CCM YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA ILANI KWA VITENDO KATIKA MANISPAA YA UBUNGO

September 04, 2017
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum A. Kalli akitoa salamu za CCM wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Zoezi la Uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo kimetoa heko kwa viongozi wa serikali Wilaya ya Ubungo chini ya Mkuu wa Wilaya Mhe Kisare Makori kwa ushirikiano wake katika utendaji na kuipaisha Wilaya katika tathmini za mafanikio kwa wananchi wake ukilinganisha na ugeni wa Wilaya kwani ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2016.

Sambamba na Mkuu huyo wa Wilaya kwa ushirikiano mkubwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo sawia na watumishi wote wameifanya Manispaa ya Ubungo kuwa kwenye rekodi ya Manispaa zinazothamini wananchi wake hususani wazee.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum Kalli wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam dhifa iliyofanyika katika viwanja vya TP Sinza E.

Kalli alitoa salamu za Chama hicho mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye pia Mhe Ummy aliahidi kutoa Bima za afya kwa watoto 100 wenye umri chini ya miaka 18 waishio katika mazingira magumu sambamba na kujenga wodi ya wazazi, watoto na maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya.

Alisema kuwa uzinduzi huo wa ugawaji wa vitambulisho ni kuonesha umma wa watanzania kuwa Wilaya ya Ubungo inawajali Wazee ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi Cha mwaka 2015-2020.

Alisema kuwa katika Sura ya nne, ibara ya 50 (P) inaeleza kuwa Halmashauri zitahakikisha wazee wanatambuliwa na kupewa matibabu bure katika Hospitali za serikali hivyo Manispaa ya Ubungo imetekeleza mkataba wa CCM na wananchi kwa vitendo ndani ya miaka miwili kabla ya kumalizika miaka mitano ya ahadi.

Kalli alisema kuwa pamoja na jambo hilo pia Wilaya ya Ubungo inapaswa kusimama kidete katika shughuli zingine mbalimbali ili kuwaletea maendeleo wananchi kutokana na imani kubwa walioionyesha Octoba 25, 2015 kwa kutoa ridhaa kwa Chama Cha Mapinduzi.

Kalli aliahidi mbele ya wahudhuriaji wa dhifa hiyo kuwa CCM itaendelea kuwaletea maendeleo wananchi huku akimpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo kwa kuiishi na kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo.

“Mgeni rasmi naahidi mbele ya hadhara hii kuwa CCM tutaendelea kuja mara kwa mara katika ofisi za serikali kukagua utekelezaji wa ilani ya ushindi mahali tutakapobaini kuwa ilani haitekelezwi tutakemea vikali kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla wake”
Wilaya ya Ubungo imekuwa Walaya ya pili katika Jiji la Dar es salaam kutekeleza agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee Octoba 1, 2009 kuwa Hospitali zote na Vituo vya Afya vya Umma kutenga dirisha na watumishi maalumu wa Afya kwa ajili ya kutoa Huduma za matibabu bure kwa Wazee.

BANDARI TANGA YAZIDI KUCHANUA KILIMANJARO CUP YAITANDIKA SCOPION YA ARUSHA VIKAPU 91-60

September 04, 2017
 Kikosi cha timu ya Bandari Tanga ambacho kinaendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi       
 kikosi cha timu ya Scopion ya Arusha  kabla ya kuanza mchezo wao na Bandari Tanga ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi

Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakisalimiana na wa timu ya Scopion ya Arusha ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi
Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakisaliana na wa timu ya Scopion ya Arusha kabla ya kuanza mechi yao na michuano ya Kilimanjaro Cup ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi
Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakichuano na timu ya Scopion ya Arusha ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi

 Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakichuana na timu ya Scopion ya Arusha ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi

 Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakipewa mawaidha na Kocha Mkuu wa timu hiyo,Mohamed Fazal wakati wa mapumziko katika mchezo wa michuano ya kikapu ya Kilimanjaro Cup ambapo Bandari Tanga illibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 ambapo leo Bandari watawavaa timu ya Mtwara kushoto n PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu
 Benchi la timu ya Bandari wakiwa kwenye umakini mkubwa
Timu ya Scopion ya Arusha Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakiwa kwenye benchi lao wakifuatilia kwa umakini mchezo baina yao na  timu ya Scopion ya Arusha ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi
Mchezaji wa timu ya Bandari Tanga akihojiwa mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa vikapu 91-60 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa KCMC mjini Moshi

Muda wa Maongezi, SMS na Data za Bure kwa Wanunuzi wa Tiketi za ‘Tigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa’

September 04, 2017

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko Tigo, William Mpinga(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa kutangaza ofa maalum za vifurushi zitazotolewa ununuapo tiketi ya tamasha la Tigo Fiesta kwa njia ya Tigo pesa. Pembeni ni Afisa Biashara wa Tigo, Edwin Mgoa

Tigo inatoa dakika 100 za muda wa maongezi, SMS  100 SMS na and 100 Mbs za data kwa manunuzi yote ya tiketi kupitia TigoPesa



Dar es Salaam, Jumatatu 4 Septemba, 2017- Huku ikiwa imebakia siku chache tu kabla ya onesho la kwanza la msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa kufanyika jijini Arusha, wadhamini wakuu kampuni ya Tigo inazidi kutoa ofa kabambe kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za awali kupitia huduma ya TigoPesa.

Tigo inatoa dakika 100 za bure, SMS 100 za bure, na  kifurushi cha 100Mbs cha data bure kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zaoTigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa kupitia huduma ya TigoPesa.

Akitangaza ofa hiyo murwa jijini Dar es Salaam jana, Mkuu Mtendaji wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa ofa hii mpya ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100Mbs za  data inaenda sambamba na ofa iliyopo sasa ya punguzo ya bei asilimia 10% kwa tiketi zote za awali za Tigo Fiesta 2017 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa au huduma ya kuhamisha fedha ya mitandao mingine yote ya simu nchini.

‘Kama tulivyoahidi hapo awali, tuna furaha kuthibitisha kuwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za ‘Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa’ kupitia Tigo Pesa, moja kwa moja watapata bonasi ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100 Mbs za data bure kutoka Tigo. Hii ni pamoja na ofa nono ya punguzo la 10% wanayopata wateja wote wa simu za mkononi wanaonunua tiketi zao za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya huduma ya kuhamisha fedha kwa njia ya mtandao wa simu.’

RITTA KABATI AIPONGEZA NURU FM RADIO KUANZISHA MASHINDANO YA MAMA MSOSI

September 04, 2017
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea wakati wa kutambulisha shindano la mama msosi linalolaratibiwa na kituo cha radio Nuru FM 93.5 Iringa katika viwanja vya Kata ya Kihesa.
Msimamizi wa vipindi vya Nuru fm radio na ndio Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya mama msosi mkoani Gerald Malekela akiongea na hadhara iliyokuwa imejitokeza wakati wa utambulisho wa shindano hili
Baadhi ya washiriki wa shindano la mama msosi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati

Na fredy Mgunda, Iringa.

Shindano la mama msosi linaloratibiwa na kituo cha radio cha Nuru fm mkoani Iringa limetambulishwa rasmi kwa wakazi wa manispaa ya Iringa likiwa na lengo la kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa kina mama na jamii kwa ujumla,shindano hilo litawapa washindi kumi na nane kwa kila kata ya manispa ya Iringa ambapo kila mshindi atajinyakulia mtungi mmoja wa shirika la gesi la mihan.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa shindano hilo mwenyekiti wa kamati ambaye pia ni msimamizi wa vipindi vya Nuru fm radio Gerald Malekela alisema kuwa wameamua kutoa elimu  ya mazingira kwa kuifikia jamii moja kwa moja kwa njia ya kuandaa shindano ambalo limeanza kwa mafanikio makubwa.

“Kutoa  elimu kuna njia nyingi sana hivyo nuru fm radio 93.5 Iringa tumeamua kutoa elimu ya utunzaji wa mazingiri kwa wakazi wa mkoa wa iringa kwa kutumia mashindano ya kupika na ndio maana unaona wananchi wamejitokeza kwa wingi sasa nauhakika elimu ya utunzaji wa mazingira imewafika na itaendelea kuwafikia” alisema Malekela.

Malekela aliwataka wakinamama ambao hawajachukua fomu za kushiriki shindano hili walizuate kwenye kata na hapa radio nuru fm ili kupata elimu bure ya mazingira ,ujasiliamali na kujua jinsi ya kutumia nishati mbadala ambayo haina madhara makubwa kwa jamii tofauti na ukataji miti hovyo.

MHE UMMY MWALIMU AZINDUA UGAWAJI WA VITAMBULISHO VYA TIBA KWA WAZEE MANISPAA YA UBUNGO

September 04, 2017
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 amezindua Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya TP Sinza E Waziri Ummy alipongeza uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa kutambua umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuwatambua Wazee katika Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma za matibabu bila vikwao.

Alisema kuwa Wazee ni asilimia 5.6 ya wananchi wote wa Tanzania idadi ambayo kwa kiasi kikubwa inaleta msukumo wa nchi kuweka mifumo madhubuti ya kuhudumia Wazee ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa Huduma katika matibabu.

Alisema kuwa Jambo hilo ni kuzingatia ukweli kwamba Wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na umri mkubwa na mtazamo wa Jamii ambao umekuwa ukichangia ukiukwaji wa haki na maslahi ya Wazee katika ngazi mbalimbali.

Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeingia kwenye rekodi kwa kuwatambua Wazee wasio na uwezo kwani watapatiwa vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma za matibabu Bure.

Mhe Ummy alisema kuwa Halmashauri zingine kote nchini zinapaswa kuanzisha haraka zoezi la kuwathamini Wazee kwa kuwapatia Huduma Bora za afya kabla ya kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee kote nchini kwa kuanzisha dirisha maalumu na wataalamu wa kuwahudumia Wazee.

Alitoa Rai kwa watoa Huduma wa Afya kuviheshimu vitambulisho wakati wote Wazee wanapoenda navyo kupatiwa matibabu huku akiwasihi Wazee kutumia vitambulisho hivyo kwa kuzingatia maelekezo sio kwa kuwapa watu wengine wasiohusika navyo.

Aidha waziri Ummy ameahidi bima ya afya kwa watoto 100 wenye umri chini ya miaka 18 wanaoishi kwenye mazingira magumu wilaya ya Ubungo na uandikishwaji utaanza leo pia ameahidi kujenga wodi ya wazazi, watoto na maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya wilaya ya ubungo mara baada ya kusikia hotuba ya kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Ubungo.
Muheshimiwa waziri ameiomba jamii kujiunga na bima za afya za gharama nafuu ili kupunguza mzigo kwa halmashauri na kulinda afya za wananchi
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alisema kuwa lengo la uzinduzi huo wa ugawaji wa vitambulisho ni kuonesha umma kuwa Wilaya ya Ubungo inawajali Wazee ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi Cha mwaka 2015-2020, sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na sera ya Afya ya Mwaka 2007.

Mhe Makori alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha Wazee wote nchini wanapata Huduma Bora za afya bila vikwao hivyo Wilaya ya Ubungo imeanza na utoaji vitambulisho kea Wazee 7296 waliojiandikisha na zoezi hilo litakuwa endelevu.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya Tiba kwa Wazee alisema kuwa Manispaa ya Ubungo imetekeleza agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee Octoba 1, 2009 kuwa Hospitali zote na Vituo vya Afya vya Umma kutenga dirisha na watumishi maalumu wa Afya kwa ajili ya kutoa Huduma za matibabu bure kwa Wazee.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Manispaa ya Ubungo ina jumla ya Vituo 19 vya kutolea Huduma za afya ikiwa ni pamoja na Hospitali moja, Vituo vya afya vitatu, Zahanati 15, na Kliniki Moja ya Mama na Mtoto hivyo Vituo hivyo vyote vitaanza kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee wasio na uwezo bila malipo.

MWISHO.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akizungumza wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu (Wa Tatu Kushoto) akionyesha vitambulisho vya Wazee akiwa na viongozi wengine wa Chama na serikali Wilaya ya Ubungo wakati wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na baadhi ya Wazee walioshiriki uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Ubungo Bi Maria Maliwa akisoma taarifa ya huduma za afya, Ustawi wa jamii na Msamaha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika uzinduzi wa vitambulisho vya msamaha kwa wazee wa Manispaa ya Ubungo.
Zoezi la Uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akimpatia Mzee Ferooz Kafuru kitambulisho Cha matibabu wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum A. Kalli akitoa salamu za CCM wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.

Kalli amepongeza uongozi wa serikali Wilaya ya Ubungo kwa kutekeleza ilani ya CCM ya ushindi yenye mkataba na wananchi kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akiteta Jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo mara baada ya kuzindua Huduma ya Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Walaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisalimiana na Wazee waliofika kushuhudia zoezi la uzinduzi wa vitambulisho kwa Wazee wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo lilifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akimpatia Bi Theresia Mbimbo kitambulisho Cha matibabu wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Madiwani wa Manispaa wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 

TMA yatabiri msimu wa mvua za vuli mwezi Oktoba hadi Disemba 2017

September 04, 2017
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli unaoanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2017. Kushoto ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa akishiriki katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli unaoanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2017. Kushoto ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa pamoja na Mkurugenzi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang’a (kulia) wakishiriki katika mkutano huo.
Sehemu ya waandishi wa habari wakishiriki katika mkutano huo na TMA ikitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli unaoanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2017.

Sehemu ya waandishi wa habari wakishiriki katika mkutano huo na TMA ikitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli unaoanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli unaoanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2017. Kulia ni Mkurugenzi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang’a akiwa katika mkutano huo.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli unaoanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2017. Kwa mujibu wa taarifa ya utabiri iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi ambapo mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza Septemba, 2017 katika maeneo mengi ya Ziwa Viktoria na mwezi Oktoba, katika ukanda wa pwani, na baadaye mwezi Novemba katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki. 

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum Afungua Mkutano wa 34 th Task Force Of Senior Officials Meetings Zanzibar Beach Resort Zanzibar

September 04, 2017
Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed akifungua Mkutano wa 34 wa Nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika (17th ESAAMLG  Council of Ministers and 34th Task Force Senior Officials Meetings Zanzibar Beach Resort Zanzibar') kuhusiana na kudhubiti Utakasishaji wa Fedha Haramu kwa Nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar na kushirikisha Nchi 18 za ukanda huo Mkutano hu utakuwa wa Siku wa siku tano hadi tarehe 8 mwezi huu.
Waziri wa Fedha na Mipango akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa kimataifa unaofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar na kuwashirikisha Wadau wa Nchi 18 za Mashariki na Kusini Mwa Afrika uliofunguliwa leo hadi tarehe 8/9/2017.
Viongozi wa meza kuu wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed akifungua mkutano huo katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. 
Wajumbe wa mkutano huo kutoka Tanzania wakifuatilia ufunguzi huo wa Mkutano wa 34 wa ESAAMLG unaofanyika katka ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Kikosi Kazi Mirirai Chirambe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Wajumbe wa Mkutano huo wakifuatilia hutuba ya ufunguzi ikitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed. 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nchini Lusotho Ms. Teboho Mukela akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa 34 wa Nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika kuzungumzia mkakati wa kupiga vita Utakatishaji wa Fedha Haramu unaofanyika Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Resort Mazizini.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kupambana na Utakasishaji wa Fedha Haramu kwa Nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dr Elianonye Kisanga, akizungumza wakati wa mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. unaowakilisha na Nchi 18 za ukanda huo. akitowa maelezo ya Ajenda ya mkutano huo kwa wajumbe baada ya kufunguliwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed.
Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed akiwa na viongozi wa meza kuu wakifuatilia maelezo ya Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo Dr. Kisanga, akitowa maelezo baada ya uzinduzi huo.

KANISA LA ABC LASIMIKA WACHUNGAJI WAKE NA KUWEKA WAKFU WAANGALIZI, LAWATAKA KUWAUNGANISHA WATANZANIA

September 04, 2017
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Rev. Flaston Ndabila, akitoa mahubiri  katika ibada  maalumu ya kuwasimika wachungaji watano na kuwawekea wakfu wengine watano kuwa waangalizi wa kanisa  hilo katika ibada iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.


 Mwangalizi  wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka  America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja akiwasalimia waumini wa kanisa hilo. Mchungaji Agbeja aliongoza ibada hiyo. Kulia ni Mtumishi wa Mungu, Zephaniah Andrew Nyambele ambaye alikuwa ni Mkalimali katika ibada hiyo. 

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Asumpter Mshama  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ibada hiyo akizungumza kwa niaba ya serikali.

 Wachungaji waliosimikwa. Kutoka kushoto ni  Ezekiel Katani kutoka Mbeya, Mbarikiwa Mwakatika kutoka Morogoro na  Leonard Mandia, Cosmas Nchimbi Morogoro na Joel Nsalila kutoka Dar es Salaam.
 Wachungaji waliowekwa wakfu kuwa waangalizi wa kanisa hilo katika majimbo. Kutoka kushoto ni Prince Twahir Rubeya, George Ntara,, John Muhembano, Lois Malali na Nathaniel Ndabila kutoka Mbeya na wengine waliobaki wanatoka Dar es Salaam.
 Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Kwaya ikiimba nyimbo za kusifu.