MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA MAENDELEO (UNDP)

MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA MAENDELEO (UNDP)

October 18, 2016


Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Lawrence Lachmansingh (wapili kushoto) na Nirina Kiplagat, walipofika kwa ajili ya kujadiliana juu ya masuala ya amani na maendeleo.Kulia ni Katibu wa naibu waziri, George Mwansasu.Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam. 
Meneja Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo.Katikati ni Mshauri wa Mradi kutoka UNDP, Lawrence Lachmansingh. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Mshauri wa Mradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Lawrence Lachmansingh (wapili kushoto), akizungumza na Naibu Waziri waWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo.Watatu kushoto ni Meneja Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat na kulia ni Katibu wa Naibu Waziri, George Mwansasu. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiagana na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat (aliyeshikana naye mkono) na ) Lawrence Lachmansingh, baada ya kumaliza majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akiwasindikiza wageni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat na Lawrence Lachmansingh(kushoto), baada ya kumaliza majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam..

MBUNGE LEMA AZUA TAHARUKI UZINDUZI WA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO JIJINI ARUSHA LEO.

October 18, 2016


Picha ikionyesha wa kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,Wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na Mtoto Duniani Edru Broun
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa hutuba.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.

Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuvuruga ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa  ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na mbunge Lema.

Kabla ya vurugu hizo mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (maternity Afrika ).

Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo gafla mbunge lema alipo simama na kupinga hotuba hiyo hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu .

“mkuu wa mkoa acha kupotosha uma ,mchungaji simamisha hutuba ya mkuu wa mkoa imejaa siasa anaongea uongo anaongea vitu asivyo vijua,sitakubali huu uongo uendee siwezi kubali hutuba iendelee kwani anaongea uongo ,akitaka atumie nguvu ya polisi siogopi kufa ila nataka ukweli ,na aondoe siasa aseme ukweli hili jamboni lamaendeleo ya wananchi na nikwaifada ya wananchi haswa mama na mtoto tena wale wasio jiweza kwaiyo naomba mkuu wa mkoa acha uwongo”alisikika Lema akisema kwa sauti kubwa huku akimsogelea mkuu huyo wa mkoa.

Jambo hilo liliwalazimu baadhi ya wageni wa alikwa wakiwemo wakinamama kumpigia magoti mbunge huyo alionekana akiwa na jazba kubwa huku akimsogelea mkuu huyo wa mkoa swala ambalo lingeweza kusabisha uvunjifu wa amani .

Licha ya Vurugu hizo na kelele za wananchi walionekana nao kupinga hotuba hiyo ya mkuu wa mkoa,Mkuu wa mkoa wa Arusha aliendelea kuhutubia akiwa anaeleza kuwa eneo hilo lilitolewa na marehemu Nyaga Mawala kwa serekali ili liendelezwe kwa kujengwa hospitali na mama na mtoto kitendo ambacho kiliendeleza kelele za wananchi zikipinga hotuba hiyo wakidai mkuu wa mkoa anapotosha .“hili jambo sio la siasa tusiingize siasa ,na kama kunamtu anampango wa kufanya siasa apa anapoteza muda wake mimi ni mkoa na ninafahamu historia ya eneo hili”alisema Gambo

Kwa upande wake mfadhili wa maradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya Festula Duniani Dkt.Edru Broun alieza kusikitishwa na tukio lilijitokeza na kuwataka viongozi waweke pembeni siasa zao na tofauti zao na wamatangulize mungu ili kutimiza shabaha ya ujenzi wakituo hicho cha hospitali kitakachoweza kumsaidi mama na mtoto.

Alisema kuwa ujenzi wa hopitali hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni sita na kwa awamu ya kwanza kiasi cha shili bilioni tatu kitatumika kujenga hospitali hiyo fedha ambazo zitatolewa na wafadhili kutoka shirika la mama na mtoto (martenity Afrika).

Kwa upande wake mwenyekit wa Tasisi ya maendeleo ya jiji la Arusha (ARDF) Elifuraha Mtowe Alisema kuwa eneo la kujegwa hospitali hiyo lilitolewa na marehemu Nyaga Mawala nakwa ARDF kupitia ofisi ya mbunge wa jimbo la Arusha mjini ndipo taasisi yao ya ARDF ikamamua kutafuta mfadhili ndipo walipompata MartenityAfrika.

Alisema kuwa tangu wampate mfadhili waliingia mkataba na wakakubaliana hospitali iishe ndani ya mika mitano lakaini mfadhili mwenyewe aliwaakikishia kuwa hospitali hiyo itaisha mapema iwezeka kwani itakamilika ndani ya mwaka mmoja tu ili mama na mtoto aweze kupata huduma kwa araka zaidi.

Awali mbunge Lema aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa mkoa huyo alikuwa amegoma kuja kuzindua hospitali hiyo hadi pale mbunge huyo alipoamua kumpiga simu katibu mkuu kiongozi John Kijazi na kumwambia kuwa mkuu wamkoa kagoma kuja kuzindua hospitali hiyo ndipo katibu mkuu alipoamua kupiga simu wizara ya tamisema ambapo ndio walimpigia simu mkuu wamkoa ili aweze kufika kwenye uzinduzi huo.

WAZIRI NAPE AKIWASILISHA MUSWADA WA HABARI KUIBADILI TAALUMA

October 18, 2016
SERIKALI imewasilisha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Muswada wa Huduma za Habari ikieleza kuwa ni sheria itakayoleta mageuzi makubwa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akiwasilisha muswada wa sheria hiyo leo mjini Dodoma ambapo amesema sasa sekta ya habari inakwenda kuwa taaluma kamili.

Waziri Nnauye amesema Sheria hii italeta mifumo ya kisasa ya usimamizi wa sekta ya habari na mifumo ambayo inaweza kugusa au kubadili namna wanahabari walivyozoea kutenda au kufikirika kwa sasa lakini akasema sekta hiyo iwe tayari kwa mabadiliko.

“Niwaombe wanatasnia wenzangu tuwe tayari kwa mabadiliko haya ili taaluma yetu iheshimike na sisi wenyewe tuheshimike zaidi” alisisitiza Mhe. Nnauye.Aidha Mhe. Nnauye ametoa wito kwa wadau wote kuunga mkono muswada huo utakaojadiliwa katika Bunge lijalo la Novemba mwaka huu. 

“Tuko hapa kuboresha na sio kusuguana tukae tuiandae tasnia bora zaidi kwa kupitia na kutoa maoni juu ya Muswaada huu wa Sheria ya Huduma za Habari 2016” alifafanua Mhe. Nnauye.Ameongeza kuwa kwa sasa hadi wakati wa Bunge lijalo Serikali ipo tayari kupokea na kuyafanyia kazi maboresho yatakayolenga kufikia maono ya muswada huu kutoka kwa wadau ili kuipa heshima stahiki sekta ya habari.

Alisema kuwa muswada huo licha ya huu utatatua changamoto za kutotambulika kwa sekta ya habari kama taaluma kamili inayopaswa kuheshimiwa, pia utatatua changamoto ya kukosekana vyombo madhubuti na huru vya usimamizi wa tasnia.

Alisema kutokana na hayo muswada unapendekeza kuundwa kwa Bodi ya Ithibati itakayoainisha sifa za mwanahabari na kuwasajili.Aliitaja taasisi nyingine inayoundwa kuwa ni Baraza Huru la Wanahabari ambalo litakuwa na wajibu wa kuandaa na kusimamia maadili ya wanahabari na watawajibishana wenyewe kwa wenyewe.

Wasomi wanena

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Benson Bana anasema kuwa kuja kwa sheria hiyo ni jambo la busara kwa sababu kwa sasa weledi wa uandishi wa habari uko chini.

“Sheria hii iwe na makali zaidi kwa wanahabari ambao watakiuka utaratibu na maadili. Hakuna nchi ambako wanahabari wanajiendea tu bila uratibu,” alisema,Alisema ni vyema na ni wakati mauafaka kwa sekta ya habari kuwa taaluma kamili na kushauri kuwa wanaoitumikia fani hiyo kwa sasa wawe tayari kwa mabadiliko.

Naye Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt William John Walwa alisema sheria imekuja wakati muafaka na inapaswa kutatua changamoto za fani hiyo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mswada wa Sheria ya Huduma za Habari 2016 leo Mjini Dodoma Oktoba 18,2016.

MAKAMBA ATOA MIFUKO 100 YA SARUJI KWA KIJIJI KILICHOHIFADHI MAZINGIRA

October 18, 2016



Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba katika mkutano na wananchi katika Kijiji cha Katarukila akiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Katurukila na kuwapongeza kwa kuwa Kijiji cha mfano kwa kuonyesha jitihada za dhati za kuhifadhi mazingira.



Bwana Candidius Songela akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akingalia ramani inayo onyesha eneo lenye mgogoro baina ya wanakijiji wa Katarukila na mwekezaji. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo.



Na Lulu Mussa,Kilombero

Wananchi wa Kijiji cha Katurulika, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro wameahidiwa Mifuko mia moja ya saruji ili kukamilisha ujenzi wa zahanati  katika tarafa yao inayohudumia wakazi wa vijiji sita.
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kutoa mifuko hiyo ndani ya wiki moja ikiwa ni pongezi kwa Kijiji hicho kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira na msitu wa Magombera.
Awali,  Bwana Dandidius Songela alimfamisha Waziri Makamba changamoto wanazokutana nazo katika Kijiji chao kuwa, ni pamoja na mgogoro baina ya Kijiji cha Katarukila na mwekezaji anayehodhi sehemu ya eneo la Kijiji na kusababisha uharibifu wa mazingira. Waziri Makamba aliwasihi wanachi wa Kijiji cha Katarulika  kuwa ni jukumu lao msingi kulinda msitu huo  kwa nguvu zao zote na kubainisha kuwa Hifadhi endelevu ya mazingira ndio mustakabali wa maisha yao.
Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) kumpa mwekezaji huyo "Restoration Order"  kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004  kwa kumtaka arejesha mazingira katika hali yake ya asili, kwakuwa ni eneo tengefu.
kwa upande mwingine Waziri Makamba amemwagiza Mkurugenzi wa  Wilaya ya Kilombero Bw. Dennis Londo kuhakikisha wanasheria wa Manispaa wanahudhuria kesi baina yao na mwekezaji huyo bila kukosa kila inapotajwa na baada ya kuhumu kutolewa Waziri Makamba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza kwa kina endapo kulikua na mianya yoyote ya rushwa katika mchakato wa kumilikisha ardhi ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara.
Waziri Makamba yuko ziarani Kilombero kuangalia changamoto za mazingira na awali alitembelea Mto Mkondoa Wilayani Kilosa.