WAKAGUZI WA MIGODI WAPIGWA MSASA

WAKAGUZI WA MIGODI WAPIGWA MSASA

December 15, 2014
unnamed
Baadhi ya Wakaguzi wa Madini kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi kuandaa miongozo (checklist) ili itakayosaidia katika kutekeleza shughuli za ukaguzi wa migodi.
unnamed1
Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje (katikati) akiongea jambo wakati akifungua rasmi kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini , Uratibu, Mhandisi John Shija, kulia ni Mhandisi Laurian Rwebembera.
unnamed2
Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Madini, Mhandisi Noel Baraka akiongea jambo wakati akitoa mada kuhusu Ukaguzi wa Madini wakati wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi nchini.
unnamed3
Mtaalamu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Chagwa Marwa, (kushoto) akichangia jambo wako wa majadiliano ya kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi. Anayesikiliza ni Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi, Assa Mwakilembe.
…………………………………………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Mwanza
Wakaguzi wa Migodi kutoka mikoa mbalimbali nchini wamekutana katika kikao kazi kwa lengo la kuandaa miongozo (checklist) itakayo wawezesha kutekeleza kikamilifu majukumu yao wawapo katika shughuli za ukaguzi wa migodi.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho, Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje amewataka wakaguzi hao kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kufanyika kwa ukaguzi yakinifu ili kuwezesha usalama migodini.
Mhandisi Samaje ameongeza kuwa, wakaguzi wa migodi wanao wajibu kuhakikisha usalama na afya migodini na kuongeza kuwa, masuala ya uhifadhi wa mazingira pia ni jambo la kuzingatia wakati wa kufanya ukaguzi.
“Naomba tuwe makini katika kutoa maoni yatakayosaidia kuandaa ‘checklist’, tumieni uzoefu mlionao tuboreshe jambo hili, ongezeni masuala mapya ambayo yatakuwa na manufaa katika shughuli za ukaguzi wa migodi. Lazima tutofautishe kutembelea na kukagua migodi,” ameongeza Samaje.
Aidha, amewataka kuwa makini na kutekeleza shughuli hizo kitaalamu kutokana na umuhimu wake na kuongeza, “tukikutuma kufanya ukaguzi, tunataka uende kama mtaalamu kweli unayefahamu majukumu yake. Kwa hiyo, maoni mtakayotoa leo, yatakua na mchango mkubwa katika shughuli za ukaguzi,” amesisitiza Samaje.
Katika kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa zikilenga kuwajengea uwezo wa namna bora ya kufanya shughuli za ukaguzi migodini.
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAFANIKIWA KWA ASILIMIA 98.

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAFANIKIWA KWA ASILIMIA 98.

December 15, 2014
unnamed
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Hawa Ghasia akiwaeleza waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana kote nchini ambapo umefanikiwa kwa asilimia 98%,kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
unnamed2
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Hawa Ghasia akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi wa Serikali uliofanyika jana kote nchini.
………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi- maelezo
Serikali imesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana Kote Nchini umefanikiwa kwa Zaidi ya asilimia 98% katika Mikoa yote .
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa ufafanuzi kuhuzi mafanikio ya uchaguzi huo.
Akifafanua Mh. Ghasia amesema kwa kiwango kikubwa wananchi walijitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi wao katika ngazi ya Mitaa,Vijiji, na Vitongoji.
Akizungumzia mafanikio ya Uchaguzi huo Mh. Ghasia alitaja Mikoa ambayo uchaguzi umefanyika katika Halmashauri na Kata zote kuwa ni Arusha,Mbeya,Kagera,Njombe,Singida,Lindi,Ruvuma,Katavi na Geita.
Mikoa Mingine iliyofanya vizuri katika uchaguzi huo ni Iringa,Dodoma,Mtawara ambapo Mh. Ghasia aliwapongeza Viongozi na wataendaji wote wa Mikoa na Halmashauri hizo pamoja na wananchi kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya hadi kufanikisha uchaguzi huo.
Akitoa ufafanuzi Zaidi kuhusu maboresho yaliyofanywa na Serikali katika uchaguzi huo Mh. Ghasia amesema kuwa mojawapo ni kuwepo kwa utaratibu wa kupiga kura kwa kutumia karatasi maalum zilizochapishwa kitu ambacho katika uchaguzi uliopita hakikuwepo.
Akizungumzia Mikoa ambayo baadhi ya Halmashauri zimeahirisha uchaguzi ama Halmashauri yote au sehemu ya Kata zake kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuchelewa kufika kwa vifaa vya kupigia kura Mh.Ghasia aliitaja kuwa ni Kilimanjaro katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Hai,Manyara katika Halmashauri za Hanang na mbulu.
Mikoa Mingine ni Morogoro katika Halmashuri ya Wilaya ya Ulanga na Mvomero,Mkoa wa Shinyanga Halmashauri ya Wilaya ya Msalala,Mkoa wa Simiyu Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Itilima ambapo Mikoa mingine ambayo kasoro ndogondogo zilijitokeza na kupelekea uchaguzi kuahirishwa katika baadhi ya Kata ni Kigoma,Mwanza,Tabora,Tanga,Mara,Rukwa,Pwani na Dar es salaam.
Akizungumzia Hatua zitakazochukuliwa na Serikali kufuatia dosari zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo Mh. Ghasia amesema Mikoa yote imetakiwa awasilishe taarifa rasmi na kamilifu kuhusu yaliyojitokeza katika Halmashauri zao ambapo Wizara yake itachambua taarifa hizo ili kubaini chanzo cha kasoro zilizojitokeza ili hatua stahiki zichukuliwe.
Kuhusu Halmashuri ambazo hazikufanya uchaguzi kutokana na kasoro mbalimbali Mh. Ghasia amesema kwa mujibu wa Kanuni zinatakiwa kurudia uchaguzi huo ndani ya siku saba kama kanuni za uchaguzi huo zinavyoelekeza.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini alitoa wito kwa vyombo vya habari kuweka uzalendo mbele katika kuripoti habari za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kusaidia Taifa kukamilisha mchakato huo muhimu.
Akifafanua Sagini amesema ni vyema vyombo vya Habari vikaonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uchaguzi huo pamoja na kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi ya Mitaa,Vijiji, na Vitongoji ulifanyika tarehe 14/12/2014 kote nchini ambapo taarifa za awali zimeonyesha kuwa zoezi la kupiga kura lilienda vizuri katika Mikoa Mingi.
MWAKILISHI MPYA WA WHO ZANZIBAR ATAMBULISHWA.

MWAKILISHI MPYA WA WHO ZANZIBAR ATAMBULISHWA.

December 15, 2014

Benki ya NBC yawapiga jeki vijana na kuwakumbuka yatima

December 15, 2014


Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa (kushoto) akitoa elimu kuhusu ujasiriamali na baadhi ya vijana kutoka vyuoni walio katika kambi maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya Maa Media kwa udhamini wa NBC mjini Bagamoyo, Pwani hivi karibuni. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya shs milioni 100 ambapo mbali na ujasiriamali vijana hao walifundishwa pia madhara na jinsi ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya.
Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kulia), akisalimiana na Meneja Miradi wa Kampuni ya Maa Media, Albany James wakati yeye na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa (kulia) walipotembelea kambi ya vijana iliyoandaliwa na Maa Media ili kuwafundisha masuala ya ujasiriamali, madhara na jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya shs milioni 100 kwa ajili ya kambi hiyo iliyofanyika mjini Bagamoyo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Lekoko Furaha.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Njombe, Sady Mwang’onda (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa vyakula, sabuni, mafuta na vitu vingine kwa walezi wa kituo cha watoto yatima cha Imiliwaha ikiwa ni moja wa matukio kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani mjini Njombe hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Njombe, Sady Mwang’onda akifanya mahojiano na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula, sabuni, mafuta na vitu vingine kwa walezi wa kituo cha watoto yatima cha Imiliwaha ikiwa ni moja wa matukio kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani mjini Njombe.
Vijana wakijiweka sawa kabla ya kuanza kwa mafunzo yao.
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Rukia Mtingwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari wakati uongozi wa benki hiyo ukitembelea kambi ya vijana iliyoaandaliwa na Maa Media kwa udhamini wa benki ya NBC.

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI SAMPULI ZA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA MADARASA YA AWALI KATIKA MANISPAA YA LINDI MJINI

December 15, 2014


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift Kyando mara baada ya kuwasili kwenye viwanja wa Shule ya Msingi Rahaleo iliyoko Manispaa ya Lindi Mjini kwa ajili ya kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kupitia taasisi yake kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Madarasa ya Awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo wakiwa pamoja na walimu wao wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati anawasili shuleni hapo tarehe 15.12.2014.
Sampuli za madawati yaliyotolewa na Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi kabla ya kukabidhi sampuli za madawati yaliyotolewa na Taasisi yake kwenye shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini kwenye sherehe fupi iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Rahaleo tarehe 15.12.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikabidhi sampuli za madawati yaliyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift Kyando kwa ajili ya Shule za Msingi zenye madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Shule ya Msingi ya Rahaleo tarehe 15.12.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na binti Naida Seleman anayesoma darasa la awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo mara baada ya Mama Salma kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kwenye Shule za Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, wanafunzi wa madarasa ya awali wanaosoma katika Shule ya Msingi Rahaleo na walimu wao wakati wa sherehe ya kukabidhi sampuli za madawati tarehe 15.12.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.

Yaya wa Uganda afungwa jela

December 15, 2014

Yaya wa Uganda aliyejipata pabaya kwa kumchapa mtoto wa mwajiri wake, amehukumiwa jela miaka minne kwa kosa la kumtesa mtoto.

Kisa cha yaya huyu kilizua hasira miongoni mwa watu wengi katika mitandano ya kijamii pale kanda ya video iliibuka mitandaoni ikimwonyesha yaya huyo akimchapa na kumkanyaga mtoto mwenye mwaka mmoja unusu.
Jolly Tumuhirwe, mwenye umri wa miaka 22, alinaswa kwa kamera ya siri akionekana akimchapa na kumkanyaga mtoto huyo pamoja na kumzaba kofi.
Mnamo siku ya Ijumaa, Jolly alikiri kumshambuilia mtoto akisema alikuwa analipiza kisasi kwani mamake mtoto huyo naye alikuwa amezoea kumchapa.
Hata hivyo mama huyo alikanusha madai ya Jolly ambaye polisi walikuwa wamesema wangemshitaki kwa kosa la jaribio la mauaji ila kiongozi wa mashitaka akasisitiza kuwa ingekuwa vigumu kuthibitisha hilo.
Hakimu mkuu Lillian Buchan aliambia Tumuhirwe kwamba alitenda uhalifu ambao hauna hata kisingizio.
Alisema adhabu aliyompa inamtosha kulingana na makosa yake kwa kumtesa mtoto ambaye hana hatia.
Babake mtoto huyo, Eric Kamanzi alisema aliweka kamera ya siri nyumbani kwake baada ya kuwa na shauku kumhusu mfanyakazi huyo.
Kanda ya video iliyomuonyesha Jolly akimtendea unyama mtoto, ilitoka kwenye kamera ambayo Bwana Kimanzi aliweka nyumbani kwake baada ya kushuku kuwa mtoto wake alikuwa anatendewa unyama na pia baada ya kumapata mtoto wake akiwa na alama za majeruhi mwilini mwake.
Alimshitaki mwanamke huyo kwa polisi na kisha kuisambaza kanda hio kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya hukumu kutolewa,Kamanzi alisema: "sio juu yetu kuamua adhabu anayofaa kupewa Jolly. ''
"tunatumai kuwa hili ni funzo kwa wafanyakazi wengi wa nyumbani kwamba huwezi tu kwenda kwa nyumba ya mtu na kumtesa mtoto na kutarajia kuondoka tu kama ulivyoingia. ''