule za sekondari za tarafa hiyo ambazo zipo kwenye ujenzi na shule hizo ni Ibumu na Nyanzwa ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kuwapunguzia umbali wa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kuifuata shule.

“Naombeni tuzikamilishe shule hizi kwa wakati ili kuwapunguzia umbali wa kusoma watoto wetu haiwezekani wanafunzi hadi kuikuta shule moja ni umbali wa zaidi ya kilometa kumi na tatu ,jamani hawa ni watoto zetu na maisha yao yanategemea elimu hivyo ni lazima tuwekeze kwenye elimu” alisema Masenza

Masenza aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wapelekwe shule kwa wakati na wazazi wote ambao hawajawapeleke shule watoto wao wachukuliwe hatua kwa kuwa Rais hataki kuskia kuwa mtoto hajaenda shule.

“Jamani Rais ameagiza kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuwa shule hata kama hawana sare za shule sasa huyo mzazi gani ambaye hatakiwa kuwa peleka shule naombeni kabla sijawakulia hatua nyinyi viongozi basi hakikisheni wanafunzi wote waliofaulu wanakwenda shule” alisema Masenza

Lakini mkuu wa mkoa alifanya ziara kwenye shule ya sekondari Kihesa manispaa ya Iringa na akatoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000),shule ya sekondari  Ilambilole shilingi milioni moja(1,000,000) na shule ya msingi Matembo nako alitoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000) pesa zote hizo ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule.

Aidha Masenza alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa mkoa wa Iringa kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Masenza

Sipia Kinyowa ni kaimu mtendaji wa kata ya Nyanzwa, Amidu Kilamba diwani wa kata ya Nyanzwa,Hemerd Wiliamu diwani wa kata ya Ibumu na Justine Mgina mtendaji wa kata ya Ibumu ni baadhi ya viongozi waliompungeza mkuu wa mkoa kwa ziara aliyoifanya ya kimaendeleo na kimkatikati kuhakikisha wanafunzi wote wanatakiwa kufika shule na kusoma bila kubuguziwa na mtu yeyeto.

“Leo tumefarijiaka sana kuona mkuu wetu kaja na mikakati hasa ya kusaidia kukuza maendeleo kwenye sekta ya elimu hivyo hatuna budi kumuunda mkono kuhakikisha kuwa mambo aliyoyaongea tunayafanyia kzi ili kuhikisha wanafunzi wanasoma” walisema vingozi