*UJIO WA KOCHA MPYA WA SIMBA AACHIWE AFANYE YAKE BILA KUINGILIWA

December 01, 2013

Mashabiki wa Timu ya Simba, wakimpokea kwa shangwe na nderemo, kocha wao mpya aliyetua nchini leo machana. 


Mara kadhaa kumekuwa kukitokea furaha kwa mashabiki, viongoni na hata wachezaji wa Klabu zetu kubawa hapa nchini, wakati wanapokuwa wanamkaribisha Kocha mpya ama kumtambulisha kwa mbwembwe nyingi, lakini anapotokea kukosea kidogo haijalishi ni muda gani amekwisha kaa na Klabu husika, anaweza kutimulia ama kuanzishiwa mizengwe hadi akakata tamaa ya kuonyesha yale yote aliyojiandaa nayo kuifanyia Klabu husika. 


Wakati umefika sasa kwa Klabu zetu kufunguka kifikra na kuwa na upeo wa kufikiri ili kuziendeleza klabu zetu, kwa kuwaachia makocha waweze kufanya yale yanayostahili bila kuingiliwa na viongozi ama watu flani kwa pesa zao ama umaarufu wao katika klabu. Huko nyuma walikwishapokelewa makocha kadhaa kama alivyofanyiwa kocha huyu leo na waliondoka kimya kimya huku wengine wakiondoka klabuni kwa mafalakano na viongozi wa klabu.

Kocha huyo akikabidhiwa taji la maua na mashabiki baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar leo.
Akipata menu.....
Kocha huyo akiongozana na baadhi ya viongozi wa Simba wakati alipotembelea na kukagua uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo wa Kinesi.Picha kwa Hisani ya Lenzi ya Michezo na Sufianimafotoblog

*KILIMANJARO STARS YAITANDIKA SOMALI BAO 1-0 MICHUANO YA CHALLENGE

 Beki wa Kilimanjaro Stars, Erasto Nyoni (kulia) akichuana kuwania mpira na Hassan Ali Roble wa Somali, wakati wa mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mchana wa leo, Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya. katika mchezo huo Kilimanjaro Stars ilishinda bao 1-0.

WAKAZI 4737 MKOA WA TANGA WAGUNDULIKA KUWA NA MAAMBUKIZO MAPYA YA UKIMWI.

December 01, 2013



Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Benedict Ole Kuyan wakinyoosha mishumaa
kuashiria wakazi wa mkoa wa Tanga wakiungana wa wengine duniani
kuadhimisha siku ya ukimwi duniani.maadhimisho hayo kwa ngazi ya Mkoa
wa Tanga yalifanyika kijiji cha Duga Wilaya ya Mkinga.

mhandisi ushauri wa miradi ya majaribio ya barabara mkoa wa Tanga,Daniel Kemwa akipima virusi vya ukimwi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyofanyika kimkoa katika Kijiji cha Duga Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga.anayempima ni mshauri nasaha na mpimaji wa VVU  wa asasi ya Save The Society for HIV/AIDS ,Ali
Maghasa.
Burhani Yakub,Mkinga.
Jumla ya wakazi 4737 wa mkoa wa Tanga wamegundulika kupata
maambikizi mapya ya virusi vya ukimwi na 123 miongoni mwao wamekufa katika kipindi cha kuanzia januari hadi septemba mwaka huu.

Mratibu wa ukimwi Mkoa wa Tanga,Selemani Msangi alitoa taarifa hiyo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika mji mdogo wa  Duga  Wilayani.

NDEGE ILIYOPOTEA MSUMBIJI YAPATIKANA

December 01, 2013
Uwanja wa ndege wa Luanda, Angola.


NDEGE iliyopotea tangu juzi baada ya kuruka kwenye anga ya Msumbuji kuelekea Angola ikiwa na watu 34 imepatikana katika mbuga za wanyama Kaskazini Magharibi mwa Namibia.

Msemaji wa Polisi nchini Namibia amesema ndege hiyo iliteketea yote huku kukiwa hakuna aliyenusurika.

Ndege hiyo namba TM470 iliondoka Maputo nchini msumbiji tangu siku ya ijumaa na ilikuwa ikielekea Luanda nchini Angola.

NDERUMAKI WA TSN, MISS TANZANIA HOYCE TEMU WALA NONDO ZA UZAMILI SAUT

December 01, 2013

Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Serikali kama Daily News na Habari Leo Bw Gabriel Nderumaki (kulia) akiwa na aliyekuwa Miss Tanzania, Hoyce Temu pamoja na Afisa Uhusiano kutoka office ya Rais anayeshughulikia mazingira, Lulu Musa wakisoma kijitabu  cha matokeo  ya wahitimu wa mahafali ya 15 ya Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine yaliyofanyika jana jijini Mwanza. Wote watatu walihitimu shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Umma katika chuo hicho.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHEREHESHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM, LEO.

December 01, 2013


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, wakati alipotembelea katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA, katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na yeye kuzaliwa salama.